Website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?

Unaweza kuwa unajiuliza, “Sasa nimeshafungua website na ninazo akaunti za Twitter, Facebook na Instagram, lakini mbona watu hawatembelei tovuti yangu? nakosea wapi?“ Ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote ambaye hapendi kufanikiwa. Hakuna mfanyabiashara ambaye hapendi kupata Faida kubwa ya kifedha na wateja. Hakuna mtu ambaye hapendi kuingiza PESA. Ukweli ambao unaweza usiambiwe na Web-Designer unayempa kazi ya kukutengenezea website ya biashara yako ni kwamba: “Kumiliki Website na akaunti za mitandao ya kijamii (Zana za kimtandao) hakukufanyi kufanikiwa direct katika biashara hasa za mtandaoni” -Faustine Kimath Lakini kwanini umiliki hio website yenyewe, ilhali unaweza kutumia mitandao ya kijamii kuendesha biashara yako izuri tu? Majibu yanapatikana ukifuatilia makala hii hapa Kwanini ni Muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako? Baada ya hapo utagundua pamoja na kuwa na website bado kuna zana nyingi sana za kimtandao (Digital Tools) ambazo unaweza kuzitumia kuwafikia wateja wako sambamba na website yako kama zana kuu. Sasa … Continue reading Website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?