Website zinazotembelewa na watu wengi kila siku zina nini ambacho hujakifahamu bado?

Dec 21, 2021 Technology Updates
website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?

Unaweza kuwa unajiuliza, “Sasa nimeshafungua website na ninazo akaunti za Twitter, Facebook na Instagram, lakini mbona watu hawatembelei tovuti yangu? nakosea wapi?” Leo nataka nikwambie kuhusu website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado? Makinika hapa.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote ambaye hapendi kufanikiwa. Hakuna mfanyabiashara ambaye hapendi kupata Faida kubwa ya kifedha na wateja. Hakuna mtu ambaye hapendi kuingiza PESA.

Ukweli ambao unaweza usiambiwe na Web-Designer unayempa kazi ya kukutengenezea website ya biashara yako ni kwamba:

“Kumiliki Website na akaunti za mitandao ya kijamii (Zana za kimtandao) hakukufanyi kufanikiwa direct katika biashara hasa za mtandaoni”

-Faustine Kimath

Lakini kwanini umiliki hio website yenyewe, ilhali unaweza kutumia mitandao ya kijamii kuendesha biashara yako izuri tu? Majibu yanapatikana ukifuatilia makala hii hapa Kwanini ni Muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako?

Baada ya hapo utagundua pamoja na kuwa na website bado kuna zana nyingi sana za kimtandao (Digital Tools) ambazo unaweza kuzitumia kuwafikia wateja wako sambamba na website yako kama zana kuu. Sasa uzitumie vipi zana hizo ili ile Kiu yako ya kufanikiwa ikapate kutimilika?

Websites za kisasa zinatengenezwa zikiwa ni chanzo muhimu cha taarifa za kuaminika kuhusu Biashara/Kampuni yako. Hivyo website yako inafanya kazi ya kukutambulisha mtandaoni 24/7.

Sasa leo ukimaliza kusoma makala hii kuhusu website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado? Utapata uelewa hata siku ukifungua website yako ufahamu iwekwe vitu gani vitakavyoongeza idadi ya watu wanaoitembelea pamoja na kunasa wateja:

Kipengele namba 8 kitakufungua kichwa sana. Twende mpaka mwisho:

1. UBUNIFU:

Siku zote hakikisha unawapa wateja wako vitu wanavyopenda wao, sio unavyotaka wewe. Hata unapofikiria kubuni tovuti, hakikisha tovuti hio inafanana na aina ya wateja wako. Hivyo fanya utafiti wa kujua wateja unaowalenga ni wa namna gani kwanza.

Duru zinaonyesha 94% ya vitu vinavyomvutia mteja kwa mara ya kwanza kabisa (first impression) ni ubunifu uliotumika kutengeneza website hio. Ubunifu unajumuisha rangi za tovuti, mijongeo ya picha, aina za maneno (fonts) n.k

2. KASI YA KUFUNGUKA:

Kwa kawaida 94% ya watu huchukua si zaidi ya sekunde 5 kusubiri kurasa ya tovuti ifunguke. Baada ya hapo huachana na ukurasa huo na kuendelea na mambo mengine ya mtandaoni. Imagine tovuti yako inachukua zaidi ya sekunde 10 kufunguka sasa. Nani ataitembelea mara ya pili?

3. MATUMIZI YA ANWANI ZA NDANI

Unapokuwa na tovuti yenye anwani za ndani (internal links) za kutosha katika kurasa mbalimbali, unaiweka tovuti yako kwenye nafasi ya kutembelewa mara kwa mara tena na watu wengi zaidi.

Anwani hizi zinarahisisha kupatikana kwa taarifa kwa haraka na wepesi zaidi ndani ya tovuti yako.

Anwani hizo pia hutumika kama maneno ya msingi (keywords) katika injini za matafuto ya kimtandao kama Google. Hivyo mtu anapo-google inakuwa rahisi kupata majibu, bidhaa au/na huduma zinazotolewa kupitia tovuti yako.

4. MAUDHUI YA VIDEO:

Zamani ilikua si rahisi kurusha maudhui ya video mtandaoni na yakawafikia watu wengi kutokana na uduni wa teknolojia. Lakini siku hizi mambo ni tofauti sana. Maudhui ya video yamekuwa yakiwafikia watu wengi zaidi na kwa haraka sana. Angalia namna YouTube inayoshika kasi pale msanii wako unayempenda akiachia wimbo mpya. Siku hizi hata kukiwa na matukio muhimu ya Kitaifa, watu wengi huyafuatilia kupitia YouTube kuliko televisheni za kawaida.

Kwanini? Kwa sababu YouTube inapatikana kwenye smartphone, stesheni za televisheni hazipatikani kirahisi kwenye smartphones, hivyo nyakati hizi ukiwa popote kwenye mihangaiko yako ni rahisi kufuatilia maudhui ya video kupitia simu yako yenye intaneti kuliko wakati mwingine kwenye historia ya mwanadamu.

Maendeleo ya kiteknolojia yamerahisisha sana usambazwaji wa video mtandaoni. Hivyo unapofikiria kufungua/kuiimarisha website yako, hakikisha pia unaweka maudhui ya video ambayo yatawafanya watu wazidi kumiminika na kufaidi thamani ya maudhui hayo kirahisi.

5. MATUMIZI YA BLOGU

Kwa ulimwengu huu, masoko ya bidhaa na huduma yamehamia mtandaoni na hivyo kusababisha ushindani kuwa mkubwa sana ukiongozwa na uwepo wa maudhui mbalimbali yanayopandishwa kila siku.

Hivyo, tovuti yako inapaswa kuwa na kitu kipya kila leo.

Tovuti yenye Blogu ina nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwafikia watu wengi na kutembelewa kila siku tofauti na tovuti ambazo hazina sehemu ya Blogu. Kwenye blogu ndipo unapoweza kuweka maudhui ya kuwasaidia wateja wako kufikia malengo yao na kutatua changamoto wanazokutana nazo kila siku kupitia biashara yako. Hapa utagundua kwanini ni muhimu kuwa na website ya biashara yako?

6. MATUMIZI YA PICHA

Je, wajua kwamba picha ndio kiungo rahisi zaidi katika kuhudumia mteja? Zinamfanya mteja kukumbuka kuhusu huduma/bidhaa yako, ni nyepesi na rahisi kutumia. Maudhui yako yakiwa na picha, 65% ya wanaotembelea tovuti yako watakukumbuka hata wakitoka mtandaoni.

Mfano ukiitizama picha hii hapa chini wazo linalokujia haraka ni kwamba sasa ni wakati wa sikukuu ya Christmass, na kwa kuwa umeiona hapa picha hio bila shaka ukiiona sehemu nyinngine utakumbuka tu kwamba “Faustine alishawahi kuipost pia hii picha“. Unaiona nguvu ya picha hapo sasa? Imagine bidhaa zako unazipiga picha kali za kiubunifu na kuziweka kwenye tovuti yako sasa.

website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?

7. UMUHIMU WA S.E.O

Kama unahitaji mafuriko ya watu yazidi kumiminika katika tovuti yako kila siku, hiki kipengele cha SEO huwezi kukikwepa. Hii ni Teknolojia inayorahisisha matafuto ya mtandaoni na kuelekeza wapi pa kupata majibu na taarifa zaidi.

Imagine google inawaelekeza wateja waje kwako kupata taarifa, huduma na bidhaa muda wote ambao wewe umelala zako, au muda ambao wewe haupo mtandaoni ikiwa tu tovuti yako utakuwa umeiunga na miundombinu ya SEO. Hii S.E.O inahusisha matafuto katika mifumo ya maneno ya msingi (keywords) ambayo unakuwa ukiyatumia mara kwa mara katika tovuti yako na mifumo yako ya utoaji huduma. Hii imekuja kurahisisha sana maisha. Halafu cha ajabu zaidi, ni rahisi sana kuitumia. Ungependa kufahamu zaidi kuhusu SEO? Njoo WhatsApp sasa hivi kwa kugusa namba hii hapa 0765834754

8. UTATUZI WA KERO/CHANGAMOTO:

Jambo muhimu zaidi linalowavuta watu wengi kutembelea tovuti mbalimbali ni Nafasi ya Kutatua kero/changamoto zinazowakabili. Watu hawatembelei tovuti tu ilimradi, wanatafuta suluhu ya kero zinazowakabili kwenya shughuli zako za kila siku. Hivyo, zingatia hilo.

Hapa tunarudi kwenye SEO ambapo huduma hii itakurahisihia solution unazotoa kupitia website yako ziweze kuwafikia wateja wako haraka sana pale wanapozitafuta huko mtandaoni. Katika hili hakikisha website yako ina ukurasa uitwao Maswali yaulizwayo mara nyingi zaidi au Frequently Asked Questions (FAQs).

Je tovuti yako ina maudhui yanayotatua changamoto gani kwa wateja wako. Tuambie kwenye comments.

Unajiuliza utakuwa unatatua changamoto zipi? 1. Chunguza wateja wako uwafahamu wanapitia changamoto zipi, 2. kisha Jifunze namna ya kutoa huduma bora. 3. Fundisha kwa kuandika kutoka kwa wataalam wa copywriting. Rudia no.1.

-Faustine Kimath

9. MATUMIZI YA FOMU ZA MAULIZO:

Kama unataka tovuti yako ivutie watu wengi zaidi basi moja kati ya SIRI muhimu ni kuweka “fomu ya maulizo” ambayo inampa mtu yeyote anayetembelea tovuti yako nafasi ya kuuliza chochote kuhusu huduma/bidhaa zako. Muhimu sana hii, na siri ya kufanikiwa katika hili ni kuitengeneza fomu yako iwe fupi na ya kufurahisha (yani inatakiwa mtu akiiona tu ajisemee “loh, hebu niulize kuhusu … hapa chap“).

Fomu hii ni kipengele kinachoweza kuwabadili watembeleaji (visitors) kuwa wateja haraka sana.

10. HUDUMA KWA WATEJA:

Hata kama ukiyafanya yote uliyojifunza leo hapa kwanzia 1-9 lakini ukawa huna huduma nzuri kwa wateja wako na watu wanaotembelea tovuti yako na kuuliza maswali kwa lengo la ufafanuzi, ndugu, bado safari ya mafanikio itakuwa ndefu kwako.

Huduma kwa wateja inajumuisha namna unawasikiliza wateja wako, namna unavyojibizana nao (kwa maandishi au kwa sauti), muda unaotumia kuhudumia wateja wako na namna unavyoweza kuhimili hasira na mtazamo hasi kutoka kwa wateja na watu mbalimbali.

thamani vs gharama, nafuu iko wapi? fahamu siri za kuweza kushawishi wateja katika biashara yako.

website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?
Thamani vs Gharama: Nafuu iko wapi?

Vyote hivyo vinachangia kuongeza au kupunguza idadi ya watu wanaotembelea tovuti yako kwasababu takwimu zinaonyesha 95% ya wateja husambaza maneno kuhusu huduma mbovu walizopata na 89% kati yao huacha kabisa kufanya kazi na yule aliyetoa huduma mbovu zaidi unaweza kupitia makala hii hapa Umuhimu wa Takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa Wateja.

Tovuti ni sehemu muhimu sana katika kuhudumia wateja wa biashara yako pamoja na kujitangaza hasa katika zama hizi za kidijitali.

Huna haja ya kusambaza CV na makaratasi. Tunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya karatasi ambazo zinatokana na ukataji wa miti.

ZIADA: Hata ukisema uyafanye hayo yote 10 ambayo umeyaona kwenye makala hii ya leo, bado nature itakudai kitu kimoja cha muhimu zaidi. Nacho ni muendelezo (consistency) katika utendaji wako wa kusimamia biashara katika mazingira yote, mtandaoni na ana kwa ana. Fahamu kuwa hakuna mafanikio ya ghafla au mafanikio ya bahati mbaya. Yeyote unayemwona amefanikiwa (hata kwa bahati nasibu), lazima alistruggle kutengeneza mfumo mzuri wa kiutendaji ili kumsaidia katika kusimamia biashara yake katika viwango vinayotakiwa.

Umejifunza nini kwenye makala hii ya leo kuhusu website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado? Tuambie kwenye comments hapa chini. Pia hakikisha una-share makala hii pamoja na watu wako wa karibu ili kusudi somo hili liwafikie watu wengi zaidi.

website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?
mpesa lipa namba yetu
One thought on “Website zinazotembelewa na watu wengi kila siku zina nini ambacho hujakifahamu bado?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *