WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?

Apr 22, 2021 Technology Updates
website inasaidia vipi kuimarisha biashara yako?

Dunia ya leo inatawaliwa na Mapinduzi ya 4 ya Viwanda yanayoongozwa kwa Teknolojia, hivyo kuwa na website katika biashara yako ni muhimu sana. 85% ya vijana hutumia intaneti kwa matumizi yao ya kila siku. Kama ni hivyo, basi website inasaidia vipi kuimarisha biashara yako? Fuatilia makala hii ya leo mpaka mwisho kufahamu zaidi..

Katika makala yetu iliyowasilishwa hapa mnamo June 25, mwaka 2020 ilieleza kwa mapana kuhusu KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO, yaani kwanini uwe na website katika biashara yako leo hii? Hata hivyo leo hii tutazitazama na kuzichambua kazi sita (6) tu muhimu zaidi za website katika biashara yako. Faida nyingine nyingi kuhusu website huwa tunaziweka kwenye status zetu za WhatsApp kwa kugusa namba yetu hii hapa 0765834754. Save hio namba kisha tuma ujumbe wenye jina lako ili uanze kufaidi tips, updates, ushauri na huduma nyingi kutoka Rednet Technologies.

Unajua website inakupa faida zipi katika biashara yako? Ungana nami leo mpaka mwisho wa makala hii tuchimbue kila kitu. Twende kazi..

Sasa, website inasaidia vipi kuimarisha biashara yako leo?

1. UWEPO MTANDAONI: Jambo la kwanza kabisa website inakupatia uwepo wa biashara yako mtandaoni pasi na shaka. Kama ujuavyo idadi kubwa ya watu hutafuta bidhaa/huduma kwa njia ya mtandao (95% ya matafuto huanzia mtandaoni kabla ya kukiendea kitu halisi).

Mtandao wa Google ni sehemu kubwa na muhimu ya kutoa huduma hio ikifuatiwa na injini zingine kama Bing na Yahoo. Website inakupa utambulisho rasmi na usio na shaka kwa mtu yeyote duniani.

Hivyo usipoweka biashara na mawasiliano yako mtandaoni, hakuna mtu atajua kuwa biashara yako ipo hai. Website huziambia Injini za matafuto (Search Engines) kama Google kuwa biashara inafanya kazi fulani na huonyesha pia mawasiliano yako, hii huwezeshwa na mfumo wa matafuto na ulinganifu uitwao Search Engine Optimization (SEO). Hapa pia kuna tips na updates nyingi zaidi huwa tunashare kupitia namba yetu ya WhatsApp umeiona pale juu.

Kama biashara haipatikani kwenye matafuto ya kimtandao, inamaanisha biashara hio haipo mtandaoni. kufahamu kwa mukhtasari kuhusu SEO fuatilia makala hii hapa chini;

2. ENGAGEMENT(USHIRIKA): Uwepo wa tovuti mtandaoni huongeza Ushirika kati yako mtoa huduma/bidhaa na wateja wako wote. Tovuti hutengeneza mahali mahususi kwa wateja kushiriki kwa kuelimika kuhusu bidhaa/huduma, kutoa maoni, kero, kununua na kuwasiliana na muuzaji kirahisi.

Tovuti bora hutoa fursa kwa mteja kuuliza kuhusu bidhaa/huduma, kuomba appointment, kutoa maoni au/na kujifunza zaidi kuhusu bidhaa/huduma zinazopatikana katika biashara hio. Hakika huyu ndiye mfanyakazi unayemtaka kwenye biashara yako, ambaye yupo macho 24/7 kuhudumia wateja wako.

3. KUKUSANYA WATEJA: Kama kuna mahali unaweza kutega nyavu ya kuvua wateja wengi kirahisi, basi ni kwa kumiliki website ya biashara yako. Hii hukutaarifu pale mteja atakapokutafuta kupitia mawasiliano ambayo yamewekwa kwenye website.

Pia unaweza kukusanya data kuhusu mwenendo wa idadi ya watu wanaotembelea tovuti yako na hivyo kujua biashara yako inakuwa kwa kiwango gani. Hii huwezeshwa kwa kupitia kipimo cha Google kiitwacho Search Console ambayo hutoa taarifa kuhusu mwenendo mzima wa wateja wanaotembelea tovuti ndani ya wiki, mwezi, robo na mwaka mzima. Haya yote yanawezeshwa kirahisi sana unapotumia huduma za internet na teknolojia za Google. Kufahamu zaidi kuhusu hili fuatana na makala hii hapa chini:

4. KUOKOA MUDA: Website yako inakusaidia kuokoa muda na pesa kama mfanyabiashara. Hebu fikiria maelezo ambayo inakubidi kuyatoa kila mara kwa kila mtu unayekutana naye kuhusu biashara yako. Lakini mara hii hilo halipo tena. Website yako itafanya kazi hio 24/7 bila kuchoka. Hakikisha tu unalo bando la huduma za internet ili kukurahisishia kutoa taarifa muhimu kuhusu bidhaa na huduma unazotoa kupitia kurusa za website yako. Hii ni kwa sababu Bando lako ni Mtaji tosha kabisa katika kuokoa muda na kuimarisha website yako.

5. KUWAFIKIA WATU WENGI ZAIDI: Website inakupa nafasi ya kuwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi. Fikiria namna unavyoweza kutembelewa na wateja wengi kama inavyoonekana kwenye picha hapa. Je ungeweza kufanya haya mwenyewe? Hii ndio njia bora kutanuka haraka kibiashara. Hapa ukitumia vizuri Nguvu ya Mitandao ya Kijamii kwa hakika utaweza kuwafikia watu wengi sana ndani ya muda mchache.

Faida za website

6. FAIDA YA KIUSHINDANI: Kama unahitaji kuwa na watu wa uhakika ambao watakutafuta ili wawe wateja wako wa kudumu na kuwashinda washindani wako katika biashara, basi bila shaka unahitaji kuwa na Website. Website yako lazima iwe na taarifa zote muhimu kuhusu bidhaa/huduma zako.

Hapa ndipo unapokuja kujitofautisha na washindani wako na kuweza kuwashinda. Hakikisha website yako inasheheni taarifa muhimu zote, si zile unazozijua wewe, lakini ziwe zile ambazo mteja atazihitaji kuhusu bidhaa/huduma unazotoa. Makinika vizuri hapa.

Zaidi ya yote, Website yako ni Bango namba moja katika kuitangaza Biashara yako. Website Inakusaidia sana katika kutangaza bidhaa/huduma zote ambazo unazitoa. Ukiwa na website gharama ya kujitangaza kupitia televisheni au kuwalipa watu hushuka maradufu. Shukrani kwa website. Kuhusu namna bora ya kuitangaza biashara yako fuatana na makala hii hapa kujua kwa undani.

Leo bila shaka umepata majibu muhimu kuhusu website inasaidia vipi kuimarisha biashara yako? Tips, Updates na Ushauri mwingine tunaendelea kuutoa BURE kabisa kupitia Status zetu za WhatsApp kwa kugusa namba yetu hii hapa 0765834754. Hakikisha umeisave halafu tuma ujumbe wenye jina lako uanze kujua zaidi kuhusu Faida na Umuhimu wa Website katika biashara yako.

Una maoni au lolote kuhusu website inasaidia vipi kuimarisha biashara yako? Tafadhali, acha comment yako hapo chini na changia hoja yako. Karibu sana.

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

https://rednet.co.tz

Kwanini uwe na website ya biashara yako?
2 thoughts on “WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *