Unawezaje kutumia Digital Tools ili kuimarisha biashara yako mtandaoni?

Jan 13, 2022 Technology Updates
Kwanini usalama wa kimtandao (cyber security) ni muhimu kwako?

Kama huwezi kuendesha biashara yako ukiwa nyumbani au ukiwa safarini nje ya mkoa/nchi, nakushauri, hii 2022 hakikisha unatumia vema Digital Tools utakazojifunza leo katika kuimarisha biashara yako.

FAQ 1: Digital Tools ndio zipi?

ANS: Website, ecommerce store, twitter account, insta page, facebook, Linkedin, Zoom, CH, Whatsapp na Telegram.

FAQ 2: Nawezaje kuzitumia hizo Digital Tools kuimarisha biashara yangu?

ANS: i. BLOG SECTION:

Kwa website, hakikisha ina kipengele cha “Blog” ambapo utaweza kupost Updates mbalimbali kuhusu biashara yako mara kwa mara ili mteja apate solution ya changamoto zinazomkumba mara kwa mara.

ii. Tumia S.E.O:

Kuhakikisha biashara yako inapatikana google ikitokea mtu yeyote aki-search kuhusu huduma unazotoa. Mfano: ikiwa unauza chakula basi hakikisha katika blogs zako unatumia zaidi maneno kama “Wali, ugali, biriani, juisi ya miwa, chakula kitamu, sambusa za nyama nk”

Kwa sababu maneno hayo kitaalam yanaitwa “Keywords” ambayo ni rahisi kwa mtu yeyote kuyaandika akiwa anatafuta sehemu pa kupata huduma nzuri anazohitaji. So hakikisha unayatumia barabara kabisa kuendana na aina ya biashara yako.

iii. GOOGLE MAP:

Ni changamoto sana kwa wajasiriamali wengi. Unakuta eidha mtu hajui kuitumia au basi tu haoni haja ya kuitumia. Leo nataka nikusanue, hii Google Map inawainua sana watu mtandaoni. Kama unafanya biashara/una ofisi, ingia google map, sajili biashara yako chap.

Ingia google kisha andika (Aina ya biashara unayofanya au unayotaka kutafuta) kisha ikifuatiwa na maneno “near me” Mf: web designer near me, au food provider near me, au kitu chochote kama mifano inavyoonekana hapo. Halafu jiulize kwanini biashara yako haipo kwenye hizo listings?

iii. GOOGLE MY BUSINESS:

Katika jukwaa la Google unao uwezo wa kutengeneza wasifu (profile) wa biashara yako ukaweka details zote kama jina la biashara, mahali ilipo, huduma unazotoa au bidhaa unazouza, offers, mawasiliano yako n.k. Hii ndio njia rahisi zaidi ya kufanya S.E.O.

Hizo details unazoweka kwenye Akaunti yako ya Google My Business zinaisaidia sana biashara yako kuonekana kirahisi pale mtu anapotafuta vitu vinavyofanana na huduma unazotoa kupitia Injini za matafuto kama Google na Bing. Jaribu hii leo uone NGUVU ya SEO. Utanishukuru badae.

iv. SEARCH CONSOLE:

Hii ni Dashboard ya Google ambayo inakuonyesha namna website yako inaperform katika matafuto yanayofanyika huko mitandaoni. Kupitia matafuto hayo, google itai-rank website yako kwa mujibu wa inavyotafutwa na watu mbalimbali duniani kote.

Website zinazotembelewa zaidi na watu hutokea katika page ya kwanza kabisa pale mtu anapo-search kuhusu jambo analotaka mtandaoni. Ukiangalia kwa upande wetu, mpaka kufikia tar1/1/, tovuti yako ya https://rednet.co.tz imepata nafasi ya 7.6. Nia ni kufikia nafasi 3 za juu.

v. Katika matumizi ya Social Media kanuni zipo wazi. Hakikisha maudhui unayoweka kuhusu biashara yako 80% ni kuhusu VALUES ambazo biashara yako inampatia mteja, na 20% ikiwa ni kuhusu MATANGAZO ya bidhaa/huduma unazotoa.

vi. WHATSAPP:

Moja kati ya Tools zenye nguvu zaidi katika kuimarisha biashara kwa njia ya mtandao ni kupitia Whatsapp.

WHY WHATSAPP?

Je wajua kuwa watumiaji wa Whatsapp kwa wastani hufungua App hio mara 23 kwa siku, huku zikitumwa meseji milioni 29 kila dakika katika app hio?

Hii inakuhakikishia kwamba ukiitumia vizuri App ya whatsapp unajiweka kwenye nafasi nzuri ya KUSTAWISHA biashara yako kimtandao na kuongeza MAUZO, tena BILA GHARAMA yoyote ile ya kulipia matangazo.

Pia kupitia features za Whatsapp Status, Whatsapp Broadcast, Groups, Videos and Voicenote, sasa kutoa VALUES za biashara yako kwa wateja imekuwa rahisi. Unaweza kutengeneza Funnels hapo, ukabadili watu unaowasiliana nao kutoka WATU WA KAWAIDA kuwa WATEJA wako kirahisi zaidi.

Muhimu, hakikisha unapotumia hii mitandao ya kijamii basi walau uwe unaweka posts/tweet mbili kwa siku, kila siku (consistently).

Mwaka huu 2022, unao uwezo wa kumanage biashara zaidi ya 1 na zote zikaenda kwa ufanisi unaotakiwa kwa kupitia matumizi SAHIHI ya Digital Tools ulizojifunza leo. Usipoteze nafasi yako LEO sasa kufanya hivyo.

Una changamoto yoyote katika kutumia Digital Tools katika kuimarisha biashara yako? Tucheki kupitia DM yetu au Chati nasi Whatsapp kuitia namba 0765834754 ili kusudi tukushauri BURE kabisa namna ya kutatua changamoto hizo haraka iwezekanavyo.

OFA YA MWAKA MPYA 2022:

OFA YA KUPATA WEBSITE YAKO
OFA YA MWAKA MPYA 2022

Tunayo OFA YA MWAKA MPYA 2022 hapa ambapo, Ukitengeneza website kwetu unapata huduma za SEO kwa Google My Business, Search Console na Google Map BURE KABISA. Pia tutakuwa tunakushauri namna nzuri ya kuendesha website yako ili ikuletee faida kila siku.

Changamkia OFA hii kabla haijakwisha kwa sababu “Biashara asubuhi, jioni mahesabu”. OFA inakwisha tarehe 31/01/2022, hivyo wakati unapanga mipango yako ya kufanyia kazi mwaka huu, weka akilini pia namna utakayoweza kufanikiwa katika biashara zako mtandaoni kwasababu nyakati hizi zinakutaka ujifanyie tathmini binafsi kama kampuni inayofanya tathmini mwenendo wake. Weka mipango ya mwaka kisha igawe katika shughuli za miezi mitatu mitatu, fanya kazi kuifanikisha. Mwisho wa mwaka fanya tathmini uone jinsi umefanikiwa katika mwaka wako.

Cheers.

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER)5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

mpesa lipa namba yetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *