Tag: viwanda na biashara

UGUNDUZI WA KITEKNOLOJIA KUELEKEA KATIKA MUSTAKABALI WA SEKTA YA UZALISHAJI

Katika zama hizi za mapinduzi ya 4 ya Viwanda duniani, teknolojia inakuja na mapinduzi makubwa katika kuunganisha nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kidijitali katika mifumo ya uzalishaji duniani (mass production). Kasi ya maendeleo ya kiteknolojia inatajwa kuchochea mabadiliko katika namna watu wanaishi na kufanya kazi katika nyanja zote za uzalishaji, uchumi na viwanda, pengine na zaidi ili kuhakikisha bidhaa zinazalishwa katika ubora unaotakiwa, kujali muda pamoja na matakwa/mahitaji ya watumiaji. kufahamu zaidi kuhusu mapinduzi ya 4 ya viwanda duniani tayari tumekuwekea makala maalum kupitia link hii hapa https://rednet.co.tz/fahamu-kuhusu-mapinduzi-ya-4-ya-viwanda-duniani/ yenye kichwa “FAHAMU KUHUSU MAPINDUZI YA 4 YA VIWANDA DUNIANI” kisha tuendelee na mada yetu ya leo.

Katika nyanja tano (5) za kiteknolojia hatua mbalimbali za kiufundi huja na viwango mbalimbali katika kutafuta mustakabali wa uzalishaji. Kwa kuangazia;

Teknolojia ya Roboti (Advanced Robotics): Ni teknolojia kubwa duniani yenye soko la takribani dola za kimarekani 35 bilioni na Teknolojia ya 3D Printing yenye soko la ukubwa wa dola bilioni 5. Teknolojia hizi zenye historia kubwa katika maendeleo ya Viwanda zinatajwa kuwa na mahitaji makubwa ya soko haswa katika nyanja ya jiografia na viwanda.

Teknilojia zingine kama Akili Isiyo ya Asili (Artificial Intelligence) na Enterprise Wearables, Ambazo kwa pamoja zina soko la thamani ya takribani dola 700milioni zipo kwenye hatua nzuri zaidi ya kufanikiwa na kuwafikia watu wengi zaidi. Kwa sasa Amerika ya Kaskazini, Ulaya na sehemu za Asia (China, Japan na Korea Kusini) zinaongoza kwa matumizi ya Teknolojia hizi tajwa huku maeneo mengine ya dunia yakishika mkia.

Changamoto; Nchi za Afrika, haswa zile zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, zinaweza vipi kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma zake kwa kutumia Teknolojia na kufaidika na Mapinduzi ya 4 ya Viwanda Duniani?

Ili kufikia kasi inayotakiwa katika kutafuta fursa mbalimbali katika zama za mpinduzi ya 4 ya kidijitali Duniani, Kampuni na wadau wanapaswa kubadili mtindo wa kufanya Biashara zao kutoka Kushawishi Wateja Wanunue Bidhaa/Huduma (Push into the Market) kuelekea Kubuni Bidhaa maalum kwa matakwa ya Mteja mmoja mmoja katika muktadha wa Kiteknolojia. (Pull from the Customer).

Kiasili dunia imeumbwa katika mifumo ya kufanya kazi, ikijumuisha vitendea kazi (assets) na maarifa/ujuzi yenye kuleta ufanisi. Hata hivyo, Maarifa ya Kiinjinia ya Hali ya Juu, mipango na mabadiliko ya kiteknolojia huleta gharama za juu katika utekelezwaji wa miradi ya kufikia mapinduzi ya kidijitali haswa barani Africa. Je, suluhu ya changamoto hii ni nini?

Ili kufaidika na ukuaji wa kasi katika mabadiliko chanya ya kidijitali kuelekea mapinduzi ya 4, Kampuni zilizo katika nyanja Uzalishaji mali zinahitaji malengo ya muda mrefu (long-term vision), kujenga na kuimarisha jumuiya baina ya nchi/kampuni zenye nguvu zaidi ya kidijitali, kuongeza ujuzi na maarifa katika ubunifu wa bidhaa/huduma, kuongeza vitendea kazi (computer, smartphones, huduma za internet, masomo ya sayansi ya computer), kuongeza ujuzi na mbinu za kuongeza/kutanua masoko, viwanda na mahitaji ya wateja.

Kama unahitaji kuendelea kufanikiwa na kuwa na uwezo wa kushindana katika zama hizi za mapinduzi ya kidijitali, huna budi kujiweka tayari kukabiliana na kasi kubwa ya mabadiliko, kuipanga biashara yako katika mtindo wa ‘Kuvuta’ Wateja zaidi kuliko ‘Kushawishi’. Na zaidi huna budi kukuza Biashara yako kwa namna ya kufikisha Bidhaa/Huduma zako kwa wateja wengi na maeneo tofauti tofauti kila siku bila kuchoka. Hili ni somo muhimu sana katika kubuni mbinu mbadaka ya kuendesha Biashara yako kisasa zaidi.

Uwekezaji unaofanywa katika sekta ya uzalishaji mali unaakisi malengo makubwa ambayo yanalenga katika kufikisha bidhaa na huduma kwa soko la watu duniani kote. Zaidi kuhusu uwekezaji unaweza kusoma makala maalum kupitia link hii hapa https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA”

Umejifunza kitu gani kipya leo. Tafadhali tuambie.