Tag: vijana na mitandao

mbinu ya ufungani (commitment) katika biashara

JITAFUTE KWANZA ILI UFANIKIWE

Mwaka 2017 wakati tunaanzisha Rednet Technologies tulikua na vision kubwa sana, kama ile watoto wadogo wanavyoota kuwa Marubani na Wanasheria. Hata hivyo kuifanyia kazi vision hio haijawahi kuwa rahisi. Jasho, Damu na Machozi haviepukiki.

Vision ya Rednet Technologies ilikuwa ni “Kuhakikisha Tunawafikia Wafanyabiashara wote wadogo na wale wa kati wanaofanya shughuli zao katika eneo la Afrika Mashariki na Kati, na kuimarisha Biashara zao kwa matumizi ya Teknolijia za kisasa kutoka kwetu”.

Hio Vision inahitaji Maarifa, Ujuzi, Muendelezo (Consistency), Ubunifu na zaidi, Teamwork. Kama wewe ni mfanyabiashara na una ndoto za kufanikiwa katika shughuli zako basi hili la Teamwork unapaswa kulitazama kwa macho ma3. Leo tutachambua kwa undani hapa kwenye TEAMWORK.

Ile Team yetu ya kwanza tulitamani ingeweza kufanikiwa kuifikisha Rednet pale inatakiwa kufika. Lakini haikuweza kufanya hivyo. Hivyo, mwezi March, 2018 Rednet Technologies ilisitisha Operations zake kwa kipindi cha Mwaka mzima mpaka May 2019. Kilikua ni kipindi kigumu mno kwangu binafsi kwasababu mimi ndiye nilikua Visionary Leader.

Nilitamani sana Rednet Ifanikiwe, roho yangu ilikua ikiniuma sana kuona juhudi zangu hazikuwa zikizaa matunda. Kila mbinu niliyokua naitumia haikunipa majibu ya kufurahisha. Hata hivyo hio 2019 tulipata kazi chache za kuwahudumia wateja wetu, lakini bado hatukuweza kutanua vizuri mtandao wa wateja wetu na kushirikiana nao kwenye shughuli zao vile inavyotakiwa.

Hali hii ilikwenda mpaka Octoba, 2020, mwaka jana tu hapo kabla ya ule Uchaguzi Mkuu ambapo JEOFFREY alinipa idea ya kimapinduzi sana.

JEOFFREY NI NANI?

Huyu Jeoffrey ni rafiki yangu wa zamani sana. Tulisoma wote shule ya msingi japo yeye alinizidi darasa moja. Na zaidi tuliishi wote mtaa mmoja kwa kipindi kirefu sana katika maisha yetu, zaidi ya miaka 18. Kipindi chote icho sikuwahi kujua kuwa mfumo wake wa biashara utanifaa.

Huyu jamaa ana biashara yake ya kusambaza vifaa vya miundombinu ya maji kama koki, elbows, mabomba n.k. Zaidi yeye amejisajili kwenye mfumo wa manunuzi ya serikali (TaNEPS). Huko anapata tenda nyingi sana kuhusu miradi ya maji ya serikali nchi nzima. Kifupi yupo vizuri yani.

Hio siku sasa alinijia akihitaji nimtengenezee ecommerce website ili kusudi aweze kuuza bidhaa zake kwa rejareja kwa wateja wake nje ya mfumo wa manunuzi. Hivyo akanipatia nyaraka za wasifu wa kampuni (Company Profile) yake. Sasa wakati naifanya hio kazi yake nikawa najiuliza, hivi mimi nashindwaje kutanuka kama jamaa yangu hapa.

Najua hata wewe unayesoma unajiuliza hili swali “NAWEZAJE KUTANUA BIASHARA YANGU?” Well, kupitia vikao vichache nilivyokaa na huyu jamaa yangu, nikaweza kugundua namna ambayo tunaweza kusambaza Bidhaa na Huduma zetu kwa watu wengi na kwa haraka zaidi.

Hivyo, tukaanzisha Huduma ya Kusambaza Vifaa vya Ofisini na Computer kama mafile, diaries , flash disks, antivirus na vitu vya stationery unavyovijua. Wateja wetu wakubwa tuloanza nao walikua ni makampuni na taasisi ambazo kimsingi wametupa ushirikiano mkubwa sana.

Tumekuwa tukipokea Oda kutoka sehemu mbalimbali na tumeweza kukuza mtandao wa wateja wetu haraka na kwa ufanisi mkubwa kupitia huduma hii. Jambo hili likatulazimu kwenda mbele zaidi ambapo sasa kupitia tovuti yetu ya https://rednet.co.tz unaweza ku-request oda na tukakufikia.

Urafiki wetu na Jeoffrey ukazidi kuota mizizi ambapo sasa tunashirikiana kwenye mambo mengi sana ya kikazi. #VijanaWenzangu mimi huwa nawaambia “Tutumiane vizuri katika shughuli zetu za kiuchumi. Delegate your tasks kwa kuwa baraka zipo kwenye KUTOA zaidi kuliko kwenye KUPOKEA”.

Mimi rafiki zangu nawapa michongo mingi sana, ya muda mrefu na ile ya muda mfupi. Kadhalika rafiki zangu wananipa michongo mingi sana, ya muda mrefu na ile ya muda mfupi. Wataalam wanakwambia “Your Network is Your Net worth”. Kuna maana kubwa sana kwenye huo msemo ukitafakari.

Kama connections ulizonazo hazikutumii vizuri sasa usilalamike, watumie wewe kwenye mishe zako. Yes, maana hai-make sense kuwajua watu wazuri wanaoweza kuipush biashara yako halafu huwatumii eti kwa kuwa wao hawakutumii kwenye mishe zao. How? Make sure you get upper hand on it.

KARIBU KATIKA HUDUMA MPYA:

Website yetu sasa tumeiweka ili kusudi kukupa wewe uwezo wa kuchagua huduma unayotaka kisha sisi tutapata request yako, tutakutumia Quotation ukiridhia tunakupatia huduma yako katika muda ambao utapanga wewe. Upewe nini zaidi?

Kwa vifaa vya Ofisini (stationeries) kama wino wa printa, flash disks, rim paper, peni (box) n.k gusa link hii https://rednet.co.tz/services/your-order/… Link hio itakupeleka direct kwenye ukurasa utakaokupa nafasi ya kutuambia huduma unayohitaji ukiwa popote Duniani.

Pia tumekuletea huduma mahsusi kwa ajili yako iitwayo “JIHUDUMIE” kupitia link hii https://rednet.co.tz/services/jihudumie-leo/… ambapo humo ndani utajipatia huduma kama zinavyoonekana kwenye picha hapa.

CHANGAMOTO:

1. KUWA RASMI: Najua watu wengi humu mitandaoni biashara zenu si rasmi, kwa maana ya kwamba hazijasajiliwa katika Mamlaka za Kiserikali (BRELA, TRA, HALMASHAURI, BENKI etc). Sasa mtindo huu wa Usambazaji unakutaka kusajili biashara yako kwa kuwa biashara/kampuni yako sasa inakwenda kufanya kazi na biashara/kampuni zingine (B2B). Matumizi ya Quotations, Proforma Invoice, Tax Invoices, EFD receipts na Delivery Notes kwenye mtindo huu wa Biashara ni kama Katiba katika utawala wa Nchi. Eneo hili kama Mjasiriamali unapaswa kuwalo makini sana yani.

Hivyo ifanye biashara/kampuni yako kuwa rasmi kwanza ili kujihakikishia unafanya shughuli zako bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Mfano humu ndani kuna nyakati mtu fulani (Jei Zii) alimchongea jamaa wetu wa tabata kuhusu sabuni zake ikapelekea hadi operations kusimama kwa muda.

2. UCHELEWESHWAJI WA MALIPO: Kuwa msambazaji/Supplier maana yake ni kwamba unafanya kazi kwa pesa yako na pesa hio utaingiziwa baada ya mwezi mmoja mpaka miezi sita. Hivyo, kukaa muda mrefu bila kuingiziwa pesa si kazi ndogo, uvumilivu lazima uchukue nafasi yake hapa.

3. MTAJI: Kama ulivyoona hizo changamoto zingine hapo juu, kufanya usambazaji lazima uwe na Mtaji wa kutosha kuweza kuhudumia Wateja wako kikamilifu kabla wao hawajakuingizia pesa siku za mbeleni. Hapa lazima uwe na pesa ya kufanya kazi mkononi ili usije ukatolewa katika game.

Hata hivyo, changamoto hizi hazitakiwi kukurudisha nyuma, katika harakati za kujitafuta lazima uhakikishe unapambana kwa njia zozote ili kusudi mafanikio yako yakapate kujidhihirisha. #VijanaWenzangu muda wa kupambania future zenu ndio sasa. Pambaneni haswa.

ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara

IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA

Zama hizi kuhoji umuhimu wa mitandao ya kijamii ni sawa na kuhoji umuhimu wa mwanga wa Jua duniani. Google, Facebook, Twitter, Instagram na Whatsapp ndio injini za biashara mitandaoni. Kivipi? Sasa kwenye makala ya leo nataka ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara hio unayoifanya. Twende pamoja mpaka mwisho.

Imefika muda sasa, mitandao ya kijamii si sehemu ya anasa tena bali ni nyenzo muhimu katika uendeshaji wa biashara. Sasa imekuwa rahisi kuwasiliana na wapendwa wetu wakiwa popote duniani, tena kwa gharama ndogo sawa na bure. Pia imekuwa rahisi sana kuwasiliana na wateja wapya.

Mpaka kufikia January 2018 duniani kulikua na watumiaji wa huduma za internet takriban 4.02 bilioni, sawa na 53% ya idadi nzima ya watu. Kati ya hao, watumiaji wa mitandao ya kijamii wanafikia 3.2 bilioni sawa na 42% ya watu wote duniani. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes. Hapa Tanzania mpaka kufikia mwezi Mei 2021 kumeripotiwa kuwa na watumiaji wa huduma za intaneti zaidi ya milioni 29. Huku watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kielekroniki wakifika milioni 32, chanzo TCRA.

#VijanaWenzangu kama wewe ni mfanyabiashara basi bila shaka namba hizi huwezi kuzipuuza. Utafiti huo kwako unapaswa kuwa ni hazina katika biashara zako ambayo utaitumia kwenye kusaka wateja wapya, kuwasiliana nao, kuwaongeza na kuhakikisha wanabaki kuwa wateja wako.

Matangazo ya televisheni na redio yanakwenda kufa kifo cha taratibu. Mitandao ya kijamii inateka jukwaa la Ushindani wa biashara hasa katika idara ya Masoko na Mauzo. Kama hutumii mitandao ya kijamii kwa kukuza na kuimarisha biashara yako basi jua uko nyuma sana kiushindani.

Kujua kwanini unapaswa kuitangaza biashara yako, fuatana na Makala hii hapa KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?. Sasa ukishajua sababu hizo, Leo tunakwenda kujua Kwanini Utumie Mitandao ya Kijamii kama nyenzo muhimu katika biashara yako. Makinika.

MANUFAA YA MITANDAO KATIKA BIASHARA:

Kama umekuwa ukijiuliza “Hivi hii akaunti yangu ya twitter/instagram/facebook naweza vipi kuitangazia biashara zangu? Hivi nitaweza kweli?” Basi leo tuzione faida muhimu za mitandao ya jamii katika kuimarisha biashara.

i. KATIKA KUKUZA BRAND: Kwa mujibu wa mtandao wa “We Are Social’s Digital” mwaka 2018 ilionekana kwamba Facebook ndio mtandao wa pili ambao unafuatiliwa zaidi duniani, ukifuatiwa na mtandao wa Youtube. Kwenye hio orodha mtandao wa Google ndio ulikua unaongoza kwa kufuatiliwa.

Hii ina maanisha kuwa, watu wanatumia muda mwingi mtandaoni. Mitandao hio pia hutumika kama vyanzo vya taarifa kuhusu bidhaa/huduma za biashara/kampuni/shirika fulani. Facebook peke yake ina zaidi ya kurasa (Pages) milioni 60 ambazo hutumika kama Brands za biashara mbalimbali kila siku. Hapa sasa ndipo unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara.

nguvu ya mitandao ya kijamii

Katika mtandao wa twitter pia mambo ni moto. Kwa mujibu wa @Twitter Sababu kuu ya watu kutumia mtandao wa twita ni “kugundua jambo jipya na/au la kusisimua”. Haya hebu tuambie hapa, wewe ni nini kilikufanya kuanza kutumia mtandao wa twita? Ile sababu ya watu kupata kitu kipya imefungwa kwenye design ya twita ambayo inawafanya watu wapate taarifa na mambo mapya na yenye kusisimua ambayo haswa Biashara na makampuni yanavitafuta. Hivyo katika biashara mtandao wa twita unafaida zaidi kulinganisha na mitandao mingine kama Instagram na Quora kutokana na namna yake ilivyobuniwa.

ii. KATIKA KUJENGA UAMINIFU (LOYALTY): Mwaka 2017 utafiti uliofanywa kwa watu wa masoko 5,700 ulionyesha kuwa 69% sawa na watu 3,933 walijenga uaminifu kwa wateja wao kupitia matumizi kibiashara ya mitandao ya kijamii (social media marketing).

Vilevile 66% ya watumiaji wa mitandao wa umri kati ya miaka 18-24 ni waaminifu kwa akaunti wanazozifuatulia kwenye mitandao ya kijamii. 60% ya walio na miaka 25-34 hupendelea kutumia bidhaa/huduma za biashara wanazozifuatilia kupitia Facebook, Twitter na Instagram.

iii. KATIKA MAUZO: Mtandao wa “We Are Social’s Digital” umeripoti kuwa 17% ya idadi nzima ya watu duniani hununua bidhaa na kulipa bills kwa njia ya mtandao. Kwa kuwa % kubwa ya watumiaji ni wa umri kati ya miaka 18-34, hawa hufanya manunuzi kwa ushawishi wa mitandao ya kijamii. Hapa ni muhimu sana ukiwa na website yako. Kwanini, Kwasababu website yako inaelezea kiundani sana kuhusu biashara yako pamoja na bidhaa/huduma zake. Unawezaje sasa kupata website yako? Gusa hapa kujua utaratibu.

FAIDA ZA MITANDAO

Sasa twende kuziona faida ambazo mitandao ya kijamii inaweza kuiletea biashara yako na kuweza kukusaidia kukuunganisha na wateja, kushirikisha, kukuza na kuimarisha biashara yako zaidi.

1. KUKUZA UTAMBULISHO WA BIASHARA: Ikizingatiwa nusu ya idadi ya watu duniani ni watumiaji wa mitandao, kumbe basi matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ni mbinu bora ya kuhakikisha biashara yako inajulikana zaidi duniani. Mfano tizama ilivyo ngumu kutangaza biashara mtaani katika kulipia gharama za matangazo ya televisheni na redio.

2. KUHUISHA BIASHARA: Siku hizi imekuwa ngumu sana kuamini bidhaa/huduma mpaka upate uthibitisho hai. Yaani uhakikishe hio biashara/kampuni ipo kweli na si matapeli. Hivyo, kupata wateja unatakiwa uonyeshe sehemu inayoishi (human side) ya biashara yako ambayo ni thamani ambayo biashara yako inaitoa kwa jamii. Mfano; hapa unaweza kueleza faida, umuhimu na namna za kutumia bidhaa/huduma yako. Elimu hii inapaswa iwe inatolewa mara kwa mara kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii. Mbinu hii hufanya biashara yako iweze kuishi katika maisha ya watu kila siku.

3. KUONGEZA TRAFFIC: Machapisho ya mitandaoni huchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza traffic kwenye tovuti yako. Unaposhirikisha maudhui yaliyo kwenye tovuti kupitia machapisho unayoweka kwenye akaunti za mitandao unaiongezea thamani biashara kwenye shughuli za watu za kila siku kwa wao kuzidi kutembelea tovuti yako.

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni

4. KUONGEZA WATEJA: Bila shaka dhumuni lako kubwa la kufanya biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuongeza wateja. Sasa mitandao hii inakupa njia nafuu zaidi ya kupata wateja wa bidhaa/huduma yako.

5. KUWASILIANA KWA UKARIBU: Ule msemo wa “Dunia ni kama kijiji” umefanya iwe rahisi zaidi kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii. Yaani kupitia mitandao, sasa unao uwezo wa kuwasiliana kwa ukaribu na wateja wako kuhusu ubora wa bidhaa/huduma, kiwango, malipo n.k bila kujali umbali.

Hii imefanya iwe rahisi kutoa Huduma Bora kwa Wateja na kuimarisha uhusiano na ushirikishwaji wa wateja katika kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango pamoja na kuhudumu kwa weledi wa hali ya juu zaidi. Unaposhindwa kufanya hivi unajiweka kwenye nafasi mbaya ya kukosa wateja na kushindwa kimbinu na washindani wako katika biashara.

POINT YA ZIADA: Vilevile ni muhimu kujua watu wanasemaje kuhusu washindani wako kwenye biashara. Utajuaje? Ukifuatilia machapisho ya watu mbalimbali kuhusu washindani wako utagundua udhaifu na matamanio ya watu ambayo wewe unaweza kuyatumia ili kuvuta wateja wengi kwako.

Kwa dunia ya leo ya mtandaoni, mambo yanaenda kwa kasi sana. Na huwezi kukubali kuachwa nyuma kizembe. Mitandao imerahisisha kujua kipi watu wanahitaji kwa sasa na kipi watakihitaji kesho. Hivyo kuwa makini kwenye kufuatilia mahitaji ya wateja wako na soko zima kwa ujumla kwa sababu unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara unapata faida ya kushindana na washindani wengine na kuwashinda kirahisi.

Kiufupi kufanya biashara kupitia Mitandao ya Kijamii kunahitaji Mbinu na Ubunifu. Fanya vyote ulivyovipata leo kwenye makala hii katika mtindo wa MBINU na UBUNIFU. Uko na swali? Tafadhali tunakukaribisha kupitia comments hapa chini. Hakikisha una kushare ili makala hii iwafikie wengi zaidi.

Vyanzo: https://www.forbes.com/sites/forbescommunicationscouncil/2018/05/11/how-social-media-can-move-your-business-forward/?sh=60e12c604cf2

https://coschedule.com/blog/benefits-of-social-media-marketing-for-business

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu(website design, logo design, Digital consultacy n.k) BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

FAHAMU KUHUSU MAGEUZI YA ICT KATIKA UWANDA WA SIASA

Ama kwa hakika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA/ICT) imeendelea kushika kasi katika nyanja mbalimbali za kijamii. Biashara zinazidi kuimarika, Jamii inaunganika, uchumi unainuka na Siasa inapata sura mpya. Muunganiko wa Siasa na Teknolojia unagusa michakato, wasifu za watu, jitihada za kujinasua katika changamoto mbalimbali pamoja na harakati zingine za kijamii zinazohusidha matumizi ya huduma za intaneti na ICT. Katika fumbo hilo wataalamu wa siasa wakagundua njia za kuboresha mifumo ya kisiasa na kuratibu ushawishi wao katika jamii kirahisi zaidi.

Sasa leo tuone maeneo 5 muhimu ambayo ICT imekuwa chachu ya maendeleo katika uwanda wa kisiasa barani Afrika, hususan Kusini mwa jangwa la Sahara:

1. KUBADILI TAWALA

Katika kipindi cha mwaka 2009-2012 katika nchi za kiarabu kulitokea kitu kilichoitwa “Vuguvugu la Kimapinduzi” au “Arab Spring” ambapo serikali nyingi za kiarabu zilijikuta zikipinduliwa kwa nguvu ya wanachi. Kufikia mwaka 2012 dunia ilikua na 61% ya nchi 195 ambazo ndizo zilikua zilitambulika kwa kufanya Chaguzi za Kidemokrasia. Hio ni sawa n nchi 118. Lakini bada ya hapo nchi zinazojiendesha kidemokrasia ziliongezeka kufuatia maandamano nchini Moldovia mwaka 2009, Tunisia (2010/11, Misri (2011) na Iran (2009 mpaka sasa) Mapinduzi hayo ya kubadili tawala hasa zile za Kiimla yalipangwa na kuanzishwa kwa msaada wa kiteknolojia huku mtandao wa Twitter ukihusika kukusanya na kuhamasisha watu kuanzisha vuguvugu la maandamano katika nchi za kiarabu. Hawa waarabu walijua kwelikweli kutumia mitandao.

2. KUTUNGA NA KUENDESHA SERA

Hivi sasa hakuna mtu asiyejua au kutumia mfumo wa malipo ya kiserikali wa eGovernment. Sasa unajua mfumo huo ulianzia wapi? Achana na siasa kabisa. Kwanza tuone hio eGovernment ni kitu gani? Huo ni mfumo wa matumizi ya ICT katika ofisi za umma inazohusisha mifumo ya kiutawala ya kiuweledi inayotumia maarifa na ujuzi wa computer na huduma za intaneti ili kuhakikisha huduma za kijamii zinaimarika na kuchochea demokrasia na nguvu ya ushawishi katika chaguzi za kisiasa na sera za jamii. Umeona siasa imerudi tena apo Wahenga wanakuambia, “Siasa ni kama maji tu, usipoyaoga utayanywa.” Wahenga bwana. Sasa mifumo hii ya eGovernance hutumiwa na taasisi za serikali katika kuhudumia Mashirika mengine ya kiserikali (G2G) mfano Polisi na TRA, Mashirika ya Kiserikali kwa wanachi(G2C) mfano LUKU na Mashirika ya Serikali kwa Biashara (G2B) mfano TRA na Wafanyabiashara. Hii sera ys kuanzishwa kwa mifumo ya eGovernance japo imeanzishwa kwa sera za kisiasa lakini imeleta mapinduzi makubwa sana katika zoezi la ukusanyaji wa mapato na utunzaji wa rekodi za mauzo na manunuzi.

3. SIASA KAMA SIASA

Japokuwa kwenye nchi nyingi haswa zile za kidikteta kumekuwepo na makatazo ya kufanya siasa za wazi, Matumizi ya Teknolojia na mitandao ya kijamii yamewezeshwa kufanyika kwa siasa pasi na haja ya kukusanya watu viwanjani. Matumizi ya mifumo ya computer na mitandao ya kijamii wamewsrahisishia Wanasiasa kutengeneza akaunti zao zinazowapa fursa ya kukutana na wananchi na kufanya siasa kirahisi sana. Hata hivyo hii bado ni changamoto kwa nchi nyingi zinazoendelea kama Tanzania ambapo watumiaji hai wa huduma za internet walikua ni 23.14milioni sawa na 38.7% ya wananchi wote. Pia watumiaji wa mtandao wa facebook wamefikia 4.27milioni. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tovuti ya http://internetlivestats.com kufikia mwezi December, 2019. Sasa namba hizi zinakupa picha gani katika uwanda wa siasa nchini? Inaonekana kuwa bado watumiaji hai wa mitandao ya kijamii ni wachache kuwakusanya mtandaoni kwa wakati mmoja, hivyo kufanyika kwa siasa katika mitandao ya kijamii inaonekana bado ni mtihani kwa wanasiasa barani Afrika hasa nchini Tanzania. Licha ya changamoto hizo, bado teknolojia inao mchango wake katika siasa wakati wa kufanya kampeni na uchaguzi ukizingatia Haba na Haba hujaza kibaba. Hivyo katika kampeni za kisasa, ili mwanasiasa apate kuingia katika mfumo wa utoaji wa maamuzi wa Taifa (Legislative level). Hana budi pia awe na ushawishi wa kisiasa katika mitandao ya kijamii. Huko ndipo unakutana na wanachi kirahisi na kusambaziana taarifa mbalimbali kwa wepesi zaidi. Kama afanyavyo Mh. Hamis Kigwangwala tu katika mtandao wa twitter, interractions za mara kwa mara muhimu nyie.

4. ONLINE VOTING (e-Voters System)

Kama ulikua hujui basi mwaka 2005 nchi ya Estonia iliweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza duniani kutumia mfumo wa kimtandao wa upigaji kura (e-Voters System)na kwanzia hapo mfumo huo umekuwa ukisambaa katika nchi na maeneo mbalimbali duniani. Mfumo huu unahusisha sehemu 3 ambazo ni Mpiga Kura, Mamlaka za Usajili na Watu wa Kuhesabu Kura ambao wote hapa sasa hufanya kazi katika mifumo maalum ya kuhakikisha kura zinapigwa kimtandao na kwa usahihi na usalama wa hali ya juu. Hapa bwana usipokua makini wadukuzi wanaweza kupiga tukio uchaguzi ukaharibika ndani ya dakika kadhaa tu.

KWANINI ONLINE VOTING SYSTEM?

Wakati mfumo huu unatengenezwa na kuzinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Estonia, lengo kuu lilikua ni kuhakikisha shughuli za uchaguzi zinafanyika kwa haraka, wepesi na kwa usahihi zaidi bila kuathiri shughuli zingine za kiuchumi. Lakini leo hii ambapo dunia inapitia katika changamoto ya Ugonjwa wa #COVID19, ipo haja na hitaji kubwa la matumizi ya e-Voters Systems katika chaguzi za kisiasa sehemu mbalimbali duniani. Wakati mamlaka zikikataza mikusanyiko ya watu, uvaaji wa barakoa, kutogusana na kuzingatia social distance (sijui kiswahili chake kwa kweli), hakuna wakati sahihi wa kuanza kutumia e-Voters Systems kama sasa. Wanaharati na wananchi kwa ujumla hatuna budi kupigia chapuo mgumo huu uanze kutumika mara moja ikiwezekana kuanzia uchaguzi wa Octoba 2020 sio tu kuhakikisha tahadhari dhidi ya Coron zinachukuliwa, lakini zaidi kuongeza Usahihi na Usalama wa kura katika zoezi la Uchaguzi.

5. MATUMIZI NA UCHAMBUZI WA DATA

Teknolojia kwa mapana yake imekua nyenzo muhimu sana katika kukusanya, kuchakata na kuhifanyi data mbalimbali ambazo hutumika maeneo kadha wa kadha katika kufanyia Tafiti, Kupima mwenendo wa mwanasiasa au chama pamoja na kuhifadhi kumbukumbu. Sasa matumizi ya mitandao kama Facebook, Instagram, Twitter pamoja na tovuti/blogu za wanasiasa/vyama, zimekuwa zikichochea sana juhudi na harakati zao katika kuhakikisha wanaboresha nafasi na ushawaishi wao wa kisiasa katika jamii wanazohudumu. Teknolojia imezidi kuwa muhimu sana katika uga huu wa kisiasa.

BONUS POINT:

Matumizi madogo ya teknolojia (hafifu) yameleta madhara makubwa sana katiks mifumo ya siasa hasa barani Afrika. Hizi vita za wenyewe kwa wenyewe, vurugu na wakati mwingine mauaji katika mchakato wa uchaguzi ni matokeo ya siasa mbovu na ufinyu wa teknolojia usiotakiwa.

Pia kuna hizi makala hapa tayari tumekuandalia ambazo zitakupa mwanga zaidi katika kufanya maamuzi na kutumia teknolojia ili kuleta tija zaidi. Gusa link kisha makinika:

  1. https://rednet.co.tz/fanya-maamuzi-sahihi-katika-muda-sahihi/ yenye kichwa “FANYA MAAMUZI SAHIHI KATIKA MUDA SAHIHI”
  2. https://rednet.co.tz/ifahamu-nguvu-ya-mitandao-ya-kijamii/ yenye kichwa “IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO”
  3. https://rednet.co.tz/biashara-yako-inaweza-vipi-kuwa-taasisi-imara/ yenye kichwa “BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA”