Tag: uwekezaji

OFA YA MSIMU WA SABASABA

Mwaka 2016 wakati nawaza kufungua kampuni from scratch nilifikiri kupata wateja itakuwa rahisi tu. Nikawaza nikimaliza mchakato wa BRELA, TRA na Leseni basi nikituma proposals zangu kwa watu walau 10 ntakuwa nimeshapata wateja wangu nianze kuingiza pesa.

Sasa nilipoanza kutafuta wateja nikawa nashangaa, kila ninapoenda nasikilizwa tu lakini sitafutwi tufanye kazi. Mteja wangu wa kwanza nilikuja kumpata August, 2018 (mwaka mmoja baada ya kufungua kampuni rasmi mwaka 2017). Sikujua maisha yangekuwa magumu kiasi kile.

ILIKUAJE NIKAPATA MTEJA?

Kutokana na kushamiri kwa vitendo vya Utapeli wa mtandaoni, watu wamekuwa waoga sana katika kufanya biashara mtandaoni. Watu wanatapeliwa jamani, kuweni makini mno na miamala mnayofanya kwenye simu zenu pamoja na humu mtandaoni ndugu zangu.

Ilinichukua muda mrefu, almost miaka miwili mpaka nilipogundua MBINU ya kuchapisha makala zenye maudhui muhimu kwa biashara za wajasiriamali kupitia kurasa zangu za LinkedIn, Instagram na Twitter huku nikiziunga na link ya tovuti ya kampuni ambayo ndipo nilipoweka makala kamili.

Baada ya watu kutembelea kurasa zangu za mtandaoni na tovuti yangu na kuona “Thamani ya maudhui” niliyokua nayatoa ndipo nilipopata mteja wa kwanza wa uhakika ambaye mpaka leo bado tunaendelea kufanya kazi pamoja na wateja wengine wengi kutokea hapo.

NILICHOGUNDUA:

Mpaka mtu afanye kazi/biashara na wewe lazima:

1. Awe anakufahamu au tayari anazo taarifa zako za kutosha.

2. Anakuamini (kwamba utafanya kazi yake kwa viwango anavyotaka na pesa yake haiendi bure).

3. Anakupenda (ni ngumu kufanya biashara na mtu ambaye hampendani).

Jiulize hapo, Unaweza vipi kumshawishi mtu ambaye hakufahamu kabisa (a total stranger) akuamini na akupe kazi zake uwe unamfanyia kwa kiwango anachokitaka? Pitia makala hii hapa kwenye link https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kuweza-kushawishi-wateja-katika-biashara-yako/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUWEZA KUSHAWISHI WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO”

Nafahamu kuna muda unapitia wakati mgumu sana katika kutafuta wateja wapya katika biashara yako ili kujitanua zaidi, lakini hujui ufanyeje. Hata hivyo, MBINU BORA ya kutanua biashara yako kwa watu usiofahamiana nao kabisa, hasa watu wa mtandaoni (Digital Neighbors) ni hii hapa:

1. Badili matumizi ya Mitandao ya kijamii kwa kupost maudhui kuhusu Thamani ya bidhaa/huduma yako katika maisha ya mtu ili kumvutia awe mteja wako. Weka tips kama Aina za bidhaa/huduma, Bidhaa feki zinajulikana vipi, bidhaa zako zina utofauti gani na zingine, ubora uko vipi nakadhalika.

2. Fungua website ili kujiweka katika mazingira ya kujulikana kwa Utalaam wako mahsusi. Website ndio CV ya biashara yako mtandaoni. NOTE: Mteja atafanya kazi na wewe kiuhakika kwa kuwa wewe ni Mtaalam katika fani fulani na sio salesperson kama wengine pale akiona website yako.

3. Hakikisha mtu aki-search huduma/bidhaa unazouza kupitia google basi anakupata mara moja. Hii kitaalam inaitwa S.E.O (Search Engine Optimization). Hii inakupa fursa bora ya kutanua biashara yako hasa katika matafuto ya mtandaoni ambayo yatawasaidia wateja kukufikia kirahisi.

Sasa, kwa kufahamu hilo, Natoa OFA YA MSIMU WA SABASABA ambapo utakapofungua website yako kwenye msimu huu tutakufanyia SEO, tutakupa tips za kutoa maudhui ya kuvutia wateja kwenye mitandao yako ya kijamii pamoja na kukufanyia Web maintenance BURE kwa mwaka mzima.

Bei ya OFA hii ni laki tano tu (500,000/-) unapata vyote nilivyokutajia. OFA hii itakapokwisha gharama zitarejea kufikia laki tisa elfu hamsini tu (950,000/-) kwa website peke yake. Hivyo wahi kabla OFA haijakwisha. Karibu Tufanye kazi.

Kwa maswali au maulizo yoyote tafadhali tumia mawasiliano yetu yanayopatikana katika tovuti hii.

ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara

IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA

Zama hizi kuhoji umuhimu wa mitandao ya kijamii ni sawa na kuhoji umuhimu wa mwanga wa Jua duniani. Google, Facebook, Twitter, Instagram na Whatsapp ndio injini za biashara mitandaoni. Kivipi? Sasa kwenye makala ya leo nataka ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara hio unayoifanya. Twende pamoja mpaka mwisho.

Imefika muda sasa, mitandao ya kijamii si sehemu ya anasa tena bali ni nyenzo muhimu katika uendeshaji wa biashara. Sasa imekuwa rahisi kuwasiliana na wapendwa wetu wakiwa popote duniani, tena kwa gharama ndogo sawa na bure. Pia imekuwa rahisi sana kuwasiliana na wateja wapya.

Mpaka kufikia January 2018 duniani kulikua na watumiaji wa huduma za internet takriban 4.02 bilioni, sawa na 53% ya idadi nzima ya watu. Kati ya hao, watumiaji wa mitandao ya kijamii wanafikia 3.2 bilioni sawa na 42% ya watu wote duniani. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes. Hapa Tanzania mpaka kufikia mwezi Mei 2021 kumeripotiwa kuwa na watumiaji wa huduma za intaneti zaidi ya milioni 29. Huku watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kielekroniki wakifika milioni 32, chanzo TCRA.

#VijanaWenzangu kama wewe ni mfanyabiashara basi bila shaka namba hizi huwezi kuzipuuza. Utafiti huo kwako unapaswa kuwa ni hazina katika biashara zako ambayo utaitumia kwenye kusaka wateja wapya, kuwasiliana nao, kuwaongeza na kuhakikisha wanabaki kuwa wateja wako.

Matangazo ya televisheni na redio yanakwenda kufa kifo cha taratibu. Mitandao ya kijamii inateka jukwaa la Ushindani wa biashara hasa katika idara ya Masoko na Mauzo. Kama hutumii mitandao ya kijamii kwa kukuza na kuimarisha biashara yako basi jua uko nyuma sana kiushindani.

Kujua kwanini unapaswa kuitangaza biashara yako, fuatana na Makala hii hapa KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?. Sasa ukishajua sababu hizo, Leo tunakwenda kujua Kwanini Utumie Mitandao ya Kijamii kama nyenzo muhimu katika biashara yako. Makinika.

MANUFAA YA MITANDAO KATIKA BIASHARA:

Kama umekuwa ukijiuliza “Hivi hii akaunti yangu ya twitter/instagram/facebook naweza vipi kuitangazia biashara zangu? Hivi nitaweza kweli?” Basi leo tuzione faida muhimu za mitandao ya jamii katika kuimarisha biashara.

i. KATIKA KUKUZA BRAND: Kwa mujibu wa mtandao wa “We Are Social’s Digital” mwaka 2018 ilionekana kwamba Facebook ndio mtandao wa pili ambao unafuatiliwa zaidi duniani, ukifuatiwa na mtandao wa Youtube. Kwenye hio orodha mtandao wa Google ndio ulikua unaongoza kwa kufuatiliwa.

Hii ina maanisha kuwa, watu wanatumia muda mwingi mtandaoni. Mitandao hio pia hutumika kama vyanzo vya taarifa kuhusu bidhaa/huduma za biashara/kampuni/shirika fulani. Facebook peke yake ina zaidi ya kurasa (Pages) milioni 60 ambazo hutumika kama Brands za biashara mbalimbali kila siku. Hapa sasa ndipo unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara.

nguvu ya mitandao ya kijamii

Katika mtandao wa twitter pia mambo ni moto. Kwa mujibu wa @Twitter Sababu kuu ya watu kutumia mtandao wa twita ni “kugundua jambo jipya na/au la kusisimua”. Haya hebu tuambie hapa, wewe ni nini kilikufanya kuanza kutumia mtandao wa twita? Ile sababu ya watu kupata kitu kipya imefungwa kwenye design ya twita ambayo inawafanya watu wapate taarifa na mambo mapya na yenye kusisimua ambayo haswa Biashara na makampuni yanavitafuta. Hivyo katika biashara mtandao wa twita unafaida zaidi kulinganisha na mitandao mingine kama Instagram na Quora kutokana na namna yake ilivyobuniwa.

ii. KATIKA KUJENGA UAMINIFU (LOYALTY): Mwaka 2017 utafiti uliofanywa kwa watu wa masoko 5,700 ulionyesha kuwa 69% sawa na watu 3,933 walijenga uaminifu kwa wateja wao kupitia matumizi kibiashara ya mitandao ya kijamii (social media marketing).

Vilevile 66% ya watumiaji wa mitandao wa umri kati ya miaka 18-24 ni waaminifu kwa akaunti wanazozifuatulia kwenye mitandao ya kijamii. 60% ya walio na miaka 25-34 hupendelea kutumia bidhaa/huduma za biashara wanazozifuatilia kupitia Facebook, Twitter na Instagram.

iii. KATIKA MAUZO: Mtandao wa “We Are Social’s Digital” umeripoti kuwa 17% ya idadi nzima ya watu duniani hununua bidhaa na kulipa bills kwa njia ya mtandao. Kwa kuwa % kubwa ya watumiaji ni wa umri kati ya miaka 18-34, hawa hufanya manunuzi kwa ushawishi wa mitandao ya kijamii. Hapa ni muhimu sana ukiwa na website yako. Kwanini, Kwasababu website yako inaelezea kiundani sana kuhusu biashara yako pamoja na bidhaa/huduma zake. Unawezaje sasa kupata website yako? Gusa hapa kujua utaratibu.

FAIDA ZA MITANDAO

Sasa twende kuziona faida ambazo mitandao ya kijamii inaweza kuiletea biashara yako na kuweza kukusaidia kukuunganisha na wateja, kushirikisha, kukuza na kuimarisha biashara yako zaidi.

1. KUKUZA UTAMBULISHO WA BIASHARA: Ikizingatiwa nusu ya idadi ya watu duniani ni watumiaji wa mitandao, kumbe basi matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ni mbinu bora ya kuhakikisha biashara yako inajulikana zaidi duniani. Mfano tizama ilivyo ngumu kutangaza biashara mtaani katika kulipia gharama za matangazo ya televisheni na redio.

2. KUHUISHA BIASHARA: Siku hizi imekuwa ngumu sana kuamini bidhaa/huduma mpaka upate uthibitisho hai. Yaani uhakikishe hio biashara/kampuni ipo kweli na si matapeli. Hivyo, kupata wateja unatakiwa uonyeshe sehemu inayoishi (human side) ya biashara yako ambayo ni thamani ambayo biashara yako inaitoa kwa jamii. Mfano; hapa unaweza kueleza faida, umuhimu na namna za kutumia bidhaa/huduma yako. Elimu hii inapaswa iwe inatolewa mara kwa mara kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii. Mbinu hii hufanya biashara yako iweze kuishi katika maisha ya watu kila siku.

3. KUONGEZA TRAFFIC: Machapisho ya mitandaoni huchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza traffic kwenye tovuti yako. Unaposhirikisha maudhui yaliyo kwenye tovuti kupitia machapisho unayoweka kwenye akaunti za mitandao unaiongezea thamani biashara kwenye shughuli za watu za kila siku kwa wao kuzidi kutembelea tovuti yako.

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni

4. KUONGEZA WATEJA: Bila shaka dhumuni lako kubwa la kufanya biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuongeza wateja. Sasa mitandao hii inakupa njia nafuu zaidi ya kupata wateja wa bidhaa/huduma yako.

5. KUWASILIANA KWA UKARIBU: Ule msemo wa “Dunia ni kama kijiji” umefanya iwe rahisi zaidi kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii. Yaani kupitia mitandao, sasa unao uwezo wa kuwasiliana kwa ukaribu na wateja wako kuhusu ubora wa bidhaa/huduma, kiwango, malipo n.k bila kujali umbali.

Hii imefanya iwe rahisi kutoa Huduma Bora kwa Wateja na kuimarisha uhusiano na ushirikishwaji wa wateja katika kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango pamoja na kuhudumu kwa weledi wa hali ya juu zaidi. Unaposhindwa kufanya hivi unajiweka kwenye nafasi mbaya ya kukosa wateja na kushindwa kimbinu na washindani wako katika biashara.

POINT YA ZIADA: Vilevile ni muhimu kujua watu wanasemaje kuhusu washindani wako kwenye biashara. Utajuaje? Ukifuatilia machapisho ya watu mbalimbali kuhusu washindani wako utagundua udhaifu na matamanio ya watu ambayo wewe unaweza kuyatumia ili kuvuta wateja wengi kwako.

Kwa dunia ya leo ya mtandaoni, mambo yanaenda kwa kasi sana. Na huwezi kukubali kuachwa nyuma kizembe. Mitandao imerahisisha kujua kipi watu wanahitaji kwa sasa na kipi watakihitaji kesho. Hivyo kuwa makini kwenye kufuatilia mahitaji ya wateja wako na soko zima kwa ujumla kwa sababu unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara unapata faida ya kushindana na washindani wengine na kuwashinda kirahisi.

Kiufupi kufanya biashara kupitia Mitandao ya Kijamii kunahitaji Mbinu na Ubunifu. Fanya vyote ulivyovipata leo kwenye makala hii katika mtindo wa MBINU na UBUNIFU. Uko na swali? Tafadhali tunakukaribisha kupitia comments hapa chini. Hakikisha una kushare ili makala hii iwafikie wengi zaidi.

Vyanzo: https://www.forbes.com/sites/forbescommunicationscouncil/2018/05/11/how-social-media-can-move-your-business-forward/?sh=60e12c604cf2

https://coschedule.com/blog/benefits-of-social-media-marketing-for-business

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu(website design, logo design, Digital consultacy n.k) BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

cloud data storage

MAGEUZI YA INTANETI (IoT) KATIKA BIASHARA NA MAISHA

Teknolojia ya Internet of Things (IoT) inakuja kwa kasi sana. Mtandao wa Gartner uliripoti kuongezeka kwa vifaa vinavyounganishwa na huduma za internet kufikia 26 bilioni mpaka mwaka 2020. Sasa haya mageuzi ya intaneti (IoT) katika biashara na maisha ya mchango gani? Fuatana na makala hii mpaka mwisho kuahamu zaidi.

Leo hii utakapomaliza kusoma makala hii utafahamu kiundani juu ya namna Teknolojia ya Intaneti katika Vitu (Internet of Things au IoT) inavyoweza kubadili Biashara yako pamoja na vifaa vya kielekroniki unavyotumia nyumbani ama ofisini.

Maeneo kumi (10) muhimu ambapo mageuzi ya intaneti (IoT) katika biashara na maisha, inakwenda kuyagusa na kuleta mabadiliko makubwa katika mazingira ya kazi na jamii. Namba 7 itakushangaza sana:

1. IoT itapofika kwenye ubora wake wa matumizi, biashara nyingi zinazofanyika leo zitapotea sokoni. Mf: biashara za ugavi na usambazaji ambazo kwa sasa hutumia mtu wa tatu katika kufanya usafirishaji/usambazaji, hizi zitaweza kujiendesha kiautomatiki, yaani ukiagiza kitu mtandaoni inakupa namna ya kukufikishia bidhaa/huduma popote bila hata kujieleza. Fikiria upo Magomeni na unaagiza mafuta mtandaoni kutoka Singida, unapotoa oda yako tu, huna haja ya kusema uko wapi, unapokea zako tu ujumbe kuwa “mafuta yako yatakufikia siku fulani saa fulani mahali fulani (Mahali ambapo unakuaga muda mwingi). Life’s Simple.

mageuzi ya Intaneti (iot) katika biashara na maisha.Jihudumie leo kutoka Rednet Technologies.

2. Moja kati ya athari hasi za IoT ni pamoja na kumlazimu mtumiaji kuhakikisha vifaa vyake vinavyotumia intaneti na vilivyoungwa katika teknolojia ya IoT vinakuwa updated muda wote. Hii itaongeza gharama za bando japokuwa “Mtaka cha uvunguni sharti ainame.”

3. Mpaka kufikia 2025 soko la IoT linatarajiwa kuwa na thamani ya kati ya 3.9 $ mpaka 11.1$ trilioni kwa mwaka. Vihisishi (Sensors, RFID na Bluetooth devices) vinatajwa kuchukua zaidi ya 50% ya matumizi ya IoT vikifuatiwa na huduma za Teknolojia ya Habari (IT). hapa ndipo utakapoona sasa mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha kwa ujumla.

4. Soko la Biashara Kwa Biashara (B2B IoT Market size): 2015: soko lilikuwa na thamani ya $195 bilioni na kufikia mwaka 2020 soko lilifikia thamani ya $470 bilioni ikiwa ni ongezeko la zaidi ya dola bilioni 250 ndani ya miaka mitano tu. Yaani IoT imeimarisha sana mapato katika biashara katika nyanja za mifumo ya udhibiti, uchambuzi wa data, vifaa, network na huduma bora. IoT imekuwa mkombozi haswa.

Mfano mzuri hapa ni mifumo ya ukusanyaji kodi ya TRA. Mifumo hio imefanywa imara katika kudhibiti makusanyo ya kodi kupitia mashine za EFD ambazo zimeungwa kielektroniki ili kuwapa TRA data sahihi za kodi.

mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha.

5. Ukuaji wa IoT unaathiriwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya Teknolojia zingine. Mfano: Teknolojia ya mawingu (cloud tech) inavyokuwa na IoT nayo inakuwa sambamba. Pia IoT inasambaa kwa kasi pale uwezo wa mitandao unaposambaa zaidi. Kifupi ni ngumu kuzuia kasi ukuaji wa IoT duniani.

6. IoT itapofikia ubora wake kwenye matumizi, inatarajiwa kuwezesha kufikia vifaa vingi kwa kutumia kifaa kimoja. Fikiria unarudi zako home, ukifika nje unawasha taa za nyumba, then unawasha feni, TV na sabufa yako na kuzima Friji yote kwa kutumia simujanja yako tu yani.

7. Unazijua RFID’s? Hizi kitaalamu zinaitwa Radio-Frequency Identifications. Yani vifaa vyenye uwezo wa kuratibu utambulisho wa bidhaa/huduma. Mfano vile vitochi unaviona ukienda supamaketi pale kabla hujalipia, bidhaa yako inamulikwa na mwanga flani hivi ili kujua bei. Sasa kile kitochi kinaitwa RFID scanner. Hizi skana zipo za aina nyingi kwa minajili ya kutambua bidhaa/mtu, zingine zipo viwanja vya ndege kukagua mizigo, watu na pasi za kusafiri.

RFID’s zinahusika vipi kwenye IoT?

Teknolojia ya IoT sasa inaziwezesha hizi RFID’s katika sekta ya Ugavi na Usafirishaji ili kutoa data sahihi kuhusu ubora na idadi ya bidhaa zinazosafirishwa na kutumiwa. Kupitia IoT bidhaa inaweza kujulikana ipo wapi na lini imenunuliwa inapopita kwenye skana ambayo hutuma taarifa sahihi za bidhaa kwa mtengenezaji. Kufahamu zaidi kuhusu mchango wa RFID’s katika nyanja ya Biashara na Uchukuzi tafadhali gusa link hii MAPINDUZI YA KITEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI

8. Namba ya Vifaa vya kielektroniki vinavyoweza kuwasiliana pasi na kuingiliwa na mtu M2M (Machine To Machine) inatajwa kuongezeka kwa kasi kubwa ndani ya muda mchache tu. 2018 kulikua na vifaa 1.5 bilioni na mwaka 2020 viliongezeka kufikia 2.6 bilioni. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Statista.

9. IoT ndio suluhisho sahihi katika kutoa huduma bora zaidi kwa mteja. Yani unapotumia teknolojia ya IoT katika biashara yako, unampa mteja nafasi ya kupata huduma nyingi (mfano: kununua bidhaa/huduma, kujisafirishia na kutoa maoni) ndani ya site moja kirahisi.

10. Kuongeza Mapato: Kwa kutumia IoT matumizi katika biashara yanapungua sana kwa kuwa shughuli nyingi zinafanyika kiautomatiki kupitia mawasiliano baina ya vifaa vinavyotumia huduma za intaneti. Hakuna tena gharama kubwa za usafiri wala kukusanya data. Kifupi, yajayo yanafurahisha sana katika IoT. Makampuni mengi duniani tayari wameshanza kutumia huduma hizi yakiongozwa na makampuni ya Ugavi na Usafirishaji kama DHL, XPO Logistics na FedEx.

Biashara zinazotumia IoT hujikuta zikitumia gharama ndogo na thamani kubwa sana katika kujiendesha, jambo linalowafanya waweze kujitanua zaidi na kupata mapato lukuki. IoT ndio teknolijia ya kibiashara haswa na wajanja ndio wanaoifaidi. Usisubiri uachwe.

Kuna msemo mmoja maarufu katika IoT unasema, “If an electronic device can be connected, it should get connected” yaani, “Kama kifaa kinaweza kuunganishwa, basi na kiunganishwe”. Msemo huu ndio kwa kiasi kikubwa unaipa nguvu kasi ya IoT kuenea duniani. Umegundua nini kwenye makala hii kuhusu mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha? Tuambie kwenye comment hapo chini,..

Vyanzo: https://www.statista.com/statistics/1194677/iot-connected-devices-regionally/

https://www.huffpost.com/entry/8-ways-the-internet-of-th_b_11763836

https://www.newgenapps.com/blog/impact-of-internet-of-things-on-the-business-world/