Tag: umuhimu wa mitandao

Kwanini hupati wateja mtandaoni?

KWANINI HUPATI WATEJA MTANDAONI?

Kila mtu anapenda maisha mazuri, kufanikiwa kibiashara, kuwa na amani na uhuru wa kufanya kile kinachokupa furaha muda wowote. Sasa uko tayari kuingia gharama ili kuyapata matamanio yako? Umeshajiuliza Kwanini Hupati Wateja Mtandaoni licha ya Juhudi unazoweka?

Mwaka 2010 wakati nafungua account ya Facebook nilikua nafurahi sana kukutana na rafiki zangu tuliopotezana miaka mingi baada ya kumaliza Primary School na sekondari. Ilikua safi sana kuona picha za washkaji wakiwa na maisha yao baada ya shule.

Baadae tukaanza kupata marafiki wengine katika mtandao pendwa wa facebook. Nyakati hizo Mtandao wa Twita ulionekana kama mtandao wa Wanasiasa, Instagram ya Wasanii na Masuperstar. Ila Facebook kule wote tulionana kuwa ni level moja. So kule ndo tuliona kuna lile vibe la wote.

kwanini hupati wateja mtandaoni?

nguvu ya mitandao ya kijamii 

unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako?

Lakini miaka ilivyozidi kwenda, Matumizi ya Mitandao ya Kijamii yalikua yakibadilika mdogo mdogo, hasa baada ya kushuhudia Wasanii na watu waliokuwa na Followers wengi mitandaoni waliposhindwa kuimarisha Uchumi wao kupitia Nguvu ya Mitandao. Hapa kitu kipya kikatambulishwa.

Ilifika mahali sasa ule utaratibu wa kuwa na urafiki na wale tu uliowahi kusoma nao sasa ulipitwa na wakati na badala yake, Rafiki/Followers/Follows wa mtandaoni wakawa ni wale ambao tunashare nao “Interests” Hapo ndipo mbinu za kufanya biashara mitandaoni zilipoanza kushamiri.

Tayari nimeshakuandalia makala maalum itakayokupa mbinu muhimu za kunasa wateja mtandaoni. Kama unataka kuzifahamu mbinu hizo ili uzitumie kwenye biashara yako basi fuatana na makala hii hapa Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

MAMBO SABA (7) YANAYOKUKOSESHA WATEJA MTANDAONI

Tumeshaona jinsi Mitandao imebadilika kutoka ilipoanza, sasa kuna mambo unayoyafanya kwa kujua au kutokujua yanayokukosesha wateja. Jambo la 5 litakushtusha sana. Hebu tuyaone hapa;

1. Kutokuwa na Bidhaa/Huduma inayokutambulisha;

Hapa unatakiwa kuwa makini na kuelekeza focus yako kwenye bidhaa/huduma fulani specific. Inaweza isiwe bidhaa/huduma moja, lakini hakikisha unakuwa na ile bidhaa/huduma inayokutambulisha. Mfano: Unauza fenicha, shikilia hapo hapo.

kwanini hupati wateja mtandaoni

Zile zama leo unapost fenicha, kesho unapost computers keshokutwa unapost picha uko unasafiri, mara unapost unakula chakula., hivyo ni vitu ambavyo vinakupunguzia mvuto mtandaoni. Sisemi usipost kabisa, hasha, katika post 10, 7 ziwe ni kuhusu fenicha, 3 maisha binafsi.

2. Kushindwa kuingia kwenye Orodha ya Wanaofanya biashara kama yako mtandaoni;

Kuna ile dhana ya kuogopa ushindani au ile kuwekeana mtimanyongo na washindani wako. My friend, huku mtandaoni make sure unajenga uhusiano na kila unayekutana naye. Itakusaidia sana kuendelea kudumu sokoni.

Kuingia kwenye orodha(list) ya wafanyabishara huna budi kuwa support wafanyabiashara wenzako mtandaoni. Ndio, Wasukuma wana msemo wao wanakwambia “Scratch my back, I’ll scratch yours.”

3. Kutokua na muendelezo wa Maudhui kutasema kwanini hupati wateja mtandaoni;

Je wajua kwamba kwa siku huwa kunakuwa na posts zaidi ya milioni 50 katika mitandao mbalimbali duniani. Sasa ndugu unapost mara 1 kwa wiki unategemea nani ataiona hio biashara yako? Hakikisha unapost mara nyingi kadiri iwezekanavyo.

Njia ya Kompyuta katika kuhifadhi data utajuaje pale biashara yako inapojiendesha kwa hasara changamoto katika biashara mpya/inayoanza, hili ni funzo lisiloepukika

4. Kushindwa Kuwasiliana Vema;

Kupost bidhaa/huduma zako mtandaoni ni jambo moja, lakini uwezo wa kuwasiliana ndio muhimu sana. Shuleni tulisoma ile Communication Skills, sasa mtaani unatakiwa uwe na uwezo wa kuwasiliana na kujua wapi, sangapi useme nini. Ni maarifa hayo.

Mtaalam wa mitandao bwana @GillsaInt ana mbinu yake anakwambia katika maudhui yako unayopost mtandaoni, hakikisha 80% ni yanahusu thamani (value) za bidhaa/ huduma zako kama Faida, Jinsi ya Kutumia, Changamoto nk. Na 20% zinazobaki ndo upost sasa Matangazo ya kuuza hio biashara.

5. Kutokuwa na Miundombinu ya Kurahisisha biashara Mtandaoni;

Umeshaona wale wanakwambia No Facebook Acc, No Insta Acc, No twitter etc. Skia, kama unataka kufanya biashara ukafanikiwa mtandaoni USIFUATISHE hizo akili zao. Hakikisha una miundobinu humu mtandaoni.

Mitandao ya kijamii ndipo ilipo NGUVU halisi ya biashara ya mtandaoni. Jifunze namna unavyoweza kuitumia kwa faida ya biashara yako. Kama unataka kuifahamu NGUVU hio ya mitandao, basi fuatana na makala hio hapa kufahamu zaidi.

Lengo la kufanya biashara mtandaoni ni kuhakikisha unakuwa na wateja wengi kadiri iwezekanavyo, si ndio? Kama ni hivyo, fanya research, kisha tambua wateja wako ni kina nani na wako wapi. Fungua website yako, accounts za Insta, Facebook, Linkedin, Twitter n.k Kuwa available.

6. Kukosa Ushawishi na Ujuzi wa Kuuzia wateja Mtandaoni;

Sasa hapa naongelea uwezo wa kumshawishi mtu akapenda bidhaa/huduma zako kabla hajawa mteja wako. Kwenye hili @iamKaga pale twita anakupa funzo gani? Cha kwanza hakikisha watu wanakujua, kisha Wakupende au wapende maudhui yako, hapo ndipo watakujia.

Huo ushawishi hauji tu by default wala haujengwi ndani ya siku moja. Ushawishi ni tabia ya kuhoji na kutoa ufumbuzi juu ya changamoto zinazowakabili watu katika namna bora ya uwasilishaji. Hapa ndipo wanasiasa wanatupiga coz anaijua siri iliyopo kwnye ushawishi.

7. Kutokuwa na Njaa ya Mafanikio;

Tunarudi kulee mwanzo, unapost mara 1 kwa wiki, au mara 2 kwa mwezi halafu unasingizia huna muda wa kuandaa maudhui. Bro, ni vile tu huna njaa ya kufanikiwa. Njaa ya mafanikio ikikushika vizuri huo muda LAZIMA uupate na utautumia vizuri tu.

Kuna nyakati unabanwa na shughuli zako nyingine to the point unashindwa kuendesha biashara yako mtandaoni. Kuna nyakati nyingine unakata tamaa kwa sababu huna followers au huna idea uanzaje kuandaa maudhui ili ufikie yale matamanio yako. Ukifikia hapo wala usiwe na shaka..

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

Hata hivyo, katika biashara sio lazima kila jambo ufanye wewe mwenyewe. Nyakati hizi za mapinduzi ya teknolojia kila siku, ni muhimu kugawa majukumu kwa wataalam wa kuaminika ili kuhakikisha lengo na mipango yako inazidi kwenda kama utakavyo.

Hio ndio sababu sisi Rednet Tech. LEO hii tunakupa nafasi ya kuikuza biashara yako mtandaoni kwa;

1. Kukutengenezea Website bora.

2. Kukufanyia huduma ya SEO. Inafanyeje kazi hii? Gusa hapa kuifahamu zaidi.

3. Kukushauri aina ya maudhui ya kuyatumia kwenye kurasa zako za mitandao. Gusa hapa tuchati pale WhatsApp na upate huduma unayohitaji.

So, mambo haya 7 tuliyoyaona leo kwa uchache wake ndio yanakwambia kwanini hupati wateja mtandaoni. Umeshajua cha kufanya sasa? Hebu niambie wewe ni lipi umegundua leo kuwa ndio linakukosesha wateja? Mtandaoni hamna miujiza. Ni kuwa na maarifa na kuhakikisha unajifunza kila siku. Umependa makala hii? Share..

simu za michongo Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.

FAIDA ZA KUTUMIA GOOGLE KAMA JUKWAA LA BIASHARA YAKO

Je, unaamini kwamba matumizi sahihi ya huduma za internet na mitandao ya kijamii yana uwezo wa kukurahisishia huduma/bidhaa zako zikapatikana kirahisi na wateja wako wakiwa popote duniani? Leo nataka nikupe stori kuhusu Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.

Tizama hapa, Siku moja asubuhi kabisa ya mwezi April mwaka huu 2022 nikiwa natoka home naelekea ofisini nikapigiwa simu, kutizama ni namba ngeni, nikatafuta utulivu kisha nikapokea;

Mimi: Hello, Habari za asubuhi!

Jamaa: Salama Faustine, I hope uko poa, Bwana mimi ni fulani (jina kapuni) nimekupigia kwa sababu nahitaji website na ningependa ifanywe na kijana mzawa. Nafanya kazi katika shirika (jina kapuni) ambalo ni la kimataifa. Nilikua napitia google pale nikaona kampuni yenu ya Rednet Technologies na nikaona pia kumbe mnajishughulisha na haya mambo. Itawezekana si ndio?

Mimi: Bila shaka hilo linawezekana kabisa, unahitaji lini hii kazi yako iwe imekwisha?

Jamaa: Well, ndani ya wiki 3 ningependa iwe imekwisha, sasa nitampatia namba yako mwenzangu yupo pale ofisini kwetu, yeye sasa atakupa maelezo ya kina. Lakini naomba kujua bei itakuwaje hapo (huku anacheka kwa ufupi)

Mimi: Gharama nitataja nikishajua requirements kaka, wala usiwe na shaka.

Baada ya kuwasiliana na huyo mwenzake akanirudia…

Jamaa: Faustine, naona mmeshaelewana, Sasa the reason tumekuja kwako ni kwasababu kuna mtu tulimpaga kazi ya kutengeneza hii website yetu, lakini hajawahi kutupa ushirikiano, kazi hajamaliza, changes hataki kufanya na tukimpigia simu harespond ndani ya muda, yani ana kiburi sana yule jamaa, kusema ukweli TUMEMCHOKA.

Mimi: (Kiukweli nilijiskia vibaya sana, ndugu zangu ule msemo wa “Mteja ni Mfalme” una maana kubwa sana hapa. Nikamwambia) Kaka, pole sana, utakavyokuwa unafanya kazi kwetu nakuahidi hio kadhia hutakutana nayo.

Jamaa: Kweli? Ok, turudi kwenye bei sasa, utatuchaji kiasi gani?

Mimi: Kwa nature ya Organization yenu hapo mpaka kazi inakamilika itacost 850,000/- tu.

Jamaa: Faustine, mbona bei ipo juu sana, tutaweza kufanya kazi kweli?

Mimi: Kaka, bei iko fair sana hio ukizingatia tutawatengenezea pia business emails BURE na kuwafanyia maintenance BURE kwa mwaka mzima. Anytime hapo mkitaka kufanya changes, tutazifanya BURE kabisa. Hapo unasemaje?

Jamaa: Hapo sio mbaya, walau naona dalili hautakuwa kama jamaa wa mwanzo. Ila bei bado hujashusha..

Mimi: Kaka, lipia 400k leo, baadae utalipa 250k, then finally tutakapomaliza kazi, utalipia 200k ambayo itakuwa imebaki. Hapo je?

Jamaa: Ok, Nataka na hio website pia iwe inapatikana mtu akisearch Google, ili wateja watupate kama sisi tulivyokupata wewe.

Mimi: Ahaa, hio sasa ni huduma nyingine, inaitwa Search Engine Optimization (SEO). Ndo inaiwezesha website kupatikana google.

Jamaa: Na hio utatuchaji au bei yake ndio inakuja na ya website direct?

Mimi: Hio gharama yake ni tofauti kaka.

Jamaa: Ambayo ni ngapi? Usinilalie bwana ndugu yangu.

Mimi: Hio kwa sababu ni kazi ya muendelezo, utakuwa unalipia kila mwezi, ambapo gharama yake ni 100,000/- tu.

Jamaa: sema Faustine mna bei nyie. Ehe niambie, kwenye hio laki 1 mtakuwa mnafanya nini na nini?

Mimi: Hapo tutakuwa tunakuandikia makala (blog posts) mbili kwa mwezi ambazo zitahusu shughuli mnazofanya, tutaweka picha, pamoja na kuzioptimize ili iwe rahisi kupatikana google mtu akiwa anatafuta taarifa zinazowahusu.

Jamaa: Faustine, hapo umeniweza. Basi wacha tuandae contract, halafu next week tutakuita ili tusign, kazi ianze mara moja. Ila usiniangushe bwana.

Mimi: Kaka wala usiwaze, tufanye kazi.

Basi Bwana baada ya simu hio ndio uhusiano ukajengwa na kazi ikaanza kama hivyo.

Na baada ya kazi hio kuisha, jamaa yetu aliweza kutuunganisha kwa watu wengine watano (5) ambao walitamani kupata huduma kama ambayo aliipata kutoka kwetu. Na hatimaye wamekuwa wateja wetu wa kudumu. Unadhani hao walivutiwa na nini? Fuatilia makala hii hapa kufahamu siri za utoaji huduma bora kwa wateja.

Unachoweza kujifunza ili uweze kuzipata Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.

Katika mazingira ya kazi, hasa huku mtandaoni ambapo mara nyingi tunakutana na watu tusiowafahamu (strangers) ni muhimu sana kuzingatia haya yafuatayo;

1. KAULI NJEMA

2. UAMINIFU

3. KUMJALI MTEJA na MAUMIVU YAKE (Mara kwa mara muulize kama anaridhika na huduma anazopata kutoka kwako na nini unaweza kufanya ili kazi yake ifanyike kwa ubora anaotarajia).

Kauli Njema zitakufunulia fursa nyingi na kukuletea wateja wengi sana huku mtandaoni, acha tabia ya kutukana, kudhalilisha au/na kudharau watu. Kumbuka teknolojia haisahau.

Uaminifu utajenga uhusiano mzuri na wa kudumu na mteja wako.

Kumjali mteja kutafanya azidi kukupa kazi nyingi zaidi mbeleni, na hata kukuunganisha kwa watu wake wengine anaowafahamu.

Siri ya kufanya kazi vizuri na mteja ipo kwenye hayo mambo matatu. Ukiyazingatia, hakika huwezi kufeli. Zaidi kama unahisi bado hujajua namna unaweza kushawishi mteja kwenye biashara yako fuatana na makala hii hapa tumekuandalia.

HABARI NJEMA KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU

Sasa kuelekea mwisho wa Mwaka tunakupa ZAWADI ya kuifikisha biashara yako mtandaoni na kukusanya wateja kutoka kila pembe ya nchi. Fungua website leo kwa 500,000/- tu (badala ya 850,000/-) upate na huduma ya SEO BURE (badala ya 100,000/- kwa mwezi) maintenance BURE mwaka mzima pamoja na Ushauri BURE kabisa. Hata hivyo, ZAWADI hii haitamfikia kila mtu. Zawadi hii ni kwa watu 10 tu wa mwanzo, na itadumu mpaka tar 10 December. Baada ya hapo tunakwenda likizo ya Christmas.. So kama unahitaji ZAWADI hii WAHI nafasi mapema ili pia uzipate Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.

OFA ya Msimu wa Sikukuu 2022
Sherehe za Christmas na Mwaka Mpya Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.

Baada ya OFA hii ukihitaji website ni 850,000/-, huduma ya SEO ni 100,000/- kwa mwezi na pia tutafungua group la Whatsapp kwa yeyote atakayehitaji ushauri au atayehitaji kuuliza jambo lolote kuhusu Website, SEO, Social Media Marketing, Digital Marketing na Tech kwa ujumla wake. Kuingia kwenye group hilo itakugharimu 5,000/- tu kwa mwezi.

So ukiliona Tangazo hili, mtaarifu na mwenzako ambaye unahisi atahitaji kunufaika na ZAWADI hii.

Wewe kama unafanya biashara, basi kama unataka kufanya vizuri sokoni, hakikisha unajenga URAFIKI na wateja wako. Hii ni kwa sababu ni rahisi sana MTEJA kuwa RAFIKI yako kama utatengeneza UHUSIANO mzuri kati yenu. Hii ndio SIRI ambayo hakuna mtu atakwambia kirahisi.

Kufanya biashara mtandaoni ni Uwekezaji muhimu sana, na kwa maendeleo yaliyopo kwa sasa duniani, imekuwa ni rahisi mno kutumia huduma za Internet katika kuwafikia wateja popote walipo duniani.

Kuna mtu aliwahi kuniuliza, “Sasa nawezaje kutumia Internet kufanya biashara yangu?”

Jibu: Unaweza fanya haya yafuatayo ili uweze kupata Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako.:

1. Tumia Website na mitandao ya kijamii kutoa elimu kuhusu bidhaa/huduma zako.

2. Tumia SEO ili kurahisisha maudhui yako yanapatikana kirahisi katika Google.

3. Fanya matangazo (Paid Ads/Sponsored Ads) ili kuwafikia wateja wengi kwa haraka.

4. Jifunze kuuza katika Maandishi (Copywriting). Jaribu kadiri unavyoweza.

5. Tumia WhatsApp yako vizuri kibiashara (Status, Broadcast, Groups n.k).

Ukiona haya yanakuwa magumu kwasababu upo busy au vinginevyo, usikubali sasa biashara yako ife/ishindwe kufanya vizuri mtandaoni.

Tafuta mtaalamu wa kufanya biashara mtandaoni, mpe targets zako, kubaliana nae katika malipo, kisha mpe kazi ili biashara yako izidi kupaa mtandaoni kwa sababu ni muhimu sana ukazipata hizi Faida za kutumia Google kama Jukwaa la biashara yako. Sio lazima kila kitu ukifanye wewe mwenyewe kwa sababu hakuna ajuaje kila kitu.

Ni mategemeo yangu umepata kitu kipya leo. Kumbuka ZAWADI yetu ya kufunga Mwaka inakwisha tarehe 10 December, halafu hii ni maalum kwa watu 10 tu watakaowahi kujinyakulia website zao.

Tutumie ujumbe sasa hivi au tuchek kupitia mawasiliano haya;

Call/WhatsApp: +255765834754

Email: info@rednet.co.tz

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni. Branding vs Marketing. Kipi ni kipi?

JINSI YA KUONGEZA MBINU ZA KULIFIKIA SOKO MTANDAONI

Kila mtu atakwambia post insta, facebook, tumia funnels, weka status za kutosha Whatsapp. Mwingine atakwambia kusanya namba za simu uwapigie, tuma emails kila siku nk. Sasa utafanyaje kuongeza mbinu za kulifikia soko? Utakapomaliza makala hii ya leo utafahamu kiundani kuhusu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni. Utafanyaje, twende sambamba mpaka mwisho.

Zama hizi za Internet na huduma za mitandao ya kijamii zimekuja na mgawanyiko wa watu. Kila mtu anatumia mtandao wa kijamii anaoona unampendeza. Sio ajabu uone kuna mtu hana account ya facebook lakini kutwa yupo instagram/twitter. Hata hivyo ukiwa mjasiriamali lazima ufike kote.

UNALIFIAJE SASA HILO SOKO LA MTANDAONI?

1. Kwa kutumia Mitandao kama Whatsapp, Instagram, Twitter na Facebook, sasa unaweza kueneza maudhui yako kote kote kwa mtindo wa Copy & Paste. Ndio sio dhambi kufanya C&P ikiwa maudhui ni yako. Hata hii makala usishangae kuikuta kwa page zatu za LinkedIn na Instagram. Hapa ni muhimu sana Ukaifahamu Nguvu ya Mitandao ya Kijamii katika biashara yako.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba mitandao hii imetofautiana, hivyo maudhui unayopost twitter inabidi UYAHARIRI ili yaendane na aina ya watu katika mitandao mingine kama Website yako, Facebook, Instagram na LinkedIn. So kazi ya kueneza maudhui haiwi ngumu kuvile hapa, sivyo?

2. Pia unaweza kuanzisha kampeni fulani na kisha unaieneza kwa njia ya barua pepe. Kufanikiwa kwenye hili kwanza unapaswa ukusanye anwani za barua pepe nyingi (walau elfu moja) na kisha uifanye kampeni yako kwa uweledi wa hali ya juu ndani muda fulani. Hii ndio Email Marketing.

E-Mail Marketing in Business
mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

NB: Kampeni yako haipaswi kuwa na ujumbe wa kupandikiza chuki au viashiria vya ubaguzi wa namna yoyote kwa sababu kampeni za namna hio huleta hisia mseto kwa watu na kukujengea taswira mbaya. Barua pepe zako unaweza kuzikusanya kwa njia ya Newsletter au kawaida (ile ya kuomba).

3. Tumia Social Media Analytics Tools: Kama unasambaza maudhui yako kupitia mitandao ya kijamii, siku hizi kuna namna ambayo unaweza kupima mwenendo wa machapisho yako kirahisi tu. Katika twita kuna Twitter Analytics na Insta kuna Insights.

social media analytics tools
mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

Hizo tools zitakwambia maudhui yako yamewafikia watu wangapi (impression), wangapi wameshiriki mjadala (engagement), wangapi wameclick links na umepata wafuasi wangapi baada ya kuchapisha maudhui. Ukishajua hayo itakusaidia sana kuboresha zaidi Machapisho yako yajayo.

Mitandao ya kijamii hasa Mtandao wa GOOGLE ina nguvu ya ajabu sana katika kuwafikia watu wengi ndani ya muda mfupi tu. Ni muhimu basi ukajua namna ya kucheza na mitandao hii ambayo kila mtu duniani anatamani awe mtumiaji wa kila siku. Kufahamu zaidi kuhusu nguvu hio gusa hapa;

4. Tumia Web Analytics Tools; Kama tayari unayo website ya biashara au page ya blogu yako, basi ni muhimu sana ukaweza kufuatilia na kujua ufanisi wake kwa watu wanaoitembelea. Unajua watu wangapi wanatembea website yako kila siku? Makala zipi ulizoandika zinafuatiliwa zaidi?

Watu wanaotembelea website yako wanatokea wapi? Katika Injini za Kimtandao, website yako iko katika nafasi gani? Majibu ya maswali yote haya unaweza kuyapata kwa kutumia tools kama Google Search Console, ahrefs, winch, clutch n.k Hivi ndo virutubisho vya website yako mtandaoni.

5. Tumia Content Management System (CMS); Ukiwa muandishi ambaye ungependa maudhui yako yazidi kufanya vizuri mtandaoni basi unapaswa kutumia mbinu mbadala zitakazokusaidia tena na tena. Sikuhizi mambo yamerahisishwa, WordPress ndio CMS maarufu zaidi lakini ukiacha hio kuna Joomla, Drupal, Magento, Shopify na Prestashop (kwa ajili ya e-commerce). Ukiwa na hizo tools inakuwa rahisi kwako kuandika maudhui ambayo yatakuwa rahisi zaidi kunaswa na Injini za Mtandaoni kama Google, Ask na Bing. Umeshawahi kutumia CMS gani? Tuambie hapa leo..

Content Management System
mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

6. Tumia SEO Hapa sitasema mengi kwa sababu tumeshaongea mengi huko nyuma. Kifupi hii SEO (Search Engine Optimization) ni teknolojia iliyopo kwenye software za mtandaoni zenye uwezo wa kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kama websites, blogs, mitandao ya kijamii n.k

Cha kuzingatia zaidi unapofanya SEO ni matumizi ya Keywords sahihi kwa ajili ya soko lako ulilochagua kuhudumia (niche), Picha unazotumia lazima ziwe na maelezo tambuzi (alt text), matumizi ya links pamoja na ujuzi wa kuuza kwa kupitia maandishi(copywriting skills) Zingatia sana haya kwasababu hii ndio mbinu bora sana katika kufahamu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

Yaani SEO ni SUMAKU inayovuta taarifa kutoka sehemu mbalimbali za watu (open source information) na kuzigawa kwa mtu yeyote ambaye atatafuta taarifa hizo. Umeshaielewa jinsi SEO inavyofanya kazi sasa? Kufahamu zaidi fuatana na makala hii hapa;

7. Fanya Mara kwa Mara; Umeshayaona haya tuliyoyaelezea leo? Sasa kama unataka kufanikiwa katika kuipeleka mbali biashara yako huku mtandaoni, basi SIO LAZIMA uyafanye yote, aghalabu, unaweza kufanya matatu au manne ili ujiweke kwenye nafasi nzuri katika kuimarisha ushawishi wako huku Mtandaoni. Lakini katika kuzifanyia kazi mbinu hizi basi ni muhimu mbinu hizi uzifanye MARA KWA MARA, yaani uwe na consistency. Usifanye mara mbili kisha ukakata tamaa. Andika machapisho 500, tuma emails 2000, rudia na rudia. Njiani utagundua ile njia sahihi zaidi.

Umegundua nini kwenye makala hii ya leo? Umeshafahamu kiundani kuhusu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni? Una la kuongezea, swali au changamoto?

Tafadhali weka maoni yako hapa au kama unahitaji kuwasikiana nasi kupitia emails au Whatsapp, tafadhali fanya hivyo; Whatsapp/Call: +255765834754 Email: info@rednet.co.tz

VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE)

VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE)

Baada ya kuripotiwa kupatikana kwa kirusi kinachofuta data zote kwenye mifumo ya kopyuta (Wiper) katika shambulizi la hivi karibuni, serikali ya Ukraine inasema “Shambulizi hili ni la kiwango cha tofauti kabisa”. Sasa leo tuone kwa undani vita vya kimtandao kati ya Urusi na Ukraine (Cyber Warfare) kwa sababu ni jambo linaloathiri hali ya uchumi ya kila mwanadamu aishie duniani kwa sasa. Vilianza lini na vinaathiri vipi uchumi na maendeleo ya Teknolojia? Twende sambamba mpaka mwisho wa makala hii.

Jumatano ya tar 23 February, 2022 tovuti (websites) za benki kadhaa na idara za serikali nchini Ukraine hazikupatikana hewani, ambapo kampuni ya usambazaji wa huduma za internet (ISP) ya Netblocks ilidai kutokea kwa shambulizi la DDoS (Distributed Denial of Services). Agalia hii tweet yao hapa..

VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE), Shambulizi la DDoS attack.

Lakini hii si mara ya kwanza kuripotiwa mashambukizi ya Kimtandao ambayo yanadaiwa kufanywa na Urusi.

Mashambukizi ya Kimtandao ambayo yalishawahi kufanywa hapo awali na Urusi:

Mwaka 2008 wakati Urusi inaondoa majeshi yake nchini Georgia, Rais Vladimir Putin aliongoza jitihada za kuliimarisha jeshi lake kisasa katika upande wa vita za kimtandao na mbinu zake kijasusi. Ikumbukwe Rais Putin ni ex-KGB. So ni Jasusi mbobevu kabisa kwenye uga huu.

Hivyo kwanzia hapo Urusi imekua ikitumia mashambulizi ya kimtandao kuvuruga na kubomoa taarifa na mifumo ya kimtandao ya adui. Hii imekua ni mbinu mtawalia katika medani za kivita kwanzia hapo na zimekuwa zikiratibiwa na Idara kuu ya Ujasusi jeshini iitwayo GRU.

Hii GRU kwa kifupi ni Glavnoye Razvedyvatelnoye Upravlenie (inasomwa ivyo ivyo kama inavyoandikwa). Jaribu kusoma kwa sauti tuone..

Hii ni Idara ya Ujasusi Jeshini huko Urusi. Kwa huku kwetu tungeiita Millitary Intelligence (MI). Huku ndo Ujasusi haswa unapofanyika.

Idara hii haina uhusiano wa moja kwa moja na shirika kongwe la Ujasusi la KGB kwa kuwa shirika lile lilishakufa na badala yake likazaliwa shirika la FSB ambalo kazi yake kuu kimsingi ni kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu watu, miundombinu, usalama ndani ya nchi na mipakani n.k.

Kwa kirefu kuhusu mashirika haya ya kijasusi na namna yanavyofanya kazi tafuta kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI kilichoandikwa na @YerickoNyerereT pamoja na kile cha @habibu_anga kiitwacho OPERESHENI ZA KIJASUSI. Wacha tuendelee na mada yetu tuloanza nayo.

MASHAMBULIZI KATIKA VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE)

  1. December 2015, idara ya GRU ilishambulia mitandao ya mifumo ya viwanda nchini Ukraine kwa virusi haribifu (malwares). Hii ilisababisha kukatika kwa umeme kwa zaidi ya masaa 6 katika maeneo ya Magharibi ya Ivano-Frankivsk. Hali hii iliathiri nyumba za makazi takriban 700,000.

Shambulizi hili pia lilifanywa December 2016 ambapo Urusi ilidaiwa kutengeneza kirusi kilichoitwa Crash Override ambacho kilielekezwa kwenye Gridi ya Umeme ya Ukraine. Madhara ya shambulizi hili yaliathiri takriban 1/5 (moja ya tano) ya uwezo wa jiji la Kiev kusambaza umeme.

VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE)

Gridi ya Umeme

Sababu inayodhaniwa kusababisha shambulizi hili kutekelezwa inatajwa ni majaribio ya kuharibu vinu vya Nyuklia kwa kutumia mitandao ya kompyuta. Hii ni kwasababu Vinu vya Nyuklia kwa kiasi kikubwa hutumia Nguvu za Umeme na Huduma za Mitandao ya Kompyuta katika kujiendesha kwake.

Hivyo kushambulia Gridi ya Umeme kwa mafanikio kutafanya uwezekano wa kushambulia Kinu cha Nyuklia kuwa rahisi kupitia Shambulizi la Kimtandao. Umeona watu walivyo na akili apo sasa.

2. Mwaka 2020 Marekani iliwakamata maafisa 6 wa GRU kwa tuhuma za kusambaza shambulizi lililoitwa NotPetya ransomware. Shambulizi hili liliathiri mifumo ya kompyuta dunia nzima na lilisababisha hasara ya 1 Billion dola za Kimarekani.

SHAMBULIZI LA KIMTANDAO HARIBIFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA la NOTPETYA

VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE)

Shambulizi hilo linatajwa kama “SHAMBULIZI LA KIMTANDAO HARIBIFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA” Fuatana na makala kuhusu Mashambulizi ya Kimtandao kufahamu zaidi.

3. Haijatosha hiyo, January 2021, Urusi iliandaa shambulizi lingine ambalo lililenga servers za Microsoft Exchange. Shambulizi hili liliwapa wadukuzi uwezo wa kuingia kwenye akaunti za emails za watu dunia nzima, lakini target yao ilikua ni Ukraine, Marekani na Australia.

KUMBUKA HAYA KATIKA VITA VYA KIMTANDAO KATI YA URUSI NA UKRAINE (CYBER WARFARE):

Katika uwanja wa kivita, wahusika huwa wanajulikana wazi wazi. Lakini katika Vita vya Kimtandao ni ngumu sana wahusika kujitaja hadharani. Hicho ndo kinachoendelea ambapo Urusi mara zote imekuwa ikikana kuhusika katika mashambulizi hayo. Hata China na Marekani huwa hawakubali.

Hii ni kwasababu Wadukuzi hutumia Kifaa kilichodukuliwa kama silaha kuendeleza mashambulizi. So Mdukuzi anaweza kuwa yupo Iringa akadukua compyuta iliyopo NewYork, halafu compyuta hio ikatumika kushambulia mifumo ya kimtandao iliyopo Berlin, Ujerumani. Umeona mambo hayo bwana..

Hivyo ku-trace-back mpaka kumpata mdukuzi halisi ni ngumu sana kwa kuwa mashambulizi haya hufanywa kwa kutumia mbinu za hali ya juu sana ya kijasusi na kiteknolojia. Ndio maana tunasema hapa kila siku, “Security is a myth“. Kwamba usijione upo salama sana uwapo mtandaoni.

Hata hivyo, makampuni ya kiteknolojia duniani huiba na kutumia taarifa za watu kwa sababu za kuimarisha biashara zao kwa kutumia Data Mining na Data Warehousing. Baada ya kupata taarifa hizo hutumia teknolojia mbalimbali mfano Artificial Intelligence katika kuboresha huduma zao.

Ufanyeje sasa ili uwe salama Mtandaoni?

Dunia ya leo inahitaji umakini sana ili kujiepusha na mazingira ambayo yanaweza kukupelekea kudukuliwa. Mazingira hayo ni pamoja na KUACHA tabia ya kuclick links au kufungua picha na video unazotumiwa na watu usiowafahamu, kuwa makini na tovuti unazotembelea pamoja na kuimarisha passwords zako.

Zaidi kuhusu namna bora ya kujilinda uwapo mtandaoni tayari tumeshakuwekea mbinu mbalimbali kupitia makala yatu hii hapa USALAMA WA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI MTANDAONI.

Tumeona Marekani na washirika wake wakiiwekea Russia vikwazo vya kiuchumi na kuwabana matajiri wa Kirusi. Je hatua hii itarudisha nyuma juhudi za Urusi katika kuimarisha ushawishi wake katika eneo la Ulaya Mashariki? vita vya kimtandao kati ya Urusi na Ukraine (Cyber warfare) itakuwa na mchango gani katika mgogoro huu?

Tusubiri tuone itakavyokuwa. Tutaendelea kukupa updates za kinachoendelea kwenye mgogoro huu wa Ukraine na Urusi hasa katika eneo letu mtambuka la Kiteknolojia, Biashara na Uchumi.

Rejea zimetoka https://bbc.com, https://www.theguardian.com/international, https://theconversation.com/global

Je umependezwa na makala zetu zilizomo katika website yetu hapa?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) na QR CODE ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA kwenye picha hapa muda wote 24/7.

Kwanini uwe na website ya biashara yako?

D.R.C NDANI YA E.A.C, MFANYABIASHARA ANAFAIDIKA VIPI?

Hatimaye tar29 March Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilipata kibali cha kuwa mwanajumuiya wa Afrika Mashariki (EAC) na mwezi July mwaka huo 2022 DRC iliingia rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuwasilisha matakwa yote makao makuu ya jumuiya hio jijini Arusha. Hii ni baada ya kuendesha mchakato uliodumu kwa takriban miaka minne. Sasa DRC inapoingia ndani ya EAC mfanyabiashara anafaidika vipi?

DRC inakuwa mwanachama namba 7 wa EAC huku ikiwa ndio nchi kubwa zaidi kijiografia katika ukanda huo. Inasemekana DRC ndio nchi yenye rasilimali (madini, mafuta, misitu n.k) nyingi zaidi duniani. Pia nchi hio ina idadi ya watu takribani milioni 90 ambao ni mtaji muhimu kiuchumi.

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU D.R.C:

Kukubalika kwa DRC kunamaanisha kwamba soko la Afrika Mashariki linatanuka na kuwafikia watu zaidi ya milioni 300 waishio ndani ya jumuiya hio tu, huku uchumi wa jumla ukiwa na thamani ya 250$ bilioni. Sasa DRC ina nini cha ziada usichokijua?

1. MIPAKA YA KIJIOGRAFIA:

Ikiwa ndio nchi ya pili kwa ukubwa wa jiografia barani, DRC inapakana na nchi zingine 9. Nchi hizo ni Angola, Burundi, Jumhuri ya Afrika ya Kati, Rwanda, Jamhuri ya Congo (Brazaville), Sudani Kusini, Uganda, Zambia na Tanzania. Muingiliano wa kibiashara ni mkubwa sana hapa.

Zaidi upande wa magharibi mwa jiji la Kinshasha inapakana na bahari ya Atlantiki. Sasa Kongo kupakana na nchi 9 na kuwa na ufukwe wa bahari ya Atlantiki kunaifanya iweze kutanua fursa kwa wafanyabiashara kupitisha mali kwenda nchi nyingi zaidi barani na hata nje ya bara.

DRC na mipaka yake. Milango ya biashara za kimataifa kwa EAC.

2. KUHUSU VIVUTIO VYA UTALII:

Mbuga ya wanyama kongwe zaidi barani ipo DRC, inaitwa Virunga. Hapo utawakuta wale Sokwe wakubwa (Gorillas), simba na tembo. Lakini mbuga hii ipo kwnye tishio la kutoweka kwa sababu kuna mafuta na kampuni ya Uingereza ya Soco tayari imetia timu kuanza kuchimba mafuta hapo mbugani.

Hawa gorilla ni kivutio kizuri sana cha utalii lakini miaka ya hivi karibuni wamekuwa adimu na kutokana na shughuli za mwanadamu, wanyama hawa wapo kwnye tishio la kutoweka kabisa. Je, DRC kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutadhibiti hatari ya sokwe hawa kutoweka?

Kuhusu namna utalii unaweza kuleta manufaa katika biashara tafadhali fuatana na makala hii hapa chini:

3. KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NA MIUNDOMBINU:

Ni 1.8% tu ya barabara nchini DRC ndio ina kiwango cha lami, huku chini ya 10% ya nyumba za makazi ndio zina umeme. Hii ni hali mbaya sana katika kukuza uchumi wa Taifa. Hata hivyo Benki ya Dunia imetangaza kifurushi za 1$ bilioni kwa ajili ya miundombinu ya DRC.

Moja kati ya vitu vinavyorudisha nyuma juhudi za wajasiriamali na mashirika kuwekeza nchini DRC ni maendeleo duni ya miundombinu. Ukizingatia ukubwa wa nchi hio, imekuwa ni nafuu kusafiri kwa njia ya anga kuliko barabara. Sasa @jumuiya itachangia vipi maendeleo ya miundombinu?

4. BIASHARA ZA NJE YA NCHI (EXPORTS):

Muziki wa DRC ndio mali inayouzwa zaidi nje ya nchi (export). Kuanzia miaka ya 90 muziki wa Bolingo ndio ulikua unasikilizwa na kupendwa zaidi bara zima la Afrika. Ndio maana wasanii kama Fally Ipupa na Koffi Olomide ni matajiri sana. Madini na malighafi zingine zote chali.

5. LUGHA INAYOTUMIKA ZAIDI:

Jiji la Kinshasa ni la pili kwa matumizi ya lugha ya Kifaransa likitanguliwa na jiji la Paris. Yaani Wakongo hawa wanaongea kifaransa zaidi kuliko hata miji ya nchini Ufaransa. Hata hivyo hii inachangiwa na idadi ya watu wanaoishi kwenye jiji hilo, watu milioni 10 mchezo!

Ukiacha Kifaransa raia wa Kongo pia wanazungumza lugha zingine kama Kilingala, Kiingereza, Kiswahili na lugha za makabila asilia. Hivyo ukiwa kama mfanyabiashara na moja kati ya lugha tajwa unazifahamu vyema basi nafasi ni yako kuingia DRC na kutanua biashara zako.

6. KUHUSU UGONJWA WA EBOLA:

Kwamba kupata Ebola nchini DRC ni rahisi kama kupata mafua ukiwa sehemu nyingine? HAPANA. Baada ya ugonjwa huo kufumuka mwaka 1995 na kuua watu zaidi ya 200, milipuko mingine ya ugonjwa huo imekuwa ikidhibitiwa kwa kiwango kikubwa. Hivyo Congo ni salama.

7. KUHUSU MADINI:

Lile bomu la atomiki lililodondoshwa kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki katika WWII lilitengenezwa kwa madini ya Uranium kutoka mgodi wa Shinkolobwe, mkoani Katanga nchini DRC. Hata hivyo mgodi huo ulifungwa mwaka 2004 kutokana na kuishiwa madini ukiiacha DRC patupu.

Kongo imenyonywa sana katika madini yake. Hali kadhalika nchi zingine katika Jumuiya zimepitia hali hio. Hivyo itakapowekwa sera ya pamoja ya kulinda na kusimamia rasilimali zilizopo ndani ya Jumuiya, bila shaka madini na rasilimali ambazo zipo DRC zitakuwa na manufaa sana.

8. HISTORIA YA UNYONYAJI:

Mfalme Leopold II wa Ubelgiji alijitangazia Kongo kuwa mali yake binafsi kuanzia mwaka 1870. Koloni hilo ndio lilikua mali binafsi kubwa zaidi kuwahi kumilikiwa na mtu mmoja kwenye historia. Umiliki huo ulisababisha vifo vya watu milioni10. Huu ndio mwanzo wa nchi kuharibika.

Mfalme Leopold II aliagiza watu kukusanya zao la mpira ambalo kwa kipindi hiko ndio lilikua zao bora zaidi la kibiashara. Wale walioshindwa kukusanya zao hilo kama kodi waliadhibiwa kwa kunyimwa chakula na kukatwa mikono yao. Ukatili huo ulikua mbaya sana dhidi ya ubinaadam.

9. HALI YA USALAMA NA VITA:

DRC imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na migogoro isiyokwisha ambayo imepelekea vifo vya watu takriban milioni 6. Hali hio ya vita visivyokwisha imepewa jina la “Vita vya Dunia vya Afrika”.

Vita hivyo kwa sehemu kubwa vimekuwa vikisababishwa na vikundi fulani (kampuni, mashirika na raia wa kawaida) kugombania rasilimali katika eneo fulani. Huyu anataka kuchimba, raia wanataka kunufaika. Je, DRC kuingia kwenye @jumuiya itasaidia kumaliza janga la vita visivyokwisha?

10. KUHUSU MTO CONGO:

Ukiwa na urefu wa kilomita 4,700, mto Congo ndio mto mrefu wa pili barani Afrika ukitanguliwa na mto Nile. Pia huo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani. Cha kufurahisha zaidi, Mto Congo na Mto Nile yote inapatikana katika EAC. Inakupa picha gani hii kiuchumi?

Je, EAC itaweza kuzalisha umeme wa pamoja kupitia sehemu za mto huo? Je shughuli za kiuchumi kama uvuvi, usafiri, utalii biashara ya mazao ya misitu zitaweza vipi kusimamiwa na Jumuiya kuhakikisha faida zinarudi kwa wanachi wa Kongo na wa jumuiya nzima kiujumla?

ZIADA: MSITU WA CONGO

Msitu wa pili kwa ukubwa duniani, msitu wa Congo unapatikana nchini DRC. Hata hivyo msitu huo ni mkubwa kiasi kwamba umeingia kwenye nchi zingine kama Cameroon, Jamhuri ya Afrika Ya Kati, Jamhuri ya Congo(Brazaville), Guinea ya Ikweta na Gabon. Msitu huu ni utajiri mtupu.

msitu wa mvua wa Congo
Msitu wa Congo

Katika msitu huo kuna fursa nyingi zikiwamo biashara ya magogo, madawa ya kutibu watu, mazao na wanyama, mbao, karatasi na bidhaa zote zitokanazo na misitu. Ukiwa kama mfanyabiashara ambaye sasa una uhuru wa kwenda kuwekeza DRC kirahisi, utaitumiaje fursa hii?

Sasa hayo ni baadhi ya mambo ambayo pengine ulikua huyafahamu kuhusu DRC. Mambo hayo kama yakifanyiwa kazi ipasavyo ndani ya @jumuiya basi ni wazi kutapunguza hali ya umasikini na kuimarisha amani kwa watu wa Kongo na kuimarisha uchumi wa Jumuiya nzima. Mapema mwaka 2021 jumuiya ya nchi za Afrika kwa kauli moja ilianzisha eneo huru la biashara barani (AfCFTA) ambapo nchi wanachama wanaweza kufanya biashara kwa uhuru bila ya vizuizi vya mipakani. Zaidi soma hapa chini

Jumuiya hii inatoa uhuru kwa wanachi wake kuishi na kufanya biashara popote ndani ya nchi wanachama. Jambo hili linatoa fursa kwa Wajasiriamali wa aina zote kuzurura na kutafuta masoko yao kirahisi. Ukiweza vema kutumia majukwaaa ya kimtandao kama websites, mitandao ya kijamii ujue unayo nafasi ya kuwafikia watu milioni 300 waishio ndani ya Afrika Mashariki. Sasa tuambie wewe mtu wa Teknolojia, website designer, mtaalam wa kutengeneza android app, mkulima, engineer nk, unataka ufaidike vipi hapa? Tuambie..

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER)5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

M-PESA LIPA NAMBA