Tag: uchumi

fahamu siri za kuweza kushawishi wateja katika biashara yako.

THAMANI vs GHARAMA, NAFUU IKO WAPI?

Ubora wa kazi una THAMANI kubwa sana kuliko GHARAMA za kuifanya kazi hio. Unaweza lipia mradi kwa milioni5, lakini usikupe matokeo yale ulijipangia mwanzoni. Pia unaweza lipa laki 5 ya mradi na ukapata matokeo mazuri zaidi. Ufanyeje?

Warren Buffet amewahi kunukuliwa akisema “Price is what you pay, value is what you get.” akimaanisha, “Gharama ndio unayolipa, thamani ndio unayopata”. Kifupi ni kwamba thamani ndio msingi wa bidhaa/huduma huku gharama ikiwa ni makubaliano ambayo yanatangulizwa na muuzaji.

Kujua tofauti kati ya Gharama na Thamani ni moja kati ya mbinu bora zaidi za kufanya Uwekezaji. Zaidi kuhusu uwekezaji tayari tumeshakuwekea makala kupitia link hii https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye Kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA” Ukimaliza hapo tuendelee..

Unaposhindwa kutofautisha kati ya Gharama na Thamani kama mfanyabishara unajiweka kwenye mtego wa kukosa wateja, kutoaminika kwa Wawekezaji wakubwa, Kupoteza points dhidi ya washindani wako kibiashara na mwisho kuiweka biashara yako katika majanga ya kudhoofika na hatimaye kufa.

Unawezaje kupata bidhaa zinazouzwa kwa gharama za chini kuliko thamani yake halisi?

Jibu ni kufanya tathmini kwa kutumia viwango vya bei ambazo ni tofauti kabisa na gharama zinazotangazwa sasa. Hapa unaweza kuangalia bei, miaka 3 iliyopita ilikuaje na miaka 3 ijayo itakuwaje.

Bwana Phil Town, ameweka zoezi la kufanya Tathmini makini kwa kupitia hatua nne alizoziita “Four M’s”. Tuzione chap chap:

1. MEANING: Hatua ya kwanza kabla hujawekeza katika bidhaa/huduma fulani lazima ujiridhishe kuwa bidhaa/huduma hio ina maana sana kwako. Ikiwa na maana utapata fursa ya kuichunguza na kuielewa vyema, na kujituma ipasavyo katika kufanya biashara hio.

2. MOAT: (Upekee ambao hauwezi kuigwa na wengine): Unapochagua bishara ya kuwekeza ama bidhaa/huduma, unatakiwa uifanye iwe katika mtindo ambao washindani wako hawawezi kukuiga. Mfano: Duniani kuna makampuni mengi tu ya vinywaji laini (soft drinks) lakini Coca cola ni moja na itaendelea kubaki hivyo.

Hivyo hebu tuambie hapa biashara yako ina utofauti gani ambao washindani wako hawawezi kuiga kamwe?

3. MANAGEMENT: Je wajua kuwa Chanzo kikubwa kwa biashara kufa ni watu wanaoiendesha? Hivyo unapofikiria kuwekeza kwenye biashara lazima eneo ya utawala na uendeshaji wa shughuli linasimamiwa na watu wenye Weledi, Waaminifu na wanaojali maisha ya biashara hio.

4. MARGIN OF SAFETY: Kama umeshajiridhisha na hizo hatua 3 zilizopita, sasa hebu tizama pia namna unaweza kuweka mtaji ama kununua hisa bila kupoteza pesa na uhakika wa pesa yako kurudi.

Kila biashara inahitaji kitu fulani ambacho kitaitofautisha na washindani wake wengine sokoni. Sasa mchakato wa kutafuta tofauti hizo inaitwa “Positioning”. Hii mbinu inaziwezesha biashara kukazia sehemu fulani ya soko/wateja ili kujiimarisha zaidi kwenye sehemu hio. Unafanyaje?

MBINU ZA KUFANYA POSITIONING:

1. KUPUNGUZA GHARAMA: Ukifanya uchunguzi vizuri sokoni hasa kwenye mitaa ambayo wanafanya biashara ya aina moja mf: Kariakoo kila mtaa una shughuli yake maarufu zaidi kama mtaa wa livingstone ni maarufu kwa vyombo vya ndani.

So ukijigundua kuwa upo kwenye aina hii ya biashara, mbinu bora hapo ni kupunguza gharama za bidhaa zako kwa kiwango kidogo kuliko washindani wako. Lengo ni kuhakikisha unakuwa na mzunguko wa haraka wa mauzo ya bidhaa/huduma zako kwa faida ndogo ili mzigo wako uishe mapema.

2. UBORA: Kama unataka kujitofautisha na washindani wako, basi mbinu bira na ya kuaminika ni kuhakikisha bidhaa/huduma zako ni za Ubora wa hali ya juu. Unapozingatia Ubora unajiweka kwenye nafasi ya kupata wateja wa kuaminika, wateja wa kudumu na wateja wa uhakika ktk biashara.

3. MAKUNDI YA KIJAMII (DEMORGRAPHIC): Baadhi ya biashara huamua kujihusisha na makundi fulani tu ya kijamii ili kujiletea faida zaidi. Mfano: kwenye TV na redio vinatengenezwa vipindi mahsusi kwa Vijana, watu wa makamu na watu wa dini fulani kwa siku zao. Umeshawahi fanya hii?

Mbinu hii inafaa sana pale unapoyapata makundi hayo karibu na eneo lako la biashara au watu wanaokufuatilia zaidi mtandaoni wakawa ni wanamna hio. Vinginevyo unajiweka kwenye hatari ya kukosa soko kubwa nje ya hao uliolenga kuwahudumia.

4. HUDUMA BORA: Huwa inatokea kwa baadhi ya biashara ushindani unakuwa mkubwa sana kiasi kwamba mbinu 3 tulizoziona awali haziwezi kufanya kazi. Yani watu wanashikana kooni haswa. Hapa ndipo mbinu ya kutoa Huduma Bora kwa wateja inapokuja kuleta tofauti.

Zoezi la kutoa Huduma Bora ni pana na linahitaji ubunifu mwingi. Na hii inatoa fursa kwa biashara kubuni namna nzuri ya kuhudumia wateja wake ili kuhakikisha wateja wanafurahia bidhaa/huduma na kuzidisha mauzo. Mfano: unaweza kuanzisha dawati la wateja kutoa maoni live ili waweze kuona mawazo yao yakifanyiwa kazi. Unaweza kuanzisha kurasa za mitandao ya kijamii ili kukusanya kero za wateja na kuzifanyia kazi vizuri. Pia unaweza kutengeneza mzunguko kwa wateja wako kushiriki kama mabalozi wa kuitangaza biashara yako kwa watu wengine. Unaionaje hii?

UNAWEZA VIPI KUDADAVUA NA KUWASILISHA THAMANI YA BIASHARA YAKO KWA MTEJA WAKO?

Tafiti zinaonyesha kuwa watu hawapendi kabisa kutangaziwa ama kulazimishwa kununua kitu hasa huku mtandaoni. Mfano: Tizama unavyopata kero pale unapoangalia vidio YouTube mara katikat linakuja Tangazo Ama pale unataka kufungua ukurasa fulani mara unafunguka ukurasa wa tangazo kwanza kabla hujafika pale ulitaka kwenda. Hio kero ndio inatakiwa ikufanye uitazame biashara yako katika jicho la Kitaalamu kwa kutatua changamoto na si la Kibiashara kwa kuuza Bidhaa/huduma yako.

Unapotoa Elimu katika namna ya Utaalam wa kutatua changamoto fulani, unamfanya mteja atake kuondokana na kero zinazomsumbua kwa kutumia Bidhaa/Huduma zako. Hii ni tofauti kabisa pale unapotaka kuuza bidhaa. Ukifanya hivyo hutatui changamoto bali unakuwa kero kwa mteja.

Thamani ya Biashara yako inaonekana katika kutatua changamoto za mteja wako na Urahisi wa kutumia bidhaa/huduma yako. Hivyo lazima uhakikishe kuwa unachokitangaza ni Ile Namna Bidhaa zako zinaweza kutatua changamoto fulani ya mteja kwa urahisi.

Pia lazima uhakikishe suluhu yako inakwenda sambamba na hisia za mteja wako. Kwa kuwa kitaalam watu hununua bidhaa/huduma kutokana na hisia walizo nazo muda huo. Mfano kuna watu watakwambia kuwa wakiwa na hasira ama furaha sana kwao huo ndo muda wanafanya shopping kubwa zaidi.

Mzazi anapotaka kununua keki ya birthday ya mwanae hanunui tu keki tamu, lazima pia ahakikishe keki hio inakwenda kum-suprise mtoto kwa muonekano wake wa kuvutia. Ni mbinu ya kihisia hapo inatumika. Hivyo unapotaka kuongeza Thamani ya biashara yako unatakiwa kuzingatia hilo pia.

Umejifunza nini kwenye makala hii ya leo? Tafadhali weka maoni au mtazamo wako katika sehemu ya comments hapo chini..

Vyanzo: https://www.forbes.com/sites/forbesfinancecouncil/2018/01/04/the-important-differences-between-price-and-value/?sh=133fd5c94237

https://www.weebly.com/inspiration/difference-between-value-and-cost/

https://yourbusiness.azcentral.com/different-types-strategies-business-1348.html

BANDO LAKO NI MTAJI

Imagine una ofisi yako (eneo la biashara) na pia unayo akaunti yako ya twita, Instagram au facebook. Lakini hujui namna ya kutengeneza mvuto kwa watu ili wakutafute, wakufollow, wakuamini na wafanye biashara na wewe. Unafanyaje?

Imagine hujawahi kutengeneza mahusiano ya kibiashara na followers wako, hata mmoja yani. Kuna muda unatamani biashara yako iwe kubwa lakini hujui mbinu gani unaweza kutumia ili kuhakikisha biashara yako inazidi kuwa Imara kila siku. LEO Nazungumza na wewe hapa.

1. CHANGAMKA: Kabla ya yote, fahamu kuwa biashara inafanyika vizuri katika mazingira yaliyojengwa kwa mahusiano imara, hivyo hebu tizama unahusiana vipi na watu waliokuzunguka na followers wako. Hili ni eneo pana ambapo unatakiwa ufahamu saikolojia ya watu wako hasa wateja na kujua namna ya kukabiliana nao positively. Maana mitandaoni kuna kila aina ya watu na tabia zao, kuna wenye kiburi, kuna wababe, wachechi, wajeuri, wanafunzi, wenye hekima, wapole, wenye lugha chafu na micharuko. Sasa jukumu lako ni kuwajua na kukabiliana nao bila kukwazana.

Humu mitandaoni wewe kama sio mtu maarufu basi hakikisha unakuwa mchangamfu kwa kadiri ya inavyowezekana. Kuwa “mchangamfu” haina maana uwe mwenye kiherehere, shobo au mtu wa kujipendekeza, lakini ujue namna kuchangia mijadala mbalimbali na kujihusanisha na watu vizuri.

2. KUWA MTAALAM: Kwenye biashara hili ni eneo muhimu sana, yani sawasawa na uti wa mgongo. Watu wengi hudhani biashara ni kuuza na kununua tu, ofcourse wako sawa. Hata hivyo ili biashara yako iweze kunawiri katika mazingira ya mtandaoni yaliyojaa ushindani wa kila aina, unapaswa kujua zaidi ya “kuuza na kununua”. Humu mtandaoni watu hukwepa sasa matangazo, hivyo “unapoweka tangazo lako hakikisha halionekani kama TANGAZO bali lionekane kama HABARI MPYA kwa yeyote anayesoma.”

Mtego ndo upo hapo. Lazima uwe mtaalam wa kuhudumia faida zinazotokana na bidhaa/huduma zako. Usiuze tu ukaishia hapo, hebu kuwa MLEZI wa mteja wako. Binafsi nina LIST ya wateja wangu ambapo huwa nawatumia updates mbalimbali kuhusu hali ya biashara na uchumi katika muktadha wa teknolojia BURE kabisa. Ungependa kuwa kwenye list hio?

3. FUNGUA WEBSITE: Kwa kasi ambayo teknolojia inakwenda nayo nina uhakika usingependa kupitwa na fursa lukuki zinazokoja na mapinduzi haya ya 4 ya viwanda yanayoendelea duniani. Fikiria, Kusini mwa Jangwa la Sahara kunakadiriwa kuwa na watumiaji wa internet zaidi ya milioni 400. Nchini Tanzania kunaripotiwa kuwa na watumiaji wa internet zaidi ya milioni 24 mpaka kufikia mwaka 2020.

Sasa kwa kutumia hilo Bando lako la internet, unalitumiaje kuwafikishia watu hawa bidhaa/huduma yako? Website ni kifaa (Digital tool) muhimu na mahsusi kwa kuwafikia watu wengi ndani ya muda mchache sana. Kwenye website unao uwezo wa kutoa huduma za kushauri na mafunzo nakdhalika. Zaidi unaweza kujua faida za kuwa na website kupitia link hii https://rednet.co.tz/website-inasaidia-vipi-kuimarisha-biashara-yako/ yenye kichwa WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?

Kuweza kupata website yako wasiliana nasi kupitia namba 0765834754 au email info@rednet.co.tz ili tukusaidia kutatua changamoto zinazokukabili. USIBAKI NYUMA.

4. KUWA MKWELI/TABIRIKA/AMINIKA: Moja kati ya eneo ambalo linawapa changamoto wafanyabiashara wengi ni hili la kuwa mkweli. Wateja wengi huwa wanakwazika sana wanapofanya kazi na wafanyabiashara ambao si wakweli. Hiki ni kitu kibaya sana na hata wewe usingependa kikutokee.

Unapojijenga kwa kuwa mkweli unatengeneza mazingira ya kuaminika ambayo yatakufanya upendwe na watu na wao waweze kufanya biashara na wewe bila wasiwasi. Hata wewe mfanyabiashsra, siku ukiwa mteja usingependa kukutana na mtoa huduma ambaye si mkweli/mwaminifu, si ndio?

Bando lako ni muhimu sana katika uendeshaji wa biashara yako katika zama hizi za kidijitali. Lazima ujue namna nzuri ya kuendesha akaunti yako ya mtandao wa kijamii ili ilete tija kiuchumi katika biashara yako. Unahitaji mtu wa kuendesha akaunti yako? Wasiliana nasi mara moja.

UNAWEZA VIPI KUKABILIANA NA HASARA KATIKA BIASHARA YAKO MWAKA HUU 2021?

Huwa ni kawaida kwa biashara kupata hasara, hasa zile changa/zinazoanza. Lakini inapotokea biashara inapoteza pesa nyingi kuliko inavyoingiza, Juhudi za dhati zinahitajika kujinasua kwenye tabu hio.

Hasara inaweza kuwa katika namna ndogo kama kukosa dili fulani ulikua unafukuzia, kupoteza mteja, kupoteza vifaa vya kazi mpaka hasara kubwa kama kushindwa kulipa mahitaji ya biashara kama bili za umeme, mishahara na gharama za mawasiliano. Hali hii ilivyokutokea ulifanyaje?

Hata hivyo, Mjasiriamali bora huwa hatambuliwi kwa uwepo wa hasara katika biashara, bali Ule uwezo wake wa kudili na mazingira yanayoleta hasara mpaka kuhakikisha biashara inatamalaki kwa faida kutoka kwenye kivuli cha Hasara na majanga. Jinsi ya kupenya kwenye nyakati ngumu, ndipo anapopatikana mjasiriamali bora zaidi. Wahenga walishasema “Bahari tulivu haizalishi nahodha hodari.” Kumbe basi ubora upo kwenye Mawimbi, Hofu, Mkazo(pressure), Wasiwasi, Hasara na Woga.

Kwenye mazingira hayo ndipo Tuzo ya Ubora inapopatikana, Ndipo uaminifu kwa mteja unapojileta ndipo Uchumi unapotengeneza misingi yake na ndipo wateja watakapoongezeka kama sisimizi waonapo sukari. Lakini lazima kwanza ujue unatakiwa ufanye nini unapokuwa katka mazingira kama hayo? Na utajuaje kuwa upo kwenye mazingira hayo hatarishi? Lazima kichwa chako kiwe wazi kwanza kwanza kabla hatujasonga mbele.

UTAJUAJE KUWA BIASHARA YAKO INAJIENDESHA KWA HASARA?

Kiufupi Biashara kujiendesha kwa hasara ni pale matumizi yanapokuwa makubwa kuliko fedha inayoingia. Haya matumizi sio lazima yawe mpya, yanaweza kuwa ni yale yale kama bili za umeme, maji, mtangazo, mishahara n.k

Mara nyingi matumizi hayo yako hivyo hivyo (constant). Japokuwa mara nyingi fedha inayoingia huwa haitabiriki hasa kwa bishara inayoanza. Hii inaweza kusababishwa na biashara kutokuwa na wateja wa kudumu, mabadiliko katika mahitaji na uelekeo wa masoko pamoja na ujuzi katika kufanya matangazo na mauzo.

Hata hivyo hali hii haipaswi kuwa ya kudumu. Mara nyingi huwa ni ya mpito tu. Lakini kama biashara yako mara kwa mara inajikuta ikijiendesha kwa hasara, my friend unatakiwa ujitafakari upya jinsi unaendesha biashara. Tafuta ushauri wa kitaalam na ikibidi usimamizi wa karibu(mentorship) kutoka kwa wataalam mbali mbali katika maswala ya biashara na usimamizi.

Hizi hapa ni Dalili za biashara inayojiendesha kwa hasara:

•Biashara haina pesa za kulipia gharama za uendeshaji (umeme, maji, mishahara, malighafi/raw materials, matangazo nk). Ukiona umefika hali hii jua ni Red light hio. Jipange.

•Salio lililopo bank/mobile-money ni 0 au negative (una madeni), na bahati mbaya hujui namna gani utaweza kupandisha salio lako kufikia mahali pa kujimudu. Hapa yani ujue kuwa umeshaishiwa mbinu. Rudi vitabuni/mtandaoni, soma, jirekebishe na waone wataalam wakupe direction mpya.

•Hauuzi kwa kiwango kile ambacho kimepangwa kwenye Business Plan. Hii Business Plan ni muhimu sana kuwa nayo kama mfanyabiashara makini. Hii ndio inabeba mipango na malengo yote ambayo biashara inatakiwa kuifikia ndani ya muda uliowekwa (2yrs, 5yrs, 10yrs etc).

Muhimu sana hio document kuwa nayo. Ukihitaji tafadhali wasiliana nasi kupitia mawasiliano haya 0765834754 au info@rednet.co.tz

Biashara za kisasa zinafanywa kwa kuzingatia Ujasusi wa Kiuchumi kwa sana. Na hakuna Ujasusi usio na mipango. Na mipango utaikuta katika Business Plan.

Tuendelee, Sasa unapokuwa kwenye mazingira hayo ya hasara, kuna namna nyingi ambazo unaweza kudili nayo. Leo hii tutadiscuss mbinu 9 za kukabiliana na hasara pindi inapotokea kwenye biashara yako. Namba 7 itakushangaza sana.

1. JIANDAE: Huna haja ya kuweka mipango mingi ya namna ya kukabiliana na mazingira ya hasara, hata hivyo jambo la muhimu zaidi ni Kujiandaa kisaikolojia kwamba Hasara ipo kwenye biashara na inaweza kutokea muda wowote. Matarajio yako yasiwe makubwa kuliko uhalisia. Hapo utafeli.

Kama unadhani kuwa mambo yatakwenda sawia na mipango yako uliyoiweka kukabiliana na hali ngumu, basi siku mambo yakienda tofauti unaweza kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kuliko vile ingetarajiwa. Keep calm and let yourself soar through the storm, like an eagle in the air.

2. TAFUTA NAMNA YA KURUDISHA NGUVU: Nyakati ngumu na hasara kwenye biashara huumiza sana moyo, hudidimiza juhudi na kukatisha tamaa. Lakini kamwe nyakati hizi hazidumu, wanadumu watu imara. Hivyo yakupasa kuwa imara mda wote unakiwa mjasiriamali. Unaweza kujipa mapumziko, likizo ama kujiweka mbali na mazingira ya kazi kwa muda huku ukitafakari kwa kina nini kilikukwamisha na hatua gani unaweza kuzichukua ili kukabiliana na changamoto hizo. Matumizi ya vileo si mazuri hapa kwenye jambo hili.

3. USIAMUE KWA HISIA: Ukiwa kwenye hali ya mkazo huku ukiandamwa na hasara katika biashara, mara nyingi unaweza kujikuta ukiwa na hasira, huzuni, woga na hofu. Huu si wakati wa kufanya maamuzi hasa yahusuyo biashara yako. Tulia na tafuta suluhu kupitia watalaam au marafiki wema.

4. KUWA NA MTANDAO SAIDIZI: Hapa nazungumzia jumla ya watu wote unaokutana nao kila siku katika shughuli za kibiashara na kazi. Hawa watu wanapaswa wawe wasaidizi wako pale utakapowahitaji. Unapaswa kuwa na watu ambao ni assets na uepuke wale ambao ni liabilities (mzigo).

5. TATHMINI HALI YAKO: Hasara ni funzo moja zuri sana katika maisha ya biashara imara. Ni nafasi yako kujifunza wapi ulikosea na nini unapaswa kufanya ili wakati ujao hasara ipungue au iondoke kabisa biashara izalishe faida tu. Utumie vizuri wakati huu kufanya uchambuzi yakinifu.

6. USIISHI KWENYE HASARA: Katika historia hakuna mtu ambaye alifanikiwa sana na hakupata hasara. Kila shujaa unayemjua, pamoja na mafanikio yake, lakini wakati fulani alishapata hasara. Kinachomfanya mtu kuwa shujaa ni uwezo wa kunyanyuka na kutoruhusu hasara kuathiri utendaji.

7. TENGANISHA HASARA YA BIASHARA NA UTENDAJI WAKO BINAFSI: Ni ngumu mno kutenga mambo ya kibiashara na maisha binafsi. Kama biashara yako imepata hasara, ni biashara sio mkeo nyumbani au watoto au wewe binafsi, ndugu au marafiki. Usijilaumu wala usimlaumu mtu. Focus na biashara na hakikisha utendaji wa biashara hauathiri amani na utulivu ukiwa katika mazingira ya nje ya kazi. Watu wengi wamejikuta wakiingia katika migogoro mikubwa katika ndoa, familia na marafiki kutokana na kuchanganya biashara na undugu. Ni vitu visivyochangamana asilani na umakini mkubwa sana unahitajika kiuweledi katika kusimamia misingi ya kibiashara katika mahusiano ya familia.

8. ELEWA MAZINGIRA UNAYOJIHUSISHA NAYO: Mbinu bora zaidi ya kumshinda adui ni kumjua vizuri adui huyo. Kamwe huwezi kupigana na adui ambaye humjui sawia. Hivyo chukua muda kujua kwanini unapata hasara na ufanyeje ili hatimaye uweze kupata faida.

9. JIFUNZE: Vyovyote itakavyokuwa, maisha lazima yaendelee. Lakini kuendelea kujifunza ndio jambo muhimu ambalo unapaswa kulifanya mara zote. Maisha ya mfanyabiashara ni mfululizo wa mafunzo yasiyokwisha. Hivyo usikaze mishipa ya shingo, jifunze kila inapobidi ili kujiimarisha.

Pamoja na yote, kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na hali ngumu na hasara. Hata hivyo mbinu ulizozipata leo zimethibitishwa kitaalam katika kuokoa biashara yoyote katika janga la hasara. Share, reply na Retweet ili madini haya yawafikie wafanyabiashara wengi zaidi.

Pitia makala hizi hapa ambazo zinarandana na somo ulilolipata hapa leo. Zitakusaidia sana:

  1. https://rednet.co.tz/kwanini-uitangaze-biashara-yako/ yenye kichwa “KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?”
  2. https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA”
  3. https://rednet.co.tz/biashara-yako-inaweza-vipi-kuwa-taasisi-imara/ yenye kichwa “BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA?”
  4. https://rednet.co.tz/website-inasaidia-vipi-kuimarisha-biashara-yako/ yenye kichwa “WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?”