Tag: uchaguzi2020

FAHAMU KUHUSU MAGEUZI YA ICT KATIKA UWANDA WA SIASA

Ama kwa hakika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA/ICT) imeendelea kushika kasi katika nyanja mbalimbali za kijamii. Biashara zinazidi kuimarika, Jamii inaunganika, uchumi unainuka na Siasa inapata sura mpya. Muunganiko wa Siasa na Teknolojia unagusa michakato, wasifu za watu, jitihada za kujinasua katika changamoto mbalimbali pamoja na harakati zingine za kijamii zinazohusidha matumizi ya huduma za intaneti na ICT. Katika fumbo hilo wataalamu wa siasa wakagundua njia za kuboresha mifumo ya kisiasa na kuratibu ushawishi wao katika jamii kirahisi zaidi.

Sasa leo tuone maeneo 5 muhimu ambayo ICT imekuwa chachu ya maendeleo katika uwanda wa kisiasa barani Afrika, hususan Kusini mwa jangwa la Sahara:

1. KUBADILI TAWALA

Katika kipindi cha mwaka 2009-2012 katika nchi za kiarabu kulitokea kitu kilichoitwa “Vuguvugu la Kimapinduzi” au “Arab Spring” ambapo serikali nyingi za kiarabu zilijikuta zikipinduliwa kwa nguvu ya wanachi. Kufikia mwaka 2012 dunia ilikua na 61% ya nchi 195 ambazo ndizo zilikua zilitambulika kwa kufanya Chaguzi za Kidemokrasia. Hio ni sawa n nchi 118. Lakini bada ya hapo nchi zinazojiendesha kidemokrasia ziliongezeka kufuatia maandamano nchini Moldovia mwaka 2009, Tunisia (2010/11, Misri (2011) na Iran (2009 mpaka sasa) Mapinduzi hayo ya kubadili tawala hasa zile za Kiimla yalipangwa na kuanzishwa kwa msaada wa kiteknolojia huku mtandao wa Twitter ukihusika kukusanya na kuhamasisha watu kuanzisha vuguvugu la maandamano katika nchi za kiarabu. Hawa waarabu walijua kwelikweli kutumia mitandao.

2. KUTUNGA NA KUENDESHA SERA

Hivi sasa hakuna mtu asiyejua au kutumia mfumo wa malipo ya kiserikali wa eGovernment. Sasa unajua mfumo huo ulianzia wapi? Achana na siasa kabisa. Kwanza tuone hio eGovernment ni kitu gani? Huo ni mfumo wa matumizi ya ICT katika ofisi za umma inazohusisha mifumo ya kiutawala ya kiuweledi inayotumia maarifa na ujuzi wa computer na huduma za intaneti ili kuhakikisha huduma za kijamii zinaimarika na kuchochea demokrasia na nguvu ya ushawishi katika chaguzi za kisiasa na sera za jamii. Umeona siasa imerudi tena apo Wahenga wanakuambia, “Siasa ni kama maji tu, usipoyaoga utayanywa.” Wahenga bwana. Sasa mifumo hii ya eGovernance hutumiwa na taasisi za serikali katika kuhudumia Mashirika mengine ya kiserikali (G2G) mfano Polisi na TRA, Mashirika ya Kiserikali kwa wanachi(G2C) mfano LUKU na Mashirika ya Serikali kwa Biashara (G2B) mfano TRA na Wafanyabiashara. Hii sera ys kuanzishwa kwa mifumo ya eGovernance japo imeanzishwa kwa sera za kisiasa lakini imeleta mapinduzi makubwa sana katika zoezi la ukusanyaji wa mapato na utunzaji wa rekodi za mauzo na manunuzi.

3. SIASA KAMA SIASA

Japokuwa kwenye nchi nyingi haswa zile za kidikteta kumekuwepo na makatazo ya kufanya siasa za wazi, Matumizi ya Teknolojia na mitandao ya kijamii yamewezeshwa kufanyika kwa siasa pasi na haja ya kukusanya watu viwanjani. Matumizi ya mifumo ya computer na mitandao ya kijamii wamewsrahisishia Wanasiasa kutengeneza akaunti zao zinazowapa fursa ya kukutana na wananchi na kufanya siasa kirahisi sana. Hata hivyo hii bado ni changamoto kwa nchi nyingi zinazoendelea kama Tanzania ambapo watumiaji hai wa huduma za internet walikua ni 23.14milioni sawa na 38.7% ya wananchi wote. Pia watumiaji wa mtandao wa facebook wamefikia 4.27milioni. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tovuti ya http://internetlivestats.com kufikia mwezi December, 2019. Sasa namba hizi zinakupa picha gani katika uwanda wa siasa nchini? Inaonekana kuwa bado watumiaji hai wa mitandao ya kijamii ni wachache kuwakusanya mtandaoni kwa wakati mmoja, hivyo kufanyika kwa siasa katika mitandao ya kijamii inaonekana bado ni mtihani kwa wanasiasa barani Afrika hasa nchini Tanzania. Licha ya changamoto hizo, bado teknolojia inao mchango wake katika siasa wakati wa kufanya kampeni na uchaguzi ukizingatia Haba na Haba hujaza kibaba. Hivyo katika kampeni za kisasa, ili mwanasiasa apate kuingia katika mfumo wa utoaji wa maamuzi wa Taifa (Legislative level). Hana budi pia awe na ushawishi wa kisiasa katika mitandao ya kijamii. Huko ndipo unakutana na wanachi kirahisi na kusambaziana taarifa mbalimbali kwa wepesi zaidi. Kama afanyavyo Mh. Hamis Kigwangwala tu katika mtandao wa twitter, interractions za mara kwa mara muhimu nyie.

4. ONLINE VOTING (e-Voters System)

Kama ulikua hujui basi mwaka 2005 nchi ya Estonia iliweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza duniani kutumia mfumo wa kimtandao wa upigaji kura (e-Voters System)na kwanzia hapo mfumo huo umekuwa ukisambaa katika nchi na maeneo mbalimbali duniani. Mfumo huu unahusisha sehemu 3 ambazo ni Mpiga Kura, Mamlaka za Usajili na Watu wa Kuhesabu Kura ambao wote hapa sasa hufanya kazi katika mifumo maalum ya kuhakikisha kura zinapigwa kimtandao na kwa usahihi na usalama wa hali ya juu. Hapa bwana usipokua makini wadukuzi wanaweza kupiga tukio uchaguzi ukaharibika ndani ya dakika kadhaa tu.

KWANINI ONLINE VOTING SYSTEM?

Wakati mfumo huu unatengenezwa na kuzinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Estonia, lengo kuu lilikua ni kuhakikisha shughuli za uchaguzi zinafanyika kwa haraka, wepesi na kwa usahihi zaidi bila kuathiri shughuli zingine za kiuchumi. Lakini leo hii ambapo dunia inapitia katika changamoto ya Ugonjwa wa #COVID19, ipo haja na hitaji kubwa la matumizi ya e-Voters Systems katika chaguzi za kisiasa sehemu mbalimbali duniani. Wakati mamlaka zikikataza mikusanyiko ya watu, uvaaji wa barakoa, kutogusana na kuzingatia social distance (sijui kiswahili chake kwa kweli), hakuna wakati sahihi wa kuanza kutumia e-Voters Systems kama sasa. Wanaharati na wananchi kwa ujumla hatuna budi kupigia chapuo mgumo huu uanze kutumika mara moja ikiwezekana kuanzia uchaguzi wa Octoba 2020 sio tu kuhakikisha tahadhari dhidi ya Coron zinachukuliwa, lakini zaidi kuongeza Usahihi na Usalama wa kura katika zoezi la Uchaguzi.

5. MATUMIZI NA UCHAMBUZI WA DATA

Teknolojia kwa mapana yake imekua nyenzo muhimu sana katika kukusanya, kuchakata na kuhifanyi data mbalimbali ambazo hutumika maeneo kadha wa kadha katika kufanyia Tafiti, Kupima mwenendo wa mwanasiasa au chama pamoja na kuhifadhi kumbukumbu. Sasa matumizi ya mitandao kama Facebook, Instagram, Twitter pamoja na tovuti/blogu za wanasiasa/vyama, zimekuwa zikichochea sana juhudi na harakati zao katika kuhakikisha wanaboresha nafasi na ushawaishi wao wa kisiasa katika jamii wanazohudumu. Teknolojia imezidi kuwa muhimu sana katika uga huu wa kisiasa.

BONUS POINT:

Matumizi madogo ya teknolojia (hafifu) yameleta madhara makubwa sana katiks mifumo ya siasa hasa barani Afrika. Hizi vita za wenyewe kwa wenyewe, vurugu na wakati mwingine mauaji katika mchakato wa uchaguzi ni matokeo ya siasa mbovu na ufinyu wa teknolojia usiotakiwa.

Pia kuna hizi makala hapa tayari tumekuandalia ambazo zitakupa mwanga zaidi katika kufanya maamuzi na kutumia teknolojia ili kuleta tija zaidi. Gusa link kisha makinika:

  1. https://rednet.co.tz/fanya-maamuzi-sahihi-katika-muda-sahihi/ yenye kichwa “FANYA MAAMUZI SAHIHI KATIKA MUDA SAHIHI”
  2. https://rednet.co.tz/ifahamu-nguvu-ya-mitandao-ya-kijamii/ yenye kichwa “IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO”
  3. https://rednet.co.tz/biashara-yako-inaweza-vipi-kuwa-taasisi-imara/ yenye kichwa “BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA”