Tag: teknolojia za uvuvi

FAHAMU KUHUSU UVUVI NA BIASHARA YA SAMAKI BARANI AFRIKA

Japokuwa inafanyika zaidi maeneo ya vijijini na katika hali duni ya zana za utendaji, elimu pamoja na teknolojia, sekta ya uvuvi na biashara ya samaki bado inahangaika katika kujiboresha huku ikifichwa katika kivuli cha shughuli za Kilimo na Ufugaji. Mbaya zaidi sekta ya uvuvi na biashara ya samaki bado haijapewa umuhimu inayostahili barani humo. Zaidi sekta hio hutoa chakula cha kuwalisha watu zaidi ya milioni 200 barani humo na nje ya bara la Afrika. Leo sasa fahamu kuhusu Uvuvi na biashara ya samaki barani Afrika. Twende mpaka mwisho.

Benki ya Dunia inaripoti kwamba shughuli za uvuvi na biashara ya samaki huchangia moja kwa moja dola za kimarekani $24 bilioni katika uchumi wa Afrika kwa ujumla, ikiwakilisha 1.3% ya jumla ya pato la ndani (GDP) la Afrika katika mwaka 2011. Vile vile sekta hio imezalisha ajira kwa zaidi ya watu milioni 12 ambapo 58% kati yao ni wavuvi na 42% wanajihusisha na kuandaa samaki waliovuliwa kabla ya kuwapeleka sokoni. Tanzania peke yake, sekta ya uvuvi imetoa ajira kwa watu 183,000 mpaka kufikia mwaka 2014 (chanzo: Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi) Ikionekana kwamba shughuli za uvuvi hufanywa zaidi na wanaume, 59% ya shughuli za kuandaa samaki kabla ya kuwaingiza sokoni hufanywa na wanawake.

Ukiachana na faida za samaki kama chakula katika kupatikana kwa virutubisho muhimu kama vitamini, protini na mafuta, zaidi, sekta ya Uvuvi na biashara ya samaki inachangia sehemu muhimu sana katika kuendesha maisha ya watu haswa vijana ikiwa watachukua angalizo katika fursa zilizopo kwenye sekta hio.

Changamoto; Je, kuna fursa zipi katika kufanya shughuli hii ya uvuvi na biashara ya samaki katika kukuza uchumi? Teknolojia ina mchango gani katika kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja kupitia setka hii?

Tishio kubwa katika shughuli za uvuvi na biashara ya samaki ni athari zinazotokea katika mazalio ya samaki baharini, mtoni, ziwani au kwenye mabwawa. Umoja wa Mataifa na nchi  jumuishi duniani zimeingia uwoga juu ya upatikanaji wa hazina ya samaki katika soko la dunia. Shirika linaloshughulikia maswala ya Chakula duniani, FAO, limetabiri kwamba zaidi ya 70% ya aina (species) za samaki zinakaribia kuangamia au zimevunwa sana ambapo aina za samaki kama Tuna, Swordfish, Haddock na Flounder zipo katika tishio la kuangamia. Zaidi, uvuvi unaotumia chandarua au baruti huweza kusababisha kunaswa au kuuwawa kabisa kwa samaki na viumbe wengine wa baharini ambao hawajapangwa kuvuliwa kama ngasa, pomboo na papa.

Hata hivyo, shughuli za uvuvi zina faida gani katika maisha ya mwanadamu ikijumuisha?

  1. CHAKULA;  Samaki ni chanzo cha vitamini na protini katika lishe haswa ya mwanadamu ambapo madaktari na wadau wa sekta ya afya hushauri ulaji wa nyama nyeupe mfano samaki zaidi katika mlo. ulaji wa samaki kwa wingi huchochea ukuaji bora wa afya ya akili pamoja na wingi wa protini katika nyama hio huku ikiwa na kiasi kidogo cha lehemu (cholesterol) zaidi kuliko nyama nyekundu mfano ng`ombe, mbuzi na kadhalika.Ripoti zinaonyesha kwamba wakazi wa nchi za ukanda wa bahari ya Pacific peke yake hupata zaidi ya 25% na 69% ya protini za wanyama wanaokula kila siku kutoka katika samaki. Hii imepelekea shughuli za uvuvi na biashara ya samaki kukua kwa kiasi kikubwa kama shughuli rasmi ya kiuchumi ambayo imeajiri watu takribani milioni 200 dunia nzima na ikizalisha pato la dola za kimarekani zaidi ya 80 bilioni kwa mwaka.
  2. UKUAJI WA UCHUMI; Sekta hii ya uvuvi inachangia kwa kiasi kikubwa sana katika ukuaji wa uchumi barani Afrika mpaka dunaini kote ambapo watu zaidi wa milioni 200 wamejipatia ajira kupitia sekta hio. Nchini Uganda kwa mfano, uvuvi wa ziwani umekuwa na thamani ya zaidi ya dola $200 milioni  kwa mwaka ikiwa ni mchango wa 2.2% katika pato la taifa (GDP) la nchi hio. Vile vile watu zaidi ya 135,000 wamepata ajira kama wavuvi katika sekta hio na wengine 700,000 zaidi katika mchakato wa kuandaa samaki kabla hawajafikishwa sokoni na hivyo kuzalisha zaidi ya dola $87.5 milioni kama mapato ya biashara za nje ya nchi (exports earnings). Hapa miundombinu ya barabara na reli ina mchango mkubwa sana katika kuhakikisha kitoweo hiki kinamfikia mlaji kikiwa katika ubora wa hali ya juu. Kufahamu zaidi kuhusu mchango wa miundombinu pitia makala hii hapa;
  1. Vile vile nchini Tanzania kupitia katika mabwawa, maziwa, mito na bahari vilivyomo nchini humo, sekta ya uvuvi na biashara ya samaki imetoa ajira za moja kwa moja kwa watu takribani 183,800 na wengine zaidi ya 4,000,000 wakijihushisha kama watengenezaji wa vyombo vya uvuvi (ngalawa, boti, ndoano, neti n.k), waaandaaji wa samaki kabla hawajafikishwa sokoni, wachuuzi na wafanyabiashara wa samaki wa jumla na rejareja. Sekta hii ya uvuvi na biashara ya samaki inawapatia watu kipato cha fedha za kigeni, pamoja na kitoweo kwa watu waishio pwani ya bahari ya hindi pamoja wa walaji wa samaki kutoka sehemu zingine katika nchi hio ambapo sekta hio huchangia katika pato la taifa takribani 2.4%. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi katika mwaka 2016.

Kiujumla, mpaka kufikia mwaka 2001 uta fahamu kuhusu Uvuvi na biashara ya samaki barani Afrika katika masoko ya kimataifa ilikuwa na thamani ya dola $2.7 bilioni ambayo ni 5% ya jumla ya thamani ya sekta nzima ya uvuvi na biashara ya smaki duniani ambayo ni dola $56 bilioni. Kwa mujibu wa shirika la FAO, bidhaa za samaki zimejumuisha zaidi ya 10% ya jumla ya biashara za kimataifa (exports) katika nchi 11 barani Afrika.

Sasa Baada ya kuyajua Hayo Yote, Kwanini Ufanye biashara hii ya Uvuvi na samaki?

Mwaka 2019 watumiaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania waliongezeka kufikia milioni 23, ongezeko la watumiaji takribani milioni 1 kutoka mwaka jana 2018. Vile vile watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi wamefikia takribani milioni 20 hadi kufikia mwaka huu 2019. Hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.

Hivyo kupitia ripoti hio ya TCRA mfanyabiashara anaweza kuhamishia shughuli zake kupitia simu mkononi na simu janja (smartphones) katika kuhakikisha biashara yake inawafikia watu wengi zaidi katika muda mfupi kwa njia ya Teknolojia. Hata hivyo mfanyabiashara anaweza kutengeneza majukwaa ya kimtandao kama tovuti za kibiashara (online shops na ecommerce websites) ambayo anaweza kuuza bidhaa zake za samaki kirahisi katika masoko ya ndani na hata yale ya kimataifa kwa gharama nafuu zaidi kuliko ulivyokua hapo kabla.

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni

Kwa kutambua hilo, biashara ya mtandaoni imekuwa ikizidi kufanikiwa sana nyakati hizi huku ikichochewa na maboresho katika miundombinu ya uchukuzi na usafirishaji. Hivyo ni muhimu kufungua tovuti rasmi ya biashara yako ili kuipa utambulisho usio na shaka ukiwa mtandaoni. Vilevile ni muhimu kufungua akaunti za mitandao ya kijamii ili kusudu uzidi kujiweka karibu na wateja wako na kujua namna nzuri ya kuwahudumia.

Link zifuatazo zitakusaidia sana uweze fahamu kuhusu Uvuvi na biashara ya samaki barani Afrika kupitia mtandaoni iwe na mafanikio zaidi na zaidi:

  1. WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?
  2. KWANINI NI MUHIMU KUWA NA TOVUTI RASMI YA BIASHARA YAKO?
  3. IFAHAMU NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO

Je umepata nini katika mada ya leo katika ku fahamu kuhusu Uvuvi na biashara ya samaki barani Afrika?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

Kwanini uwe na website ya biashara yako?