TEKNOLOJIA YA SEO INA MSAADA GANI KATIKA BIASHARA ZA MTANDAONI?
Je, biashara yako ina uwezo wa kujiendesha hata kama haupo ofisini au pale unapofunga mlango wa ofisi? Kama jibu ni HAPANA, basi wakati wa kuhamisha biashara yako mtandaoni ni SASA kwa sababu Teknolojia haikusubiri wewe ndugu. Leo unapojiuliza teknolojia ya SEO ina msaada gani katika biashara za mtandaoni? majibu yote muhimu utayapata hapa. Cha kufanya, Fuatana nasi mpaka mwisho wa makala hii.
Imagine wateja wako wanaweza kufanya shopping wakiwa huko huko makwao, wengine wanasoma makala zinazotatua changamoto mbalimbali zinazowakabili na wengine wamepata mawasiliano yako mtandaoni. Yote hayo yanafanyika wewe ukiwa safarini, nyumbani, shambani au ukiwa na mishe zingine nje kabisa ya mtandao.
Faida ni nyingi sana ukiwa unafanya Online Business: Yani ukishakuwa na website inayofanya kazi sawia, ukawa na accounts za mitandao ya kijamii zinazoitambulisha biashara yako kila siku, hapo unafika kwenye hatua ambayo Internet inakufanyia kazi, na sio wewe kuwa Mtumwa wake.
NINI KINAKWAMISHA WATU WENGI SASA?
Watu wengi hudhani kuwa biashara za mtandaoni ni rahisi tu. Kwamba TCRA wameripoti kuwa kuna watumiaji wa internet milioni 29 kufikia October2021, so ukipost biashara yako itawafikia watu milioni29 chap. NO! Maisha si rahisi kiasi hiko asee!
Hii ni kwasababu miundombinu ya kimtandao (websites, blogu na mitandao ya kijamii) imetengenezwa katika namna ambayo inaheshimu Algorithms (mtiririko rasmi) fulani wa maneno, taaluma, mijadala, picha na mahusiano ili kuongeza ufanisi. Ndio maana tunasema kila siku Fuata Ushauri wa kitaalam.
Algorithms hizo huchochewa na mfumo wa kurahisisha utafutaji wa taarifa mtandaoni ujulikanao kama S.E.O (Search Engine Optimization). Mfumo huu huchukua links na maneno(keywords) yanayotumika zaidi katika blogu, websites na social networks na kuyaweka kwenye injini za matafuto kama Google na Bing.
Hivyo, kama unajua ama hujui, chochote unachokiandika sana katika social networks, blogs na websites huchukuliwa na kuwekwa katika Google na Bing. Lakini sio kila kitu unachokitafuta google utakipata kikiwa katika nafasi za juu pale google, Hapana, mambo hayaendi hivyo.
Kuna taarifa ukiitafuta utaipata kutoka kwenye biashara fulani ikiwa juu kabisa ukurasa wa mbele pale google. Taarifa hiohio pia unaweza kuipata kwenye blogu/website ambayo ipo ukurasa ya pili, wa tatu au wa 10.
Ubaya ni kwamba mteja hatatafuta jina la blogu/website yako, bali ataandika changamoto anayotaka kukabiliana nayo au kuhusu taarifa anayotaka kuitafuta mtandaoni. Mfano huandika kupitia google kutafuta “kirefu cha TEHAMA” “Biashara ipi ina faida zaidi Tanzania?” “Siri ya kuwa tajiri Afrika” “Mbinu za kufanikiwa kimaisha/kibiashara” “laptop za bei nafuu Tanzania“, “viatu vikali“, “Faida za TEHAMA“, “Faida za Website” “nyimbo za bongo fleva 2022”, “Laptop za bei nafuu zinapatikana wapi?” “Faida za kilimo cha mananasi/tikitimaji” “Chakula kitamu zaidi Tanzania” nakadhalika.
Sasa, kupitia maneno hayo ya S.E.O umegundua nini?
Ngoja nikwambie kitu, Kama unafanya biashara mtandaoni, zingatia maneno ambayo yanatumiwa zaidi na watu wengi au yanayotafutwa zaidi na wateja katika Industry yako. Jiulize, kama wewe ndo ungekuwa mteja unatafuta kujua kuhusu bidhaa/huduma flani, ungeandika nini pale Google?
Sasa hayo maneno ambayo ungeyaandika google ndio chambo ambayo unapoyatumia mara kwa mara katika blogu/website/social media yako, basi unajiweka kwenye nafasi ya kupatikana kirahisi zaidi pale mteja akitaka kutafuta kuhusu huduma/bidhaa zako. Zingatia sana hilo.
Na hio ndio SIRI ambayo wengi wanaojiita “Wataalam wa SEO” hawatakwambia kuhusu teknolojia ya SEO ina msaada gani katika biashara za mtandaoni. Kuna watu hawaoni sababu ya kuwa na Website/Blog kwasababu vitu hivyo HAVIWAINGIZII pesa direct.
Kuna mmoja nilifanya naye nae kazi akaniambia kilichomkuta mwaka 2018, “Bwana mi nilishawahi kuwa na website ila mwaka ule mzima yani haikunipa hata mia, na niliilipia mnaita ‘Hosting Fee’ sijui. Sikuwahi kuona umuhimu wake, so nikaachana nayo”.

Najua hili hata wewe unalihofia Kwanza fahamu haya yafuatayo:
Kuwa na website hakukufanyi kupata wateja wengi kama hutafanya yafuatayo ili ufahamu teknolojia ya SEO ina msaada gani katika biashara za mtandaoni:
1. Hujatengeneza account ya Google Map: Zamani Google walikuwa wakitumia Application ya Google My Business ili kuwarahisishia wafanyabiashara waweze kuunda profiles zao na ziweze kupatikana kirahisi mtandaoni. Lakini baadaye waliona App ya Google Map inao uwezo wa kubeba taarifa zote muhimu, hivyo App ya Google My Business ikafikia mwisho wake hapo. Stori nzima ipo hapa. Google Map sasa huifanya biashara yako iweze kusajiliwa, kutambulika na kupatikana rasmi na kirahisi katika mtandao wa Google. Yani apa unatengeneza Profile ya biashara yako direct na kumruhusu mteja aweze kuona mpaka mahali biashara yako ilipo.

2. Hujaunganisha blog/website yako na huduma za Search Console: Hii Search Console kazi yake kubwa ni ku-crawl, yani kukusanya taarifa zote za website yako kama huduma/bidhaa unazohusika nazo, links za Menu (Home, contacts etc) Mada unazoziweka, mijadala na maneno unayotumia humo Kutengeneza links ziitwazo SITEMAPS na kuziweka kwnye injini za matafuto ya mtandaoni ili mteja akitafuta anachokitafuta basi google/bing iweze kuileta website yako ukurasa wa mbele kabisa. So ukifanyia kazi vema hiki kipande, Google itai-rank website yako katika nafasi za juu.

3. Huweki maudhui kwenye website/blog yako: Yule jamaa yangu nilikwambia pale juu kuwa hakuona umuhimu wa kuwa na website, changamoto kubwa alikuwa nayo ni kushindwa kuwa na website inayoruhusu kuweka maudhui frequently. Unakuta website ina tabs za Home, Services, About na Contacts peke yake tu, wala haina sehemu ya blog/news au sehemu ya kufanya shopping. Kwa biashara za kisasa hii ni changamoto kubwa sana kama bado hujafahamu teknolojia ya SEO ina msaada gani katika biashara za mtandaoni.
Fahamu tu kwamba website ambayo haina uwezo wa kuweka maudhui mara kwa mara kupitia Kipengele cha Blog/News ni NGUMU sana kutokea kwenye ukurasa wa kwanza wa google. Hii ni kwasababu Maudhui unayoweka kwenye kipengele cha Blog/News huifanya website yako kuwa ya Kipekee na inayojiboresha kila siku.
Na hivyo ni rahisi google kui-rank website yako katika nafasi za juu pale mtu akitafuta taarifa ambazo pia zinapatikana kwenye website yako. Hii ndo silaha ambayo itaiwezesha biashara yako kuweza kujitangaza yenyewe na kukusanya wateja wengi huku wewe ukiendelea na mishe zingine.
4. Hausambazi Mukhtasari wa taarifa (updates) zinazopatikana kwenye website yako: Ndio, SEO inafanya kazi automatic unapounganisha website yako na huduma ulizozisoma hapo awali, Lakini, ni muhimu pia kusambaza Updates kuhusu taarifa unazoweka kwnye website yako katika social accounts zako za instagram, facebook, twitter nakadhalika.
Hapa unatengeneza kitu kinaitwa BACKLINKS. Tayari nimeshakuwekea elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa Backlinks katika kuhakikisha website yako inafanya vizuri pale Google.. Fahamu tu kuwa ili Website yako iweze kuwa imara mtandaoni lazima links zake zipatikane kwenye media zingine kama Linkedin, Facebook, Twitter, ZoomTanzania, Clutch n.k.
Huko ndo Jikoni kwenye haswa, Kwa sababu, ukiachana na Google, kwenye mitandao hio ndipo watu wengi hushinda wakijadiliana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa, michezo na burudani. So ukiwapelekea solution kuhusu changamoto zao kisha ukawapa link, guess what will happen?
Kujua zaidi namna ya kuongeza traffic kwenye website yako tafadhali tembelea makala hii hapa chini:
KWANINI TUNA-SHARE SIRI HIZI KUHUSU TEKNOLOJIA YA SEO INA MSAADA GANI KATIKA BIASHARA ZA MTANDAONI?
Siku zote maendeleo mazuri ya mgonjwa ndo mafanikio ya daktari. Hivyo wewe mjasiriamali ukifanikiwa ktk website yako, huo ni ushindi pia kwetu developers na wataalam wa SEO. I hope elimu hii inakwenda kutibu changamoto zako katika biashara za mtandaoni?
Kwa makala nyingine nyingi zaidi, endelea kuperuzi ukurasa wetu wa https://rednet.co.tz/blog kila mara ambapo utagundua makala muhimu za kuimarisha uchumi wako binafsi na wa biashara/kampuni yako.

Msaada binafsi tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
