Tag: technology

this is why you need backlink for your website

This is why you need backlinks for your website to rank higher and perform better on Google search appearances.

These backlinks are the links to your websites that are mentioned/found on other websites/platforms i.e LinkedIn, Facebook, Instagram, Twitter, Bbc, Aljazeera, government websites, and other organizational and private websites. Today we will learn why you need backlinks for your website to rank higher and perform better on Google search appearances. Get to the bottom of this article.

Why Backlinks?

  1. They give your website a higher Domain Authority: This is the status of Influence in Search Engines. The most influential websites/platforms (LinkedIn, Facebook, BBC, Rednet Technologies) have more Domain Authority than less effective websites.
the domain authority for your website

2. They rank higher your website in Search Engines: If your website has 20 quality backlinks, that means, there are 20 attractive links to your websites that were mentioned by other websites/platforms. That means your website will perform better than the one with 10 poor backlinks.

3. They give your website a Unique Identity: Considering the type of keywords you are using on your website, your backlinks will make sure that the website is very unique on Google Search Appearances. i.e If you have mechanical keywords, don’t expect to appear in food searches.

4. They increase traffic to your website; Since Backlinks are the referral points that other websites endorse for your website, it is likely to increase the number of visitors to your website. This is very powerful in doing #SEO intelligently.

5. Increase Customers for your Services/Products; The easy way of getting customers in Digital Infrastructures is through #SEO and specific Backlinks. Considering the previously mentioned advantages, backlinks will increase your customer base gradually but very surely.

How Do You Get Those Backlinks?

After knowing the advantages of Backlinks, you would want to know how to create them so as to get the benefits out of it asap. Here are a few of what you can do.

  1. Add Internal Links; Internal Links are the links that refer to the topic you’re discussing with the previous topics that you already published before in your older posts. These will give enough details to your visitors on different articles just inside your website.
  2. Add Outbound Links; These are the links coming from other websites that support your points in the article. This gives your readers points of reference, and more is very good in #SEO ranking. The outbound links provide citations to your visitors always. You need them.
  3. Ask other publishers to mention the links from your website in their publications. Here you create the links of your articles as Outbound links on other publishers’ websites. If your links appear in other websites’ content, potential referrals are created to rank it higher.
  4. Publish your articles on other platforms like Linkedin, Facebook, and Medium. If your article has more internal links and outbound links it will be great in Google Search Appearances and #SEO.
  5. Make sure the images that you’re using in your articles have “alt text and meta tags” details with the same words as your topic/keyphrases. This will improve the Image Search in #Google. You know how many images are doing fine in impression nowadays!
alt text and meta tags for your website

6. Update your Articles frequently: The new algorithm of google makes recent posts appear higher on search appearances than old posts. Also if you update your post google will count it as a new article. You want to do this.

Tools to consider

After doing everything that you read in today’s article, please do not forget to check how your website is doing in #SEO and Keyword performance. You can use tools like Google Search Console or Jetpack (for WordPress).

If you will get interested in improving your website in terms of building backlinks and doing SEO for it to perform better on Google Search, please contact me to get your website done today.

Also if you will like to send us a tip to motivate us to prepare great content for you, please use the code below.

Kwanini uwe na website ya biashara yako?

Do you have something to ask or comment on? Please share with me here in the comment section or contact me through the following details:

Call/Whatsapp: +255765834754

Email: info@rednet.co.tz

web: https://rednet.co.tz

Unawezaje kutumia Digital Tools ili kuimarisha biashara yako mtandaoni?

Kama huwezi kuendesha biashara yako ukiwa nyumbani au ukiwa safarini nje ya mkoa/nchi, nakushauri, hii 2022 hakikisha unatumia vema Digital Tools utakazojifunza leo katika kuimarisha biashara yako.

FAQ 1: Digital Tools ndio zipi?

ANS: Website, ecommerce store, twitter account, insta page, facebook, Linkedin, Zoom, CH, Whatsapp na Telegram.

FAQ 2: Nawezaje kuzitumia hizo Digital Tools kuimarisha biashara yangu?

ANS: i. BLOG SECTION:

Kwa website, hakikisha ina kipengele cha “Blog” ambapo utaweza kupost Updates mbalimbali kuhusu biashara yako mara kwa mara ili mteja apate solution ya changamoto zinazomkumba mara kwa mara.

ii. Tumia S.E.O:

Kuhakikisha biashara yako inapatikana google ikitokea mtu yeyote aki-search kuhusu huduma unazotoa. Mfano: ikiwa unauza chakula basi hakikisha katika blogs zako unatumia zaidi maneno kama “Wali, ugali, biriani, juisi ya miwa, chakula kitamu, sambusa za nyama nk”

Kwa sababu maneno hayo kitaalam yanaitwa “Keywords” ambayo ni rahisi kwa mtu yeyote kuyaandika akiwa anatafuta sehemu pa kupata huduma nzuri anazohitaji. So hakikisha unayatumia barabara kabisa kuendana na aina ya biashara yako.

iii. GOOGLE MAP:

Ni changamoto sana kwa wajasiriamali wengi. Unakuta eidha mtu hajui kuitumia au basi tu haoni haja ya kuitumia. Leo nataka nikusanue, hii Google Map inawainua sana watu mtandaoni. Kama unafanya biashara/una ofisi, ingia google map, sajili biashara yako chap.

Ingia google kisha andika (Aina ya biashara unayofanya au unayotaka kutafuta) kisha ikifuatiwa na maneno “near me” Mf: web designer near me, au food provider near me, au kitu chochote kama mifano inavyoonekana hapo. Halafu jiulize kwanini biashara yako haipo kwenye hizo listings?

iii. GOOGLE MY BUSINESS:

Katika jukwaa la Google unao uwezo wa kutengeneza wasifu (profile) wa biashara yako ukaweka details zote kama jina la biashara, mahali ilipo, huduma unazotoa au bidhaa unazouza, offers, mawasiliano yako n.k. Hii ndio njia rahisi zaidi ya kufanya S.E.O.

Hizo details unazoweka kwenye Akaunti yako ya Google My Business zinaisaidia sana biashara yako kuonekana kirahisi pale mtu anapotafuta vitu vinavyofanana na huduma unazotoa kupitia Injini za matafuto kama Google na Bing. Jaribu hii leo uone NGUVU ya SEO. Utanishukuru badae.

iv. SEARCH CONSOLE:

Hii ni Dashboard ya Google ambayo inakuonyesha namna website yako inaperform katika matafuto yanayofanyika huko mitandaoni. Kupitia matafuto hayo, google itai-rank website yako kwa mujibu wa inavyotafutwa na watu mbalimbali duniani kote.

Website zinazotembelewa zaidi na watu hutokea katika page ya kwanza kabisa pale mtu anapo-search kuhusu jambo analotaka mtandaoni. Ukiangalia kwa upande wetu, mpaka kufikia tar1/1/, tovuti yako ya https://rednet.co.tz imepata nafasi ya 7.6. Nia ni kufikia nafasi 3 za juu.

v. Katika matumizi ya Social Media kanuni zipo wazi. Hakikisha maudhui unayoweka kuhusu biashara yako 80% ni kuhusu VALUES ambazo biashara yako inampatia mteja, na 20% ikiwa ni kuhusu MATANGAZO ya bidhaa/huduma unazotoa.

vi. WHATSAPP:

Moja kati ya Tools zenye nguvu zaidi katika kuimarisha biashara kwa njia ya mtandao ni kupitia Whatsapp.

WHY WHATSAPP?

Je wajua kuwa watumiaji wa Whatsapp kwa wastani hufungua App hio mara 23 kwa siku, huku zikitumwa meseji milioni 29 kila dakika katika app hio?

Hii inakuhakikishia kwamba ukiitumia vizuri App ya whatsapp unajiweka kwenye nafasi nzuri ya KUSTAWISHA biashara yako kimtandao na kuongeza MAUZO, tena BILA GHARAMA yoyote ile ya kulipia matangazo.

Pia kupitia features za Whatsapp Status, Whatsapp Broadcast, Groups, Videos and Voicenote, sasa kutoa VALUES za biashara yako kwa wateja imekuwa rahisi. Unaweza kutengeneza Funnels hapo, ukabadili watu unaowasiliana nao kutoka WATU WA KAWAIDA kuwa WATEJA wako kirahisi zaidi.

Muhimu, hakikisha unapotumia hii mitandao ya kijamii basi walau uwe unaweka posts/tweet mbili kwa siku, kila siku (consistently).

Mwaka huu 2022, unao uwezo wa kumanage biashara zaidi ya 1 na zote zikaenda kwa ufanisi unaotakiwa kwa kupitia matumizi SAHIHI ya Digital Tools ulizojifunza leo. Usipoteze nafasi yako LEO sasa kufanya hivyo.

Una changamoto yoyote katika kutumia Digital Tools katika kuimarisha biashara yako? Tucheki kupitia DM yetu au Chati nasi Whatsapp kuitia namba 0765834754 ili kusudi tukushauri BURE kabisa namna ya kutatua changamoto hizo haraka iwezekanavyo.

OFA YA MWAKA MPYA 2022:

OFA YA KUPATA WEBSITE YAKO
OFA YA MWAKA MPYA 2022

Tunayo OFA YA MWAKA MPYA 2022 hapa ambapo, Ukitengeneza website kwetu unapata huduma za SEO kwa Google My Business, Search Console na Google Map BURE KABISA. Pia tutakuwa tunakushauri namna nzuri ya kuendesha website yako ili ikuletee faida kila siku.

Changamkia OFA hii kabla haijakwisha kwa sababu “Biashara asubuhi, jioni mahesabu”. OFA inakwisha tarehe 31/01/2022, hivyo wakati unapanga mipango yako ya kufanyia kazi mwaka huu, weka akilini pia namna utakayoweza kufanikiwa katika biashara zako mtandaoni kwasababu nyakati hizi zinakutaka ujifanyie tathmini binafsi kama kampuni inayofanya tathmini mwenendo wake. Weka mipango ya mwaka kisha igawe katika shughuli za miezi mitatu mitatu, fanya kazi kuifanikisha. Mwisho wa mwaka fanya tathmini uone jinsi umefanikiwa katika mwaka wako.

Cheers.

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER)5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

mpesa lipa namba yetu

Website zinazotembelewa na watu wengi kila siku, zina nini ambacho hujakifahamu bado?

Unaweza kuwa unajiuliza, “Sasa nimeshafungua website na ninazo akaunti za Twitter, Facebook na Instagram, lakini mbona watu hawatembelei tovuti yangu? nakosea wapi?

Ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote ambaye hapendi kufanikiwa.

Hakuna mfanyabiashara ambaye hapendi kupata Faida kubwa ya kifedha na wateja.

Hakuna mtu ambaye hapendi kuingiza PESA.

Ukweli ambao unaweza usiambiwe na Web-Designer unayempa kazi ya kukutengenezea website ya biashara yako ni kwamba:

“Kumiliki Website na akaunti za mitandao ya kijamii (Zana za kimtandao) hakukufanyi kufanikiwa direct katika biashara hasa za mtandaoni”

-Faustine Kimath

Lakini kwanini umiliki hio website yenyewe, ilhali unaweza kutumia mitandao ya kijamii kuendesha biashara yako izuri tu? Majibu yanapatikana ukifuatilia makala hii hapa Kwanini ni Muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako?

Baada ya hapo utagundua pamoja na kuwa na website bado kuna zana nyingi sana za kimtandao (Digital Tools) ambazo unaweza kuzitumia kuwafikia wateja wako sambamba na website yako kama zana kuu. Sasa uzitumie vipi zana hizo ili ile Kiu yako ya kufanikiwa ikapate kutimilika?

Websites za kisasa zinatengenezwa zikiwa ni chanzo muhimu cha taarifa za kuaminika kuhusu Biashara/Kampuni yako.

Hivyo website yako inafanya kazi ya kukutambulisha mtandaoni 24/7.

Sasa leo ukimaliza kusoma makala hii utapata uelewa hata siku ukifungua website yako ufahamu iwekwe vitu gani vitakavyoongeza idadi ya watu wanaoitembelea pamoja na kunasa wateja:

Kipengele namba 8 kitakufungua kichwa sana. Twende mpaka mwisho:

1. UBUNIFU:

Siku zote hakikisha unawapa wateja wako vitu wanavyopenda wao, sio unavyotaka wewe. Hata unapofikiria kubuni tovuti, hakikisha tovuti hio inafanana na aina ya wateja wako. Hivyo fanya utafiti wa kujua wateja unaowalenga ni wa namna gani kwanza.

Duru zinaonyesha 94% ya vitu vinavyomvutia mteja kwa mara ya kwanza kabisa (first impression) ni ubunifu uliotumika kutengeneza website hio. Ubunifu unajumuisha rangi za tovuti, mijongeo ya picha, aina za maneno (fonts) n.k

2. KASI YA KUFUNGUKA:

Kwa kawaida 94% ya watu huchukua si zaidi ya sekunde 5 kusubiri kurasa ya tovuti ifunguke. Baada ya hapo huachana na ukurasa huo na kuendelea na mambo mengine ya mtandaoni. Imagine tovuti yako inachukua zaidi ya sekunde 10 kufunguka sasa. Nani ataitembelea mara ya pili?

3. MATUMIZI YA ANWANI ZA NDANI

Unapokuwa na tovuti yenye anwani za ndani (internal links) za kutosha katika kurasa mbalimbali, unaiweka tovuti yako kwenye nafasi ya kutembelewa mara kwa mara tena na watu wengi zaidi.

Anwani hizi zinarahisisha kupatikana kwa taarifa kwa haraka na wepesi zaidi ndani ya tovuti yako.

Anwani hizo pia hutumika kama maneno ya msingi (keywords) katika injini za matafuto ya kimtandao kama Google. Hivyo mtu anapo-google inakuwa rahisi kupata majibu, bidhaa au/na huduma zinazotolewa kupitia tovuti yako.

4. MAUDHUI YA VIDEO:

Zamani ilikua si rahisi kurusha maudhui ya video mtandaoni na yakawafikia watu wengi kutokana na uduni wa teknolojia. Lakini siku hizi mambo ni tofauti sana. Maudhui ya video yamekuwa yakiwafikia watu wengi zaidi na kwa haraka sana. Angalia namna YouTube inayoshika kasi pale msanii wako unayempenda akiachia wimbo mpya. Siku hizi hata kukiwa na matukio muhimu ya Kitaifa, watu wengi huyafuatilia kupitia YouTube kuliko televisheni za kawaida.

Kwanini? Kwa sababu YouTube inapatikana kwenye smartphone, stesheni za televisheni hazipatikani kirahisi kwenye smartphones, hivyo nyakati hizi ukiwa popote kwenye mihangaiko yako ni rahisi kufuatilia maudhui ya video kupitia simu yako yenye intaneti kuliko wakati mwingine kwenye historia ya mwanadamu.

Maendeleo ya kiteknolojia yamerahisisha sana usambazwaji wa video mtandaoni. Hivyo unapofikiria kufungua/kuiimarisha website yako, hakikisha pia unaweka maudhui ya video ambayo yatawafanya watu wazidi kumiminika na kufaidi thamani ya maudhui hayo kirahisi.

5. MATUMIZI YA BLOGU

Kwa ulimwengu huu, masoko ya bidhaa na huduma yamehamia mtandaoni na hivyo kusababisha ushindani kuwa mkubwa sana ukiongozwa na uwepo wa maudhui mbalimbali yanayopandishwa kila siku.

Hivyo, tovuti yako inapaswa kuwa na kitu kipya kila leo.

Tovuti yenye Blogu ina nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwafikia watu wengi na kutembelewa kila siku tofauti na tovuti ambazo hazina sehemu ya Blogu. Kwenye blogu ndipo unapoweza kuweka maudhui ya kuwasaidia wateja wako kufikia malengo yao na kutatua changamoto wanazokutana nazo kila siku kupitia biashara yako.

6. MATUMIZI YA PICHA

Je, wajua kwamba picha ndio kiungo rahisi zaidi katika kuhudumia mteja? Zinamfanya mteja kukumbuka kuhusu huduma/bidhaa yako, ni nyepesi na rahisi kutumia. Maudhui yako yakiwa na picha, 65% ya wanaotembelea tovuti yako watakukumbuka hata wakitoka mtandaoni.

Mfano ukiitizama picha hii hapa chini wazo linalokujia haraka ni kwamba sasa ni wakati wa sikukuu ya Christmass, na kwa kuwa umeiona hapa picha hio bila shaka ukiiona sehemu nyinngine utakumbuka tu kwamba “Faustine alishawahi kuipost pia hii picha”. Unaiona nguvu ya picha hapo sasa? Imagine bidhaa zako unazipiga picha kali za kiubunifu na kuziweka kwenye tovuti yako sasa.

7. UMUHIMU WA S.E.O

Kama unahitaji mafuriko ya watu yazidi kumiminika katika tovuti yako kila siku, hiki kipengele cha SEO huwezi kukikwepa. Hii ni Teknolojia inayorahisisha matafuto ya mtandaoni na kuelekeza wapi pa kupata majibu na taarifa zaidi.

Imagine google inawaelekeza wateja waje kwako kupata taarifa, huduma na bidhaa muda wote ambao wewe umelala zako, au muda ambao wewe haupo mtandaoni ikiwa tu tovuti yako utakuwa umeiunga na miundombinu ya SEO. Hii S.E.O inahusisha matafuto katika mifumo ya maneno ya msingi (keywords) ambayo unakuwa ukiyatumia mara kwa mara katika tovuti yako na mifumo yako ya utoaji huduma. Hii imekuja kurahisisha sana maisha. Halafu cha ajabu zaidi, ni BURE kabisa kuitumia.

8. UTATUZI WA KERO/CHANGAMOTO:

Jambo muhimu zaidi linalowavuta watu wengi kutembelea tovuti mbalimbali ni Nafasi ya Kutatua kero/changamoto zinazowakabili. Watu hawatembelei tovuti tu ilimradi, wanatafuta suluhu ya kero zinazowakabili. Hivyo, zingatia hilo.

Je tovuti yako ina maudhui yanayotatua changamoto gani kwa wateja wako. Tuambie kwenye comments.

Unajiuliza utakuwa unatatua changamoto zipi? 1. Chunguza wateja wako uwafahamu wanapitia changamoto zipi, 2. kisha Jifunze namna ya kutoa huduma bora. 3. Fundisha kwa kuandika kutoka kwa wataalam wa copywriting. Rudia no.1.

-Faustine Kimath

9. MATUMIZI YA FOMU ZA MAULIZO:

Kama unataka tovuti yako ivutie watu wengi zaidi basi moja kati ya SIRI muhimu ni kuweka “fomu ya maulizo” ambayo inampa mtu yeyote anayetembelea tovuti yako nafasi ya kuuliza chochote kuhusu huduma/bidhaa zako. Muhimu sana hii, na siri ya kufanikiwa katika hili ni kuitengeneza fomu yako iwe fupi na ya kufurahisha (yani inatakiwa mtu akiiona tu ajisemee “loh, hebu niulize kuhusu … hapa chap“).

Fomu hii ni kipengele kinachoweza kuwabadili watembeleaji (visitors) kuwa wateja haraka sana.

10. HUDUMA KWA WATEJA:

Hata kama ukiyafanya yote uliyojifunza leo hapa kwanzia 1-9 lakini ukawa huna huduma nzuri kwa wateja wako na watu wanaotembelea tovuti yako na kuuliza maswali kwa lengo la ufafanuzi, ndugu, bado safari ya mafanikio itakuwa ndefu kwako.

Huduma kwa wateja inajumuisha namna unawasikiliza wateja wako, namna unavyojibizana nao (kwa maandishi au kwa sauti), muda unaotumia kuhudumia wateja wako na namna unavyoweza kuhimili hasira na mtazamo hasi kutoka kwa wateja na watu mbalimbali.

Vyote hivyo vinachangia kuongeza au kupunguza idadi ya watu wanaotembelea tovuti yako kwasababu takwimu zinaonyesha 95% ya wateja husambaza maneno kuhusu huduma mbovu walizopata na 89% kati yao huacha kabisa kufanya kazi na yule aliyetoa huduma mbovu zaidi unaweza kupitia makala hii hapa Umuhimu wa Takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa Wateja.

Tovuti ni sehemu muhimu sana katika kuhudumia wateja wa biashara yako pamoja na kujitangaza hasa katika zama hizi za kidijitali.

Huna haja ya kusambaza CV na makaratasi. Tunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya karatasi ambazo zinatokana na ukataji wa miti.

ZIADA: Hata ukisema uyafanye hayo yote 10 ambayo umeyaona kwenye makala hii ya leo, bado nature itakudai kitu kimoja cha muhimu zaidi. Nacho ni muendelezo (consistency) katika utendaji wako wa kusimamia biashara katika mazingira yote, mtandaoni na ana kwa ana. Fahamu kuwa hakuna mafanikio ya ghafla au mafanikio ya bahati mbaya. Yeyote unayemwona amefanikiwa (hata kwa bahati nasibu), lazima alistruggle kutengeneza mfumo mzuri wa kiutendaji ili kumsaidia katika kusimamia biashara yake katika viwango vinayotakiwa.

Umejifunza nini kwenye makala hii ya leo? Tuambie kwenye comments hapa chini. Pia hakikisha una-share makala hii pamoja na watu wako wa karibu ili kusudi somo hili liwafikie watu wengi zaidi.

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER)5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

mpesa lipa namba yetu