FAHAMU ATHARI ZA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19) NA JINSI YA KUPAMBANA NALO KATIKA BIASHARA BARANI AFRICA
Ugojwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona umetangazwa kama janga la kidunia baada ya kuathiri maelfu ya watu duniani kote. Janga hili linatajwa kuzorotesha uchumi wa kidunia. Ugonjwa huu unasambaa haraka na namba ya wagojwa na waathirika inakwenda ikibadilika kila siku. Makala haya yanaakisi takwimu za ugojwa kufikia March 9, 2020.
Takribani wiki kumi na mbili (12) zilizopita nchi ya China iliripoti uwepo wa virusi vipya kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO). Virusi hivyo vinavyotambulika kama SARS-CoV-2 Vinavyosababisha ugonjwa wa Corona, COVID-19 ambao ulisambaa haraka sana katika jiji la Wuhan na baadae kusambaa China nzima. Nchi hio imekumbwa na changamoto kubwa katika nyanja ya huduma za kibinadamu ambapo zaidi ya visa 80,000 vimesharipotiwa vikisababisha vifo vya watu takribani 3,000 nchini China peke yake. Uginjwa huo tayari umeshavuka mipaka kufikia maeneo mbalimbali ya dunia kama Asia Mashariki (Korea Kusini iliyoripoti visa 7,000, hali kadhalika Singapore na Japan), Mashariki ya Kati (ikianzia Iran iliyoripoti visa 6500), Bara Ulaya (ikijumuisha eneo la Lombardy Kaskazini mwa Italy lililoripoti visa zaidi ya 7,300 na kusambaa zaidi maeneo mbalimbali mwa bara Ulaya ), Marekani ambapo vimeripotiwa visa zaidi ya 200.
Leo hii uchumi wa china ambao umepata ushawishi mkubwa katika uchumi wa dunia ikichangia kwa 17% ya GDP ya dunia nzima huku sekta ya biashara ikichangia 34% ya GDP ya ndani. takwimu hizo ni zaidi ya hali ilivyokuwa mwaka 2003 wakati ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege (SARS) ulipolipuka kwa mara ya kwanza.
Ripoti ya Frost & Sullivan inasema kwamba katika hali mbaya zaidi au janga ambapo ugonjwa utaathiri watu wengi zaidi duniani kabla haujadhibitiwa mpaka kufikia mwezi June-July, pato la taifa (GDP) katika ngazi ya dunia litashuka chini kwa 2%.
Changamoto: Unaweza vipi kufanya biashara kwa kupitia mtandao katika hali ya majanga kama ilivyo sasa?
Kwa mujibu wa taasisi ya NRF (National Retail Federation) ya nchini Marekani, imekadiriwa kwamba biashara za rejareja zitabakia katika hali yake ya ukuaji zikiwa na 3.7% mpaka 4.2% ya kiwango cha ukuaji. Hata hivyo, serikali mbalimbali duniani zimekuwa zikichukua hatua kadhaa wa kadha katika kukabiliana na homa hio ya virusi vya COVID-19 ikiwemo kupulizia dawa katika sehemu mbalimbali zinazohusisha mikutaniko ya watu kamaa vituo vya mabasi, vituo vya treni, viwanja vya ndege, bandari, barabara za mitaani, maofisini, shuleni na vyuoni. hata hivyo, watu wamehimizwa kubakia majumbani mwao na kuwatenga wagonjwa na washukiwa wa ugonjwa huo kwa muda mpaka pale watakapopona.
Unaweza Vipi Kuhamishia Biashara yako Mtandaoni?
Kuanzisha biashara ya mtandaoni kunahitaji juhudi zaidi kukabiliana na changamoto za kisheria na maswala ya fedha ambazo haziepukiki. Ni muhimu sana kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa wataalamu ambao ni wanasheria na mawakili pamoja na wahasibu na wabobezi wa maswala ya kifedha kabla hujaanza biashara ya kimtandao. Hata hivyo, utakapofikia utayari wa kufanya biashara katika mtandao, utahitaji kiasi kidogo zaidi cha pesa kumudu gharama za uendeshaji wa biashara kuliko ilivyokuwa awali.
Uzuri wa matumizi ya internet ni kwamba unaweza kuzindua biashara na kujipatia pesa katika mtandao kwa mtaji kiduchu au wakati mwingine bila ya hata kuwa na mtaji wa kuanza nao. Kama ukiuelewa mfumo wa uendeshaji wa masoko ya kimtandao (online marketing), au ukiwa mashuhuri katika mitandao ya kijamii, ni dhahiri utaona wepesi sana kufanya biashara yako katika mitandao ya kijamii na internet. hata hivyo, haikuhitaji kuwa nguli ili kuanza biashara mtandanoni.
1. Chatbot business
Unazifahamu chatbot? Bila shaka. Hii ni njia mpya na bora zaidi ya kuwasiliana na wateja wako ambapo ukifungua tovuti nyingi za kisasa utaona alama ya kuandika ujumbe ambayo mara nyingi huandikwa (chat, chat with us, ) au mara nyingine utaona alama ya kuandika ujumbe. Ujio wa Chatbot umerahisisha sana kuwasiliana kati ya Biashara/Kampuni na mteja moja kwa moja. hivyo matumizi ya Chatbot yamerahisisha sana huduma bora kwa wateja na kuboresha utoaji wa bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja. Matumizi ya mitandano ya kijamii kama Facebook, Instagram na Whatsapp yamefanya matumizi ya Chatbots kuwa mepesi na rahisi zaidi kutumia.
3. Ad management business
Katika dunia ya leo iliyojaa ushindani mkali wa kibiashara, kama hujajua soko lako liko wapi ni ngumu sana kukabiliana na washindani wako ambao wengine unaweza usiwajue kama hautakuwa makini na kufuatilia taarifa na mienendo ya matakwa ya wateja kwa wakati. Matangazo katika biashara ndio moyo wa kuendesha soko lako katika uelekeo unaotakiwa (wa kutengeneza faida). Sasa ndani ya majanga kama Ugonjwa huu wa Corona ambapo watu wengi duniani wanahimizwa kufanyia kazi zao majumbani. huna budi kutangaza biashara yako kupitia matangazo ya kulipia katika injini kama Google, Bing na Ask pamoja na mitandao kama YouTube, Instagram, Twitter na LinkedIn. Hii inasaidia sana kuwafikia wateja wengi wenye uelekeo na uhitaji wa huduma/bidhaa zako katika muda mchache na hivyo kuongeza wateja wako duniani kote bila ya kulazimika kufanya maonyesho au semina. Kama bado hujajua jinsi utaweza kutangaza biashara yako kupitia huduma kama Google Adsense, tafadhali wasiliana nasi tukupatie ushauri mzuri wa jinsi ya kufanya.
Tizama hapa, kwa mujibu wa ripoti ya eMarketer, matumizi katika matangazo ya kidijitali nchini Marekani peke yake yatayazidi matumizi ya matangazo ya kawaida (traditional ads) kwa mara ya kwanza mwaka huu 2020. Mpaka kufikia mwaka 2023 matumizi ya matangazo ya kidijitali yatayazidi yale ya kawaida kwa theluthi mbili ya jumla ya matumizi ya sekta nzima ya media.
4. SEO business
Huitwa Search Engine Optimization (SEO) ambayo ni huduma inayorahisisha upatikanaji wa taarifa za kibiashara au binafsi kirahisi zaidi katika injini za kutafuta taarifa kama Google, Bing na Ask. Mada hii ya SEO imekuwa ikijadiliwa na kutumika sana duniani lakini sasa ndio wakati mahsusi wa kuhakikisha biashara yako inapatikana kirahisi katika injini za kutafutia taarifa. Ukweli ni kwamba wakati matangazo ya kulipia yanapozidi kushamiri duniani kwa kiwango kikubwa nyakati hizi, uwezo wa taarifa za biashara yako kuonekana kirahisi katika injini za kimtandao kama Google bado hakuna ushindani mkali, hata hivyo eneo hili linabaki kuwa na thamani zaidi katika kuendesha bishara kisasa zaidi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa.
Linapokuja swala la kutafuta maneno muhimu (keywords) kupitia injini za kimtandao, thamani ghafi ya SEO huonakana pale taarifa inayotakiwa kuonekana juu zaidi katika majibu baada ya kutafuta. Takribani 40% ya watu hugusa jibu la kwanza katika injini baada ya kutafuta na hivyo ukurasa wa kwanza hujumuisha 91% ya taarifa zilizotafutwa na kusambazwa, ikionekana juu kabisa katika SERPs (Google Search Engine Results Pages) hivyo kufanya njia hii ya SEO kutumiwa zaidi na wadau wa masoko ya kimtandao duniani kote.
5. Vacation rental business
Mahsusi kwa wale wafanyabiashar wa nyumba za kupanga, hoteli pamoja na nyumba za wageni (Guest Houses and Lodges), biashara ya kupangisha nyumba imekuwa ikishamiri sana zama hizi za mapinduzi ya kidijitali. Japokuwa biashara hii haitajwi sana katika mada mbalimbali duniani, inaweza ikakufanya ukafikiri kuhusu makampuni makubwa duniani kama AirBnB au HomeAway, kwingineko kuna biashara ndogondogo zilizopo mtandaoni kama InviteHome ya Michael Joseph na MyDalali ya Emmanuel Njavike kutoka nchini Tanzania na wengine wengi sana waliojikita maeneo mbalimbali duniani. Linapokuja swala la nyumba za kupanga na biashara inayohusu maswala hayo, makampuni huingiza kati ya 10% mpaka 40% katika mapato kulingana na viwango vya kupangisha nyumba duniani ambavyo hutegemea mahali nyumba ilipo na sera za utawala.
Kuanzisha biashara hii ya kukodisha nyumba mtandaoni maarufu kama udalali wa nyumba unahitaji mtaji kiduchu tu ikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa miundombinu bora ya kimtandao (softwares and Applications) ambazo zinasaidia kuhifadhi taarifa pamoja na kuelekeza wapi nyumba/hoteli zinapatikana katika namna iliyo rahisi kutumika na mtu yeyote duniani.
6. Webinar business
Najua unachofikiri. Unawaza kwamba utaanzaje kufanya biashara yako kupitia kwa njia ya Webinar? unahisi kwamba huwezi kufanya webinar? Sasa hakujawahi kuwa na njia rahisi ya kuwafikia wateja wako na kuwasiliana nao moja kwa moja kwa njia ya mtandao zaidi ya kutumia Webinar. Hata hivyo, webinar ni nini? Hii ni njia ya kufanya semina au kampeni moja kwa moja kwa njia ya mtandao. Unahitaji camera na Bando tu katika simu yako kufanikisha jambo hili. Jiulize, kuna mtu mwingine anaelewa biashara unayoifanya ikijumuisha huduma na bidhaa kuliko wewe mwenyewe? Sasa hii inakupa nafasi ya kuwakusanya wateja na wafanya biashara wenzako na kuwaelezea nini unachokifanya, offer, kampeni maalum unayoendesha na bidhaa/huduma mpya. Hayo yote unaweza kuyafanyia nyumbani kwako tu na kuwafikia maelfu wa watu ulimwenguni kote. Unaweza au huwezi?
Jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba, hulazimiki hata kuwa na bidhaa/huduma zako pekee ndio uweze kufanya webinars. Mtaalamu wa webinars Jason Fladlien ambaye ni muanzilishi mwenza wa kampuni ya Rapid Crush alifanikiwa kutengeneza utajiri wa takribani dola milioni 100 za kimarekani kwa kuuza bidhaa mbalimbali kupitia webinars. Alichofanya ni aliwakusanya watu kama inavyofanyika katika magroup ya whatsapp, then wanapokuwa online anakuw anaendesha vipindi vya mauzo na hivyo kujipatia wateja kirahisi kabisa. Umeshaiona nguvu ya webinars sasa?
Njia bora ya kuanza kufanya biashara kupitia Webinars ni kutafuta bidhaa au huduma utakayoweza kuipigia chapuo, unatafuta watu sahihi wenye uhitaji na bidhaa/huduma hio halafu unawasha kamera yako na kuendesha kipindi kuhusu bidhaa/huduma hio. Kanuni hio iliyoanza kutumiwa na Fladlien na baadaye ikachukuliwa na bwana Russell Brunson ambaye kwa kushirikiana na bwana Jim Edwards walitengeneza software iitwayo Funnell Script, mahsusi kabisa kwa ajili ya kufanyia shughuli za webinars.
7. Business coaching
Business coaching au mafunzo na ushauri wa kibiashara ni kipawa ghafi (skills) sana haswa nyakati hizi za mapinduzi ya kiteknolojia na biashara za kimtandao. Watu wanaohodhi vipawa hivi vya kutoa mafunzo na ushauri wa kibiashara wamekuwa na nafasi muhimu sana nyakati hizi kwa kuzingatia msaaada wa majukwaa mbalimbali na mitandao ya kijamii.
Watu wabobezi kama Dan Lok, Simon Sinek na Joel Nanauka wamekuwa mashuhuri sana katika biashara hii ya mafunzo na ushauri wa kibiashara wakifuatiwa na wataalamu wengine wengi duniani. Mafanikio yao yamejengeka katika matumizi ya mitandao kama YouTube na Zoom ambapo kupitia majukwaa hayo, wafanyabiashara pamoja na watu wengine wanaotaka kujifunza vipawa mbalimbali katika uwanda wa kibiashara hujiunga huko na kupata elimu wakiwa popote duniani. Jinsi nzuri ya kufanikiwa katika biashar hii ni kuhakikisha unaonyesha thamani katika biashara za watu wanaofuatillia maudhui katika chaneli akaunti zako za mitandao ya kijamii, na baadaye wakulipe katika utendaji wao wa kibiashara za kila siku.
Kwa kifupi hizo ni baadhi ya njia ambazo unaweza kuzitumia kuhakikisha biashara yako inaendelea kuwepo karibu na wateja wako haswa katika kipindi hiki cha majanga ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). Suluhisho mbadala linapatikana katika mapinduzi ya 4 ya viwanda yanayoendelea duniani yakichochewa na kasi ya ukuaji wa kiteknolojia na internet.
Anza kufanya biashara yako leo kwa kutumia moja kati ya njia zilizoelezewa hapo juu kisha jikinge na Corona pamoja na majaga na matishio mengine yanayoweza kutokea duniani kama vita, tufani, mafuriko na tofauti za kidiplomasia kama ambavyo ilitokea mwaka 2019 nchini Afrika Kusini kulipotoea machafuko na mauaji ya raia wa kigeni yaliyoitwa Xenophobia.
Usisite kuwasiliana nasi katika kubadili biashara yako kuelekea katika miundombinu ya kimtandao, kwa uchache kama ilivyoainishwa katika makala haya. USIBAKI NYUMA!!!