Tag: social media marketing

ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara

IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA

Zama hizi kuhoji umuhimu wa mitandao ya kijamii ni sawa na kuhoji umuhimu wa mwanga wa Jua duniani. Google, Facebook, Twitter, Instagram na Whatsapp ndio injini za biashara mitandaoni. Kivipi? Sasa kwenye makala ya leo nataka ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara hio unayoifanya. Twende pamoja mpaka mwisho.

Imefika muda sasa, mitandao ya kijamii si sehemu ya anasa tena bali ni nyenzo muhimu katika uendeshaji wa biashara. Sasa imekuwa rahisi kuwasiliana na wapendwa wetu wakiwa popote duniani, tena kwa gharama ndogo sawa na bure. Pia imekuwa rahisi sana kuwasiliana na wateja wapya.

Mpaka kufikia January 2018 duniani kulikua na watumiaji wa huduma za internet takriban 4.02 bilioni, sawa na 53% ya idadi nzima ya watu. Kati ya hao, watumiaji wa mitandao ya kijamii wanafikia 3.2 bilioni sawa na 42% ya watu wote duniani. Hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes. Hapa Tanzania mpaka kufikia mwezi Mei 2021 kumeripotiwa kuwa na watumiaji wa huduma za intaneti zaidi ya milioni 29. Huku watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kielekroniki wakifika milioni 32, chanzo TCRA.

#VijanaWenzangu kama wewe ni mfanyabiashara basi bila shaka namba hizi huwezi kuzipuuza. Utafiti huo kwako unapaswa kuwa ni hazina katika biashara zako ambayo utaitumia kwenye kusaka wateja wapya, kuwasiliana nao, kuwaongeza na kuhakikisha wanabaki kuwa wateja wako.

Matangazo ya televisheni na redio yanakwenda kufa kifo cha taratibu. Mitandao ya kijamii inateka jukwaa la Ushindani wa biashara hasa katika idara ya Masoko na Mauzo. Kama hutumii mitandao ya kijamii kwa kukuza na kuimarisha biashara yako basi jua uko nyuma sana kiushindani.

Kujua kwanini unapaswa kuitangaza biashara yako, fuatana na Makala hii hapa KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?. Sasa ukishajua sababu hizo, Leo tunakwenda kujua Kwanini Utumie Mitandao ya Kijamii kama nyenzo muhimu katika biashara yako. Makinika.

MANUFAA YA MITANDAO KATIKA BIASHARA:

Kama umekuwa ukijiuliza “Hivi hii akaunti yangu ya twitter/instagram/facebook naweza vipi kuitangazia biashara zangu? Hivi nitaweza kweli?” Basi leo tuzione faida muhimu za mitandao ya jamii katika kuimarisha biashara.

i. KATIKA KUKUZA BRAND: Kwa mujibu wa mtandao wa “We Are Social’s Digital” mwaka 2018 ilionekana kwamba Facebook ndio mtandao wa pili ambao unafuatiliwa zaidi duniani, ukifuatiwa na mtandao wa Youtube. Kwenye hio orodha mtandao wa Google ndio ulikua unaongoza kwa kufuatiliwa.

Hii ina maanisha kuwa, watu wanatumia muda mwingi mtandaoni. Mitandao hio pia hutumika kama vyanzo vya taarifa kuhusu bidhaa/huduma za biashara/kampuni/shirika fulani. Facebook peke yake ina zaidi ya kurasa (Pages) milioni 60 ambazo hutumika kama Brands za biashara mbalimbali kila siku. Hapa sasa ndipo unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara.

nguvu ya mitandao ya kijamii

Katika mtandao wa twitter pia mambo ni moto. Kwa mujibu wa @Twitter Sababu kuu ya watu kutumia mtandao wa twita ni “kugundua jambo jipya na/au la kusisimua”. Haya hebu tuambie hapa, wewe ni nini kilikufanya kuanza kutumia mtandao wa twita? Ile sababu ya watu kupata kitu kipya imefungwa kwenye design ya twita ambayo inawafanya watu wapate taarifa na mambo mapya na yenye kusisimua ambayo haswa Biashara na makampuni yanavitafuta. Hivyo katika biashara mtandao wa twita unafaida zaidi kulinganisha na mitandao mingine kama Instagram na Quora kutokana na namna yake ilivyobuniwa.

ii. KATIKA KUJENGA UAMINIFU (LOYALTY): Mwaka 2017 utafiti uliofanywa kwa watu wa masoko 5,700 ulionyesha kuwa 69% sawa na watu 3,933 walijenga uaminifu kwa wateja wao kupitia matumizi kibiashara ya mitandao ya kijamii (social media marketing).

Vilevile 66% ya watumiaji wa mitandao wa umri kati ya miaka 18-24 ni waaminifu kwa akaunti wanazozifuatulia kwenye mitandao ya kijamii. 60% ya walio na miaka 25-34 hupendelea kutumia bidhaa/huduma za biashara wanazozifuatilia kupitia Facebook, Twitter na Instagram.

iii. KATIKA MAUZO: Mtandao wa “We Are Social’s Digital” umeripoti kuwa 17% ya idadi nzima ya watu duniani hununua bidhaa na kulipa bills kwa njia ya mtandao. Kwa kuwa % kubwa ya watumiaji ni wa umri kati ya miaka 18-34, hawa hufanya manunuzi kwa ushawishi wa mitandao ya kijamii. Hapa ni muhimu sana ukiwa na website yako. Kwanini, Kwasababu website yako inaelezea kiundani sana kuhusu biashara yako pamoja na bidhaa/huduma zake. Unawezaje sasa kupata website yako? Gusa hapa kujua utaratibu.

FAIDA ZA MITANDAO

Sasa twende kuziona faida ambazo mitandao ya kijamii inaweza kuiletea biashara yako na kuweza kukusaidia kukuunganisha na wateja, kushirikisha, kukuza na kuimarisha biashara yako zaidi.

1. KUKUZA UTAMBULISHO WA BIASHARA: Ikizingatiwa nusu ya idadi ya watu duniani ni watumiaji wa mitandao, kumbe basi matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ni mbinu bora ya kuhakikisha biashara yako inajulikana zaidi duniani. Mfano tizama ilivyo ngumu kutangaza biashara mtaani katika kulipia gharama za matangazo ya televisheni na redio.

2. KUHUISHA BIASHARA: Siku hizi imekuwa ngumu sana kuamini bidhaa/huduma mpaka upate uthibitisho hai. Yaani uhakikishe hio biashara/kampuni ipo kweli na si matapeli. Hivyo, kupata wateja unatakiwa uonyeshe sehemu inayoishi (human side) ya biashara yako ambayo ni thamani ambayo biashara yako inaitoa kwa jamii. Mfano; hapa unaweza kueleza faida, umuhimu na namna za kutumia bidhaa/huduma yako. Elimu hii inapaswa iwe inatolewa mara kwa mara kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii. Mbinu hii hufanya biashara yako iweze kuishi katika maisha ya watu kila siku.

3. KUONGEZA TRAFFIC: Machapisho ya mitandaoni huchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza traffic kwenye tovuti yako. Unaposhirikisha maudhui yaliyo kwenye tovuti kupitia machapisho unayoweka kwenye akaunti za mitandao unaiongezea thamani biashara kwenye shughuli za watu za kila siku kwa wao kuzidi kutembelea tovuti yako.

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni

4. KUONGEZA WATEJA: Bila shaka dhumuni lako kubwa la kufanya biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuongeza wateja. Sasa mitandao hii inakupa njia nafuu zaidi ya kupata wateja wa bidhaa/huduma yako.

5. KUWASILIANA KWA UKARIBU: Ule msemo wa “Dunia ni kama kijiji” umefanya iwe rahisi zaidi kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii. Yaani kupitia mitandao, sasa unao uwezo wa kuwasiliana kwa ukaribu na wateja wako kuhusu ubora wa bidhaa/huduma, kiwango, malipo n.k bila kujali umbali.

Hii imefanya iwe rahisi kutoa Huduma Bora kwa Wateja na kuimarisha uhusiano na ushirikishwaji wa wateja katika kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango pamoja na kuhudumu kwa weledi wa hali ya juu zaidi. Unaposhindwa kufanya hivi unajiweka kwenye nafasi mbaya ya kukosa wateja na kushindwa kimbinu na washindani wako katika biashara.

POINT YA ZIADA: Vilevile ni muhimu kujua watu wanasemaje kuhusu washindani wako kwenye biashara. Utajuaje? Ukifuatilia machapisho ya watu mbalimbali kuhusu washindani wako utagundua udhaifu na matamanio ya watu ambayo wewe unaweza kuyatumia ili kuvuta wateja wengi kwako.

Kwa dunia ya leo ya mtandaoni, mambo yanaenda kwa kasi sana. Na huwezi kukubali kuachwa nyuma kizembe. Mitandao imerahisisha kujua kipi watu wanahitaji kwa sasa na kipi watakihitaji kesho. Hivyo kuwa makini kwenye kufuatilia mahitaji ya wateja wako na soko zima kwa ujumla kwa sababu unapo ijue nguvu ya mitandao ya kijamii katika biashara unapata faida ya kushindana na washindani wengine na kuwashinda kirahisi.

Kiufupi kufanya biashara kupitia Mitandao ya Kijamii kunahitaji Mbinu na Ubunifu. Fanya vyote ulivyovipata leo kwenye makala hii katika mtindo wa MBINU na UBUNIFU. Uko na swali? Tafadhali tunakukaribisha kupitia comments hapa chini. Hakikisha una kushare ili makala hii iwafikie wengi zaidi.

Vyanzo: https://www.forbes.com/sites/forbescommunicationscouncil/2018/05/11/how-social-media-can-move-your-business-forward/?sh=60e12c604cf2

https://coschedule.com/blog/benefits-of-social-media-marketing-for-business

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu(website design, logo design, Digital consultacy n.k) BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.