JINSI YA KUANZISHA WEBSITE
Japokuwa anafanya vizuri mno katika biashara ya kusambaza vifaa vya miundombinu ya maji (mabomba, koki, elbow n.k) huku akipata tenda nyingi kupitia mfumo wa TaNEPS, lakini alitamani sana jinsi ya kuanzisha website na kufikisha bidhaa zake kwa watu binafsi mbali na serikali na mashirika ya kimataifa ambayo amekuwa akifanya nayo kazi. Katika stori hii ya leo utashuhudia siri za kuzingatia jinsi ya kuanzisha website ili biashara yako izidi kushamiri huku mtandaoni. Makinika.
Sasa jamaa yetu huyu yuko busy sana na hio miradi yake kiasi kwamba hana muda wa kuandika makala kwenye mitandao au kupush hashtags au kutweet na kupost mara kwa mara kuhusu huduma anazotoa. Hata hivyo aliazimia kufanya kazi na watu binafsi, mahoteli, shule binafsi, hospitali n.k.
Huwa anazunguka nchi nzima akifanya kazi na serikali na mashirika ya kimataifa kuhakikisha miundombinu ya maji safi na salama inafika kila kijiji. So kwa nature ya kazi yake, tunaweza kusema jamaa hana Time Advantage ya kutumia mitandao ya kijamii ili watu binafsi waweze kumfahamu, kumuamini na kufanya nae kazi. Hata hivyo experience yake imemfanya aaminiwe na serikali pamoja na mashirika yanayotumia mfumo wa TaNEPS. LAKINI; Jamaa yetu huyu bado alitamani kufanya kazi na watu binafsi, afunge mabomba kwenye nyumba binafsi, hoteli, bar n.k hata hivyo bahati mbaya watu binafsi hawatumii mfumo wa TaNEPS katika kutafuta huduma/bidhaa wanazohitaji. So jamaa akafanyaje?
Mwaka 2018 akafungua ecommerce website ambayo baada ya mwaka mmoja website ile ilishindwa kumletea matunda yale aliyotarajia. Akaishia kusema, “Nilifunga website lakini haikuniingizia hata mia kwa mwaka mzima, nikaamua kuachana nayo.” Hii imeshawahi kukukuta wewe? tuambie kwenye comment hapo chini.

Kama unajua uchungu wa kuwekeza na kuvuna hasara nadhani utakuwa umemuelewa jamaa hapo. So mwaka huu 2022 nikakutana na huyu jamaa yangu, anaitwa Steven (tumuite Stivu leo), akanieleza kuhusu kiu yake ya kufanya kazi na watu binafsi na namna alivyopata hasara ya website mwaka 2018.
Katika maongezi yetu alitamani kutumia Nguvu ya Intaneti na Mitandao ya kijamii ili aweze kufanikiwa katika kuwafikia watu binafsi ukizingatia jamaa yupogo busy na TaNEPS + kukusanya materials na kuzifikisha site hivyo kumfanya asiwe na muda na kuweka updates mitandaoni.
Ushauri huu utakufaa hata wewe, zingatia sana:
1. Hakikisha unafahamu ndani nje kuhusu soko la watu wenye njaa na huduma zako: Hapa Stivu ana advantage upande mmoja kwa kuwa tayari anaaminiwa na serikali na mashirika ya nje. Kimbembe ni watu binafsi. So unapaswa kuwajua wateja wako kwa kupost/kutweet kuhusu bidhaa/huduma zako na thamani unayoitoa kwa mteja pindi atakapoamua kufanya kazi na wewe ajue kabisa kwamba bidhaa/huduma yako itakwenda kumtatulia changamoto yake flani. Hii inapaswa kufanywa mara kwa mara ili kusudi kuchuja na kuwapata watu wanaokufuatilia (followers) na kuwafanya wakujue, wakuamini na baadaye wafanye kazi na wewe.

So hapa Stivu ali #FuataUshauri kwamba anapaswa kutafuta mtu wa kumsaidia kuhakikisha biashara yake inatengeneza ushawishi kwnye mitandao ya kijamii kwasababu yeye mwenyewe hawezi kufanya kila kitu afterall. Hii inaitwa LEVERAGING.
2. Hakikisha jina la biashara yako (Brand Name) ni rahisi kutamkika na kinahusiana na wateja wako:
Hapa kwa Stivu hakukua na shida, lakini kwako wewe inawezekana hujafahamu kuhusu hili. Imagine una mgahawa wa chakula halafu unakuta umeandikwa JOY ELECTRONICS. Imagine yani.
Hii kitu ukitaka kufanikiwa zaidi hakikisha Brand Name yako ipo clear from the beginning, hasa linapokuja swala la Online Business ambapo huku mtandaoni kuna makelele mengi mno. Sema kabisa JOY RESTAURANT (Food Providers in Arusha). Hii itakusaidia kukufanya uwe specific na ujulikane exactly unafanya biashara gani na unapatikana wapi kabla hata mtu hajaanza kujiuliza zaidi.
Hii pia inaipa biashara yako advantage pale mtu anapotaka kufika ofisini kwako kupitia Google Map. Mteja hasumbuki yani kuuliza uliza njiani au kuwa na hofu ya kupotea.
3. Fanya Kazi:
Hata kama tayari biashara yako imeshasimama physically, lakini kama unataka kuihamishia biashara hio mtandaoni; Huna budi kuwekeza muda wako katika kudadisi kuhusu Wateja, Washindani wako ni kina nani, wanafanya nini kufanikiwa kuteka masoko na wewe ufanye nini.
Hivyo, roughly ndani ya miezi 6 ya kwanza unatakiwa kuwekeza masaa 60 kwa wiki (wastani wa masaa 8 kwa siku) ili kuchunguza na kujua namna ya kuandika copies zitakazofanya bidhaa/huduma zako ziuzike mtandaoni. Copies hizo zinaweza kuwa ni makala, tweets, fliers etc.

Ujuzi huu wa COPYWRITING ni muhimu sana na ukiwa tayari kujifunza huwezi kushindwa kuuweza. Hii ndio sumaku ya kunasa wateja huku mtandaoni sasa. Lazima uhakikishe unaandika kile ambacho mteja wako atakiadika akiwa anatafuta suluhisho la changamoto zake.
Kwenye maandishi yako maneno kama “Faida za Tehama”, “Kirefu cha TEHAMA”, “Jinsi ya kuwa na mwonekano mzuri”, “Jinsi ya kufanikiwa katika biashara ya chakula”, “Faida za website”, “mbinu za kutumia Mitandao ya kijamii”, “jinsi ya kuanzisha website”, “mbinu za kufanikiwa katika kilimo”, “nguo za bei nafuu”, “Ofa ya Sikukuu”, “Makosa 10 usiyotakiwa kufanya katika…” nakadhalika.
Ukitazama hapo utagundua maneno hayo ndio haswa huandikwa kwenye mitandao mbalimbali pale mtu anapotafuta kitu fulani, si ndio? Basi na wewe katika maandiko/copies zako hutakiwi kuyaacha kabisa kwa sababu ndo sumaku yenyewe hio.
4. Zifahamu hatua za awali za kufanya S.E.O:
Kwenye makala zetu zilizopita tumejadili kuhusu Teknolojia hii ya S.E.O inavyoweza kuimarisha biashara yako pindi pale mteja anapotafuta huduma kupitia mtandao wa Google. Pitia hapa kwenye tweet yetu kama ilikupita hii hapa chini.
Awali umeona aina za maneno ambayo unapaswa kuyatumia mara kwa mara katika maandiko yako ili kuwanasa wateja wengi zaidi huku mtandaoni. Katika S.E.O maneno hayo huirahisishia google katika kuchambua keywords na kuzipandisha juu pale mtu anapotafuta tarifa. Hivyo, website yenye keywords nyingi ndio huchaguliwa kirahisi katika mtandao wa google na kuwekwa juu ili mtu anapotafuta basi website hio inatokea kwenye nafasi za juu kabisa. Fikiria mtu ameandika “Jinsi ya kupika chakula kizuri cha ndizi” au “jinsi ya kuanzisha website” na mara links za website yako ya mgahawa wa chakula inatokea ya kwanza kabisa pale google. Inafurahisha eh?
Fahamu kwamba mtu hataandika jina la biashara yako pale google akiwa anatafuta suluhisho kwa changamoto zake. Watu hawajali kuhusu jina la website yako hata, watu wanajali kuhusu namna ya kutatua changamoto zao ndio maana ni rahisi sana mtu kuandika hizo keywords nilizokutajia mifano yake hapo awali na hayo maneno ndio haswa hutumika katika S.E.O kuinua website yako mtandaoni. Unahitaji kuyatumia sana maneno hayo katika website yako.
Kwa kifupi unaweza kufanya S.E.O kwa website ya biashara yako mtandaoni kwa Kuilocate kwenye Google Map, Kusajili akaunti za Google My Business na Search Console. Hii itaifanya website yako iweze kuwa-ranked na Google kwenye nafasi za juu pindi mtu atakapokuwa anatafuta huduma.
5. Fahamu kuwa kufanikiwa kupata watembeleaji wengi kwenye website yako (Organic Traffic) kunachukua muda (walau miezi 6 mpaka mwaka):
Katika muda huu unatakiwa ufanye kazi ya kuweka maudhui, kuandika Keywords zinazovutia wateja (copywriting inaingia hapa), kufanya maintenance ili kuhakikisha website yako ina-run kwa kasi mda wowote mtu akiifungua.
Pia ni muhimu kutengeneza Backlinks. Hizi ni links za website yako ambazo zinaatikana kwenye websites na majukwaa mengine ya mtandaoni mf: umeandika makala halafu unaenda kui-share ZoomTanzania, LinkedIn au unaweza kuomba wadau wako wakashare links zako kwenye accounts zao za twitter, medium, facebook au hata kwenye websites zao kama wanazo. Ndio maana tunasisitiza kujenga Business Relationships, yaani uwe na uhusiano mzuri na wafanyabiashara wenzako humu mtandaoni ndo utatoboa.
Kuhusu namna unavyoweza kuifanya website yako iweze kutembelewa na watu wengi zaidi tumeshakuandalia makala maalum hii hapa chini:
KUMBUKA:
Marekebisho ya website huwa hayaishagi daima. Hii ni kwa sababu Teknolojia inabadilika kwa kasi sana na wewe kama mfanyabiashara hutapenda kuona website yako inaonekana vilevile tangu mwaka juzi. Ndio maana unatakiwa kuzurura mtandaoni na kutizama website zingine uone ziko vipi na ujitathmini unawezaje kuhakikisha website yako inaonekana MPYA, bora na yenye kukidhi matakwa ya wateja wako muda wote ili ufahamu jinsi ya kuanzisha website kabla hujafanya makosa zaidi.
Fahamu tu kwamba hutengenezi website kwa ajili yako, HAPANA. Unatengenza website kwa ajili ya wateja wako wapate kitakachowasaidia. So hudumu kwa nguvu zako zote huku ukiongeza maarifa kila leo.

Website yako ndiyo RECEPTIONIST wa ofisini kwako. Hakikisha anapendeza na ana taarifa zote ambazo unataka mteja wako akija azipate.
We jiulize kwanini mara nyingi Wanaume hawakuwagi Receptionists?
Utagundua “Receptionist LAZIMA awe mrembo haswa. Lazima avutie mteja kutaka kuuliza jambo”.
Hiyo kwanzia leo nategemea utakuwa ukiitizama website yako kwa jicho la tofauti na iliyokuwa hapo kabla. Kufahamu Kwanini umiliki website ya biashara yako tafadhali fuatana na makala hii kwa kugusa alama ya link hapa chini:
Kupata website yako imara na mahsusi kwa ajili ya kuimarisha biashara yako huku mtandaoni tafadhali wasiliana nasi kwa kututumia ujumbe kupitia kitufe cha Whatsapp unachokiona kwenye ukurasa huu.
Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?
Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
