UNAWEZA VIPI KUKABILIANA NA HASARA KATIKA BIASHARA YAKO MWAKA 2021 – 2025?
Huwa ni kawaida kwa biashara kupata hasara, hasa zile changa/zinazoanza. Lakini inapotokea biashara inapoteza pesa nyingi kuliko inavyoingiza, Juhudi za dhati zinahitajika kujinasua kwenye tabu hio. Sasa jiulize katika kipindi hiki unaweza vipi kukabiliana na hasara katika biashara yako mwaka 2021 – 2025? Makinika mpaka mwisho wa makala hii kufahamu hizo siri.
Hasara inaweza kuwa katika namna ndogo kama kukosa dili fulani ulikua unafukuzia, kupoteza mteja, kupoteza vifaa vya kazi mpaka hasara kubwa kama kushindwa kulipa mahitaji ya biashara kama bili za umeme, mishahara na gharama za mawasiliano. Hali hii ilivyokutokea ulifanyaje?
Hata hivyo, Mjasiriamali bora huwa hatambuliwi kwa uwepo wa hasara katika biashara, bali Ule uwezo wake wa kudili na mazingira yanayoleta hasara mpaka kuhakikisha biashara inatamalaki kwa faida kutoka kwenye kivuli cha Hasara na majanga. Jinsi ya kupenya kwenye nyakati ngumu, ndipo anapopatikana mjasiriamali bora zaidi. Wahenga walishasema “Bahari tulivu haizalishi nahodha hodari.” Kumbe basi ubora upo kwenye Mawimbi, Hofu, Mkazo(pressure), Wasiwasi, Hasara na Woga.
Kwenye mazingira hayo ndipo Tuzo ya Ubora inapopatikana, Ndipo uaminifu kwa mteja unapojileta ndipo Uchumi unapotengeneza misingi yake na ndipo wateja watakapoongezeka kama sisimizi waonapo sukari. Lakini lazima kwanza ujue unatakiwa ufanye nini unapokuwa katka mazingira kama hayo? Na utajuaje kuwa upo kwenye mazingira hayo hatarishi? Lazima kichwa chako kiwe wazi kwanza kwanza kabla hatujasonga mbele.
UTAJUAJE KUWA BIASHARA YAKO INAJIENDESHA KWA HASARA?
Kiufupi Biashara kujiendesha kwa hasara ni pale matumizi yanapokuwa makubwa kuliko fedha inayoingia. Haya matumizi sio lazima yawe mpya, yanaweza kuwa ni yale yale kama bili za umeme, maji, matangazo, mishahara n.k
Mara nyingi matumizi hayo yako hivyo hivyo (constant). Japokuwa mara nyingi fedha inayoingia huwa haitabiriki hasa kwa bishara inayoanza. Hii inaweza kusababishwa na biashara kutokuwa na wateja wa kudumu, mabadiliko katika mahitaji na uelekeo wa masoko pamoja na ujuzi katika kufanya matangazo na mauzo.

Hata hivyo hali hii haipaswi kuwa ya kudumu. Mara nyingi huwa ni ya mpito tu. Lakini kama biashara yako mara kwa mara inajikuta ikijiendesha kwa hasara, my friend unatakiwa ujitafakari upya jinsi unaendesha biashara. Tafuta ushauri wa kitaalam na ikibidi usimamizi wa karibu(mentorship) kutoka kwa wataalam mbali mbali katika maswala ya biashara na usimamizi.
Hizi hapa ni Dalili za biashara inayojiendesha kwa hasara:
•Biashara haina pesa za kulipia gharama za uendeshaji (umeme, maji, mishahara, malighafi/raw materials, matangazo nk). Ukiona umefika hali hii jua ni Red light hio. Jipange.
•Salio lililopo bank/mobile-money ni 0 au negative (una madeni), na bahati mbaya hujui namna gani utaweza kupandisha salio lako kufikia mahali pa kujimudu. Hapa yani ujue kuwa umeshaishiwa mbinu. Rudi vitabuni/mtandaoni, soma, jirekebishe na waone wataalam wakupe direction mpya.
•Hauuzi kwa kiwango kile ambacho kimepangwa kwenye Business Plan. Hii Business Plan ni muhimu sana kuwa nayo kama mfanyabiashara makini. Hii ndio inabeba mipango na malengo yote ambayo biashara inatakiwa kuifikia ndani ya muda uliowekwa (2yrs, 5yrs, 10yrs etc).
Muhimu sana hio document kuwa nayo. Ukihitaji tafadhali wasiliana nasi kupitia mawasiliano haya WhatsApp namba 0765834754 au barua pepe; info@rednet.co.tz
Biashara za kisasa zinafanywa kwa kuzingatia Ujasusi wa Kiuchumi kwa sana. Na hakuna Ujasusi usio na mipango. Na mipango utaikuta katika Business Plan.
Tuendelee, Sasa unapokuwa kwenye mazingira hayo ya hasara, kuna namna nyingi ambazo unaweza kudili nayo. Leo hii tutadiscuss mbinu 9 za kukabiliana na hasara pindi inapotokea kwenye biashara yako. Namba 7 itakushangaza sana.
1. JIANDAE: Huna haja ya kuweka mipango mingi ya namna ya kukabiliana na mazingira ya hasara, hata hivyo jambo la muhimu zaidi ni Kujiandaa kisaikolojia kwamba Hasara ipo kwenye biashara na inaweza kutokea muda wowote. Matarajio yako yasiwe makubwa kuliko uhalisia. Hapo utafeli.

Kama unadhani kuwa mambo yatakwenda sawia na mipango yako uliyoiweka kukabiliana na hali ngumu, basi siku mambo yakienda tofauti unaweza kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kuliko vile ingetarajiwa. Keep calm and let yourself soar through the storm, like an eagle in the air.
2. TAFUTA NAMNA YA KURUDISHA NGUVU: Nyakati ngumu na hasara kwenye biashara huumiza sana moyo, hudidimiza juhudi na kukatisha tamaa. Lakini kamwe nyakati hizi hazidumu, wanadumu watu imara. Hivyo yakupasa kuwa imara mda wote unakiwa mjasiriamali. Unaweza kujipa mapumziko, likizo ama kujiweka mbali na mazingira ya kazi kwa muda huku ukitafakari kwa kina nini kilikukwamisha na hatua gani unaweza kuzichukua ili kukabiliana na changamoto hizo. Matumizi ya vileo si mazuri hapa kwenye jambo hili.
3. USIAMUE KWA HISIA: Ukiwa kwenye hali ya mkazo huku ukiandamwa na hasara katika biashara, mara nyingi unaweza kujikuta ukiwa na hasira, huzuni, woga na hofu. Huu si wakati wa kufanya maamuzi hasa yahusuyo biashara yako. Tulia na tafuta suluhu kupitia watalaam au marafiki wema.
4. KUWA NA MTANDAO SAIDIZI: Hapa nazungumzia jumla ya watu wote unaokutana nao kila siku katika shughuli za kibiashara na kazi. Hawa watu wanapaswa wawe wasaidizi wako pale utakapowahitaji. Unapaswa kuwa na watu ambao ni assets na uepuke wale ambao ni liabilities (mzigo).

5. TATHMINI HALI YAKO: Hasara ni funzo moja zuri sana katika maisha ya biashara imara. Ni nafasi yako kujifunza wapi ulikosea na nini unapaswa kufanya ili wakati ujao hasara ipungue au iondoke kabisa biashara izalishe faida tu. Utumie vizuri wakati huu kufanya uchambuzi yakinifu.
6. USIISHI KWENYE HASARA: Katika historia hakuna mtu ambaye alifanikiwa sana na hakupata hasara. Kila shujaa unayemjua, pamoja na mafanikio yake, lakini wakati fulani alishapata hasara. Kinachomfanya mtu kuwa shujaa ni uwezo wa kunyanyuka na kutoruhusu hasara kuathiri utendaji.
7. TENGANISHA HASARA YA BIASHARA NA UTENDAJI WAKO BINAFSI: Ni ngumu mno kutenga mambo ya kibiashara na maisha binafsi. Kama biashara yako imepata hasara, ni biashara sio mkeo nyumbani au watoto au wewe binafsi, ndugu au marafiki. Usijilaumu wala usimlaumu mtu. Focus na biashara na hakikisha utendaji wa biashara hauathiri amani na utulivu ukiwa katika mazingira ya nje ya kazi. Watu wengi wamejikuta wakiingia katika migogoro mikubwa katika ndoa, familia na marafiki kutokana na kuchanganya biashara na undugu. Ni vitu visivyochangamana asilani na umakini mkubwa sana unahitajika kiuweledi katika kusimamia misingi ya kibiashara katika mahusiano ya familia.
8. ELEWA MAZINGIRA UNAYOJIHUSISHA NAYO: Mbinu bora zaidi ya kumshinda adui ni kumjua vizuri adui huyo. Kamwe huwezi kupigana na adui ambaye humjui sawia. Hivyo chukua muda kujua kwanini unapata hasara na ufanyeje ili hatimaye uweze kupata faida.
9. JIFUNZE: Vyovyote itakavyokuwa, maisha lazima yaendelee. Lakini kuendelea kujifunza ndio jambo muhimu ambalo unapaswa kulifanya mara zote. Maisha ya mfanyabiashara ni mfululizo wa mafunzo yasiyokwisha. Hivyo usikaze mishipa ya shingo, jifunze kila inapobidi ili kujiimarisha.
Pamoja na yote, kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na hali ngumu na hasara. Hata hivyo mbinu ulizozipata leo zimethibitishwa kitaalam katika kuokoa biashara yoyote katika janga la hasara. Share, reply ili elimu hii iwafikie wafanyabiashara wengi zaidi.
Pitia makala hizi hapa ambazo zinarandana na somo ulilolipata hapa leo. Zitakusaidia sana:
- KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?
- FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA
- BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA?
- WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?
Umegundua nini baada ya kumaliza makala kuhusu unaweza vipi kukabiliana na hasara katika biashara yako mwaka 2021 – 2025? Share nasi mawazo yako katika comment hapo chini..