TEKNOLOJIA YA HUDUMA ZA FEDHA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (FINTECH)
Uchumi wa Africa mpaka sasa hukua kwa kutegemea sekta za asili kama kilimo, ufugaji na biashara. Hata hivyo ujio wa teknolojia ya huduma za kifedha kwa njia ya kielektroniki (Fintech) utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha uchumi katika kufanikisha maendeleo kiujumla. Sasa tuangalia teknolojia ya huduma za fedha kwa njia ya kielektroniki (fintech), zina mchango gani kwako leo?
Uchunguzi umeonyesha kwamba matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi yameongezeka sana ndani ya miaka 10 iliyopita ambapo imeonekana eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ndio limekuwa kinara wa kubuni na kutumia huduma hizi za kifedha kwa kutumia simu za mkononi duniani kwa sasa.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Fedha duniani (IMF) umebaini kwamba takriban 10% ya pato la taifa katika miamala ya kifedha hufanyika kwa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi. Hii ni matokeo bora zaidi ukilinganisha na 7% ya GDP katoka bara Asia na chini ya 2% ya GDP kutoka sehemu zingine za dunia.
Sasa swali, hii Fintechs ni nini!? Na ina manufaa gani kwa wafanyabiashara walio Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara?
Shirika la EY linaifafanua FinTech kama Shirika/Kampuni inayojumuisha ubunifu katika utendaji wa biashara pamoja na technolojia ya programu za kompyuta katika kubuni, kuwezesha na kusambaza huduma za kifedha. Hizi FinTechs zinaweza kuwekwa kwenye makundi mawili;
i. FinTechs zinatoa huduma za kifedha e.g TALA App.
ii. FinTech zinazowezesha huduma za kifedha Vodacom na MPESA n.k (tutayajadili zaidi kwenye makala zetu zijazo)
Sekta hii ya FinTech katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) inajumuisha zaidi ya makampuni 260 ambapo 80% katika hizo ni kampuni za ndani na 20% ni kampuni za kimataifa. Vile vile imeonekana idadi ya makampuni haya mapya imeongezeka katika kiwango cha CAGR (Compound Annual Growth Rate) cha 24% ndani ya miaka 10 iliyopita.
Hata hivyo ripoti zinaonyesha kwamba Afrika Mashariki itaendelea kuongoza katika ukuaji wa sekta hii kwa 6.3% ya ukuaji wa uchumi mwaka huu 2019. Hii ni kutokana na Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Uganda zote zinatarajia kurekodi pato la Taifa la zaidi ya 6% mwaka huu ambayo ni zaidi ya nchi zilizo maeneo mengine ya Africa. Hii ni kutokana na uwekezaji katika miundombinu na utanuzi wa huduma za kifedha na mawasiliano.
Takriban theluthi moja (1/3) ya michango ya harambee zilizofanyika barani Africa mwaka 2017 iliwezeshwa na kampuni za FinTechs. Hii inatiliwa mkazo kwa kuwa 60% ya akaunti za huduma za kifedha kwa njia ya simu duniani zimegundulika kuwepo katika eneo la SSA. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanya na benki ya Ecobank.
Pia imeonekana sekta hii ya FinTechinaendelea kuwa imara katika muda wa miaka 3 kutoka makadirio ya dola za kimarekani 200 milioni mwaka 2018 hadi 3$ bilioni mwaka 2020. Kiasi kikubwa cha uwekezaji katika muda huu kimeonekana kuelekezwa Kenya, Nigeria na Afrika Kusini. Vile vile inategemewa kwamba kufanikiwa kwa Fintechs katika nchi hizo kutatanua mafanikio katika nchi zingine za Kiafrika.
MAENDELEO: Ujio wa FinTechs umebadili sana jinsi ya kufanya biashara duniani. Kutoka Crowdsourcing ambayo ni njia inayotumika kufanya usaili wa miradi mbalimbali mtandaoni kupitia intaneti na kupokea ruzuku, mpaka njia ya huduma za kifedha kwa njia ya simu. Wafanyabiashara na wajasiriamali hawajawahi kupata njia rahisi zaidi kwenye utandaji wa biashara zao kwenye maswala ya fedha kuliko hii.
Kupitia Fintechs sasa wafanyabiashara wanaweza kusambaza bidhaa/huduma kwa watu mbali mbali na kupata malipo ndani ya muda mfupi zaidi. teknolojia ya huduma za fedha kwa njia ya kielektroniki (fintech) inazidi kujisombea watumiaji kwa sababu inaonyesha namna inavyoweza kusaidia katika kujikwamua kwenye maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni.
TEKNOLOJIA YA HUDUMA ZA FEDHA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (FINTECH) HAINA MIPAKA:
Kutuma pesa nje ya mipaka ya nchi napo imekuwa rahisi zaidi. Mfumo huu ulioondoa mipaka ya kijiografia kwenye kurusha pesa umepunguza gharama kutoka ilivyokuwa mwanzo kwa njia ya benki ambayo ni ghali mno. Hivyo FinTech imewawezesha wajasiriamali na viwanda vidogo kutuma na kupokea pesa kwa gharama ndogo zaidi.
KUONGEZA THAMANI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA: Eneo hili limetawaliwa na ubunifu ambao unawezesha kuongezeka kwa thamani katika matumizi ya huduma za kifedha. Kwa kuyumia malipo kwa njia ya simu, wateja walioko kusini mwa Jangwa la Sahara wanapata uwezo wa kupata huduma za kibenki kupitia simu za mkononi (mobile banking) pamoja na huduma zingine kama kugungua akaunti, kuchukua mkopo, kupata bima, kupata huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na masoko ya hisa. Haya yote kupitia FinTech yanawezeshwa kirahisi tuu katika simu yako ya rununu (smartphone) au laptop.

Makala haya ya leo yamelenga wafanyabiasha kujidhatiti kidijitali kwa kutumia teknolojia za kisasa katika biashara zao za kila siku ili kuweza kunufaika vyema na masoko pamoja na fursa kede ndani na nje ya nchi. Umejifunza nini hapa katika teknolojia ya huduma za fedha kwa njia ya kielektroniki (fintech) leo?
Zaidi unaweza kupitia makala hizi hapa chini ili kupata ufahamu mpana kuhusu biashara za mtandaoni:
- MAGEUZI YA INTANETI (IoT) KATIKA BIASHARA NA MAISHA
- IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO
- UNAFAHAMU NINI KUHUSU BIASHARA ZA KIELEKTRONIKI (e-COMMERCE BUSINESS)?
- FAHAMU KUHUSU BIASHARA YA FEDHA ZA KIDIJITALI (CRYPTOCURRENCY BUSINESS)
Ukiwa na lolole, tafadhali unaweza kuwasiliana nasi kupitia comments section hapo chini;