Tag: mobile applications

fahamu kuhusu teknolojia katika sekta ya habari na burudani.

FAHAMU KUHUSU TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA HABARI NA BURUDANI

Baada ya zaidi ya miaka 10 tangu vuguvugu la mapinduzi ya kidijitali lilipoanza kushika kasi barani Africa, sekta ya Habari na Burudani ambayo inawavutia vijana wengi zaidi kwa sasa imeingia katika ukurasa mpya ambapo sasa sekta ya habari imekuwa ikiendeshwa kwa msaada wa teknolojia kwa kiasi kikubwa sana. Leo sasa, uta fahamu kuhusu teknolojia katika sekta ya habari na burudani. Kuna nini humo? Makinika mpaka mwisho..

Sekta hii iliyogawanyika kwenye maeneo kama Matumizi ya IntanetiTelevisheni, Sinema, Video Games, MagazetiMajaridaVitabuMuzikiRedio na kadhalika imechagizwa sana na mapinduzi yasiyozuilika ya Intaneti barani Afrika ambapo matumizi ya simu za rununu yamejenga msingi imara kama chanzo cha maboresho, ubunifu na mapato katika sekta hii.

Changamoto; Je, Teknolojia inabadili vipi sekta hii maarufu ya Habari na Burudani barani Africa?

Kwenye makala hii tutagusia changamoto chache zinazosibibu sekta hii maarufu kabisa. Lakini kwa undani zaidi wa changamoto hizo pamoja na jinsi ya kupambana nazo, tips, ofa mbalimbali na ushauri huwa tunashare kupitia status zetu za WhatsApp, utaipata kwa kugusa namba yeu hii hapa 0765834754. Make sure umeisave kisha nitumie text yenye jina lako ili uanze kufaidi elimu ya BURE kabisa.

Makampuni, Wafanyabiashara, Wasanii na Mashirika ya serikali wanatilia mkazo katika kubuni huduma na bidhaa bora kila siku katika kuboresha utendaji wa sekta hii maarufu na inayopendwa zaidi na vijana barani Afrika ambapo tukianzia nchini Kenya sekta hii ilionyesha ukuaji wa 17.0% katika mwaka 2017, ukuaji ukichagizwa na maendeleo makubwa katika eneo la Matumizi ya Intaneti.

Vile vile ongezeko la watu katika kiwango cha CAGR (Compound Annual Growth Rate) cha 11.6 litaipaisha sekta hii mpaka kufikia pato la dola za Kimarekani bilioni 2.9 kufikia mwaka 2022 kutoka $ 1.7 bilioni zilizorekodiwa mwaka 2017. Karibu wateja wapya milioni 15 wanatarajiwa kuwa mtandaoni ndani ya miaka 4 ijayo, na zaidi kunatarajiwa kuwepo kwa huduma za kasi ya juu za intaneti.

Katika huduma za kifedha; MPESA imerahisisha sana malipo ya bidhaa/huduma mbalimbali nchi kenya na hivyo kufanya sekta ya Habari na Burudani kuzidi kuimarika.

fahamu kuhusu teknolojia katika sekta ya habari na burudani.

Huduma za Televisheni; Kenya ni moja ya nchi mwanzo barani kufanikiwa kuhamia katika mfumo wa kidijitali ambao umefungua fursa nyingi zikiwemo huduma za televisheni na utengenezwaji wa mawaidha kidijitali. Hali hii imeibua ushindani mkubwa katika eneo hili ambao unazidi kupeleka mbele na kunogesha maendeleo ya sekta hii ya Habari na burudani.

Kwa kuongezea ujio wa makampuni kama Kwese TV na Startimes ambayo hutoza kiwango kidogo zaidi cha malipo ya huduma zao kwa mwezi, kumeongeza ushindani kwa kiasi kikubwa dhidi ya kampuni kongwe ya Multichoice katika utoaji wa maudhui ya televisheni nchini Kenya.

Redio; ongezeko la huduma na vifurushi katika mashirika ya Redio unakuza kwa kiasi kikubwa sekta hii ambavyo hutoa matangazo ya biashara mbalimbali mtandaoni na katika magazeti. Redio nyingi sasa zinalazimika kuhamia katika mtindo wa mobile applications ili kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza wigo wa mapato yao.

TANZANIA:

Sekta hii ya Habari na Burudani inakuwa kwa kasi sana nchini humo ambapo kwa mwaka 2017 sekta hio iliingiza pato la dola za kimarekani milioni 496 ukiwa ni ukuaji wa 28.2% kwa mwaka. Ongezeko la watu kwa kiwango cha CAGR cha 18.3% utashuhudia mapato ya sekta hio kufikia $1.1 bilioni mwaka hadi mwaka 2022 ambayo ni mara 2.3 zaidi kulinganisha na ilivyorekodiwa mwaka 2017.

Kiujumla ni Nigeria peke yake katika Africa ndio imeizidi Tanzania katika kasi ya ukuaji wa sekta hii ya Habari na Burudani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la PwC. (Wabongo mnatisha kwa habari na bata 😂).

Internet; Kitakwimu kunatagemewa ongezeko la watumiaji wa huduma za 4G ambapo makampuni ya Vodacom na Zantel tayari yalishazindua huduma zao za 4G LTE tangu robo ya pili ya mwaka 2016. Mwaka 2017 TIGO walitangaza uwekezaji wa $70 million ili kutanua wigo wake wa kimtandao na kujiandaa na matumizi ya kasi ya 5G. Hata hivyo mpaka kufikia mwaka 2022, huduma ya kasi ya intaneti ya 3G bado itaendelea kutumika zaidi kufikia takribani 70% ya watumiaji.

Televisheni; matumizi ya huduma za ving’amuzi na televisheni yatapaa kutoka watumiaji 200,000 waliorekodiwa mwaka 2013 mpaka watumiaji 900,000 kufikia mwaka 2022 kwa huduma za televisheni za majumbani. Watumiaji wengi pia hutumia huduma za ving’amuzi kutoka kwa makampuni ya Multichoice na Startimes.

Magazeti; Ukiachana na matumizi ya intaneti yanayoshika kasi nchini Tanzania. Magazeti pia yanaongeza chachu katika uboreshaji wa sekta hii ya habari na burudani ambapo matumizi rasmi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza yamekuwa nguzo muhimu.

Lakini kwa Tanzania nyanja ya magazeti inakwenda ikibadilika kwa kasi, kwa mfano kampuni ya Vodacom imebuni application ya M-Paper ambayo imewezesha kupatikana kwa vichwa vya habari vya magazeti maarufu zaidi nchini na hivyo kufanya upatikanaji wa habari kuwa mkubwa zaidi.

Ikiwa na jumla ya mapatoyaliyotokana na matangazo kufikia dola za kimarekani milioni 91 katika mwaka 2017 na kutabiriwa kufikia $128 milioni mwaka 2022, ni dhahiri sekta ya habari na burudani inakuwa sawia nchini humo na hivyo kuchipusha milango mingi ya kibiashara kuendelea kufanyika.

AFRIKA KUSINI:

Ongezeko la watu katika nchi hii linatajwa kuwa imara kwa kiwango cha CAGR cha 7.6% kwa mapato ya watumiaji wa sekta hii ya habari na burudani kufikia mwaka 2022 ambapo mapato yatapaa kutoka Randi 93.9 bilioni zilizorekodiwa mwaka 2017 mpaka kufikia Randi 135.7 biloni mwaka 2022.

Ukiachana na mapato yanayotokana na matumizi ya Intaneti (ambayo huchagizwa na mapato yatokanayo na applications za simujanja) kuna uwanja mkubwa zaidi wa mapato ambayo huongozwa na michezo ya video (video games). Mapato kutoka kwenye michezo hii nchini SouthAfrica yanazidi maeneo mengine kama vitabu, Business-to-business (B2B) na mauzo ya majarida. Ukuaji huu katika eneo la michezo ya Video umekolezwa na ongezeko la matumizi ya simujanja, uboreshwaji wa huduma za kasi ya intaneti kutoka 3G mpaka 4G kuzidi kuongezeka jambo ambalo linaifanya watumiaji wa Afrika Kusini kuwa ni wacheza games 😁.

Televisheni; Kama ilivyotegemewa, huduma za TV na Video zitaendelea kuongoza katika kuzalisha mapato ya watumiaji, lakini muda mchache ujao Kampuni kama Netflix na Amazon Prime huduma zao zitachukuliwa kama nyongeza kunyongea kwa maudhui yao ya burudani katika soko la Afrika Kusini. Vile vile malipo ta TV yataongeza Randi bilioni 6 mpaka kufikia mwaka 2022 kwa kiwango cha 5% ya CAGR japokuwa ukuaji wa mwaka-kwa-mwaka unategemewa kuoungua kwa 2.6%.

Matangazo; nyanja hii iliathiriwa zaidi katika mwaka 2017 na mazingira ya uchumi wa Afrika Kusini ambapo kulikuwa na ukuaji wa tahadhari wa 2.1% tu mwaka kwa mwaka. Hata hivyo, maboresho yanategemewa mpaka kufikia mwaka 2022, ikiwa na 3.3% ya CAGR ambayo itapaisha mapato zaidi.

Makala haya ya leo yamelenga wafanyabiasha kujidhatiti kidijitali kwa kutumia teknolojia za kisasa katika biashara zao za kila siku ili kuweza kunufaika vyema na masoko pamoja na fursa kede ndani na nje ya nchi.Umejifunza nini leo kwenye ku fahamu kuhusu teknolojia katika sekta ya habari na burudani.

Makala hizi hapa zitakupa taarifa zaidi kuhusu Teknolojia ya Habari na Burudani katika biashara yako:

  1. IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO
  2. BANDO LAKO NI MTAJI
  3. FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA

Ukiwa na lolole, tafadhali unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Karibu sana REDNET TECHNOLOGIES