Tag: mauzo

thamani vs gharama, nafuu iko wapi? fahamu siri za kuweza kushawishi wateja katika biashara yako.

FAHAMU SIRI YA KUWEZA KUSHAWISHI WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO

Umeshajiuliza, mtu mmoja anaweza vipi kuweka kitu mtandaoni akapata wateja wengi sana au kuzua mjadala kubwa sana, lakini wewe kila ukijaribu kuweka bidhaa/huduma zako bado hupati muitikio unaotakiwa? Nini huwa kinafanyika? Leo sasa fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako. Uko tayari?

Kuwa na mafanikio katika biashara kuna maana kwamba Mfanyabiashara ambaye ndiye mhusika mkuu ameweza kushawishi wateja kuweza kununua bidhaa/huduma zake kwa wingi. Hivyo mfanyabiashara lazima awe na maarifa/skills za kutosha ili kuweza kushawishi na kuuza kwa mafanikio.

MAARIFA HAYO NI YEPI?

Iwe ni kwenye mitandao ya kijamii, serikalini au mtaani, ili kuweza kuwa na ushawishi popote pale alipo mfanyabiashara, basi hana budi kuhitimu mafunzo katika nyanja ya kushawishi na kuuza (copywriting and closing skills). Mafunzo hayo si lazima uyapate darasani, leo hii utayapata hapa, soma makala hii mpaka mwisho tu:

1. MBINU YA MUITIKIO (RECIPROCITY): Kisaikolojia binadamu hujihisi kuwa na umuhimu pale anapouliza jambo fulani na kupata majibu ya kupendeza. Majibu mazuri humfanya mteja kuhitaji kuuliza/kuchimba zaidi ili aweze kupata hitaji lake ambalo mwishoni huangukia kwenye kununua. Unachotakiwa kukifanya hapa kama mfanyabiashara ni KUMSAIDIA mteja wako KUNUNUA na sio KUMUUZIA tu ilimradi upate pesa. Ukiuza tu unakuwa huna tofauti na wauzaji wengine unaowaona huko barabarani. Wewe unataka kuwa tofauti nao, si ndio?

Mfano: Kwenye mtandao wa twitter kuna watu wanaojiita “mabroo” (wale wenye followers wengi) ambao watumiaji wengi wa kawaida huwalalamikia kwa kushindwa kushiriki kwenye midahalo ya watu wengine isipokuwa wao wenyewe kwa wenyewe.

Sasa ukiwa mfanyabiashara hasa wa mtandaoni, sio lazima uwe na followers wengi ndo uwe na mafanikio, cha msingi ni kuwa na uwezo wa kumjengea mteja aitikie kile unakitoa kwake, na muitikio huo huanzia kwako kwa kujihusanisha nao kwenye mijadala na changamoto wanazokushirikisha kila mara. Hii ni kwasababu silaha kubwa unayoweza kuitumia kunasa wateja wengi zaidi ni kutengeneza MAHUSIANO mazuri na wateja wako. Hapo ndipo unapo fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako sasa.

mbinu ya muitikio katika biashara (reciprocity)
fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako

2. UFUNGANI (Commitment): Mara nyingi mtu akishajifunga kwenye jambo fulani, hubaki hapo akichuma anachokitaka. Sasa lazima uhakikishe biashara yako inakuwa kama Mgodi kwa wateja wako kuendelea kufaidi madini ambayo yamo kwenye biashara. Kwamba, lazima biashara yako itengeneze sumaku ya aina yake ili kuweza kushawishi na kunasa wateja wengi kila siku. Hizi ni zile Mbinu za kuweza kulifikia soko kubwa zaidi mtandaoni. Mfano wa sumaku muhimu ni TAARIFA, yaani ikiwa unauza viazi, basi wape wateja wako taarifa nyingi kuhusu viazi, kama unauza spare za magari waelimishe kuhusu spares mbalimbali za magari, kadhalika kwenye biashara zingine. Hii inapasawa kuwa inafanyika mara kwa mara, tena inaleta tija zaidi ikiwa itakuwa inatolewa BURE.

mbinu ya ufungani (commitment) katika biashara

Yaani hakikisha taarifa kuhusu unachouza au kuhudumu hazikauki kwa wateja wako. Kwa njia hii ndipo unapoweza kutengeneza sumaku ya kushawishi wateja wengi zaidi kujifunga katika biashara yako na kukuletea mafanikio unayoyaota. Na njia bora ya kutoa taarifa ni kupitia Website. Biashara yako ina website? Kama unayo hakikisha unaitumia vyema kwa ukuaji imara wa biashara yako. Zaidi unaweza kujua namna ya kutumia website kikamilifu kupitia hapa WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?.

3. KUWA NA MAMLAKA: Hii ni siri muhimu sana. Watu hufuata na kusikiliza ushauri kutoka kwa mbobevu/mtaalam katika jambo fulani kuliko mtu yeyote tu asiyefahamika kwa utaalam fulani. Yaani ili uwe mtaalam lazima usome sana, uwe na uelewa mpana juu ya jambo fulani na uwe na confidence katika uwasilishaji wako ambayo itakupa mamlaka ya kutengenezea ushawishi unaotakiwa.

Hivyo, unapoongelea kuhusu bidhaa/huduma zako, ongea kama Mtaalam na sio muuzaji. Ukiongea kama mtaalam kwanza utajiamini zaidi, halafu zaidi utakuwa na mamlaka katika uwasilishaji wako jambo ambalo linavuta watu wengi kufanya biashara na wewe. Jaribu hii utanipa majibu yake.

4. UFANANO: Katika mbinu kongwe zaidi ambayo imetumika kutengeneza ushawishi duniani ni hii. Hata kwa waamini wa dini ya Kikristu mfano, imeandikwa “Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake“. Yani Neno wa Mungu akajitwalia mwili ili afanane na watu ili lile kusudio lake la kuwaokomboa watu likapate kutimia.

Hali kadhalika katika biashara yako, lazima uhakikishe unatengeneza ufanano kati ya biashara yako, wewe mwenyewe pamoja na wateja wako. Hii hufanyika ili mteja ajiamini na kujihisi huru anapokujia ili aweze kutimiza hitaji lake.

mbinu ya ufanano katika biashara. Unafanana vipi na mteja wako?
fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako

Kumbuka biashara sio sehemu pa kujimwambafai kama wafanyavyo baadhi ya watu wa mitandaoni. Biashara ni watu, na watu lazima ujumuike na ufanane nao katika midahalo yao ya mara kwa mara ili kusudi waweze kukwambia mahitaji yao ambayo wewe ndiye mwenye dhamana ya kuyatimiza.

5. UADIMU (SCARCITY): Mara nyingi watu hupenda kumiliki vitu ambavyo wanavyovipenda na hawana. Mifano ipo mingi tu huko mtaani, jazia hapo. Unapouza bidhaa/kutoa huduma adimu/ambayo itakwenda kuisha baada ya muda fulani, watu hufanya haraka kununua ili wasije wakaikosa pindi itapopotea. Hivyo unapaswa kuzifanya bidhaa/huduma zako kuwa katika kiwango fulani cha uadimu ili kusudi umtengenezee mteja wako kiu ya kutaka kununua haraka iwekanavyo.

6. MKUMBO (BANDWAGON): Nadhani umeshawahi kuona hii. Hutokea pale bidhaa/huduma fulani inapotumiwa sana na watu fulani ambapo husababisha watu wengine kuitumia huduma hio. Mbinu hii imekuwa ikitumiwa sana na makampuni makubwa kwa kuwatumia wasanii/watu wenye ushawishi kwenye jamii ili wawe mabalozi na kutengeneza hali ya “mkumbo” ambao utasaidia bidhaa/huduma yao ikapate kutumika kwa wingi zaidi katika jamii. Kitaalamu mbinu hii hufanya kazi sana kuanzia maeneo ya Uswazi. Kama ulikua hufahamu, yaani fasheni zote kali za mjini huwa zinaanzia uswazi, mitindo ya kusuka, vyakula vizuri vipo huko, misemo, bidhaa nakadhalika.

Aina hii ya ushawishi si wafanyabiashara wote wanaiweza kuifanya na wala si dhambi ila ukiiweza ni moja ya mbinu bora kabisa katika kuhakikisha biashara yako inakuwa na ushawishi wenye tija kwa wateja wako. Unaweza kutengeneza mkumbo ili upate kutengeneza ushawishi wenye tija? Hebu tuone majibu yako..

SASA KWANINI MTEJA AKUCHAGUE WEWE?

Sio siri tena kuwa hisia ni silaha muhimu sana katika kujenga ushawishi katika biashara yako. Lazima uhakikishe unazijua vyema hisia za wateja wako na kuzitendea haki ipasavyo. Ufanyaje sasa ili kutibu hisia za wateja wako? Hakikisha una fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako hizi hapa.

1. WAFANYE WAJIHISI WAKIPEKEE: Kiafrika, mgeni anapokuja kwako hata kama kuna vita humo nyumbani, basi ni muda wa kuzika tofauti zote ili kuhakikisha mgeni anakirimiwa inavyotakiwa. Hii hufanyika ili mgeni huyo ajisikie vizuri na kwenda kutangaza yale mema aliyoyapata kwako.

Kunazo mbinu nyingi za kumfanya mteja akajihisi wa kipekee. Mfano kutabasamu na kusalimiana vizuri na watu kabla ya kwenda direct kwenye mambo ya kuuziana. Lengo ni kuendeleza ukarimu na hali ya urafiki makini katika kuhudumia mteja wako mara zote. Jambo hili ndilo huvutia zaidi.

unawezaje kupata wateja mtandaoni?
fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako

2. MSHIRIKISHE MTEJA KWENYE MAAMUZI: Moja kati ya vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote awe mteja wako ni kitendo cha kumshirikisha katika maamuzi hasa yale yanayohusu namna ya kumhudumia kwa viwango. Washirikishe kwa njia ya kushikana mikono, bega au simu zenu za mikononi. Maamuzi ni muhimu sana na yanaathiri mwenenedo wa biashara kwa kiasi kikubwa sana. Hakikisha muda wote unafanya maamuzi sahihi. Unawezaje kufanya hivyo? Fuatana na mada hii hapa chini;

Jambo hili hutengeneza hali ya umiliki wa huduma/bidhaa kwa mteja hata kabla manunuzi hayajafanyika, kitu ambacho huchangia kiasi kikubwa mteja kuchagua kufanya biashara nawewe. Unaweza kucomment “viatu hivi unavyoviona vinakwenda sambamba na hio suruali yako, unaonaje ukakichukua hiki?” inachagiza sana mauzo mbinu hii.

mteja mshirikishe kwenye maamuzi. Msaidie aweze kununua huduma au bidhaa yako.
fahamu siri ya kuweza kushawishi wateja katika biashara yako

3. SIMULIA STORI: Mteja angependa kufahamu vitu kama, uliweza vipi kuanzisha hio biashara unayoifanya? Ulianzia wapi? Lini? Mteja wako wa kwanza ulimpata vipi? Umepitia changamoto zipi mpaka sasa na changamoto gani huwezi kuisahau? Stori yako inashawishi kwa kiasi kikubwa sana. Unatakiwa ujifunze namna nzuri ya kusimulia stori ili kuvutia wateja wengi zaidi. Stori hizo unaweza kuwa unazisimulia mara kwa mara kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii.

Kwenye hili mitandao ya kijamii ina nguvu ya ajabu sana. Unaweza vipi kuipata na kuitumia nguvu hio? Fuatana na makala hii hapa mpaka mwisho;

4. TOA AHADI ZA UKWELI: Unapomhudumia mteja ni vema ukamhudumia katika misingi ya uwazi na ukweli katika utoaji huduma zako au bidhaa. Kama kuna kasoro yoyote ni heri ukaiainisha mapema kwa mteja ili ajue namna ya kukabiliana na bidhaa/huduma hio. Haipendezi kutokuwa mkweli.

5. TOA HUDUMA KWA VIWANGO VYA JUU: Siku zote huduma bora huenda sambamba na Heshima kwa mteja, kuzingatia muda na kufuatilia kazi. Wasiliana na mteja wako mara kwa mara ili kujua muda wa kumpatia huduma. Cha msingi ni kutoa taarifa muda wowote inapotakiwa kufanya hivyo.

Hizi ndio siri za kushawishi wateja katika biashara yako wazidi kumiminika kila siku. Hakuna miujiza dunia ya leo. Hata hivyo si lazima utumie mbinu zote ulizozipata leo kwenye biashara yako. Unaweza kutumia mbinu moja au mbili au kadhaa ambazo kwa upande wako utaona zinakufaa zaidi. Ukiwa na swali, ushuhuda au changamoto tafadhali share nasi kupitia comments hapo chini nasi kwa pamoja tutajadili ili kuzitatua. Karibu sana Rednet Technologies.

Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

mrahisishie mteja wako huduma za kifedha. Dunia ya leo si ya jana.