UTAJUAJE KAMA KIFAA CHAKO (SIMU/COMPUTER) KIMEDUKULIWA?
Katika makala iliopita kuhusu Kwanini Usalama wa Kimtandao ni muhimu kwako? Mdau mmoja aliuliza, “Sasa nitajuaje kama computer yangu imedukuliwa?” Sasa leo hii nitakujuza dalili 10 muhimu za kutambua kama kifaa chako (simu/computer) kimedukuliwa, utajuaje? Dalili ya 7 itakushangaza sana. Fuatana nami mpaka mwisho wa makala hii katika utajuaje kama kifaa chako (simu/computer) kimedukuliwa? Makinika..
Ngoja nikupe kisa: Mama mmoja alikiri kuwa mumewe alikua akifuatilia nyendo zake na jumbe za kwenye simu kwa kutumia App maalum iliyopandikiza kwenye simu hio. Alipogundua hakulifurahia jambo hilo na kuamua kuripoti polisi kwa kuingiliwa haki yake ya faragha (invasion of privacy) kwa mujibu wa sheria kabla mumewe huyo hajachukuliwa hatua stahiki. Ni kosa la jinai kuingilia faragha ya mtu katika mtandao au mawasiliano pasi na idhini yake. (SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015).
Kwa sasa duniani kunaongezeka matishio ya kimtandao yakihusisha matumizi ya programu halifu za computer (malwares) na kufanya usalama wa kimtandao kuwa katika hali tete kila uchwao. Hata hivyo, watu lazima watumie huduma za internet licha ya matishio hayo. Sasa itakuaje? utajuaje kama kifaa chako (simu/computer) kimedukuliwa?
Sasa kupambana na hali hio, programu nyingi za kuzuia uhalifu wa kimtandao (antimalware programs) zimekuwa zikitumika kufuatilia utendaji wa vifaa zikiitwa HEURISTICS ili kuhakikisha zinapambana na uhalifu wowote mpya. Lakini, uhalifu mbaya zaidi hufanyika pale kifaa kinapoangukia katika mikono ya mhalifu ambapo anaweza kuhamisha/kubadili taarifa ili uhalifu utendeke katika mfumo mwingine nje ya kifaa bila ufahamu wako. Hivyo njia bora ya kudhibiti hili ni kuhakikisha kifaa chako kipo salama katika uangalizi wako muda wote. Hizi hapa dalili 10 muhimu za kutambua kama kifaa chako (simu/computer) kimedukuliwa, utajuaje? Twende kazi..
Sasa Tuzione Dalili za kukijua Kifaa (simu/computer) kilichodukuliwa:
1. Kutokea kwa Ujumbe wenye Tishio la Kutaka Pesa (Ransomware Message): Kama kuna ujumbe ambao hakuna mtu anautaka kuupata katika kifaa chake ni huu wa kutokea kwa ujumbe au Video ghafla katika kioo cha kifaa ukimtaka kutoa kiasi cha pesa ili kutodhuru/kurudisha data zake ambazo tayari zimedukuliwa bila yeye kujua. Kufahamu zaidi kuhusu shambulizi hili la ransomware tafadhali fuatilia makala hii hapa chini
2. Kutokea kwa Browser Toolbars usizozihitaji: Imeshawahi kukutokea unafungua browser yako ukashangaa inafunguka ikiwa na vitufe/tabs/bookmarks ambazo hujawahi kuziona kabla. Hio ni ishara kwamba kunazo malwares zimepandikizwa katika kifaa chako ambazo tayari zimeanza kufanya kazi..
3. Matafuto na machanguo unayofanya katika Internet yanaelekezwa/redirected katika tovuti usizozitambua: Umeshawahi kuona pale unajaribu kutafuta kitu (mf. gari) ukashangaa unapelekwa kwenye tovuti kuhusu urembo wa nywele. Hii ni njia moja wadukuzi huitumia ili kupata clicks za matangazo na kujipatia pesa, japokuwa njia hii haiathiri sana utendaji wa kifaa chako licha ya kusababisha usumbufu katika matumizi ya huduma za internet.
4. Unapata Matangazo sumbufu ya ghafla ghafla (Pop-ups): Hii ishara maarufu sana pale kifaa chako (simu/computer) kinapokuwa kimedukuliwa.
Matangazo (pop-ups) kutoka tovuti usizozifahamu zinakuja ghafla katika kioo chako bila ya kuziamuru na kusababisha usumbufu. Ukiona hivi ujue kifaa chako kimeathirika tayari na malwares.
•Hakikisha unaziondoa toolbars zote usizozifaham katika browser yako mara tu unapozigundua.
5. Nywila/Password yako haifanyi kazi tena: Hii inawatokea watu wengi sana hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii na kupotea/kuibiwa kwa akaunti zao zenye wafuasi wengi, maudhui na kumbukumbu muhimu hivyo kupelekea kuharibika kwa biashara, wawekezaji, hadhi ya mtu katika jamii na usalama binafsi.

•Hakikisha akaunti zako zina uthibitisho zaidi ya mmoja kwa kutumia email au namba ya simu, ili isiwezekane kubadili Nywila pasi na kuthibitisha kupitia email au namba yako ya simu. Hii ni njia salama zaidi.
6. Umegundua kuna programu zimepandikizwa katika kifaa bila ya ufahamu wako: Programu hizi mara nyingi huwekwa ili kufuatilia nyendo zako mtandaoni (unawasiliana na nani, uko wapi, nywila zako za benki, mpesa, tigopesa nk) na unaweza kuziona katika Control Panel ya computer yako(kipengele cha Programs) au kwenye simu katika mkusanyiko wa Apps zako.
•Hakikisha simu/computer yako ina programu zile tu umethibitisha ziwepo ndani ya kifaa chako. Vinginevyo, fanya usafi(futa) wa ndani wa kifaa chako mara kwa mara.
7. Kipanya(Mouse pointer) inapotembea yenyewe na kufanya uchaguzi wa programu na mambo mengine bila ushiriki wako: Isipokuwa tu computer yako imepata hitilafu ya vifaa (hardware problems) au pale inapofanyika shughuli maalum katika mtandao kwa kushirikisha kifaa zaidi ya kimoja kupitia programu mf. Teamviewer ambapo unaweza kutumia kipanya cha computer yako katika computer nyingine (ambalo jambo hili ni halali kisheria na huitwa Ethical Hacking), vinginevyo mouse yako inapofanya shughuli zake pasi na ushiriki wako jua hapo kifaa chako kipo mikononi mwa wadukuzi.
Hapa dhumuni kubwa ni kuiba taarifa/fedha kutoka kwenye kifaa chako, hivyo kuwa makini na hakikisha unapozima kifaa chako zima internet/chomoa na waya wa ethernet (kama inatumia waya wa internet) kisha toa taarifa kwa wataalam wa mitandao au mamlaka za serikali. Katika tukio hili unahitaji msaada wa kitaalam ili kuhakikisha shambukizi kama hili haliji kukutokea tena. Usidharau.
8. Antivirus, Task Manager na Registry Editor za kwenye kifaa chako hazifanyi kazi, zimezimwa au zipo slow: Ukiona Antivirus yako ipo OFF wakati hukuwahi kuizima, Task manager/Registry Editor haifunguki (au inafunguka na kufunga gafla), jua hii inaweza kuwa dalili ya kifaa kuwa hatarini.
•Katika tishio hili fanya Complete restoration ya kifaa chako, kwa kuwa mpaka kufikia hatua hio hujui madhara yamefikia kiwango gani.
9. Akaunti zako kifedha ulizoziunga mtandaoni Hazina/zimepungua Pesa: Wadukuzi mara nyingi hujaribu kuiba pesa katika akaunti za watu zinazotumia huduma za internet mtandaoni. Hii hutokea pale wadukuzi wanapopandikiza malwares katika kifaa chako bila ya wewe kujua kwa kupitia picha, link au email (PHISHING ATTACK). Na hivyo kupata taarifa mbalimbali kuhusu akaunti za benki, hivyo kurahisisha uhalifu wao.

•Kujiepusha na kadhia hii, hakikisha umewasha alerts/notifications kwa kila muamala unaofanyika kuzidi kiasi fulani (threshold amount) ambapo alert hio itatumwa kwa SMS au email kuthibitisha kabla muamala haujafanyika. Hii ni muhimu sana, wasiliana na mtoa huduma wako(bank, mitandao ya simu nk).
10. Taarifa zako za siri zinapovuja bila ya idhini yako: Hakuna kitu kitakuthibitishia kuwa kifaa chako kimedukuliwa kama pale unaona taarifa nyeti za kampuni/biashara yako zimesambaa mitandaoni au kwa watu wasiostahili kuzipata. Kadhia hii ni hatari sana katika utendaji.
•Hakikisha umethibitisha jambo hilo, kisha taarifu uongozi wa kampuni haswa kitengo cha sheria, kisha fuata utaratibu wa kitaalamu katika kupambana na madhara ya shambulio hilo ili lisije kutokea tena.
NOTE: Siku zote kinga ni bora kuliko Tiba. Hakikisha unatumia njia zaidi ya moja, mfano (two steps verification method) kuhakikisha vifaa vyako vinabaki kuwa salama muda wote. Njia za kujikinga dhidi ya mashambulizi ya kimtandao tayari tumezielezea hapo juu na katika makala zetu zingine kupitia tovuti yetu maridhawa ya http://rednet.co.tz
Pia kuna makala hizi hapa ambazo zitakusaida kuimarisha biashara yako kiuchumi katika kuimarisha Usalama wako uwapo katika mitandao. Cha kufanya, gusa link kisha makinika:
- KWANINI UHAMIE WINDOWS 10 KUTOKA WINDOWS 7?
- KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE (TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?
Hizi hapa ndio dalili 10 muhimu za utajuaje kama kifaa chako (simu/computer) kimedukuliwa? Majibu tayari unayo. Ungependa kuuliza swali au kuongezea? tafadhali tuandikie katika comment hapo chini au njoo whatsapp kupitia kitufe cha whatsapp kilichopo katika ukurasa huu.
Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?
Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?
Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
