Tag: makusudio ya biashara

Makusudio (purpose) ya biashara yana umuhimu gani?

MAKUSUDIO (PURPOSE) YA BIASHARA YANA UMUHIMU GANI?

Umeshawahi kujiuliza, Hivi siku biashara yako ikifa, Je, mteja wako au/na Dunia itapungukiwa nini? Unaufanikisha vipi mpango wako wa kuhakikisha biashara yako inakuwa na upekee wake ambao unawavutia zaidi wateja? Makusudio (purpose) ya biashara yana umuhimu gani? Makinika mpaka mwisho hapa ufahamu zaidi..

Bila shaka wakati unaanzisha biashara yako kuna dhamira ambayo ilikusukuma kuanzisha biashara hio. Lakini waswahili wanasema “Mipango sio matumizi”. Kwa hakika umeshashuhudia watu wanapoanza mwaka mpya huwa wanapanga mambo mengi, lakini mangapi huwa yanafanikiwa kufikia December?

Wataalam wanakwambia “ukipanga sana utakufa na mipango yako kichwani”. Unahitaji uthubutu na utekelezaji ili kuhakikisha kile unachokipanga kinafanikiwa. Kusudio (Purpose) la biashara ni utamaduni wa kuendesha biashara katika uelekeo ule ambao wewe mfanyabiashara umeunuia tangu mwanzo. Leo hapa tutashare mambo machache kuhusu umuhimu na jinsi ya kutengeneza hayo Makusudio. Kwa undani zaidi huwa tunashare kila siku kwa wale tu wenye namba yetu ya WhatsApp kupitia status zetu. Gusa namba hii hapa 0765834754 kisha hakikisha unaisave kwenye contacts zako, ukimaliza nitumie text yenye jina lako.

KWANINI UWE NA DHAMIRA/KUSUDI (PURPOSE) KATIKA BIASHARA YAKO?

Hebu anza kujiuliza, “Kwanini ninafanya hiki ninachokifanya”. Share jibu lako kwenye replies hapo chini. Sasa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la EY mwaka 2017 ulionyesha, Wakurugenzi wa Biashara wakisema kuwa wanahitaji kufanya bidii zaidi ili kuhakikisha makusudio (purposes) yao waliyojiwekea katika biashara zao yanaleta mafanikio zaidi hasa katika maeneo ya Uongozi, Mafunzo na Huduma kwa wateja. Hii ina faida gani katika biashara?

i. UKUAJI: Kampuni/Biashara zinazoendeshwa kwa dhamira thabiti walizojiwekea hukua kwa haraka zaidi kuliko zile zenye dhamira dhaifu. Tafiti zinaonyesha kuwa 48% ya kampuni zilizojiwekea dhamira na makusudio ya dhati zimekua kwa 10% au zaidi ndani ya miaka 3 iliyopita ukilinganisha na 42% ya kampuni/biashara ambazo hazikujiwekea makusudio/dhamira kwa maendeleo yao ndani ya walau miaka 5.

Biashara zenye makusudio na dhamira inayoeleweka wa wafanyakazi ndani ya taasisi zimeonekana kuwa uwezekano wa zaidi ya 50% ya kupata masoko Mapya.

ii. KUHUSU MTEJA WA KUDUMU: Japokuwa mission na values zs biashara yako huchangia kwa kiasi kikubwa kupata wateja wa kudumu. Hata hivyo imeonekana 80% ya wakurugenzi wa biashara walikubali kuwa “Taasisi Imara ni ile inayoshirikisha makusudio yake na watu hupata wateja wengi zaidi wa kudumu”.

Jambo ambalo huongeza thamani ya biashara kwa watu kadiri ya siku za kuhudumu zinavyosonga kwa kuwa mteja amepewa nafasi ya kuona na kutambua jinsi kampuni/biashara inamjali katika kutoa bidhaa bora na huduma zinazokidhi mahitaji.

iii. KUHUSU UBUNIFU: Utafiti uliofanya na shirika la Deloitte unaonyesha kuwa Biashara yenye makusudio ya dhati huhamasisha shughuli za ubunifu zaidi kwa wafanyakazi wake kuliko zile zisizo na makusudio yaliyo wazi. Wafanyabiashara wanaozingatia dhamira na makusudio yao ya wazi katika biashara hujiweka katika nafasi ya kunasa ubunifu muhimu ambao utabadili uelekeo wa taasisi kuelekea katika mafanikio.

iv. UKUAJI WA KIUCHUMI: Hatimaye, lengo kuu la biashara/kampuni yoyote ni kuhakikisha Faida inatengenezeka na uchumi unaimarika. Hata hivyo unapokuwa na makusudio yanayoeleweka wazi ni rahisi zaidi kupata faida na kuimarisha uchumi wa biashara kwa kipindi kirefu zaidi.

Imeonekana kuwa na makusudio dhahiri huongeza hadhi ya biashsra katika jamii na kuchochea upatikanaji wa wateja wa kudumu kila kukicha. Hapo Makusudio (purpose) ya biashara yana umuhimu gani? Umeshaanza kupata picha sasa?

UNAWEZAJE KUTENGENEZA MAKUSUDIO YA BIASHARA YAKO?

Faida za kugundua makusudio ya biashara yako ni kubwa na zisiyopingika. Lakini Unapataje “Kusudi” la Biashara/Kampuni yako? Tuone hatua zifuatazo za kutengeneza Makusudio ya kuanzisha na kuendesha biashara yako.

Hatua 1: Pitia zile Core Values za biashara yako. Ni mambo yapi ambayo biashara yako inayajali zaidi (mf; Heshima, Uwajibikaji, Kuchapa Kazi, Upendo n.k) Biashara yako inazingatia mambo yepi katika utendaji wake wa kila siku? Tupe majibu katika replies hapo chini.

Hatua 2: Fuatilia kwa ukaribu biashara/kampuni ambazo zinakuvutia na ambazo ungependa kuiga utendaji wake (sio lazima biadhara/kampuni hizo uwe nazo field moja ya kuuza bidhaa au kutoa huduma) Lengo hapa ni kujifunza mambo mengi ya msingi katika utendaji wako wa kila siku.

Hatua 3: Hii ni ngumu kidogo, hebu jiulize, biashara/kampuni yako leo haipo duniani, je, wateja wako watapungukiwa na nini? Wateja wako watakukumbuka kwa lipi? Biashara/Kampuni yako itaacha legacy gani duniani? Ukipata ufumbuzi wa maswali haya utakuwa umefika mbali sana.

Hatua 4: Kama umeshafanya hatua 3 zilizopita basi hapo jua umeshafungua koki, kilichopo mbele ni kazi tu. Hebu jiulize, Biashara/Kampuni inajiwekea malengo gani ndani miaka fulani ijayo? Malengo hayo bila shaka huja kutokana na zile values zako ambazo ulishajiwekea.

Hatua 5: Sasa kusanya hayo malengo utayoyapata katika hatua iliyopita ili kutengeneza dhamira na makusudio ya kampuni/biashara yako. Ukimaliza jiulize tena, “je makusudio haya yataleta mapato?” Hakikisha makusudio unayoweka yanakusaidia kunasa mapato zaidi.

Hatua 6: Zama field sasa. Hakikisha kila mmoja anaelewa makusudio yaliyowekwa kwenye taasisi/kampuni hio mara moja. Ikitokea watu hawajaelewa makusudio hayo waelekezwe mpaka waelewe, ama sivyo badili dhamira na ibadilishwe.

Hata hivyo habari njema ni kwamba, kama unahisi hujaweza kung’amua makusudio (purpose) ya biashara hio unafanya, inawezekana kabisa hujatakari kwa kina na kuyaona. Kiuhalisia hakuna biashara ambayo haina Kusudio, lazima tu kusudio lipo na ndio linafanya biashara iendelee kuwepo.

Na zaidi inawezekana wafanyabiashara/wafanyakazi wenzako tayari wanajua wateja na dunia inataka nini kutoka kwenye taasisi yako. Hivyo mbinu ya kwanza ya kung’amua kitendawili hiki ni kubadili namna ya kuwazs na kuelewa mambo kutoka sub-conscious understanding (nimekosa kiswahili chake).

Mpaka kuwa conscious understanding. Halafu kifuatacho ni kuingiza utamaduni huo moya katika shughuli zako za kila siku katika biashara. Makusudio ni Utamaduni, sio mabadiliko ya fasheni tu. Una lolote la kuchangia na kuongezea kwenye makala yetu ya leo kuhusu Makusudio (purpose) ya biashara yana umuhimu gani? Tafadhali karibu.

Pitia makala hizi hapa ili kupata mfululizo mzuri wa maarifa kutoka kwenye somo ulilolipata leo. Gusa links zifuatazo kisha jifunze zaidi..

  1. FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA
  2. USAFIRISHAJI NA MIUNDOMBINU KATIKA USTAWI WA BIASHARA AFRIKA
  3. FANYA MAAMUZI SAHIHI KATIKA MUDA SAHIHI