JINSI YA KUONGEZA MBINU ZA KULIFIKIA SOKO MTANDAONI
Kila mtu atakwambia post insta, facebook, tumia funnels, weka status za kutosha Whatsapp. Mwingine atakwambia kusanya namba za simu uwapigie, tuma emails kila siku nk. Sasa utafanyaje kuongeza mbinu za kulifikia soko? Utakapomaliza makala hii ya leo utafahamu kiundani kuhusu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni. Utafanyaje, twende sambamba mpaka mwisho.
Zama hizi za Internet na huduma za mitandao ya kijamii zimekuja na mgawanyiko wa watu. Kila mtu anatumia mtandao wa kijamii anaoona unampendeza. Sio ajabu uone kuna mtu hana account ya facebook lakini kutwa yupo instagram/twitter. Hata hivyo ukiwa mjasiriamali lazima ufike kote.
UNALIFIAJE SASA HILO SOKO LA MTANDAONI?
1. Kwa kutumia Mitandao kama Whatsapp, Instagram, Twitter na Facebook, sasa unaweza kueneza maudhui yako kote kote kwa mtindo wa Copy & Paste. Ndio sio dhambi kufanya C&P ikiwa maudhui ni yako. Hata hii makala usishangae kuikuta kwa page zatu za LinkedIn na Instagram. Hapa ni muhimu sana Ukaifahamu Nguvu ya Mitandao ya Kijamii katika biashara yako.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba mitandao hii imetofautiana, hivyo maudhui unayopost twitter inabidi UYAHARIRI ili yaendane na aina ya watu katika mitandao mingine kama Website yako, Facebook, Instagram na LinkedIn. So kazi ya kueneza maudhui haiwi ngumu kuvile hapa, sivyo?
2. Pia unaweza kuanzisha kampeni fulani na kisha unaieneza kwa njia ya barua pepe. Kufanikiwa kwenye hili kwanza unapaswa ukusanye anwani za barua pepe nyingi (walau elfu moja) na kisha uifanye kampeni yako kwa uweledi wa hali ya juu ndani muda fulani. Hii ndio Email Marketing.

NB: Kampeni yako haipaswi kuwa na ujumbe wa kupandikiza chuki au viashiria vya ubaguzi wa namna yoyote kwa sababu kampeni za namna hio huleta hisia mseto kwa watu na kukujengea taswira mbaya. Barua pepe zako unaweza kuzikusanya kwa njia ya Newsletter au kawaida (ile ya kuomba).
3. Tumia Social Media Analytics Tools: Kama unasambaza maudhui yako kupitia mitandao ya kijamii, siku hizi kuna namna ambayo unaweza kupima mwenendo wa machapisho yako kirahisi tu. Katika twita kuna Twitter Analytics na Insta kuna Insights.

Hizo tools zitakwambia maudhui yako yamewafikia watu wangapi (impression), wangapi wameshiriki mjadala (engagement), wangapi wameclick links na umepata wafuasi wangapi baada ya kuchapisha maudhui. Ukishajua hayo itakusaidia sana kuboresha zaidi Machapisho yako yajayo.
Mitandao ya kijamii hasa Mtandao wa GOOGLE ina nguvu ya ajabu sana katika kuwafikia watu wengi ndani ya muda mfupi tu. Ni muhimu basi ukajua namna ya kucheza na mitandao hii ambayo kila mtu duniani anatamani awe mtumiaji wa kila siku. Kufahamu zaidi kuhusu nguvu hio gusa hapa;
4. Tumia Web Analytics Tools; Kama tayari unayo website ya biashara au page ya blogu yako, basi ni muhimu sana ukaweza kufuatilia na kujua ufanisi wake kwa watu wanaoitembelea. Unajua watu wangapi wanatembea website yako kila siku? Makala zipi ulizoandika zinafuatiliwa zaidi?
Watu wanaotembelea website yako wanatokea wapi? Katika Injini za Kimtandao, website yako iko katika nafasi gani? Majibu ya maswali yote haya unaweza kuyapata kwa kutumia tools kama Google Search Console, ahrefs, winch, clutch n.k Hivi ndo virutubisho vya website yako mtandaoni.
5. Tumia Content Management System (CMS); Ukiwa muandishi ambaye ungependa maudhui yako yazidi kufanya vizuri mtandaoni basi unapaswa kutumia mbinu mbadala zitakazokusaidia tena na tena. Sikuhizi mambo yamerahisishwa, WordPress ndio CMS maarufu zaidi lakini ukiacha hio kuna Joomla, Drupal, Magento, Shopify na Prestashop (kwa ajili ya e-commerce). Ukiwa na hizo tools inakuwa rahisi kwako kuandika maudhui ambayo yatakuwa rahisi zaidi kunaswa na Injini za Mtandaoni kama Google, Ask na Bing. Umeshawahi kutumia CMS gani? Tuambie hapa leo..

6. Tumia SEO Hapa sitasema mengi kwa sababu tumeshaongea mengi huko nyuma. Kifupi hii SEO (Search Engine Optimization) ni teknolojia iliyopo kwenye software za mtandaoni zenye uwezo wa kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kama websites, blogs, mitandao ya kijamii n.k
Cha kuzingatia zaidi unapofanya SEO ni matumizi ya Keywords sahihi kwa ajili ya soko lako ulilochagua kuhudumia (niche), Picha unazotumia lazima ziwe na maelezo tambuzi (alt text), matumizi ya links pamoja na ujuzi wa kuuza kwa kupitia maandishi(copywriting skills) Zingatia sana haya kwasababu hii ndio mbinu bora sana katika kufahamu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni.
Yaani SEO ni SUMAKU inayovuta taarifa kutoka sehemu mbalimbali za watu (open source information) na kuzigawa kwa mtu yeyote ambaye atatafuta taarifa hizo. Umeshaielewa jinsi SEO inavyofanya kazi sasa? Kufahamu zaidi fuatana na makala hii hapa;
7. Fanya Mara kwa Mara; Umeshayaona haya tuliyoyaelezea leo? Sasa kama unataka kufanikiwa katika kuipeleka mbali biashara yako huku mtandaoni, basi SIO LAZIMA uyafanye yote, aghalabu, unaweza kufanya matatu au manne ili ujiweke kwenye nafasi nzuri katika kuimarisha ushawishi wako huku Mtandaoni. Lakini katika kuzifanyia kazi mbinu hizi basi ni muhimu mbinu hizi uzifanye MARA KWA MARA, yaani uwe na consistency. Usifanye mara mbili kisha ukakata tamaa. Andika machapisho 500, tuma emails 2000, rudia na rudia. Njiani utagundua ile njia sahihi zaidi.
Umegundua nini kwenye makala hii ya leo? Umeshafahamu kiundani kuhusu jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni? Una la kuongezea, swali au changamoto?
Tafadhali weka maoni yako hapa au kama unahitaji kuwasikiana nasi kupitia emails au Whatsapp, tafadhali fanya hivyo; Whatsapp/Call: +255765834754 Email: info@rednet.co.tz