Tag: jinsi ya kufanikiwa

Pata huduma za Website, SEO, Social Media Marketing na nyinginezo nyingi kutoka Rednet Technologies Branding vs Marketing. Kipi ni kipi? ukweli kuhusu 'Propaganda' Jinsi ya kutengeneza Attention Mtandaoni.

Jinsi ya Kutengeneza Attention Mtandaoni

Hivi unajua kwamba aliyeshinda vita vya 2 vya Dunia ni Urusi, ndiye aliyepigana na Hitler kwa ground. LAKINI, Leo hii kila mtu anaongelea Bomu la Nyuklia la Marekani lililodondoshwa Hiroshima na Nagasaki. Unajua kwanini? Kwa sababu watu wanapenda ATTENTION duniani na leo hapa utafahamu kiundani kabisa jinsi ya kutengeneza attention mtandaoni ili uweze kunasa wateja zaidi.

Marekani ni mtaalamu haswa kwenye hilo la kutengeneza attention na kusambaza propaganda zenye manufaa ya nchi yake. Jamaa wamefanikiwa kuujaza Ulimwengu “ukweli wao” kwamba lile Bomu la Nyuklia ndo limeipa ushindi taifa hilo na kwamba kwanzia hapo wao ndo wababe duniani na hakuna mwingine. Ila nyuma ya pazia Urusi ndiye anayemiliki Nyuklia nyingi zaidi.

Kujitangazia Ushindi tu, tayari alishaanza kuteka ATTENTION duniani na mataifa mengi yalianza kuvutika katika Silaha, Siasa, Utamaduni na Biashara zingine za Kimarekani. Leo hii Marekani ndo nchi inayosifika kuuza silaha zaidi duniani, Makampuni makubwa karibu yote yapo USA, Microsoft, Google, Meta, Yahoo, Space X nakadhalika.

Marekani ndo nchi inayotambulika kwa mifumo bora ya Kidemokrasia duniani, na mambo kedekede tayari unayajua kuhusu hao jamaa. Unadhani Marekani alipata wapi sifa zote hizo? Kwamba Urusi hana huo ubavu wa kuuza silaha au teknolojia za kisasa? Jinsi ya kutengeneza attention mtandaoni is the damn strategy they rely on.

Kwenye Biashara Attention inatengenezwa vipi?

Kwenye biashara Mtandaoni hali ipo hivyo hivyo. Ushindani ni mkali mno kila siku. Ni vita. Mtandao wa Internet Live Stat unaonyesha kuwepo na websites zaidi ya Bilioni 1.9 mpaka sasa duniani. Hebu niambie unachomokaje katikati ya vurugu lote hilo kama hujajua jinsi ya kutengeneza ATTENTION? Leo hii wewe upo hapa kwenye tovuti yetu kwa sababu umeona kuna uwezekano ukaweza kuimarisha biashara yako mtandaoni kwa kutengeneza attention fulani, si ndio?

Utaniuliza; “Sasa Faustine, nawezaje kutengeneza hio ATTENTION ili niweze kusurvive huko mtandaoni?” Zipo njia nyingi, za halali na zile zisizo halali. Hapa tutaongelea zile za halali tu. Habari za kupost utupu, vichupi na makalio hapa hazipo.

Kuijuia Google leo ndo mchongo. Binafsi ningepata nafasi ya kurudi nyuma na kumshauri Faustine wa miaka 15 enzi zile, ningemshauri atie nguvu sana kwenye kuijua jinsi Google inavyofanya kazi na namna anaweza kuitumia kukuza biashara na kunasa wateja zaidi.

Leo hii unaweza kutengeneza ATTENTION ya Biashara yako kule GOOGLE kwa kuhakikisha mtu akitafuta chochote kinachohusiana na bidhaa/huduma unazozitoa kwenye biashara yako basi anakipata mara moja na anakipata kwako chap. Hii inafanyika kwa uzuri kupitia Huduma za SEO (Search Engine Optimization).

Hivi si unajua, kwa siku 1 tu huwa kunafanyika matafuto zaidi ya bilioni 3.5 kule google. Sasa kwanini bidhaa/huduma zako tukizitafuta google kule hatukupati? Kama jibu la hilo swali linakusumbua, wala usiwe na wasiwasi tena, sekunde chache zijazo utakwenda kujua cha kufanya.

Kama unatamani kutengeneza ATTENTION kule Google mpaka ifike mahali mtu akisearch kuhusu bidhaa/huduma zako akupate haraka, basi chukua SIRI hizi hapa. Leo hapa utaziona siri (4) tu;

1. Tengeneza website yako na hakikisha inafanya kazi vizuri na ina load faster. Kwanini website? Kwa sababu ni kupitia website unaweza kutengeneza maudhui mengi ndani ya chanzo kimoja, ukafanya uchambuzi kwa kina na kuelezea kwa mapana kuhusu Faida za bidhaa/huduma zako, Mbinu, Jinsi ya kutumia na taarifa zingine. Hili pia unaweza kulifanya kupitia chaneli yako ya YouTube.

2. Andika maudhui ya kutosha kuhusu Faida za bidhaa/Huduma zako, Jinsi ya kuzitumia, Jinsi ya kupambana na Changamoto, Mbinu za kutumia bidhaa/huduma hizo kwa usahihi, Madhara ya Kutotumia bidhaa/huduma zako n.k Umeona hayo maneno hayo yaliyotumika hapo? Hayo yanaitwa Keywords.

3. Hakikisha unatumia keywords nyingi zinazohusu bidhaa/huduma zako ikiwemo JINA LA BIDHAA/HUDUMA hio. Kwenye keywords hapo ndipo Google hukusanya taarifa na kuzihifadhi kwenye database yake, tayari kwa watu kupata majibu pale watakapotafuta kuhusu bidhaa/huduma hio. Ukiweza kutumia Google kama jukwaa la biashara utafaidi sana biashara yako inapokuwa mtandaoni.

4. Ambatanisha Namba yako inayopatikana katika simu za Kawaida na WhatsApp katika makala unazozichapisha kwenye website yako na mitandao yako ya Kijamii. Hio namba yako ya simu ni muhimu sana iwe hewani muda wote. Hakikisha muda wote ukitafutwa unapatikana. Hapa ndo utajua sasa kwanini Mteja achague kufanya kazi na wewe na sio mtu mwingine.

Ukifanya hivyo, utamtengenezea mteja wako mazingira ya kukupata moja kwa moja pale atakapofikwa na uhitaji wa huduma/bidhaa zako atakazoziona huko Mtandaoni. WhatsApp kupitia Status zako unaweza kuchapisha tips, ushauri, faida nk za bidhaa/huduma zako kila siku.

Sasa, tuishie hapo kwa leo, au unasemaje ndugu yangu?

Anyway, ngoja nisikuache bure, muendelezo wa SIR hizo tayari nimeuweka kwenye eBOOK yako MPYA na BORA ya SEO ambayo nimekuandalia. eBook hio inaitwa TEKNOLOJIA YA SEO; JINSI INAIFANYA BIASHARA YAKO KUWA NA SUMAKU MTANDAONI. Katika Kitabu hiko nimekuwekea SIRI 15 tayari kabisa kukufunulia wewe jinsi SEO inavyofanya kazi na namna unaweza kuitumia kukuletea manufaa zaidi kila siku. Hi ndio kitu unakihitaji sasa.

eBook hii itakusaidia kujua mambo yote muhimu kuhusu SEO, ni nini? inafanya kazi vipi? Faida zake ni zipi? Mambo yapi ya kuzingatia ili uifaidi? Kwanini hupati wateja mtandaoni? Yote hayo na mengine mengi yameelezwa kwa mapana kabisa kwenye eBook hio.

Kama nilivyokutaarifu, kuanzia ukurasa wa 27 wa eBook nimekueleza SIRI 15 ambazo zitakusaidia katika kutengeneza ATTENTION ya biashara yako mtandaoni kupitia SEO. SIRI 15!! Hizi siri wanaojiita wataalam wa SEO unaowafahamu hawawezi kukwambia kwa kuhofia kupoteza wateja ukiwemo wewe, ila mimi nimekwambia.

Utajiuliza, Kwanini nimekwambia? Kwa sababu mteja anayo haki ya kufahamu exactly kila kinachofanyika katika mradi wake. Mfano unapojenga nyumba ukikaa karibu na fundi wako utataka kujua bei ya misumari, aina za misumari, aina za milango, mbao, rangi ipi ipakwe wapi na kwanini, aina za kokoto, mchanga wa plasta ni upi na vitu kama hivyo.

Kadhalika katika SEO, ni muhimu ukafahamu kinachofanyika humo ndani, ili uweze kushiriki kufanya mwenyewe na kupata ujuzi wa ziada. Hii ndio sababu kitabu hiki kipo tayari kwa ajili yako leo.

Sasa ukitaka kuipata hii eBook njia ni hii hapa. Save namba yangu ya WhatsApp kwa kugusa namba hii hapa, 0765834754 Kisha nitumie text yenye jina lako ili niweze kukutumia eBook hio kwa WhatsApp mara moja. Kwa sasa nitaitoa eBook EXCLUSIVELY kwa watu 20 tu.

Hata hivyo eBook yetu hii sio kila mtu ataipata. Wataoweza kuipata eBook hio ni wale tu;

1. Waliopo kwenye contact list yetu ya WhatsApp. Kuingia kwenye list hio save namba yetu hii hapa 0765834754

2. eBook itatoka rasmi Usiku wa kuamkia PASAKA kwa gharama ya shilingi 50,000/-. Lakini leo hii unapouona ujumbe huu, eBook naitoa EXCLUSIVELY kwa shilingi 15,000/- tu.

Hii OFA ni kwa watu 20 tu watakaokuwa wakwanza kulipia. Baada ya hapo OFA itafungwa. Hivyo, ndugu changamka.

LIPA Sasa hivi sh 15,000/- kupitia LIPA NAMBA Yetu ya M-PESA hii hapa 5432715 au scan QR Code unayoiona hapa. Ukishafanya malipo njoo WhatsApp na screenshot ya muamala na hapo hapo utapata eBook yako uanze kuvuta wateja kwa kutumia SIRI za Ajabu za SEO katika Mtandao wa Google.

jinsi ya kutengeneza attention mtandaoni

Kumbuka Ofa ni EXCLUSIVELY kwa watu 20 tu wa kwanza kulipia. Baada ya hapo eBook itarudi bei yake halisi ya sh 50,000/-.

Kuna mtu aliwahi kuliuliza, “Sasa bro, kwanini unilipishe kufanya SEO wakati kutumia Google ni BURE kabisa?” Ungekuwa wewe ungemjibuje apo?

Sikia nikwambie kitu, Ukiona unapewa mchongo wa bure basi jua wewe ndo bidhaa hapo. Ndo ukweli huo.

Kutumia Google ni BURE. Kutumia Insta, Facebook, WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii pia ni BURE kabisa. Kwanini? Kwa sababu kwenye BURE ndo kuna utajiri umejificha hapo.

Umeelewa hapo mchezo unavyochezwa. So nakupa SIRI hii hapa; Toa maudhui yatakayotoa majibu ya changamoto BURE yawafikie watu wengi, wachuje, wachache wawe wateja wa bidhaa/huduma zako. Njoo WhatsApp sasa ufahamu zaidi kuhusu SEO na Tech kwa namba hii 0765834754.

Unatamani ujumbe huu umfikie rafiki yako wa karibu? Umejifunza nini leo katika jinsi ya kutengeneza attention mtandaoni ili uweze kunasa wateja zaidi. Unaweza kushare makala hii kwa rafiki, ndugu, boss au yeyote unayehisi anahitaji kusikia habari hii. Ni BUREE kabisa, hivyo, sambaza, uliza na comment ili ufahamu zaidi.

Cheers.

Kwanini hupati wateja mtandaoni?

KWANINI HUPATI WATEJA MTANDAONI?

Kila mtu anapenda maisha mazuri, kufanikiwa kibiashara, kuwa na amani na uhuru wa kufanya kile kinachokupa furaha muda wowote. Sasa uko tayari kuingia gharama ili kuyapata matamanio yako? Umeshajiuliza Kwanini Hupati Wateja Mtandaoni licha ya Juhudi unazoweka?

Mwaka 2010 wakati nafungua account ya Facebook nilikua nafurahi sana kukutana na rafiki zangu tuliopotezana miaka mingi baada ya kumaliza Primary School na sekondari. Ilikua safi sana kuona picha za washkaji wakiwa na maisha yao baada ya shule.

Baadae tukaanza kupata marafiki wengine katika mtandao pendwa wa facebook. Nyakati hizo Mtandao wa Twita ulionekana kama mtandao wa Wanasiasa, Instagram ya Wasanii na Masuperstar. Ila Facebook kule wote tulionana kuwa ni level moja. So kule ndo tuliona kuna lile vibe la wote.

kwanini hupati wateja mtandaoni?

nguvu ya mitandao ya kijamii 

unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako?

Lakini miaka ilivyozidi kwenda, Matumizi ya Mitandao ya Kijamii yalikua yakibadilika mdogo mdogo, hasa baada ya kushuhudia Wasanii na watu waliokuwa na Followers wengi mitandaoni waliposhindwa kuimarisha Uchumi wao kupitia Nguvu ya Mitandao. Hapa kitu kipya kikatambulishwa.

Ilifika mahali sasa ule utaratibu wa kuwa na urafiki na wale tu uliowahi kusoma nao sasa ulipitwa na wakati na badala yake, Rafiki/Followers/Follows wa mtandaoni wakawa ni wale ambao tunashare nao “Interests” Hapo ndipo mbinu za kufanya biashara mitandaoni zilipoanza kushamiri.

Tayari nimeshakuandalia makala maalum itakayokupa mbinu muhimu za kunasa wateja mtandaoni. Kama unataka kuzifahamu mbinu hizo ili uzitumie kwenye biashara yako basi fuatana na makala hii hapa Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni.

MAMBO SABA (7) YANAYOKUKOSESHA WATEJA MTANDAONI

Tumeshaona jinsi Mitandao imebadilika kutoka ilipoanza, sasa kuna mambo unayoyafanya kwa kujua au kutokujua yanayokukosesha wateja. Jambo la 5 litakushtusha sana. Hebu tuyaone hapa;

1. Kutokuwa na Bidhaa/Huduma inayokutambulisha;

Hapa unatakiwa kuwa makini na kuelekeza focus yako kwenye bidhaa/huduma fulani specific. Inaweza isiwe bidhaa/huduma moja, lakini hakikisha unakuwa na ile bidhaa/huduma inayokutambulisha. Mfano: Unauza fenicha, shikilia hapo hapo.

kwanini hupati wateja mtandaoni

Zile zama leo unapost fenicha, kesho unapost computers keshokutwa unapost picha uko unasafiri, mara unapost unakula chakula., hivyo ni vitu ambavyo vinakupunguzia mvuto mtandaoni. Sisemi usipost kabisa, hasha, katika post 10, 7 ziwe ni kuhusu fenicha, 3 maisha binafsi.

2. Kushindwa kuingia kwenye Orodha ya Wanaofanya biashara kama yako mtandaoni;

Kuna ile dhana ya kuogopa ushindani au ile kuwekeana mtimanyongo na washindani wako. My friend, huku mtandaoni make sure unajenga uhusiano na kila unayekutana naye. Itakusaidia sana kuendelea kudumu sokoni.

Kuingia kwenye orodha(list) ya wafanyabishara huna budi kuwa support wafanyabiashara wenzako mtandaoni. Ndio, Wasukuma wana msemo wao wanakwambia “Scratch my back, I’ll scratch yours.”

3. Kutokua na muendelezo wa Maudhui kutasema kwanini hupati wateja mtandaoni;

Je wajua kwamba kwa siku huwa kunakuwa na posts zaidi ya milioni 50 katika mitandao mbalimbali duniani. Sasa ndugu unapost mara 1 kwa wiki unategemea nani ataiona hio biashara yako? Hakikisha unapost mara nyingi kadiri iwezekanavyo.

Njia ya Kompyuta katika kuhifadhi data utajuaje pale biashara yako inapojiendesha kwa hasara changamoto katika biashara mpya/inayoanza, hili ni funzo lisiloepukika

4. Kushindwa Kuwasiliana Vema;

Kupost bidhaa/huduma zako mtandaoni ni jambo moja, lakini uwezo wa kuwasiliana ndio muhimu sana. Shuleni tulisoma ile Communication Skills, sasa mtaani unatakiwa uwe na uwezo wa kuwasiliana na kujua wapi, sangapi useme nini. Ni maarifa hayo.

Mtaalam wa mitandao bwana @GillsaInt ana mbinu yake anakwambia katika maudhui yako unayopost mtandaoni, hakikisha 80% ni yanahusu thamani (value) za bidhaa/ huduma zako kama Faida, Jinsi ya Kutumia, Changamoto nk. Na 20% zinazobaki ndo upost sasa Matangazo ya kuuza hio biashara.

5. Kutokuwa na Miundombinu ya Kurahisisha biashara Mtandaoni;

Umeshaona wale wanakwambia No Facebook Acc, No Insta Acc, No twitter etc. Skia, kama unataka kufanya biashara ukafanikiwa mtandaoni USIFUATISHE hizo akili zao. Hakikisha una miundobinu humu mtandaoni.

Mitandao ya kijamii ndipo ilipo NGUVU halisi ya biashara ya mtandaoni. Jifunze namna unavyoweza kuitumia kwa faida ya biashara yako. Kama unataka kuifahamu NGUVU hio ya mitandao, basi fuatana na makala hio hapa kufahamu zaidi.

Lengo la kufanya biashara mtandaoni ni kuhakikisha unakuwa na wateja wengi kadiri iwezekanavyo, si ndio? Kama ni hivyo, fanya research, kisha tambua wateja wako ni kina nani na wako wapi. Fungua website yako, accounts za Insta, Facebook, Linkedin, Twitter n.k Kuwa available.

6. Kukosa Ushawishi na Ujuzi wa Kuuzia wateja Mtandaoni;

Sasa hapa naongelea uwezo wa kumshawishi mtu akapenda bidhaa/huduma zako kabla hajawa mteja wako. Kwenye hili @iamKaga pale twita anakupa funzo gani? Cha kwanza hakikisha watu wanakujua, kisha Wakupende au wapende maudhui yako, hapo ndipo watakujia.

Huo ushawishi hauji tu by default wala haujengwi ndani ya siku moja. Ushawishi ni tabia ya kuhoji na kutoa ufumbuzi juu ya changamoto zinazowakabili watu katika namna bora ya uwasilishaji. Hapa ndipo wanasiasa wanatupiga coz anaijua siri iliyopo kwnye ushawishi.

7. Kutokuwa na Njaa ya Mafanikio;

Tunarudi kulee mwanzo, unapost mara 1 kwa wiki, au mara 2 kwa mwezi halafu unasingizia huna muda wa kuandaa maudhui. Bro, ni vile tu huna njaa ya kufanikiwa. Njaa ya mafanikio ikikushika vizuri huo muda LAZIMA uupate na utautumia vizuri tu.

Kuna nyakati unabanwa na shughuli zako nyingine to the point unashindwa kuendesha biashara yako mtandaoni. Kuna nyakati nyingine unakata tamaa kwa sababu huna followers au huna idea uanzaje kuandaa maudhui ili ufikie yale matamanio yako. Ukifikia hapo wala usiwe na shaka..

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

Hata hivyo, katika biashara sio lazima kila jambo ufanye wewe mwenyewe. Nyakati hizi za mapinduzi ya teknolojia kila siku, ni muhimu kugawa majukumu kwa wataalam wa kuaminika ili kuhakikisha lengo na mipango yako inazidi kwenda kama utakavyo.

Hio ndio sababu sisi Rednet Tech. LEO hii tunakupa nafasi ya kuikuza biashara yako mtandaoni kwa;

1. Kukutengenezea Website bora.

2. Kukufanyia huduma ya SEO. Inafanyeje kazi hii? Gusa hapa kuifahamu zaidi.

3. Kukushauri aina ya maudhui ya kuyatumia kwenye kurasa zako za mitandao. Gusa hapa tuchati pale WhatsApp na upate huduma unayohitaji.

So, mambo haya 7 tuliyoyaona leo kwa uchache wake ndio yanakwambia kwanini hupati wateja mtandaoni. Umeshajua cha kufanya sasa? Hebu niambie wewe ni lipi umegundua leo kuwa ndio linakukosesha wateja? Mtandaoni hamna miujiza. Ni kuwa na maarifa na kuhakikisha unajifunza kila siku. Umependa makala hii? Share..