Tag: invest

FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA

Watu wengi hufikiri kwamba Kuwekeza ni swala la kupata Utajiri ndani ya muda mfupi, Kustaafu mapema au kupata gawio (interest) kubwa kila baada ya muda fulani kwa haraka. Ukweli ni kwamba Kuwekeza sio chanzo cha kukufanya ushinde unakula upepo wa bahari, kutumia pesa hovyo(kula bata) au kusafiri vile unataka. Usikariri maisha, leo makinika mpaka mwisho wa makala hii ili uweze ku fahamu siri ya kufanikiwa katika kuwekeza.

Watu wanafanya kazi sana ili kupata pesa, na kazi zaidi kutunza pesa. Lakini wachache sana ndio hugundua njia bora zaidi ya kutengeneza na kuzungusha pesa katika biashara zao. Leo hii nitakujuza mambo 10 muhimu ya kuzingatia katika UWEKEZAJI (INVESTING) kwa mafanikio ya biashara yako hio hio unayoifanya/unayotaka kuifanya.

Kuwekeza zaidi katika biashara dhumuni lake ni kuhakikisha biashara yako ina uwezo wa kujiendesha yenyewe hata bila ya wewe kuwepo hapo ofisini kila siku. Sasa ili kuweza kufikia lengo hilo inatakiwa ile energy ambayo mjasiriamali anakuwa nayo wakati anaanza uwekezaji wake wa kwanza ndio hio hio anatakiwa kuwa nayo hata pale anapofanikiwa. Kama misuli inayohitaji mazoezi ili iwe mikubwa na yenye nguvu, the same kwenye biashara yako. Biashara inahitaji muendelezo wa uwekezaji ili kuleta matokeo yenye tija. Vitu kama Mtaji, Masoko, rasilimali watu, connection, wafanyakazi n.k, vinahitaji kukua sana. Hii ni muhimu sana katika ku fahamu siri za kufanikiwa katika kuwekeza popote pale duniani.

Sasa kifupi ni kwamba kuna aina nyingi sana za Uwekezaji duniani (Stocks, Bonds, Real Estate, Commodities n.k). Lakini leo tujadili kuhusu Uwekezaji kwenye Biashara Unayoifanya/Unayowaza kuifanya (kuuza viatu, nguo, chakula, furnitures n.k) Hapa nitakuwa nimekupa kitu unachohitaji sana, si ndio?

Kama umeshawahi kujaribu basi utakubaliana namimi kwamba Kutunza Fedha kwenye kibubu, chini ya godoro, benki, mpesa, tigopesa ni ngumu kweli kweli. Halafu kibaya zaidi, pesa sio kiumbe hai, usitegemee ukiichimbia itazaliana.

Hizi hapa ni njia Bora za kuwekeza na kuzungusha pesa yako vizuri ili uweze fahamu siri ya kufanikiwa katika kuwekeza:

1. FIKIRIA MBALI:

Unapotaka kuwekeza kwenye biashara yako, waza hivi; mwaka 2030 au 2040 nitakuwa katika hatua gani kibiashara? nataka niwafikie watu/wateja/maeneo mangapi mpaka mwaka 2030/2040? Ukiwa na mipango ya mbali katika biashara yako unapata energy ya kusimamia vizuri na kufanikiwa. Kila mafanikio huanzia kwenye fikra na mipango thabiti.

2. ANZA KUWEKEZA KILE ULICHONACHO:

Watu wengi hasa vijana wanapenda kufanya biashara lakini wanalalamika changamoto ni Mtaji. Fahamu, biashara ni kama ile siku mpenzi wako anapokupa taarifa za mimba. Niambie hapa kama ulianza kulea mimba kwa milioni 1 kwa mwezi ule wa kwanza. Utagundua ni ngumu. Hali kadhalika biashara yako inahitaji kulishwa kidogo kidogo kwanzia ingali ndogo.

Unailisha biashara kwa vitu kama Maarifa, aina bora za bidhaa/huduma zinazotakiwa, wapi pa kuzipata, aina za wateja, taarifa sahihi nk. Pesa ni kitendea kazi muhimu lakini tambua pesa ni sehemu ya mtaji tu.

3. WEKEZA PALE UNAPOPAWEZA

“Baba yako hawezi kukufanya uwe tajiri, wala mama yako, wala rafiki yako, wala mwalimu, wala serikali, badala yake ni wewe mwenyewe wa kubadili maisha yako ukianza na namna unavyofikiria (mindset)” Maneno sumu ya jamaa yangu SirJeff Dennis. Hapa nataka kuongelea Uwezo wako specifically. Wewe unaweza kufanya nini katika kiwango kikubwa? Na unaweza vipi kutumia huo uwezo kwa manufaa? Jitambue wewe kwanza.

4. JIFUNZE NA FANYA UCHUNGUZI

Hili swala sio la kufanya mwanzoni wakati unaanza biashara halafu unakuja kuacha mbeleni, Hapana. Kama ilivyo kuwekeza hakuna mwisho kwenye biashara yako, hakikisha pia Unaendelea kujifunza mbinu mpya na kufanya Uchunguzi kuhusu biashara mbalimbali mara zote kabla hujawekeza. Ishi nayo hii kwa sababu Elimu haina mwisho.

5. TENGENEZA NA FANYA KAZI KWENYE TIMU

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema “Kama huwezi kutengeneza pesa ukiwa umelala, huwezi kuwa tajiri”, Ni kweli kabisa. Mimi nakuongezea, kama kwenye Uwekezaji wako, wewe ndo kila kitu, hio biashara haiwezi/ni ngumu sana kukua. Gawa majukumu, sio kila kitu unataka kufanya wewe, uzalishaji wewe, marketing wewe, customer care wewe, presentations wewe. Utafeli, hakikisha mfumo wa biashara yako unaweza jiendesha wenyewe hata usipokuwepo.

 fahamu siri za kufanikiwa katika kuwekeza.fanya kazi kwenye timu

6. KUWA NA MSIMAMO (CONSISTENCE AND RESSILIENCE)

Biashara yako ili iweze kukua na kufanikiwa dhidi ya ushindani wa masoko, dhoruba za kiuchumi, teknolojia nk, Unapaswa kuwa na msimamo/consistency. Wazungu wanasema “Practice makes perfect”. Hutakiwi kukata tamaa, licha ya changamoto ambazo unaweza kukutana nazo kila siku, hakikisha unaendelea kuzalisha/kuhudumu, tafuta wateja wengi zaidi, jisahihishe, jitangaze, pambana. Uwekezaji unakuhitaji uwe na ngozi ngumu kwelikweli kwa sababu katika kuwekeza kuna nyakati za kuanguka na kukata tamaa, sasa hakikisha unao uweza wa kusimama na kuendelea kupambana.

7. KUWA MWOGA PALE WENGI WANAPOKUWA WALAFI

Ulimwengo wa Uwekezaji katika biashara unaendeshwa kiakili na kijasusi sana. Usiwe bendera kufuata upepo, Usiwe mtu wa kufuata mkumbo. Ni afadhali kuwa mwoga na kuishi miaka mingi, kuliko kuingia vitani bila maandalizi, hutachukua raundi. Tulia, changa karata zako vizuri na kwa mipango sahihi.

8. KUWA AGGRESSIVE PALE WENGI WANAPOKUWA WAOGA

Sehemu pazuri zaidi kuwekeza ni pale mahali kuna changamoto nyingi. Uwekezaji wako unapotatua changamoto hapo ndo pakutoboa kabisa. Kuna mahali hamna maji wapelekee hapo, hamna chakula, fungua mgahawa. Pambana na changamoto za wateja wako. Wasikilize wateja wako wanahitaji nini kila wakati kwa sababu kwenye maumivu ya wateja wako ndipo mafanikio ya uwekezaji wako yalipo. Shikilia hapo.

9. PUNGUZA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA

Fahamu kuwa katika biashara yako kila shilingi ina mchango muhimu katika Uwekezaji endelevu. So hakikisha unazingatia matumizi yale muhimu zaidi katika uwekezaji. Hili zoezi ni gumu lakini linawezekana ukiweka Nia ya Kukuza Biashara yako.

10. TAWANYA UWEKEZAJI/DIVERSIFY

Ili kuhakikisha biashara yako inakuwa na misuli ya kiushindani, lazima Utawanye uwekezaji wako. Unauza nguo kwa sasa, ongeza na viatu, soksi, vipodozi na jitahidi ufungue matawi mikoani. Kama unauza mbao, ongeza karakana za fenicha maeneo mbalimbali, TANUKA.

fahamu siri za kufanikiwa katika kuwekeza.

11. TUMIA VIZURI TEKNOLOJIA

Katika eneo muhimu la kuzingatia katika kufanya uwekezaji wa kibiashara, basi hakikisha unatumia vyema teknolojia katika maana ya kutumia kwa usahihi Mitandao ya kijamii, tovuti bora ya biashara yako, software za kutunza hesabu nakadhalika. Eneo la teknolojia ni pana, hivyo nimekuwekea mambo muhimu ya kuzingatia katika makala hizi hapa chini:

  1. WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?
  2. KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE RASMI YA BIASHARA YAKO?
  3. IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO
  4. MAGEUZI YA INTANETI (IoT) KATIKA BIASHARA NA MAISHA
  5. MBINU ZA KUWEZA KULIFIKIA SOKO LA MTANDAONI

NOTE: Uwekezaji katika biashara ni jambo endelevu, kama mtoto mdogo, “kadiri ya umleavyo ndivyo akuavyo.” wamesema wahenga. Ukizingatia mambo haya bila shaka bishara yako itakuwa na afya tele. Tafadhali sambaza makala haya kwa yeyote aliye karibu yako na usisite kucoment hapa chini.

Je umeweza fahamu siri ya kufanikiwa katika kuwekeza katika biashara yako kupitia makala hii ya leo? Niambie katika comments hapo chini.

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.

Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

siri ya kufanikiwa katika kuwekeza.