Tag: internet speed

fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika

FAHAMU KUHUSU MAPINDUZI YA TEKNOLOJIA YA 5G

Dunia ipo mbioni kuelekea zama za matumizi ya teknolojia ya 5G katika kasi ya Intaneti. Mpaka kufikia mwaka 2020 huduma za kibiashara za 5G zilishaanza kupatikana katika nchi zaidi ya 50 kutoka Asia, Ulaya, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kaskazini. Muongo wa 2020s’ ndio unatajwa kushuhudiwa kwa usambazaji mkubwa zaidi wa teknolojia hii ya kasi ya intaneti duniani ikijumuisha nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Sasa leo kwa uchache uta fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika.

Kufikia mwaka 2022 tu tayari kampuni ya Vodacom Tanzania walishazindua huduma zao za 5G nchini na kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano kuzindua huduma hizo. Hakika maendeleo ya teknolojia hii yanakwenda kasi sana.

Sasa ili kujua kwa undani kuhusu teknolojia hii pamoja na matarajio yake katika kufanikisha shughuli za kila siku za kibinadamu, kitengo maalum cha kijasusi katika shirika la GSMA kiliendesha ziara iliyohusisha wabia muhimu ili kupata maoni halisi ya watumiaji wa intaneti kuhusu ujio wa 5G katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara. Uchunguzi huo ulijumuisha maeneo sita ambayo ni; matumizi ya mtandao (network deployment), wigo wa mtandao (spectrum), watumiaji (use cases), mifumo ya biashara na fedha (business model and finance), sera na sheria (policy and regulations) pamoja na ushirikiano wa kibiashara na matokeo ya mbeleni.

Katika maeneo hayo walengwa waliojumuishwa walikuwa ni wasimamizi wa mashirika wa mawasiliano katika ukanda huo, kampuni za simu zilizo na hisa zaidi ya 75% kwa pamoja katika ukanda huo pamoja na wauzaji wa vifaa vya mawasiliano ambao wana hisa za zaidi ya 90% ya soko la miundombinu ya kimtandao katika ukanda huo.

Takwimu zilizotolewa na ripoti ya uchunguzi huo ambayo imechapishwa Mwezi July, 2019 zilitokana na uchambuzi wa maoni ya watu mbali mbali kuhusu 5G. Pia matokeo haya yamejumuisha data kutoka vyanzo mbali mbali vinavyohusiana na teknolojia hii ambapo wataalamu waliounda na kendeleza teknolojia hii wataangalia kwa makini watumiaji wa mfumo huu katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara, lengo kuu likiwa ni kujifunza na kujiimarisha zaidi kutoka kwa vinara wa 5G.

Teknolojia za kidijitali zimekuwa muhimu sana katika shughuli za kibinadamu za kila siku. Hii ni muhimu zaidi katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo kama teknolojia hizo zisingekuwepo mambo yangekuwa magumu zaidi kutokana na ubovu na uchakavu wa miundombinu, maswala ya fedha pamoja na ujuzi binafsi wa mtu. Sasa ripoti hio iliyotengenzwa kutokana na uchunguzi wa kitengo cha Intelijensia cha shirika la GSMA imekuja na majibu kadha wa kadha;

MAPINDUZI KATIKA KASI YA INTANETI YA 5G YAMEFIKA:

Kufikia mwisho wa mwaka 2019 kulishakuwa na mtandao mkubwa wa kasi ya 3G na 4G zaidi kuliko 2G katika ukanda huo wa kusini mwa Afrika. Hii inaonyesha ukuaji kutoka huduma za sauti mpaka huduma za data. Uwekezaji unaoendelea kufanyika katika 4G umepeleka ukubwa wa huduma za mitandao kufikia robo ya jumla ya watu waishio katika ukanda huo. Vile vile imeonekana kwamba matumizi ya simu za rununu (smartphones) yameongezeka mara mbili ndani ya miaka mitano iliyopita.

jinsi ya kuanzisha website umuhimu wa tehama.

fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika

TEKNOLOJIA YA 5G ITAKUWA NI SEHEMU YA MIUNDOMBINU BORA YA KIMTANDAO, JAPO UENEAJI WAKE HAUTAKUWA WA KASI SANA:

Katika ukanda huu, teknolojia ya 5G haizuiliki. Ni maendeleo ya kiasili kutoka katika teknolojia zilizopita. Japokuwa, kasi ya ueneaji wa teknolojia hii ya 5G si kubwa katika ukanda huu kutokana na uwepo wa teknolojia zingine kama 3G na 4G bado zina uwezo wa kumsaidia mwanadamu kufanya shughuli zake katika kasi inayoridhisha ya intaneti.

Takribani theluthi mbili (2/3) ya walioshiriki kwenye uchunguzi huu wanatarajia huduma za kibiashara za 5G kuwa katika masoko yao kabla ya mwaka 2025. Pia teknolojia hii itasaidia kupevuka na kuweza kutumika katika masoko mengine. Vile vile itaruhusu uchumi kukua kwa kutumia teknolojia ya 5G katika vifaa vya kielektroniki ambavyo vitapunguza gharama za waendeshaji na wateja. Hapa ndipo tuta fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika kwa undani wake kabisa.

UTAYARI WA SOKO NI MUHIMU KATIKA KUKUZA THAMANI YA TEKNOLOJIA YA 5G:

Kwa nchi zote zilizo katika ukanda huu utayari wa soko ni jambo muhimu zaidi kufanikisha mageuzi ya teknolojia ya kasi ya 5G. Hii itasaidia kukuza thamani katika huduma za 5G kwa wateja, waendeshaji na jamii nzima kwa ujumla. Kiwango cha utayari wa soko kinaonyesha kwamba baadhi ya nchi zinakwenda kasi kwenye matumizi ya teknolojia hio kutoka 4G.

Kufikia mwaka 2025 huduma zinazotumia teknolojia yenye kasi ya intaneti ya 5G itafikia nchi 7 zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara ikijumuisha ni Kenya, Nigeria na Afrika Kusini. Pia uchunguzi umetabiri kuwako kwa miunganiko milioni 28 ya simu kwa kutumia 5G, sawasawa na 3% ya jumla nzima ya miunganiko ya kimtandao ya simu katika ukanda huo.

MASHIRIKA NA MAKAMPUNI MAKUBWA YATAONGOZA KUANZA KUTUMIA 5G KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA:

Teknolojia ya 5G itawezesha makampuni ya mawasiliano na mashirika kuhudumu vizuri zaidi kwa wateja wao ambapo watumiaji wa mwanzoni watawezeshwa na huduma ya wireless (Fixed Wireless Access #FWA) ili kutoa changamoto kwenye matumizi, gharama na upatikanaji wa huduma za kimtandao kama huduma za satelaiti na intaneti. Hapa sasa ndipo uta fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika kwa ukaribu zaidi.

KWA WATEJA NA WATUMIAJI ITAKUWA NI ZOEZI LA MUDA MREFU:

Hii ni kutokana na udhaifu katika upatikanaji wa huduma/vifaa(simulaptop..) bora Kwa gharama nafuu pamoja na ujuzi wa matumizi ya teknolojia kama virtual reality (VR) na Augmented Reality (AR). Ubora wa vifaa kama simu za rununu (smartphones) na kompyuta ni muhimu zaidi katika zama za 5G kwa matumizi ya wateja lakini inategemewa malengo ya teknolojia hii ni kufikia vifaa vya nyumbani (Customer Premise Equipment CPE) kama routers ili kupata huduma za uhakika za wireless (FWA).

Hii ni kwa kuwa huduma hizo hupatikana kwa malipo ya kabla kutoka kwa makampuni ya simu, ambapo katika muda huo huo huduma ya kasi ya 4G itaendelea kuhudumu kwa kasi inayoridhisha na kuwafikia watumiaji wengi zaidi ambao watachangia ukuaji mzuri wa uchumi.

KIPAUMBELE KITAWEKWA KATIKA KUPATA UHAKIKA WA HUDUMA YA WIRELESS (FWA):

Ukuaji wa Matumizi ya intaneti katika vifaa kama simu na kompyuta ni mdogo mno ambao ni chini ya 2% katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara, hivyo kufanya ujio wa zama za 5G kuegemea kwanza katika CPE’s. Hii itapunguza gharama za uendeshaji lakini pia itaongeza watumiaji kwa kutumia wireless (FWA). Mbinu hii ya kufikisha teknolojia kwa jamii inalenga kwa suluhu mbadala kwa makampuni ya mawasiliano kulinganisha gharama za kuhudumia/kufikia simu moja moja na uwezo wa watumiaji wengi kuelekea zama za kasi ya 5G.

fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika

Hio ndio mantiki ya mada yetu ya leo katika ku fahamu kuhusu mapinduzi ya teknolojia ya 5G katika biashara na uchumi wa Afrika, kwa ufupi. Unataka kujua zaidi? Karibu uwasiliane nami kwa njia ya WhatsApp kupitia namba hii hapa 0765834754 Makala hizi hapa zinarandana na somo ulilolipata leo hapa. Zitakusaidia sana ukizipitia:

  1. FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA
  2. TEKNOLOJIA YA HUDUMA ZA FEDHA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
  3. FAHAMU KUHUSU MAPINDUZI YA 4 YA VIWANDA DUNIANI
  4. KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA, KUNA MANUFAA GANI KWAKO?