UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Mteja hakosei na mteja ni mfalme. Hizi ni kauli maarufu sana katika biashara duniani, lakini haswa biashara zinazofanyika kusini mwa jangwa la Sahara. Maana yake ni kwamba, Mteja anatakiwa kusikilizwa na kuridhishwa na huduma/bidhaa zinazotolewa na mfanyabiashara. Je, wewe unatumia mbinu zipi ili kuhakikisha huduma/bidhaa zako zinawaridhisha wateja wako? Katika makala yetu ya leo utakwenda kufahamu kwa undani siri na umuhimu wa takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja. Twende pamoja mpaka mwisho.
Sasa ripoti ya mwaka 2019 kutoka shirika la kimataifa la ukaguzi wa mahesabu la PwC imeonyesha kwamba 64% ya Wakurugenzi wa Makampuni na Wafanyabiashara barani Afrika hawana data na takwimu kuhusu mwenendo wa wateja wao. Inashangaza eeh?
Kwa upande mwingine ripoti ya McKinsey imeonyesha kwamba makampuni yanayotumia data na takwimu sahihi kuhusu mwenendo wa wateja wao huyazidi yale yasiyofanya hivyo kwa 85% katika ushindani wa masoko na 25% zaidi katika kuingiza mapato kila mwaka.
Zaidi 95% ya wateja huongelea zaidi huduma mbovu walizokutana nazo katika kampuni/biashara fulani (Mtandao wa American Express), hali kadhalika 89% kati yao huacha kabisa kufanya biashara na kampuni/biashara fulani baada ya kukumbana na huduma/bidhaa zisizokidhi mahitaji/viwango walivyotegemea (ripoti ya Huduma kwa wateja ya mtandao wa RightNow). Kama unaijali biashara yako na ungependa kuona inazidi kukua, makala haya ni kwa ajili yako.
Sasa Changamoto; Kuna umuhimu gani katika kumridhisha mteja wako katika biashara unayofanya baada ya kujua takwimu sahihi kuwahusu?
1. KUONGEZA MAHUSIANO MAZURI NA MTEJA; Mteja aliyeridhishwa na huduma/bidhaa zako atabaki kuwa mteja wako kwa muda mrefu zaidi kutokana na huduma bora anazopata kutoka katika kampuni/biashara yako. Hakikisha unamshirikisha mteja kufanya maamuzi katika mchakato mzima wa kuhudumia. Muulize maswali kama Unaonaje ikiwa hivi au ikionekana vile, Unajiskiaje. Mpeti peti mteja wako muda wote kama unataka aendee kutumia huduma/bidhaa zako.
2. Waswahili wanasema, Kauli Njema ni silaha. Yaani unapokuwa na Kauli njema katika kusambaza huduma/bidhaa zako, unaiweka bishara/kampuni yako katika nafasi nzuri ya kuishindani dhidi ya washindani wako katika soko. Kauli njema ni kama sumaku ambayo inawaleta pamoja wateja na huduma/bidhaa zako na hivyo kufanya wateja wako kuendelea kuwa wako, lakini zaidi kauli njema huwavuta pia wateja wapya kuanza kutumia huduma/bidhaa zitokazo katika biashara/kampuni yako.

3. KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATANGAZO; Kampuni/biashara yako inapotoa huduma bora kwa wateja wake huwafanya wateja hao kuwa mawakala ambao hutangaza huduma bora wanazopata katika kampuni/biashara hio. Kama tulivyoona hapo mwanzo, 95% ya wateja duniani hueleza katika jamii zao jinsi walivyokutana na huduma mbovu/dhaifu walizokutana nazo katika kampuni/biashara fulani. 89% kati yao huacha kabisa kujihusisha na bishara/kampuni ambayo haikuwapatia huduma bora au haujali wateja wake. Hata hivyo bado ni muhimu sana uendelee kuitangaza biashara yako. Gusa hapa kufahamu kwanini.
Na njia bora kabisa ya kutoa huduma bora na kwa wakati huo huo ukipunguza gharama za matangazo ni kwa kutumia teknolojia kama website iliyounganishwa na huduma za S.E.O. Kwanini uwe na website? Majibu yanapatikana kwenye makala hii hapa kufahamu kwanini ni muhimu kuwa na website rasmi ya biashara yako.
4. MAFANIKIO KATIKA BIDHAA/HUDUMA ZIJAZO; Kampuni/biashara hujiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa katika kusambaza huduma/bidhaa zake mpya pale inapokuwa na kumbukumbu nzuri katika kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Matokeo yake, kampuni/biashara hulenga wateja wake wa kudumu katika kusambaza huduma/bidhaa zao mpya ambapo hujihakikishia mafanikio kabla ya kuwasambazia wateja wapya. Hata hivyo wateja wanaoridhishwa na huduma bora zitolewazo hupendelea bidhaa/huduma mpya zitokazo katika kampuni/biashara walizowahi kuhudumiwa vizuri hapo mwanzo.
5. MTEJA WA KUDUMU NI LULU; Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani (#WhiteHouse) Ofisi inayoshughulikia maswala ya wateja, kwa wastani, mteja aliyeridhika na huduma/bidhaa (mteja wa kudumu) katika biashara ana thamani mpaka mara 10 zaidi kuliko thamani ya manunuzi yake ya kwanza.
Tafiti zingine zimeonyesha kwamba ni ghali zaidi ya mara 6 mpaka 7 kumpata mteja mpya kuliko kumtunza mteja wa aliyepo/wa kudumu. Taasisi za kifedha, mabenki na makampuni ya simu kwa mfano, yamejifunza sana katika hili, hivyo hawaoni tabu kuchukua hatua za ziada kuhakikisha mteja ambaye hakuridhishwa na huduma anapatitwa suluhu mbadala haraka sana kuendana na mahitaji yake. Hapa ndio utauona umuhimu wa takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.
6. WANAWEZA KUACHA KUWA WATEJA WAKO MUDA WOWOTE; Si jambo la ajabu hasa katika zama hizi za usasa mteja kuhamia kampuni yoyote atakayopenda kutumia huduma/bidhaa zake. Hii huchochewa zaidi na huduma mbovu/dhaifu za wateja wanazopatiwa zikiwemo kusubirishwa muda mrefu katika kupatiwa huduma/bidhaa/mrejesho/maoni kutoka kwenye kapuni/biashara fulani. Ni jambo lisolopendeza kabisa, lakini bado mambo kama hayo yanaendelea kutukia.
“Mteja anapokwambia hitaji lake, hakwambii tu kuhusu maumivu yake, anakwambia pia jinsi ya kutengeneza bidhaa/huduma itakayomfaa pamoja na biashara yenye ubora. Huduma kwa wateja zinatakiwa kubuniwa katika namna inayotambua changamoto hizo.” Anasema Kristin Smaby katika mtandao wa https://alistapart.com.
Huwezi kupata wateja watakaoridhika na bidhaa/huduma zako milele. Hivyo yakubidi kama mfanyabiashara kuzitafuta changamoto zinazowakabili wateja wako kwa; kuzungumza nao, waulize maswali kuhusu vile wanataka kujiskia ukiwahudumia, wape msaada pale watakapohitaji, wape ofa, punguzo la bei na mambo kama hayo. Utakapowahudumia vizuri wateja wako utakidhi mahitaji ya wote; biashara yako na wateja pia. Wao wanapata huduma bora, biashara inapata mapato na kila mmoja anabaki na furaha.
Njia bora zaidi ya kuhakikisha unazipata changamoto zinazowakabili wateja wako ni Kwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ni kiungo muhimu sana cha kuunganisha mfanyabiashara na wateja wake katika kuimarisha viwango vya utaoji huduma. Sasa unawezaje kuitumia mitando hii kwa usahihi? Tafadhali fuatana na link hii hapa.
Ni matumaini yangu leo umefahamu kwa undani umuhimu wa takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja. Utakwenda kuzitumia vipi mbinu hizi za leo? Niambie kwenye comment hapo chini..
Je umependezwa na makala yetu hii ya leo kuhusu umuhimu wa takwimu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?
Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu(website design, logo design, Digital consultacy n.k) BILA MAKATO ya miamala.
Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
