Tag: hifadhi

Hifadhi mbadala ya nyaraka (Data backup strategies)

HIFADHI MBADALA YA NYARAKA (DATA BACK UP)

Mwaka 2017 Makampuni ya CISCO na Microsoft yalitoa ripoti yao ya mwaka kuhusu Usalama wa masuala ya Kimtandao ambapo ilionekana kwamba matukio ya udukuzi yaliongezeka maradufu katika maeneo ya kibiashara/kampuni na taasisi mbali mbali. Zaidi ya hayo iligundulika kwamba biashara nyingi licha ya kuingia katika majanga ya kudukuliwa taarifa zao, zilijikuta zikipoteza vitu vingine vingi kwa wadukuzi wa kimtandao na wezi zaidi hata ya pesa na taarifa zao.Sasa leo tuone kuhusu hifadhi mbadala ya nyaraka (Data Backup), ni nini na inafanya kazi vipi. Fuatana na makala hii mpaka mwisho.

Kulingana na Shirika la Acromis, zaidi ya nusu ya biashara zote duniani ni muhanga wa matukio ya udukuzi wa kimtandao na wizi wa taarifa muhimu za taasisi. Matukio hayo yanahofiwa kusababisha hasara kwa kampuni kutokana na kuharibu taswira ya taasisi katika jamii, kushusha heshima ya wateja kwa taasisi na kupunguza uaminifu wa taasisi kwa wateja wake na jamii kwa ujumla. Kuhusiana na udukuzi na namna unavyoweza kupambana nao bila shaka utataka kujifunza kupitia makala hii hapa chini.

Ripoti hiyo ya CISCO na Microsoft pia imetaja kwamba zaidi ya aslimia ishirini na tisa (29%) ya biashara ambazo ni muhanga wa mashambulio ya udukuzi hupoteza mapato yao na takribani asilimia arobaini (40%) ya biashara hizo hupoteza asilimia ishirini (20%) ya jumla ya mapato yao kwa mwaka.

Kati ya biashara zilizopo duniani, takribani robo ya biashara hizo hupoteza nafasi muhimu sana za kuongeza wigo wa kibiashara kufuatia kupotea kwa taarifa zake kuishia mikononi mwa wadukuzi na matukio ya wizi wa nyaraka. Na zaidi ya 20% ya biashara zinazopitia katika janga ya kupotea kwa nyaraka zao muhimu hupoteza pia wateja wao. Na 40% kati yao hupoteza zaidi ya 20% ya wateja wao kila mwaka.

Sasa unaweza vipi kuhakikisha wateja wako wanaendelea kuwa kwako bila ya kuwapoteza? Hakikisha unapitia makala hii hapa ili ujue  UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA .

Zaidi ya wadukuzi wa kimtandao na matukio ya wizi wa nyaraka, Majanga ya kiasili yanayotokea duniani pia huchangia kwa kiasi kikubwa upotevu wa nyaraka muhimu za taasisi. Mafuriko, Majanga ya Moto, Hali ya unyevu unyevu, Kimbunga na Tetemeko la ardhi husababisha athari kubwa zaidi katika uhifadhi wa taarifa muhimu za taasisi. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya upotevu wa taarifu hizo muhimu za taasisi na biashara mbalimbali, wataalamu wa masuala ya uhifadhi wa taarifu na nyaraka muhimu za kibaishara na taasisi duniani kupitia katika ripoti ya mwaka ya makampuni ya CISCO na Microsoft, njia mbali mbali za hifadhi mbadala ya nyaraka (Data Backup) zilishauriwa:

1. NJIA YA 3-2-1:

Njia hii ni kanuni bora sana ya kuhifadhi nyaraka na taarifu za kampuni/taasisi au biashara kwa urahisi na wepesi zaidi. Inafanya kazi kama ifuatavyo., • Tengeneza nakala tatu (3 copies) kaika kila nyaraka zako unazozifanyia kazi kila siku. Hapa unajihakikishia kwamba hakuna tukio lolote ambalo litaweza kuziharibu nakala zote tatu kwa urahisi.

• Katika nakala zako tatu, mbili (2) zihifadhi katika mitindo (formats) tofauti ambayo inaweza kuwa disk format, tape, cloud na kadhalika.

• Nakala moja (1) iweke mbali kabisa na mahali unafanyia kazi (inaweza kuwa nyumbani, mkoani, nchi nyingine n.k) ili kuepuka hatari ya majanga ya moto, unyevu unyevu, mafuriko, vimbunga na wezi.

2. NJIA YA MTANDAO WA KOMPYUTA:

Njia hii pia imethibitika kuwa na ubora katika uhifadhi mzuri wa nyaraka. Hapa nyaraka zinahifadhiwa katika kompyuta zaidi ya moja ambazo zimeunganishwa katika mtandao fulani( inaweza kuwa LAN, MAN au WAN). Njia hii huhakikisha usalama wa nyaraka za taasisi au biashara yako kuongeza uwezo wa upatikanaji wa nyaraka kwa wahusika wale tuu waliokusudiwa kushirikiana katika kufanyia kazi na kuhifadhi nyaraka hizo katika muda muafaka.

Njia ya Kompyuta katika kuhifadhi data

3. NJIA YA INTANETI (CLOUD BACK UP):

Hii ni njia rahisi na ya kisasa zaidi katika nyanja ya uhifadhi mbadala wa Nyaraka za taasisi/kampuni au biashara yako. Katika njia hii kanuni kubwa inayotumika ni kupandisha nyaraka zako katika majukwaa ya kimtandao ambayo yanatoa huduma hio ya uhifadhi kwa njia ya Intaneti.

Mpaka kufikia mwaka 2022 katika intaneti inakadiriwa kutakuwa na zaidi ya Terabite (TB) bilioni 2 za nyaraka zitakazohifadhiwa. Mashirika na Makampuni ya kimataifa ya NASA na GOOGLE yanajipanga kila siku kuongeza nafasi ya uhifadhi katika majukwaa yao ya huduma za intaneti. Hali kadhalika makampuni mengi zaidi yanaibuka duniani na kutoa huduma hii ya uhifadhi wa nyaraka kwa intaneti ambapo huduma hii inazidi kuboreshwa kila siku.

cloud data storage

Kampuni la Microsoft kwa mfano, limeanzisha huduma ya Office 365 ambayo ni mageuzi ya Programu ya Microsoft Office ambayo watu wengi duniani wamezoea kuitumia katika kazi zao za kila siku. Hata hivyo huduma hii ya office 365 ni ya kimtandao zaidi ambapo sasa mtu unaweza kufanya kazi zako ukiwa popote na katika vifaa mbali mbali vya kielektroniki kama simu janja na kompyuta mpakato ikiwa tuu tayari umeshajipatia huduma hii kutoka Microsoft. Hali kadhalika kampuni ya Google nayo imeanzisha huduma ya Google Drive ambapo inawezesha kuhifadhi nyaraka zako vizuri, kwa muda mrefu na kwa usalama wa hali ya juu. Vile vile duniani yameanzishwa majukwaa mengine mengi ya huduma za uhifadhi nyaraka kwa intaneti kama Dropbox, Acronis Data Backup na kadhalika.

Lengo kuu la huduma hizi za hifadhi mbadala ya nyaraka (Data Backup) zako ni kuhakikisha Usalama wa taarifa zako za kibiashara au taasisi/kampuni unakuwa wa hali ya juu na hivyo kuongeza ufanisi wa huduma/bidhaa zako kila siku.

Kama una la ziada usisite kuwasiliana nasi kuweza kupata huduma bora na za kisasa za kimtandao ili kuimarisha biashara yako ili iweze kuendana na kasi ya kidunia. Wasiliana nasi kupitia mawasiliano yetu hapa au komenti hapa chini. Karibu sana.

Call/WhatsApp: +255765834754

Email: info@rednet.co.tz