Tag: efd

mageuzi ya untaneti (iot) katika biashara na maisha. ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania

UFAHAMU MFUMO WA KODI NCHINI TANZANIA

Tangu kuanza kwake ikiitwa kodi ya kichwa (Poll tax) iliyoasisiwa katika ukoloni wa Uingereza mnamo karne ya 19, mfumo wa kodi umekuwa mpaka kufikia kuwa tata sana kuuelewa sawia. Ungana nami leo ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania.

Mfumo wa kodi nchini Tanzania unajumuisha aina mbalimbali za kodi zikiwemo Kodi za Moja Kwa Moja (Direct Taxes) na Kodi zisizo za moja kwa moja (Indirect Taxes). Hivyo kodi zote zinazolipwa nchini basi zinaangukia katika moja ya sehemu hizo mbili.

Vilevile ukusanywaji wa kodi umegawanyika katika pande mbili; Serikali Kuu ambayo hukusanya kodi kupitia Mamlaka ya Kodi (TRA) na Serikali za Mitaa ambayo hukusanya kodi kupitia Halmashauri zake. Vyombo hivi hutumia teknolojia na mifumo ya kisasa katika kukusanya kodi ikijumuisha; Mfumo wa malipo ya Leseni na forodha(TANCIS), mfumo wa mapato wa Serikali za mitaa(LGRCIS), mfumo wa kuratibu mashine za mauzo ya kielektroniki (EFDMS), mfumo wa kuratibu hesabu za kifedha za serikali(IFMS), mfumo wa manunuzi ya kiserikali(PPMS) nakadhalika. Hii ni mifumo muhimu sana katika ku ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania kwa mapana yake.

Mifumo hio yote husimamiwa na mamlaka ya kodi(TRA) ili kuhakikisha mapato yote yanakusanywa na kurekodiwa kwa kiwango kinachotakiwa. Mamlaka inakusanya mapato ya sehemu 3 ambazo ni Mapato ya Ndani(Domestic Revenue), Forodha na Ushuru(Customs and Excise) pamoja na Walipa kodi wakubwa (Large Taxpayers).

Mwaka 1969 serikali ilipiga marufuku kodi ya kichwa ambayo iligeuka mwiba mchungu katika njia za ukusanywaji wake kwa wakati huo zilizolalamikiwa kuwa ni za kinyanyasaji. Huo ukawa mwanzo wa kuanzishwa kwa kodi zingine mbalimbali mpaka kufikia utitiri wa kodi ambao upo hivi sasa.

Hivi karibuni TRA ilitangaza kubadili utaratibu wa kulipa kodi ya PAYE (Pay As You Earn) kwa waajiriwa kutoka kulipwa na mwajiri/kampuni kufikia sasa ambapo kodi hio itakuwa ni wajibu wa mwajiriwa kulipa moja kwa moja kupitia Namba ya mlipa kodi (TIN Number). Tuzione aina za kodi;

1. DIRECT TAXES

Hizi ni zile kodi ambazo hulipwa moja kwa moja kutoka katika biashara/kampuni kwenda kwenye mamlaka ya kodi;

i. Corporate Taxes

Kodi hii hulipwa na makampuni/mashirika kutokana na faida wanayopata kwa mwaka mzima wa kifedha ambayo huwa ni 30% ya faida nzima ya biashara kwa mwaka mzima wa fedha. Lakini wafanyabiashara nao wana mbinu zao za kukwepa kodi kisheria ikiwemo kuorodheshwa katika Soko la Hisa(DSE) ambao hilipia 25% tu ya faida yao, jambo linalofanya TRA kupungukiwa mapato stahiki kutoka kwenye kodi hii.

Kuna kitu kinaitwa “Alternative Minimum Tax” ambayo ni kodi mahsusi kulipwa na kampuni/biashara ambazo zimerekodi hasara kwa miaka mitatu mfululizo. Katika hali hii kampuni hutakiwa kulipa 0.3% ya hesabu zao(turnover) wanazowasilisha katika mamlaka katika mwaka wa tatu wa hasara.

ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania

ii. Individual Income Tax

Hii ni kodi ambayo huchajiwa na mfanyabiashara binafsi au mwajiriwa kulingana na kipato chake. Viwango vya kodi huanzia 9% mpaka kufikia 30% ya kipato au faida katika mauzo. Hata hivyo kwa asiye raia ya Tanzania huchajiwa 20% ya jumla ya kipato chake.

iii. Withholding Tax

Hii ni ile kodi ambayo mfanyabiashara humlipisha mteja wake katika manunuzi ya bidhaa/huduma fulani. Anayepokea kodi hii anapaswa kuiwasilisha katika mamlaka ya kodi ikiwa sambamba na taarifa za malipo ya risiti zilizotolewa kwa mnunuzi. Hii ni kodi muhimu kabisa katika ku ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania.

MIKATABA YA KODI

Mpaka kufikia sasa Tanzania imewekeana makubaliano kuhusu maswala ya kodi na nchi 9. Mikataba hio ipo hai mpaka kufikia sasa. Ili uweze kupata mikataba hio tafadhali gusa link hizi zifuatazo:

1. Tanzania-Zambia Treaty:

2. Tanzania-Sweden Treaty:

3. Tanzania-Norway Treaty:

4. Tanzania-India Treaty:

5. Tanzania-Finland Treaty:

6. Tanzania-Denmark Treaty:

7. Tanzania-Canada Treaty:

8. Tanzania-South Africa Treaty:

9. Tanzania-Italy Treaty:

2. INDIRECT TAXES

Hizi ni zile kodi ambazo hazilipwi moja kwa moja katika Mamlaka za kodi. Yaani kodi hizi hulipwa katika matumizi ya bidhaa, gharama za kuagiza mizigo nje ya nchi (import duty), ushuru wa bidhaa (excise duty) pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Dhamana ya kulipa kodi hizi ambazo si za moja kwa moja humwangukia yule anayepokea malipo ya huduma/bidhaa ambaye ndiye anaichaji kodi hii, hivyo muuzaji hapa ndiye anawajibika kuilipa kodi hii katika mamlaka. Upande wa pili mlipaji mkuu wa kodi hii ni mtumiaji wa bidhaa/huduma.

Sasa tuzione hizo kodi zenyewe;

i. VAT (Value of Added Tax)

Kodi hii ya ongezeko la thamani kimsingi ipo kwenye bidhaa zote zinazotengenezwa kiwandani na kuuzwa mitaani. Yaani hii kodi unailipa kila siku unapofanya manunuzi yako ya kawaida kama vocha, sukari, mafuta, unga nk.

Kiwango cha kodi hii ni 18% ya thamani ya bidhaa unayonunua kila siku. Wafanyabiashara waliosajiliwa na mamlaka za kodi wanapaswa kuwasilisha hesabu (returns) zao kila mwisho wa mwaka wa fedha ambayo ni mwezi June. Hata hivyo kampuni zinashauriwa kufanya returns zao kila mwisho wa mwezi au kila mwisho wa robo ya mwaka (miezi 3) wanapaswa kufanya returns. Hii ni kuwarahisisha kazi ya kujumuisha hesabu za kifedha ambazo zinaweza kuwa nyingi katika kipindi cha mwaka mzima.

ii. Excise Duty

Kodi ingine ambayo hailipwi moja kwa moja ni hii excise duty (ushuru wa forodha/bidhaa). Huduma ambazo hutozwa kodi hii zinajumuisha malipo ya vocha za simu ambayo huchajiwa na kampuni za mawasiliano na matangazo ya mtandaoni (pay per view).

Kadhalika, bidhaa zinazoangukia kodi hii ni mafuta, vileo/bia, maji ya chupa, sigara, mvinyo na magari ambayo ambayo uwezo wake wa injini ni zaidi ya 1000cc.

iii. Custom/Import Duty

Hii ni kodi ya wajibu wa kawaida ambayo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu uratibu wa kawaida ya mwaka 2004 (itafute). Kwanzia mwaka 2010, wakazi wa jumuiya hio hawapaswi kulipa ushuru wa bidhaa (import duty) kwa bidhaa zote zinazozalishwa na/au kusafirishwa ndani ya mipaka ya jumuiya. Hi iliwekwa ili kuruhusu uhuru wa masoko na bidhaa.

Viwango vya kodi hii ni 0% kwa malighafi zitokazo nje ya jumuiya, mazao ya kilimo na wanyama pamoja na bidhaa za mtaji (capital goods) huchajiwa 5% mpaka 10% kwa bidhaa za kati na 25% kwa bidhaa kamili. Zaidi, vifaa vya migodini huchajiwa 0% kabla havijaanza uzalishaji, na 5% baada ya mwaka wa uzalishaji. Vifaa vya wachimbaji wa gesi na mafuta vinachajiwa 0%.

leo katika ku ufahamu mfumo wa kodi nchini Tanzania, umepata jambo gani jipya? Wakati ujao tutaona Serikali za Mitaa zinavyokusanya mapato yake nchini. Maoni yako ni muhimu, tunakusikiliza. Links hizi hapa chini zitakupa mwanga zaidi kuhusu mifumo ya kodi na umuhimu wake katika biashara yako:

  1. UNAWEZA VIPI KUKABILIANA NA HASARA KATIKA BIASHARA YAKO MWAKA HUU 2021?
  2. UFAHAMU MFUMO WA KODI NA MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA
  3. LIPA KODI KWA FAIDA YA BIASHARA YAKO