Tag: dodoma

TEKNOLOJIA KATIKA BIASHARA ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA (TECHNOLOGY IN SUB SAHARAN BUSINESS )

Kwa watumiaji wengi wa simu za mkononi waishio Kusini mwa jangwa la Sahara, simu ya mkononi si kwamba ni kifaa cha mawasiliano tu, lakini zaidi ni kifaa muhimu cha kuperuzi mtandaoni na kupata huduma mbalimbali za msingi za kibinadamu. Ujio wa simu za rununu (Smartphones) eneo hilo umekuwa maradufu katika miaka ya hivi karibuni. Watumiaji wa simu za rununu wameongezeka kutoka 25% mwanzoni mwa muongo huu (2010’s) mpaka kufikia 44% mwishoni mwa mwaka 2017. Hii ni chini ya wastani wa kidunia wa 66% katika ongezeko hilo la watumiaji wa simu za mkononi. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa shirika la kimataifa la mfumo wa mawasiliano ya simu GSMA.

Watumiaji hao wa simu ambao ni 44% ya jumla watu waishio katika eneo hilo sawa na watu milioni 444 ambao pia ni aslimia 9% tu ya watumiaji wote wa simu za mkononi duniani wanatajwa kupatikana katika eneo hilo la kusini mwa jangwa la Sahara.

Pia inatajwa kwamba ongezeko hilo la watumiaji litakuwa katika kiwango cha CAGR (Compound Annual Growth Rate) kwa 4.8 katika kipindi cha mwaka 2017 hadi 2022, ambacho ni zaidi ya mara mbili ya CAGR ya dunia nzima katika kipindi hicho hicho.

Moja ya vitu vinavyotoa nguvu katika ongezeko hili ni pamoja na uwezo wa simu za rununu (janja) kuunganisha watu wengi kupitia huduma za intaneti na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao hio ndipo panapotumiwa na watu wengi kama sehemu ya kukutana, kubadilishana mawazo, kuburudika na kufanya biashara. Hivyo kufanya mitandao hio ya kijamii kuzidi kuwa na umuhimu kadiri muda unavyokwenda.

Kibiashara hii ina maana gani?

Ripoti hio ya GSMA iliyochapishwa mwaka 2018 inataja kwamba ukuaji wa teknolojia umerahisisha mambo mengi muhimu yakiwemo utolewaji wa elimu, maswala ya afya na tiba na pia kuwezesha mazingira bora ya kufanyika biashara katika kutunza na kuonyesha kumbukumbu mbalimbali, miamala ya kifedha na jinsi bora ya kumhudumia mteja hata akiwa mbali na mzalishaji kupitia majukwaa ya huduma za kifedha za kimtandao na IoT (Internet of Things). Ripoti hio pia inaakisi kasi ya ukuaji wa matumizi ya simu za rununu (samrtphones) pamoja na vifaa vya kiteknolojia mpaka kufikia mwaka 2025 katika utendaji na utoaji wa huduma mbalimbali za kibinadamu pamoja na shughuli za kibiashara katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara.

Pia unaweza kupitia makala hizi hapa chini ambazo zinarandana na somo ulilolipata kwenye makala ya leo. Zitakusaidia sana ukimaliza kuzisoma zote.

  1. https://rednet.co.tz/unawezaje-kutumia-ujasusi-katika-biashara-yako-business-intelligence/ yenye kichwa “UNAWEZAJE KUTUMIA UJASUSI KATIKA BIASHARA YAKO?”
  2. https://rednet.co.tz/uwiano-wa-mali-assets-na-madeni-liabilities-katika-biashara-ukweli-ni-upi/ yenye kichwa “UWIANO WA MALI(assets) NA MADENI(liabilities) KATIKA BIASHARA, UKWELI NI UPI?”
  3. https://rednet.co.tz/changamoto-katika-biashara-mpya-inayoanza-funzo-lisiloepukika/ yenye kichwa “CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA MPYA/INAYOANZA, FUNZO LISILOEPUKIKA.”
  4. https://rednet.co.tz/fahamu-mchango-wa-ict-katika-maendeleo-ya-sekta-binafsi-barani-africa/ yenye kichwa “FAHAMU MCHANGO WA ICT KATIKA MAENDELEO YA SEKTA BINAFSI BARANI AFRIKA”
  5. https://rednet.co.tz/kuanzishwa-kwa-eneo-huru-la-biashara-barani-africa-afcta-kuna-manufaa-gani-kwako/ yenye kichwa “KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA, KUNA MANUFAA GANI KWAKO?”