CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA MPYA/INAYOANZA, FUNZO LISILOEPUKIKA.
Bila shaka umeshasikia misemo kama ‘survival for the fittest’ ama ‘Bahari tulivu haizalishi nahodha hodari’, wengine wanakwambia “Mwanzo mgumu”. Sasa kwenye biashara, mambo yapo hivyo hivyo, changamoto haziepukiki. Sasa leo tuazione changamoto katika biashara mpya/inayoanza, hili ni funzo lisiloepukika kabisa. Twende sambamba.
Leo hii, duniani kunaripotiwa kuwapo takriban kampuni/biashara 150 milioni zinazoanza (startups), huku kukiwa na ongezeko la kampuni hizo milioni 50 kila mwaka. Kwa wastani kuna kampuni zinazoanza 137,000 zinaanzishwa kila siku. Hebu niambie, umeshaanzisha biashara ngapi hadi leo? ngapi zimeshakufa? Ngapi upo nazo mpaka leo? tuambie kwenye comments pale chini.
Lakini swali la msingi ni je, hizi kampuni zinazoanza, zinaweza vipi kuhimili mawimbi makali ya changamoto zilizopo katika ulimwengu wa biashara duniani? haswa eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara (ambalo linatajwa kuwa na changamoto nyingi zaidi za kibiashara).

Takwimu zinaonyesha kuwa 80% ya biashara/kampuni zinazoanza hufa ndani ya mwaka wa kwanza tu tangu kuanzishwa kwake. Na katika hizo 20% zilizobaki 10% hufa ndani ya miaka mitano tangu kuanzishwa. Tatizo ni nini? Wafanyabiashara hawa wanakosea wapi? Ni changamoto gani hizo ambazo pengine wafanyabiashara/waanzilisi wa kampuni hizo hawakuwa wanazijua mpaka zinapelekea biashara/kampuni zao kufa kabla hazijafikia ndoto na malengo yale makubwa ambayo waanzilishi walijiwekea mwanzoni. Hizi changamoto katika biashara mpya/inayoanza, hili ni funzo lisiloepukika kabisa.
Sasa leo tuzione hizo changamoto katika biashara mpya/inayoanza, ni funzo lisiloepukika kweli?;
1. USHINDANI MKALI
Hakuna wakati katika historia ya mwanadamu biashara zimekuwa zikifanyikwa kwa ushindani kama sasa. Yaani usitegemee kuanzisha biashara ambayo haina ushindani. Pia ni ngumu sana kuanzisha biashara ambayo haijawahi kufanyika kabisa hapo kabla. Hivyo jipange na ujiandae kisaikolojia.
Ujio wa matumizi ya intaneti umeongeza sana hali ya ushindani ambapo kwa sasa masoko hutafutwa kwa njia za kidijitali zaidi. Biashara zinahamia mtandaoni na hivyo huna budi kuhakikisha unatafuta wateja kwa nguvu sana kwa njia za Digital marketing, social media marketing, affiliate marketing na nyingine nyingi ili kuhakikisha biashara yako inaendelea kupata wateja wapya na kuwafikia wale ulio nao kirahisi zaidi.
Lakini njia rahisi (japo sio nyepesi) ya kuepuka ushindani sokoni ni kuwa MKIRITIMBA (Being a Monopoly). Hii ni ile hali ya kucontrol soko na kukamata wateja wengi kiasi kwamba washindani wako hawana nguvu ya kupambana na wewe sokoni. Zaidi kuhusu ukiritimba fuatilia makala hii hapa
2. WATU SAHIHI
Waswahili wanasema, Biashara ni watu. Hii haiishii kwa watu kwa maana ya wateja peke yake, watu hawa haswa wanangukia kwenye wabia, wafanyakazi na washauri wako katika biashara. Hawa wana mchango mkubwa na muhimu sana katika kuua au kuendeleza biashara yako.
Hii Rednet ni mfano sahihi katika sehemu hii kwa kuwa mwanzoni Rednet Technologies ilihisusha watu 6. Lakini kutokana na kutoshare vision na sababu zingine, Rednet haikuweza kushamiri katika mwaka wake wa kwanza mpaka tulipoamua kupunguza watu mpaka kupata watu sahihi wa kufanya nao kazi kwa maslahi mapana ya kampuni. Unapoamua kuanzisha biashara/kampuni mpya hakikisha unazungukwa na watu sahihi watakaoimarisha zaidi biashara/kampuni hio. Wahenga wanasema “Ndege wanye manyoya yanayofanana, ndio wanaoruka pamoja”. Take that note.
3. MASWALA YA FEDHA
Moja kati ya vitu vinaua biashara/kampuni nyingi ni Kutokujua kutofautisha maswala ya fedha ya kampuni na yale binafsi. Elewa, ukishaingiza pesa kwenye biashara/kampuni, pesa hio sio Binafsi tena. Inatakiwa izunguke mpaka itoe return/faida ambayo ndio inaweza kutumika kwa matumizi binafsi. Hii ni changamoto kubwa na inayohitaji umakini mkubwa ili kuihimili. Lile gepu la masikini na tajiri kwa kiasi kikubwa huwa linapigwa kutokana na uwezo wa kupambana na changamoto hii.

4. UFINYU WA RASILIMALI
Miongo michache iliyopita kuanzisha biashara/kampuni mpya ilimlazimu mtu kuwa na mtaji mkubwa ama kuwa na uwezo wa kufanya harambee ya kukuza mfuko wa uwekezaji. Kwa wakati huo mawazo mengi yalishindwa kuwa biashara/kampuni zenye tija.
Lakini leo hii kunakadiriwa kuanzishwa takribani biashara mpya 137,000 kila siku duniani kote. Hii ni kutokana na kukua kwa kasi ya teknolojia katika shughuli za kibiashara ambayo imerahisisha sana upatikanaji wa rasilimali. Lakini swala la maarifa ghafi (softskills) bado limekuwa ni changamoto katika uendeshaji wa biashara nyingi ambapo licha ya kuwa na wazo zuri ama mtaji wa kifedha, bado kuwa na maarifa ya kuendesha biashara/kampuni inabaki kuwa ni changamoto. Hivyo ukitoa Wazo, Vifaa vya kufanyia kazi na Pesa ya uwezeshaji, Maarifa ni rasilimali muhimu zaidi.
5. UWEZO WA KUTOA MAAMUZI SAHIHI
Katika kuanzisha biashara/kampuni mpya, moja kati ya Changamoto kubwa zinazowakabili waanzilishi ni Uwezo wa Kutoa maamuzi sahihi kulingana na wakati na hatua biashara/kampuni inayopitia. Moja kati ya changamoto zinazosumbua sana katika biashara.
Ukiwa mfanyabiashara/mbia wa kampuni unalazimika kufanya maamuzi mengi kila siku. Katika maamuzi hayo utajikuta wakati mwingine unafanya makosa kutokana na maamuzi yako, na pengine maamhzi hayo yanaweza kukukatisha tamaa na hata kuua biashara/kampuni yako ndani ya muda mchache.
Usiogope. Hakikisha unajifunza katika kila maamuzi unayochukua hata kama hayakuleta madhara katika biashara/kampuni yako. Wahenga wanasema “Busara hujengwa katika maamuzi“. Note hio, halafu ifanyie kazi kila siku. Kulifahamu hili kwa undani fuatana na makala hii hapa..
6. KUPATA UAMINIFU WA WATEJA
Hebu niambie, ilikuchukua muda gani kupata mteja wako wa kwanza tangu ulipoanzisha biashara/kampuni yako? Cocacola ilichukua mwaka mzima kuuza chupa moja ya soda katika mwaka wake wa kwanza tangu kuanzishwa.
Rednet ilichukua miezi 8 mpaka kumpata mteja wetu wa kwanza tangu tulipoanza shughuli zetu hapo mwaka 2016. Ni wakati mgumu sana katika biashara, lakini wahenga wanasema “Mteja ni mfalme.” Hivyo kupata mfalme wa kuhudumia kwa vyovyote si rahisi. Siku zote kizuri kinajiuza chenyewe ambapo huduma nzuri huvuta wateja zaidi kwa kutumia mbinu ya “Word of mouth“. Mbinu hii huzalisha wateja wa kudumu zaidi ambao huwa mabalozi wazuri wa biashara/kampuni yako. Jinsi ya utendaji katika biashara yako lazima ijengwe kumzunguka na kuridhisha wateja wako. Mteja asiporidhika, bado hujafanikiwa kibiashara. Zaidi tiririka na makala hii hapa kwa ajili yako..
7. USALAMA WA KIMTANDAO
Wakati huu tunaoishi ni wakati wa Kidijitali. Biashara/kampuni nyingi zinazoanzishwa zama hizi hufanyia shughuli zake mtandaoni, hivyo miundombinu ya utendaji katika biashara za kisasa kwa zaidi ya 75% hutegemea Nguvu ya mtandao.
Hata hivyo, Wadukuzi wa kimtandao wanafanya mazingira ya kiutendaji mtandaoni kuwa magumu na yenye kuhofisha. Matukio ya udukuzi na uhalifu wa kimtandao yanazidi kuongezeka kila uchwao. Tafiti zinaonyesha kufukia mwaka 2021 matukio ya uhalifu wa kimtandao yatakuwa yakitokea kila baada ya sekunde 11 duniani kote. Ili kujilinda dhidi ya uhalifu huu wa kimtandao, biashara zinazoanza hazina budi kuwa na miundombinu ya kimtandao ambayo ni imara zaidi kila wakati.
Zaidi kuhusu Usalama wa kimtandao unaweza kupata makala yetu mahsusi kupitia link hii “KWANINI USALAMA WA KIMTANDAO (CYBER SECURITY) NI MUHIMU KWAKO?“
Kifupi hizo ni changamoto chache ambazo zinazikabili biashara/kampuni inazoanza, ni funzo lisiloepukika kweli kweli. Je, wewe umepitia changamoto zipi wakati unaanzisha hio biashara yako uliyo nayo? Umeshajaribu kufanya biashara ngapi bila mafanikio mpaka kufikia sasa? Tafadhali tushirikishe ili watu wengine wapate kujifunza zaidi. Karibu.
Pia hakikisha unapitia makala hizi tumekuwekea hapa chini ili kuhakikisha unapata muendelezo mzuri kutokana na somo ulilolipata kwenye makala ya leo. Gusa link kisha makinika..
- “KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?“
- “BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA?“
- “WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA“
- “IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO“
Ni matumaini yangu leo umefahamu kwa undani changamoto katika biashara mpya/inayoanza, funzo lisiloepukika. Utakwenda kukabiliana nazo vipi changamoto hizi za leo? Niambie kwenye comment hapo chini..
Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?
Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?
Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu(website design, logo design, Digital consultacy n.k) BILA MAKATO ya miamala.
Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
