Tag: Business Intelligence

KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRICA (AfCTA), KUNA MANUFAA GANI KWAKO?

January 1, 2021 ilikua ndio siku rasmi ya kuanza kwa shughuli huru za kibiashara na uchumi baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika waliokubaliana kuanzisha AfCTA. Ni furaha ilioje.

Hata hivyo kuanzishwa kwa eneo hilo (African Continental Free Trade Area) kumekuja baada ya makubaliano rasmi baina ya nchi wanachama kusainiwa ambapo ilihitajika nchi 22 walau ili eneo hilo liweze kuanzishwa rasmi (kifungu na23 cha mkataba wa makubaliano). Hivyo tar30 May 2019 nchi 24 zilisaini hati za kuwa washiriki wa kwanza kabisa wa Eneo hilo la kibiashara.

Kufikia leo hii, nchi 35 za AU tayari zimeshatia saini kujiunga katika AfCTA ambapo jiji la Accra, Ghana limewekwa kuwa Makao Makuu rasmi.

AfCTA INA MAANA GANI?

Hili ni eneo la kinadharia, yaani hakuna soko linaloonekana kama Kariakoo ndo useme AfCTA inafanyika hapa, Hapana.

Eneo hili ni Jumuiya ya Kibiashara na maendeleo kama zilivyo Jumuiya za kikanda kama EAC na SADC, isipokuwa hii AfCTA imepangwa mahsusi kujumuisha nchi zote za Afrika kwa malengo ya kiuchumi na Biashara. Hivyo nchi zinazohitaji kujiunga zitapewa mkataba wa makubaliano kabla ya kujiunga rasmi.

Kupata Waraka wa makubaliano ambao wakuu wa nchi Washiriki waliafikiana gusa link hii itakupeleka kwenda kuuona waraka huo na kuupakua ili uusome na kujua kwa undani Mambo yaliyokubaliwa, Malengo na kadhalika: https://rednet.co.tz/download/agreement-establishing-the-african-continental-free-trade-area-afcta

Kuwa mshiriki na mnufaika wa faida za eneo hili kunamtaka mwanachama wa AU kukubali na kusaini makubaliano hayo. Hivyo inawezekana nchi ikawa ni mwanachama wa AU lakini isiwe mshirika wa AfCTA kwa kuwa ni hiari kwa nchi yeyote ya Africa kuingia katika eneo hili la kibiashara.

FAIDA NI ZIPI KUWA MWANA AfCTA?

AfCTA inatajwa kuibua eneo huru kubwa zaidi la kibiashara duniani likijumuisha idadi kubwa ya washiriki. Inatarajiwa eneo hilo litawafikia watu 1.3 bilioni waishio barani Afrika lenye pato la ndani (GDP) la pamoja linalofikia $3.4 trillioni.

Makubaliano ya kuanzisha AfCTA yalilenga kuleta faida zifuatazo:

i. Kukuza Uchumi wa nchi washiriki, Kupunguza umasikini na kupanua wigo wa uchumi shirikishi ambapo:

•Watu milioni 30 watatolewa katika wimbi la umasikini uliokithiri, na wengize zaidi ya milioni 68 wanaoishi chini ya dola 5.50 kwa siku (hapa bila shaka na wewe pia umo) watapandishwa hali zao za kiuchumi.

•Bidhaa zinazouzwa nje (Exports) zinapangwa kuongezeka kufikia thamani ya dola 600 bilioni, hasa katika sekta ya viwanda na uzalishaji.

•Kutakuwa na Ongezeko la Kipato kwa watu wenye taaluma (skilled workers) na wale wasio na taaluma (unskilled workers) kwa 10.3% na 9.8% respectfully.

•Kutakuwa na ongezeko la kipato kwa Afrika kwa dola 450 bilioni kufikia mwaka 2035, ikiwa ni ongezeko la 7%. Hivyo kuongeza pato la dunia nzima kwa dola 76 bilioni.

ii. Urahisi wa watu kusafiri na kufanya biashara baina ya nchi wanachama. Hebu imagine leo hii unaweza kufikisha bidhaa/huduma zako ndani ya nchi 35 barani Afrika bila yavikwazo vya kibiashara ikiwa mtaji unao na rasilimali za kukuwezesha kusafiri pia zipo. Upewe nini tena?

iii. Kukuza/kuchochea ushindani wa kiuchumi na biashara baina ya nchi wanachama, jambo ambalo linatajwa kuboresha mazingira ya uzalishaji wa bidhaa bora na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja kwa gharama nafuu zaidi.

iii. Kuondoa vikwazo vya mipakani (trade tariffs) ambavyo vinatajwa kuleta changamoto kubwa na kufanya wafanyabiasha washindwe kuvusha bidhaa/huduma zao kwenda nje ya nchi kwa urahisi. Sasa leo AfCTA inakuwezesha kupitisha bidhaa/huduma zako ndani ya nchi 35 bila tabu yoyote.

iv. Kuchochea maendeleo ya viwanda kupitia mgawanyo wa maendeleo na upatikanaji wa rasilimali ndani ya maeneo husika. Pia kukuza sekta ya kilimo kwa kuboresha pembejeo za uzalishaji, masoko na upatikaji wa chakula. Imagine wakulima wadogo wataokolewaje hapa na hii fursa!

v. Kuweza kupambana na athari za majanga mbalimbali ya kiasili na magonjwa ya mlipuko mfano #COVID19 ambao unatajwa kusababisha hasara ya dola 79 bilioni barani Afrika katika mwaka 2020 pekee. Ugonjwa wa Korona umesababisha hasara kubwa katika utendaji wa kibiashara ikijumuisha upatikani adimu wa bidhaa, huduma za afya pamoja na chakula. Hivyo kwa kuchochea biashara za kikanda kwa kupunguza kodi na makato/taratibu za mipakani baina ya nchi washiriki, uwepo wa AfCTA unatajwa kusaidia nchi za Afrika kuchochea uchumi na kuongeza uwezo wa kupambana na majanga mbalimbali pamoja na magonjwa ya mlipuko. Mkakati wa kuanzishwa kwa AfCTA unalenga kuzipa nguvu za kiuchumi za muda mrefu nchi washiriki, hivyo eneo hilo linatajwa kuwa ni eneo muhimu zana la kimbinu za Ujasusi wa Kiuchumi.

AfCTA ni moja ya mradi wa kimkakati wa Agenda 2063 ambao ni mpango wa kimaendeleo wa miaka 50 kutoka mwaka 2023 – 2063 uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya Umoja wa Afrika (AU). Mpango huo ulilenga kuimarisha hali za kiuchumi, biashara na maendeleo baina ya nchi wanachama.

Eneo hili pia linatajwa pia kuwa muhimu sana kwa jumuiya za maendeleo barani Afrika na nchi zingine kwa kuruhusu Makubaliano ya kibiashara kama Economic Partnership Agreement (EPA, sio ile mnayoijua nyie). Makubaliano hayo yanatajwa kuimarisha kuimarisha biashara za Jumuiya kimataifa kama EU, Jumuiya ya Nchi za Asia kusini (ASEAN) na Marekani. Ama kwa Hakika Eneo hili la AfCTA lina mchango mkubwa sana wa kuimarisha biashara ndogo ndogo barani Afrika. Ni wakati wako sasa kutumia vyema kila fursa inayojitokeza kwenye eneo hili. GET IT DONE!

Zaidi pata makala hizi zinazorandana na somo ulilolipata leo. Zitakusaidia sana ukizimaliza zote. Gusa links zifuatazo:

  1. https://rednet.co.tz/umuhimu-wa-takwimu-katika-utoaji-wa-huduma-bora-kwa-wateja/ yenye kichwa “UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA
  2. https://rednet.co.tz/kwanini-ni-muhimu-kuwa-na-websitetovuti-rasmi-ya-biashara-yako/ yenye kichwa “KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE RASMI YA BIASHARA YAKO?
  3. https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA
  4. https://rednet.co.tz/teknolojia-katika-kukuza-biashara-kupitia-sekta-ya-utalii/ yenye kichwaTEKNOLOJIA KATIKA KUKUZA BIASHARA KUPITIA SEKTA YA UTALII

Marejeo:

https://au.int/en/treaties/agreement-establishing-african-continental-free-trade-area

https://www.tralac.org/resources/our-resources/6730-continental-free-trade-area-cfta.html

https://www.worldbank.org/en/topic/trade/publication/the-african-continental-free-trade-area

Photo curtesy of the “Digital Tools on Business Performance” iliyofanyika jijini Dodoma mwaka 2020.