Mfumo wa mawasiliano ya simu (mobile ecosystem) huchangia shemu muhimu sana katika uchumi wa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara? Uchumi wa nchi hizo kwa pamoja umefikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 110 ($110 b) ambayo ni sawa na 7.1% ya pato la taifa (GDP) katika mwaka 2017. Hii inajumuisha faida za moja kwa moja za mfumo huo, faida zisizo za moja kwa moja (indirect impact) pamoja na ukuaji wa uzalishaji unaoletwa na matumizi ya huduma za simu na teknolojia.
Tukigusia faida za moja kwa moja za mfumo huu wa mawasiliano ambao unajumuisha makampuni ya simu, watengenezaji wa huduma za miundombinu ya kiteknolojia, wasambazaji wa huduma/ bidhaa za simu, wafanyabiashara wa reja reja, watengenezaji wa simu na vifaa vyake pamoja na watengenezaji wa maudhui/applications/huduma za mtandaoni; mchango wao katika uchumi hukadiriwa kwa kupimwa thamani wanayochangia katika uchumi wa nchi husika ambayo hujumuisha bima ya wafanyakazi, faida ya ziada ya biashara pamoja na kodi.
Mwaka 2017, thamani iliyozalishwa na mfumo huu wa mawasiliano katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara ulikuwa dola bilioni 40 ambayo ni sawa na 2.5% ya pato la Taifa (GDP) ambapo makampuni ya simu peke yake yalijumuisha takribani 75% ya mchango huu.
Ukiachana na faida za moja kwa moja, zipo pia faida ambazo si za moja kwa moja (indirect impact) ambapo sekta hii hununua vifaa/huduma mbali mbali kutoka sekta nyingine. Kwa mfano makampuni ya simu hulazimika kununua umeme kutoka sekta ya nishati hali kadhalika wasambazaji na wafanya biashara wa reja reja wa vifaa/huduma za simu huhitaji usafiri kuwafikia wateja wao.
Kwa pamoja uzalishaji huu wa faida isiyo ya moja kwa moja ulitengeneza takribani 60$ mwaka 2017 (ambayo ni takribani 4% ya pato la taifa). Kiujumla ukiongezea na faida za moja kwa moja, sekta hii ya mawasiliano ya simu ilitengeneza 110$ bilioni sawa na 7.1% ya pato la taifa katika ukanda huu.
Hii inaleta picha gani Kibiashara?
Matumizi ya teknolojia ya simu pamoja na maendeleo ya simu za rununu (smartphones) huendesha uchumi kwa kuboresha uzalishaji, kupunguza costs za uendeshaji pamoja na kurahishisha upatikanaji wa huduma/bidhaa za kibinadamu.
Chanzo: Ripoti ya shirika la mawasiliano ya simu duniani la GSMA toleo la mwaka 2019.
Pia unaweza kupitia makala hizi hapa chini ambazo zinarandana na somo ulilolipata kwenye makala ya leo. Zitakusaidia sana ukimaliza kuzisoma zote.
Bila kujali unafanya biashara ya aina gani, teknolojia ya intaneti na kompyuta imekuwa kwa kiwango kikubwa sana duniani hivyo kupelekea kuathiri mfumo mzima wa uendeshaji biashara duniani. Mwaka 2011 mwandishi Marc Andreessen alinukuliwa akisema, “Softwares are eating the world” akiwa na maana ugunduzi wa programu za kompyuta unarahisisha shughuli nyingi za kibinadamu kufanyika kwa haraka, kwa unafuu na kwa ufanisi zaidi kila siku zinavyozidi kwenda mbele. Sasa unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako? Leo tufahamu kwa undani.
Kufikia Octoba, mwaka 2018 tovuti ya Lifehacks (lifehacks.io) iliripoti kwamba jumla ya tovuti bilioni 1.9 zilithibitika uwepo wake kwenye intaneti pamoja na kuripotiwa kuwepo kwa machapisho (posts) zaidi ya milioni tano (5) ya blogu mbali mbali duniani kila siku. Tafiti hii ya kimtandao inakupa sababu mbali mbali za kukuwezesha kufanya biashara kwa kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta. Fuatana nasi.,
1. KUWA NA MPANGO WA BIASHARA ILI KUJUA KIUNDANI UNAWEZAJE KUTUMIA TEKNOLOJIA YA INTANETI NA KOMPYUTA:
Ukiwa na ndoto za kufanya biashara yako iwe na mafanikio maradufu, huna budi kuwa na mpango madhubuti wa kibiashara ambao utaainisha aina ya biashara unayoifanya, Jina la biashara linaloendana na aina ya bidhaa/huduma unayotoa, maudhui bora ya tovuti, soko unalolilenga na mbinu stahiki za kulikamata soko la kudumu.
2. TAFUTA NA CHAGUA JINA ZURI LA TOVUTI YA BIASHARA YAKO MTANDAONI:
Unapofikiria kuanzisha biashara, fikiria soko kwanza kabla ya aina ya biashara unayoitaka. Yaani tizama kwenye jamii, changamoto zilizopo ambazo hazijatatuliwa au hazionekani kama ni changamoto sana kwa muda huo, halafu tafuta suluhisho la changamoto hizo. Suluhisho hilo liendane na Jina zuri la kuwasilisha kile unachotaka kutatua kwenye jamii.
Uza suluhisho na si bidhaa kama bidhaa. Ukishapata Jina zuri, tengeneza tovuti yako au tafuta wataalamu waliobobea kwenye ujenzi na uendelezaji wa tovuti bora za kibiashara. KUMBUKA Tovuti sio Bidhaa bali ni Jukwaa la kufanyia biashara zako kama ilivyo ofisi yako, Fremu au Meza ya kuuzia bidhaa zako kila siku. Tofauti na ofisi, fremu au meza., tovuti ni jukwaa la kimtandao linalokuwezesha kuonyesha bidhaa/huduma zako dunia nzima kiurahisi zaidi mara moja. Kuhusu Umuhimu na faida za tovuti (website) katika biashara yako tayari nimekuwekea makala hizi hapa. Zitakufaa sana katika kuimarisha biashara yako ukizipitia zote.
3. TANGAZA NA WEKA UTARATIBU WA KUFUATILIA BIASHARA YAKO:
Dunia inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya bilioni 7 mpaka sasa. Kati ya hao watumiaji wa mitandao ya kompyuta wanakadiriwa kufika bilioni 4 ikiwa ni takwimu zilizowasilishwa na yovuti ya lifehacks. Katika watu zaidi ya bilioni 4 ambao ni watumiaji mubashara wa mitandao ya kompyuta na simu, zaidi ya watu bilioni 2.234 wamegundulika kuwa ni watumiaji wa mtandao wa kijamii wa facebook peke yake.
Mfumo wa kimtandao wa kompyuta uitwao Internet Live Stats (ILS) unatumika kufuatilia watumiaji mubashara wa watumiaji wa Intaneti duniani kote kila siku. Hii ina maana kwamba zaidi ya nusu ya jumla ya watumiaji wote wa mitandao ya kompyuta na simu duniani wanapatikana facebook. Vilevile asilimia thelathini (30%) ya jumla ya idadi nzima ya watu wanaoishi duniani ni watumiaji wa facebook.
Kwa kusema hivyo, tayari tumekuwekea makala maalum itakueleza kwanini ni muhimu uitangaze biashara yako kila siku. Tafadhali ipitie makala hio mpaka mwisho kupitia link hii hapa yenye kichwa KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO.
Hivyo kwa kuutumia vyema mtandao wa facebook peke yake kibiashara unajiweka kwenye nafasi ya kuwafikia zaidi ya watu bilioni 2 ambao wanaweza kuwa wateja wazuri katika biashara unayoifanya. Vile vile watu zaidi ya bilioni 1 wamefahamika kuwa ni watumiaji wa mtandao unaoshika kasi wa Instagram.
Zaidi ya hayo pia kama mfanyabiashara mwenye kiu ya mafanikio una wajibu wa kufuatilia maendeleo ya biashara/kampuni/taasisi yako katika muktadha wa kuichumi na masoko. Biashara inabidi iwe inakua katika viwango vinavyohitajika kulingana na kasi ya soko la dunia.
Hivyo baada ya kujiuliza unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako?, sasa unao uwezo wa kufuatilia biashara yako kwa kutumia takwimu sahihi kama ongezeko la wateja ndani ya muda fulani (wiki, mwezi au mwaka), ongezeko la faida, taarifa za mapato na matumizi na zaidi, usalama wa taarifa zako kibiashara.
Pia katika ufuatiliaji unaweza kuongeza njia kusambaza taarifa kuhusu biashara yako. Moja ya njia hizo ni Search Engine Optimization ambayo ni huduma inayotolewa na makampuni ya programu za kompyuta na mitandao. Huduma hii hukupatia nafasi ya kusambaza links za tovuti au mifumo yako ya kompyuta ambapo mtu yeyote anapotafuta bidhaa au huduma zako katika mtandao, basi inakuwa rahisi zaidi kukupata kwa kuandika maneno yanayohusu huduma hio unayotoa.
4. JIBU KWA WAKATI NA KWA UWELEDI ILI UNAPOJIULIZA UNAWEZAJE KUTUMIA TEKNOLOJIA YA INTANETI NA KOMPYUTA MTANDAONI UPATE ULE MVUTO WA KIBIASHARA
Unapokuwa mfanyabiashara au mhusika katika kampuni/taasisi fulani maana yake upo hapo kwa ajili ya wateja wako, hivyo unapaswa kutoa majibu na ufafanuzi wowote unaofika kwako kutokea kwa wateja wako. Aina ya majibu au ufafanuzi wako huchangia kwa kiasi kikubwa kupata wateja wapya kila siku au kupoteza wateja kila siku. Waswahili wanasema “Kauli Njema ni Silaha.” Hivyo kwenye kauli zako za kuhudumu ni lazima uweke uweledi wa hali ya juu ili kumvutia na kumridhisha mteja na bidhaa/huduma zako.
Kulingana na elimu ya wanasaikolojia mtu yeyote hupenda kujibiwa mara moja pale anapokuwa na shauku ya kujua jambo fulani. Hivyo unaposhindwa kujibu au kutoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bidhaa/huduma kwa wakati, unajiweka kwenye nafasi mbaya ya kupoteza wateja wengi kila siku.
5. BADILIKA KULINGANA NA SOKO LINAVYOKUHITAJI KUBADILIKA:
Dhana ya Biashara na masoko inafanana na dhana ya muziki na mtu anayeucheza muziki huo. Yaani unapaswa kuendana na mdundo wa muziki pale unapokuhitaji. Hali kadhalika unapokuwa katika ulimwengu wa biashara kwa kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta soko lako linakuwa ni kuwafikia watu bilioni 7 waliopo duniani.
Na bahati ni kwamba duniani wapo watu/kampuni/taasisi nyingi ambazo zinafanya biashara unayoifanya wewe, hivyo unapaswa kuwa mbunifu kila siku, unapaswa kuongeza ubora wa bidhaa na huduma, kuongeza mtandao wa washirika wako duniani, bidhaa/huduma mpya na mambo mengi ambayo hujitokeza kila siku kulingana na uhitaji wa wateja. Hapa inakubidi uwe mwanafunzi mwenye uwezo wa kunyumbulika wakati wowote kwa ajili ya wateja wako.
Kwanini ufanye hivyo? Majibu zaidi yanapatikana kupitia makala hizi hapa:
Zaidi, tambua Tovuti ya kwanza kabisa kuundwa duniani bado ipo hewani (info.cern.ch). Tovuti hii ilitengezwa kwa lugha ya kuundia mifumo ya kimtandao ya HTML na inaonyesha mistari michache tuu. Lakini sasa mambo ni tofauti sana katika uwanda wa usanifu na uendelezaji wa programu za kompyuta na tovuti. Kama mwandishi Marc Andreessen alivyonukuliwa mwaka 2011 akisema programu za kopyuta zinaila dunia.
Je unajiandaa vipi kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako? Tafadhali toa maoni yako kupitia comments hapo chini..