Tag: biashara bomba

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

UONGOZI vs UTAWALA KATIKA MIRADI/BIASHARA, KIPI KINAFAA ZAIDI?

“Nafikiri Kiongozi mzuri ni yule anayewafanya watu wanaomzunguka kuwa bora zaidi.” Alinukuliwa Dana Brownlee (CEO Professionalism Matters). Vipi kuhusu hali ya kuwa Mtawala, inaathiri vipi biashara? Unadhani kati ya Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi? Fuatilia makala hii mpaka mwisho kufahamu zaidi.

Tunafahamu ilivyo, ukiwa mjasiriamali/mfanyabiashara huna budi kuvaa kofia nyingi, majukumu kila kona. Ukiwa mfanyabiashara jua unawajibika kujenga na kuimarisha masoko yako, kubuni/kusimamia miradi, kutunza hesabu nakadhalika.

Hata hivyo biashara inavyozidi kukua, vitu vya kusimamia pia vinaongezeka, hivyo mfanyabiashara/mjasiriamali makini lazima aanze kufikiria namna ya kuendesha biashara yake kwa urahisi bila kuathiri shughuli za kila siku. Unahitaji msaada kutoka kwa watu wengine. Wakati huu sasa ndipo anahitajika Kiongozi zaidi kuliko Mtawala, hasa katika biashara.

KIONGOZI ANA SIFA ZIPI?

i. ANAFANYA KAZI NA TIMU YAKE: Ukiwa Kiongozi hili ni jukumu muhimu sana. Usiishie tu kutoa amri na maagizo, hapo utakuwa Mtawala, tena asiyefaa. Kiongozi anafanya kazi bega kwa bega na timu yake, kila anapohitajika kuweka mchango wake anafanya hivyo. Katika biashara za kisasa hii ina maana Kusaidia hatua za uzalishaji zizidi kuwa bora, kuboresha maudhui ya mtandaoni ya kampuni, kuhamasisha viwango katika kazi, kuongea na wateja ili kuboresha huduma. Kiongozi anaelewa vyema watu wote anaofanya nao kazi na wateja anaowahudumia, muda wote yupo updated. Njia bora zaidi ya kuwasiliana na kujua tabia na mwenendo wa watendaji katika timu pamoja na mwenendo wa wateja ni kupitia mitandao ya kijamii. Sasa mitandao ina mchango gani, tafadhali pitia makala yako hii IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO.

ii. KIONGOZI BORA NI MNYENYEKEVU: Hakuna mtu anapenda kufanya kazi na mtu mwenye kiburi, majivuno au mjuaji sana. Hata hivyo inafaa sana kwa Kiongozi kutambua pale anapokosea na kujisahihisha mara moja, vile vile Kiongozi huruhusu timu yake kutambua makosa yao na kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwa kadiri zinavyotokea. Unyenyekevu (Being Humble) husaidia kuimarisha morali ya ufanyaji kazi katika miradi/biashara kuliko kiburi na majivuno.

 Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

iii. MAWASILIANO WAZI: Katika vitu muhimu vya kufanya katika kufanya biashara/mradi kwa mafanikio ni namna timu inawasiliana kwa uwazi. Kila mtu anayefanya kazi katika timu hujihisi ana umuhimu pale anapokuwa na taarifa kamili kuhusu mambo yote yanayoendelea ndani ya timu yake na pale anapoweza kuwasiliana na yeyote ndani ya timu na kujuzwa mambo kwa uwazi. Unapokuwa na jukumu la kuhudumu ndani ya timu ni muhimu kuwa straight-forward kwa kuwa biashara/kampuni yako ni taswira yako mwenyewe kama Kiongozi. Hivyo, unapokuwa muwazi katika mawasiliano pamoja na kuzingatia maadili ya kiweledi (ethical behaviors) katika utendaji wa shughuli za kila siku, timu nzima unayoiongoza itafuata taswira hio.

iv. KUWA MSIKIVU: Kama Kiongozi ni jukumu lako kusikikiza kwa umakini mara zote mwingine anapozungumza iwe katika timu ama mteja. Usikivu humpa mzungumzaji nafasi ya kusema kile anadhani kinafaa katika kuboresha shughuli za kibiashara/kimradi ambazo ni muhimu sana katika ukuaji wa kampuni/biashara. Usikivu humfanya mzungumzaji kuungana moja kwa moja na wewe kama kiongozi katika kuimarisha mradi/biashara.

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

Usikivu pia huimarisha Mvuto (impression) wako katika macho na akili za watu ulionao katika mazungumzo. Tafiti zinaonyesha mzungumzaji husema kile kilichopo moyoni mwake kuhusu vile anataka kuhudumiwa au kutoa wazo la kuimarisha biashara pale anaposikilizwa kwa umakini.

v. KUWA NA MTAZAMO CHANYA: Katika kufanya shughuli za kila siku za mradi/biashara, changamoto hazikosekani. Iwe ni changamoto ndogo au kubwa, kama Kiongozi jinsi unavyoshughulika na mazingira hasi katika mradi/biashara yako hutafsiri mengi kuhusu maarifa ya kiuongozi uliyonayo. Robert Mann (mwandishi ya kitabu The Measure of a Leader) ananukuliwa “Look at three positive things about a problem before you identify what makes it dissatisfying. The more you look at the positives in a problem, the more positive people react with one another.”

Katika utafiti wake bwana Mann aligundua kuwa baada ya watu kuona mambo mazuri katika mazingira yenye changamoto, hufikiria namna ya kukabiliana na changamoto hio ili kufikia lile jambo lenye faida. Sawa sawa na vile jinsi Kiongozi anavyotaka kuimarisha mbinu za kiutendaji.

vi. FAHAMU BIASHARA/MRADI WAKO: Njia bora ya kufahamu kitu unachokifanya ni kwa kutumia uchambuzi wa SWOT ambao unakusaidia kufahamu Strength (nguvu/faida ya biashara), Weaknesses(Udhaifu wa mradi/biashara), Opportunities (fursa zinazokuja na biashara hio) pamoja na Threats(matishio yanayoikabili biashara). Kwenye kufanya uchambuzi huu zingatia haya;

STRENGTH (Nguvu/Faida ya biashara/mradi wako): Unaweza kuboresha jambo gani zaidi ya washindani wako? Uongeze malighafi/huduma gani ambazo washindani wako bado hawana? Mteja wako anafuraha?

•WEAKNESSES(Madhaifu ya mradi/biashara): Ni malighafi/huduma gani ambazo washindani wako wanazo ila wewe bado huna? Ni kipi unahitaji kuimarisha katika mradi/biashara yako? Una uzoefu wa kutosha kushindana na wafanyabiashara wengine? Unafanyaje baada ya hapo?

OPPORTUNITIES (Fursa): Unaona fursa gani katika mradi/biashara yako? Sheria za nchi, unaweza vipi kuzitumia vizuri katika kuimarisha mradi/biashara yako? Nje ya biashara/mradi wako kuna jambo/trend gani maarufu linaendelea? Unaweza vipi kulitumia jambo hilo kwa faida yako?

Je, kuna matamasha, matukio ya kijamii katika kalenda yako hivi karibuni? Unaweza vipi kuyatumia matukio hayo kwa faida ya biashara/mradi wako?

•THREATS (Matishio yanayoweza kuikumba biashara/mradi wako): Una changamoto za kifedha? Biashara/mradi wako utajiendesha vipi? Je vyanzo vyako vya kifedha ni vya kuaminika na kutegemeka (reliability)? Biashara/mradi wako unaweza kuhimili maendeleo ya kiteknolojia yanayozidi kushika kasi duniani? Kuna mambo gani binafsi yanayoweza kuathiri biashara/mradi wako? Katika timu yako, kuna mtu anapitia wakati mgumu katika kukabiliana na mambo binafsi kama msiba, ugonjwa au harusi?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza wewe kama kiongozi pamoja na timu yako ili uweze kuifahamu biashara yako na mazingira inayopitia ili kutengeneza njia nzuri zaidi ya kufanikiwa.

MTAWALA ANAATHIRI VIPI BIASHARA/MRADI?

Mazingira ya biashara/mradi ni sehemu inayohitaji mahusiano mazuri zaidi ili kuhakikisha biashara inakuwa na kudumu kwa miaka mingi zaidi. Lakini unapoingiza Utawala unaingiza ile hali ya kuhitaji zaidi na kuweka mbele matakwa binafsi.

•Mtawala anatoa amri na maagizo pasi na kuangalia hali ya utendaji ya timu yake.

•Si mara zote mtawala anakuwa muwazi kwa timu yake. Jambo linalohatarisha utendaji bora wa timu.

•Kiburi na majivuno humfanya kiongozi bora kuwa mtawala dhalimu ambaye hahitajiki katika biashara.

Hizo ni baadhi ya athari za Uongozi na Utawala katika maendeleo ya Biashara/Miradi. Je unadhani kati ya Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi? Makala zifuatazo katika link ni muendelezo mzuri wa somo ulilolipata katika makala hii ya leo. TUJADILI..

  1. FANYA MAAMUZI SAHIHI KATIKA MUDA SAHIHI
  2. UKWELI KUHUSU PROPAGANDA
  3. KWANINI UITANGAZE BIASHARA YAKO?
Branding vs Marketing. Kipi ni kipi?

BRANDING Vs MARKETING, KIPI NI KIPI?

Unapofanya biashara, moja kati ya malengo makubwa ni Kupata/kuendelea kupata wateja kila siku. Wateja ndio Roho ya biashara. Hakuna biashara kama hakuna wateja. Lakini unawapataje wateja hao? Unatumia vipi mbinu za Marketing na Branding? Branding vs Marketing, Kipi ni kipi?

Unapokuwa unaitengeneza biashara yako unatumia mbinu nyingi sana kujitangaza na kuvuta wateja wengi kwa kadiri inavyowezekana. Kuna wanaotumia ndugu, jamaa wa karibu, classmates, colleagues n.k. Ili mradi tu connections zinahusika kwa ukubwa wake. Kuna wengine wanatumia mitandao ya kijamii, kuna wanaofanya company visits na wengine wanatumia mbinu ya Umachinga (Kutembeza Barabarani). Lakini wote hao wanatumia Mbinu mbili tu kimsingi. Ni Either Marketing au Branding.

MARKETING na BRANDING ni nini?

Marketing ni mjumuisho wa vitendea kazi, utaratibu na mbinu za kuhakikisha bidhaa/huduma zako zinapigiwa debe ipasavyo ili ziuzike. Marketing ni mbinu ya kumfanya mteja anunue bidhaa/huduma zako. Ndo kupiga debe kwenye huko. Upande wa pili, Branding ni ile namna unajiweka/unaiweka biashara yako ili iweze kupokea wateja zaidi.

unawezaje kupata wateja mtandaoni unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako?

Branding Vs Marketing. Kipi ni kipi?

Ule unauweka utambulisho wa biashara yako, unavyofanyia kazi Dira, Malengo na Mipango yako na vile vitu vinavyokufanya wewe kuwa tofauti na washindani wako kibiashara. Hio ndio BRAND yako. Kama Marketing ni sumaku ya kuvuta wateja, basi Branding ni sukari ya kuwafanya waendelee kuwepo.

KIPI KINAANZA – BRANDING au MARKETING?

Fahamu, Branding ipo kwenye ule msingi kabisa wa Mbinu zako za kimasoko (marketing strategy), hivyo Branding lazima itangulie. Ukiitengeneza vizuri Brand yako hata kama ni changa, swala la Marketing linakuwa rahisi maradufu. Brand yako unayoitengeneza ndio itawafanya wateja waendelee kukujia na kuongezeka kwa mabalozi wa kujitolea wa bidhaa/huduma zako, ambao ndio wateja wenyewe haohao. Hii inaitwa “Customer’s Loyalty” (nimekosa kiswahili chake). Mfano, tizama Pepsi, pengine ndio soda inayouzika na kunyweka zaidi duniani kwa sasa, nikikuuliza umekunywa pepsi ngapi tangu mwaka huu umeanza pasi na shaka huna jibu, yaani umekunywa nyingi zisizo na idadi. Sasa hio ni kwa kuwa watengenezaji wa soda hio walitengeneza tabia zinazokufanya uendelee kuitumia miaka na miaka. Tabia hizo ni pamoja na Usafi wa chupa, Ubora, ladha n.k.

Pata huduma za Website, SEO, Social Media Marketing na nyinginezo nyingi kutoka Rednet Technologies

Branding vs Marketing. Kipi ni kipi?

Katika biashara za namna bora zaidi ya kuji-Brand ni kutumia mitandao ya kijamii. Sasa unatumiaje mitandao ya kijamii kwa manufaa ya biashara yako? Branding vs Marketing, Kipi ni kipi? Tafadhali songa na makala hii kwenye link IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA

Hivyo linapokuja swala la marketing, ni rahisi zaidi kuipromote Pepsi ikauzika kuliko Fanta passion. Branding ni ile kutengeneza utamaduni, mhenga mmoja alishasema, “Culture eats strategy for breakfast”. Yaani hata uwe na mbinu gani, kama hujazifanya mbinu zako kuwa utamaduni unaoishi, hapo andika maumivu. Ndio maana wanamichezo makini hufanya mazoezi kama utamaduni wao wa kila siku, na ndio hao ambao wanafanikiwa zaidi. Branding vs Marketing, Kipi ni kipi?

Branding vs Marketing, Kipi ni kipi? Tofauti ni ipi?

1. Marketing ni ile mbinu ya kutengeneza mhemko(attention) kwa wateja, Branding ni namna ya kuwafanya wateja waendelee kuwa wateja wako.

2. Marketing ni mbinu ya kufanya mauzo, Branding ni namna ya kutengeneza Jina, Heshima na Ushawishi kwa wateja.

3. Branding ndio inayoanza kuonekana katika biashara yako, Marketing inafuata.

4. Mbinu za kufanya Marketing hubadilika kulingana na wakati na mahitaji, lakini Branding ni Mbinu ya kutengeneza Utamaduni wa kudumu kizazi na kizazi.

5. Branding inahusika sana katika kufanya shughuli za kila siku za ndani ya biashara/kampuni yako, na vile wateja wanaziishi huduma/bidhaa kutoka kwako. Ndio utamaduni wenyewe.

Kwa chochote unachokifanya, fahamu biashara yako ni moja kati ya biashara nyingi duniani ndani ya bahari ya Ushindani wa kimasoko. Unahitaji mbinu bora katika kutengeneza Brand (Recognition) yako pamoja na Marketing (sales) za kila siku.

Kwa maneno mengine mbinu hizi hujieleza kupitia Dira (Vision) na Malengo (Missions) ya biashara yako. Leo nataka useme hapa Vision na Missions ambazo umejiwekea katika biashara yako ni zipi? Ukiweza kuzieleza na kuzisimamia vizuri basi, basi Utakuwa unaiweka pazuri bishara yako. Mfano, Rednet Technologies ilianzishwa ikiwa na Dira(vision) ya “Kuhakikisha Wafanyabishara wadogo na wakati (SME’s) wote nchini Tanzania na Afrika Mashariki wanatumia Teknolojia za kisasa katika utendaji wa biashara zao za kila siku.”

Mipango(Missions) ipo mingi lakini baadhi ni:

i. Kutengeneza websites bora kwa matumizi ya biashara mbalimbali kama ecommerce, corporate, funding na normal profile.

ii. Kutengeneza mifumo ya kuhifandhi na kuendesha mauzo na rekodi mbalimbali za kibiashara.

iii. Kuhakikisha wafanyabiashara wanapata taarifa muhimu kuhusu mbinu, takwimu na habari za Uchumi na mabadiliko ya kibiashara haswa kupitia Mapinduzi ya Viwanda yanayochochewa na mabadiliko ya kiteknolojia yanayotokea duniani kila uchwao. Taarifa hizo unaweza kuzipata kupitia tovuti yetu maridhawa ya https://rednet.co.tz Kupitia Vision na Missions hizo ulizoziona, Niambie ni rahisi kiasi kubuni mbinu ya kufanya Marketing? Je unaweza kuanzisha Marketing strategy gani kwa wakati huu unaosoma makala hii? Majibu yote unayo wewe mwenyewe.

Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko la Mtandaoni.

Branding vs Marketing. Kipi ni kipi?

Sasa makala hizi hapa chini zitakupa muendelezo mzuri kuhusu somo ulilolipata leo. Zitakusaidia sana kama ukizisoma zote. Gusa link kisha makinika:

  1. KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE RASMI YA BIASHARA YAKO
  2. UKIRITIMBA KATIKA BIASHARA, NI ASALI AU SHUBIRI?
  3. IFAHAMU TEKNOLOJIA YA QR CODE KATIKA BIASHARA YAKO

Tueleze leo vision ya biashara yako ili tujue utamaduni wako ni upi, watu tuanze kuufuatisha. Hakikisha unasambaza makala hii kwa watu wengi kuhakikisha Biashara zinashamiri na unazidi kupata wateja wapya kupitia hapa. Tuanze.

FANYA MAAMUZI SAHIHI KATIKA MUDA SAHIHI

Hebu piga hii hesabu hapo chap. Kwa mwezi unaingiza kiasi gani kama faida kutoka kwenye biashara yako? Tuseme 500,000/-. Na matamanio yako ni kuingiza kiasi gani kila mwezi? Jiambie hapo “Nataka niwe naingiza kiasi flani kila mwezi.” Tuseme 2,000,000/- kwa kukadiria.

Sasa kwa kuzingatia mfano huo hapo juu, ukweli ni kwamba kila mwezi unavyoshindwa kufikia matamanio yako unagharamika kiasi cha shilingi milioni 1.5 kwa kutofanya maamuzi sahihi kwa wakati na kuimarisha biashara yako.

MAAMUZI SAHIHI NI YAPI?

Wahenga walishasema “Kupanga ni kuchagua.” Lakini zaidi unapochelewa kuchukua uamuzi sahihi, fahamu kuwa unajiandaa kushindwa.

“Liwezekanalo leo lisingoje kesho” wanaongezea wahenga, Hii kwenye biashara ina maana kubwa sana, hasa kama wewe ni mtu makini unayetamani kuiona biashara yako ikikua na kuzidi kufanikiwa kila siku. Sasa leo ukimaliza kusoma makala hii utakuwa umepata mbinu sahihi za kukuza faida maradufu katika biashara yako. Hakikisha unazifanyia kazi mbinu hizi:

1. TAFUTA WATEJA WAPYA

Hii ni dhahiri kabisa. Lakini inatajwa kuwa ndio mbinu ngumu zaidi kuifanyia kazi. Kupata mteja mpya sio kazi ndogo. Wateja ndio moyo wa biashara yoyote ile. Tafiti zinaonyesha hugharimu mpaka mara 8 ya pesa kumpata mteja mpya zaidi ya kiasi kinachotumika kwa mteja aliyezeoleka/wa kudumu. Njia bora ya kupata wateja wapya ni kuhakikisha unajenga ukaribu na wateja wako wote hasa waliopo kwa kuwa Kizuri chajiuza chenyewe. Wengine wanaita Network Marketing, lakini watu wa mjini wanaita Connections. Hivyo, ukitaka kuongeza wateja hakikisha unakuza Connections zako.

2. BADILI MASHABIKI KUWA WATEJA

Hivi umeshawahi kuona huku kwenye mitandao (facebook, twitter, instagram nk) kuna mtu ana followers wengi 50k, 100k, 500k lakini bado anahangaika kupata wateja pindi akitangaza biashara yake fulani. Changamoto hii imekua ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na mambo kama kununua account za mitandao ya kijamii. Mfano wewe unauza viatu halafu kwa kuwa huna followers ukatafuta account yenye followers wengi uinunue ukidhani ndo itaboost biashara yako ya viatu. Lakini bahati mbaya account uliyokuja kununua ni ya mtu aliyekuwa anapost picha za nusu uchi au maudhui ya kilimo. Unafikiri utatoboa hapo? Ni ngumu kwa kuwa awali watu walifollow accounts hizo kutokana na muendelezo wa maudhui yake. So ukinunua account kwa kigezo cha kuongeza wigo wa biashara yako, hakikisha maudhui yaliyokuwepo kabla yanaendana na unachokifanya. Hapo kutoboa ni rahisi zaidi.

3. BADILI UTARATIBU WA UENDESHAJI

Unahitaji kuongeza mapato ya biashara yako huku ukipunguza gharama za uendeshaji kwa kadiri inavyowezekana. Ili kuongeza mauzo yako hakikisha unaongeza bidhaa/huduma za ziada zinazoendana na bidhaa/huduma kuu. Yani kwa mfano unauza chakula, tengeneza na juisi/ongeza na matunda hapo. Kama unatoa huduma za kisheria basi ongeza na machapisho kuhusu sheria mbalimbali na madiliko yake mara kwa mara. Ongeza ujazo wa malighafi za biashara yako. Yani hakikisha mteja wako anakuganda kwa kuwa anafaidi zaidi ya pesa anayolipa kupata huduma/bidhaa zako. Fanyia kazi hii.

4. TANUA WIGO WA SOKO LAKO

Hapa utake usitake, Teknolojia ya ICT lazima ichukue nafasi yake. Njia bora zaidi za kisasa kuhakikisha unafikia soko kubwa zaidi duniani na kwa haraka ni kutumia Huduma za Kimtandao kama matumizi ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, instagram na LinkedIn na matumizi ya blogu na tovuti(website). Majukwaa haya ya kimtandao yamekuwa madhubuti katika kutengeneza soko kwa bidhaa/huduma mbalimbali dunia nzima. Kujua zaidi kuhusu umuhimu wa tovuti katika biashara unaweza kutembelea link hii https://rednet.co.tz/kwanini-ni-muhimu-kuwa-na-websitetovuti-rasmi-ya-biashara-yako/ yenye kichwa “KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?” . Katika kutanua wigo wako huu wa kimasoko unaweza kutengeneza magroup ya facebook au LinkedIn ili kuonyesha bidhaa/huduma zako mpya na umuhimu wake kwa wateja wako, podcasts, tutorials na demos. Pima njia ipi inakufaa na yenye gharam ndogo zaidi.

5. TIZAMA BEI ZAKO TENA

Ukichunguza utagundua kuwa mteja siku zote anataka kupata huduma/bidhaa bora kwa bei nafuu. Upande wako kama mfanyabiashara unataka kupata faida zaidi kwa kila bidhaa/huduma unayomfikishia mteja. Hivyo hapo lazima busara na ushawishi wa hali ya juu utumike ili kuhakikisha kila upande unanufaika. Huu mchezo hauhitaji hasira. Angalia sokoni kwa watu wanaofanya biashara kama unayofanya wewe, angalia bei zao, angalia huduma wanazotoa, rudi kwako sasa ili kujua utaongeza/kupunguza kitu gani ili uweze kuhimili ushindani wa soko. Ikiwezekana katika vipindi fulani katika mwaka (sabasaba, eid, nanenane, Pasaka, Christmass, Mwaka Mpya, Nyerere Day) weka punguzo la bei (discount) kwa wateja wako. Hakikisha unawaweka karibu muda wote yani. Hii itakupa nafasi kubwa ya kutengenezea biashara yako uaminifu na uthubutu wa kununua kwa mtu yeyote.

6. KUWA NA MUENDELEZO MZURI (CONSISTENCY)

Unaweza kufanya yote tuliyojadili tangu mwanzo, lakini unapokosa muendelezo hapo unajisumbua tu. Hii dunia imejaa ushindani na tambua hauko peke yako unayefanya biashara hio unayoifanya. Hivyo cha msingi ni kuhakikisha unasurvive sokoni. Ukikaa kimya, hakuna mtu atakujua, hutapata wateja wapya, hata wale waliopo wataanza kukutilia shaka. Tambua pia, gharama za uendeshaji(umeme, maji, mafuta nk) huwa hazipungui kirahisi, lakini mapato ya biashara yanategemea juhudi yako ya kuuza. Usipouza huli. Zingatia hili.

7. FANYA KAZI

Hata kwenye Biblia imeandikwa, “asiyefanya kazi na asile.” Yani hakikisha mambo haya yote tuliyojadili hapa unayaweka kwenye uhalisia. Yasiishie kwenye makaratsi tu, toka nje, kutana na watu, onyesha umuhimu wako na jiuze kibiashara kwa kadiri inavyowezekana.

Ukiona matukio kama NyamaChomaFestival au TOTBonanza, hakikisha unashiriki ili kujijenga kibiashara na kuimarisha Connections zako. Mimi binafsi hizi mambo hazinipitagi ndio maana leo najivunia kukutana na watu mbalimbali kama kaka Togolani Mavura, Debora Da Silva kutoka Amici Designs, Angelika Farhan, wataalam kutoka TOTTech na wengineo wengi na kujenga ukaribu nao katika nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi, Teknolojia na Uchumi. Kuna nguvu kubwa katika kujumuika. Hakikisha kila unapojumuika na watu mbalimbali unaitumia fursa hio kwa manufaa zaidi. Usiache nafasi hizo zikakupita hivi hivi.

Tayari tumekuwekea makala hizi hapa chini katika links ili kusudu zikusaidie kuelewa somo la leo kwa undani zaidi. Gusa link kisha makinika:

  1. https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA”
  2. https://rednet.co.tz/ifahamu-teknolojia-ya-qr-code-katika-biashara-yako/ yenye kichwa “IFAHAMU TEKNOLOJIA YA QR CODE KATIKA BIASHARA YAKO”
  3. https://rednet.co.tz/website-inasaidia-vipi-kuimarisha-biashara-yako/ yenye kichwa “WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?”

Unalo lolote la kutushirikisha? Tafadhali usisite kuwasiliana nasi muda wowote utakapohisi umekwama. Tupo hapa kukuhudumia. Karibu.

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi?

UNAFAHAMU NINI KUHUSU URASINISHAJI (HARMONIZATION) KATIKA BIASHARA

June 23 mwaka huu, Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kwa kauli moja ilipitisha muongozo wa kurasinisha shughuli za kibiashara baina ya nchi wanachama wake. Sasa unajiuliza, huo Urasinishaji ndo nini? Na una manufaa gani katika biashara yako?

Ushindani wa kimasoko ukiongezea, ukiongezea ongezeko la wimbi la wateja wa huduma za kidijtali, hali hii inaongeza changamoto kila leo katika mazingira ya kibiashara hususan barani Afrika ambapo wafanya biashara wengi bado hawatumii mwanya wa teknolojia katika shughuli zao za kiuchumi za kila siku.

Hata hivyo, bado wafanyabiashara wanaamini katika Ubunifu wa mbinu katika kukuza na kuimarisha biashara zao na kunasa wateja wengi zaidi. Hili litawezekana vipi katika mazingira ya kisasa ya Masoko Huru na matumizi makubwa ya kiteknolojia? Jibu mbadala ni Urasinishaji wa shughuli za kibiashara hasa kwa kupitia matumizi mazuri ya teknolojia za mawasiliano na habari.

URASINISHAJI NI NINI?

Ni utaratibu/mchakato wa kuoanisha/kuunganisha shughuli za kibiashara kisheria baina ya maeneo kadhaa/nchi/Jumuiya za maendeleo/Kampuni/Mashirika ili kutanua soko la wafanyabiashara, kuongeza wateja na kukuza uchumi wa washirika. Umenipata apo?

Sasa taratibu zote za kibiashara zinapokuwa sawia pamoja na utekelezaji mzuri wa sera za biashara na maendeleo, basi bila shaka biashara zitashamiri na kuongeza kasi ya kukuza uchumi imara na ongezeko la wateja wa huduma na bidhaa baina ya washirika. Urasinishaji ndio mbinu.

Ili kuweza kurasinisha biashara kwa mafanikio, leo tutajadili hatua 5 muhimu za Kuwezesha Zoezi la Urasinishaji katika Biashara yoyote (hata hio unayoifanya wewe). Hatua hizi huitwa pia Viwezeshaji vya Urasinishaji (Enablers towards Harmonization in Business). Twende nazo sasa.

1. UTAWALA BORA

Nikwambie tu, hakuna biashara ya kiungwana inayoweza kufanyika katikati ya vita na machafuko. Biashara inahitaji mazingira salama ya kufanyika. Biashara ni kama mtoto mdogo, inahitaji malezi bora ili iweze kukua, kushamiri na kurudisha faida mara dufu. Hivyo jukumu la kutunza na kudumisha mazingira ya amani na utulivu ni la kila mmoja, hasa mfanyabiashara, lazima uhakikishe eneo lako la biashara lina amani na ni salama kwa yeyote kufanya biashara na wewe. Serikali kama mlezi mkuu, husimamia amani na usalama wa nchi wakati wote kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama wA nchi kama polisi na jeshi.

2. KUONGEZA MAARIFA

Zoezi la kuoanisha shughuli za biashara mbalimbali linakwenda sambamba na kuongeza maarifa ya kufanya biashara hizo. Hivi wewe mfanyabiashara unaweza vipi kukuza mtandao wa biashara yako kabla hujaongeza maarifa kuhusu biashara yako na biashara zingine ambazo unahitaji kushirikiana nazo? Hakika, huwezi kufanya/kuendelea kufanya biashara pasi na kuwa na maarifa sahihi, utadumaa kibiashara au kuishia kufilisika tu. Maarifa ndio chakula cha biashara. Lazima uwe mjanja, usikubali kuwa hapo ulipo kila siku. Ongeza ujuzi biashara ikue io.

3. UHUSIANO NA WATU

Kama ulikua hujui, Biashara ni mahusiano na mahusiano ni watu. Na watu ndio hao unawaona kila siku na wengine huwaoni ila wapo. Jumuiya ya SADC pekee inakadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni 400. Watu wote hawa unawahusisha vipi kwenye biashara yako? una mpango gani wa kuongeza wigo wa watumiaji wa bidhaa/huduma zako? Kama unafanya biashara ambayo haiongezeki wateja, hivi unajua kuwa hio biashara inakwenda kufa muda si mrefu? Waswahili wanasema, “Ongea na watu uvae viatu.” Kalagabaho.

4. MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

Mwaka 2018 duniani yalianza mapinduzi ya 4 ya Viwanda ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusisha matumizi ya teknolojia ya kompyuta na intaneti katika nyanja mbalimbali ambazo hapo kabla hazikuwa zikitumia teknolojia hio. Matumizi ya smartphones katika kuchakata na kuhifadhi rekodi za kibiashara, matumizi yanayoshika kasi ya mitandao ya kijamii katika kutangaza na kufanya biashara, ujui wa vifaa janja vya kielektroniki (smart devices) pamoja na uanzishwaji wa Maeneo Huru ya kufanyia biashara, kwa mfano, barani Afrika mwaka 2018 ulianzishwa mchakato wa kuanzishwa kwa Eneo Huru la kufanyia Biashara (African Continental Free Trade Area) AfCFTA lenye lengo la kuruhusu nchi wanachama kufanya biashara kwa wepesi na haraka katika kukuza uchumi wao. Kufahamu zaidi kuhusu AfCFTA na faida zake katika mchakato mzima wa urasinishaji wa shughuli za kibiashara barani Afrika, tembelea makala kupitia link hii hapa https://rednet.co.tz/kuanzishwa-kwa-eneo-huru-la-biashara-barani-africa-afcta-kuna-manufaa-gani-kwako/ yenye kichwa “KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA, KUNA MANUFAA GANI KWAKO?”. Pitia hapo, kisha tuendelee..

Sasa katika njia zote hizi zilizotengenezwa katika msingi wa Kiteknolojia, jiulize, unatumiaje mianya hii iliyotengenezwa kwa ajili ya kukuza na kuimarisha biashara yako? Teknolojia ni uwanda mpana sana na unaweza kuutumia vyovyote vile kuendana na mahitaji ya biashara yako. Kwa taarifa ushauri wa jinsi ya kutumia teknolojia vyema, usisite kuwasiliana nasi sasa kwa kutembelea tovuti yetu maridhawa ya www.rednet.co.tz, tupigie simu au tutumie barua pepe.

5. VIPIMO NA UFUATILIAJI

Ili mambo yote tuliyoyaona yaweze kufanyika kwa usahihi, hakuna budi kila hatua ipimwe na kufuatiliwa vizuri ili kuhakikisha hatua zimefuatwa sawia katika kurasinisha biashara kwa manufaa ya wote. Waswahili wanasema “Biashara haina undugu” Na pia “Kwenye kazi ifanyike Kazi”. Hivyo kwa jinsi hii sheria zilizowekwa wakati wa kuanzishwa kwa urasinishaji lazima zifuatwe ili kuhakikisha kila mshirika wa Urasinishwaji huo anafaidika sawa sawa na juhudi zake.

BONUS POINT:

Urasimishwaji unaweza kufanyika na kuhusisha biashara yoyote. Mfano mfanyabiashara wa viungo vya chakula kama nyanya, karoti, hoho, Anaweza kuungana na mfanyabiashara wa chakula katika migahawa katika biashara zao halafu mambo yakawa safi kabisa. Pia mtunzi wa hadithi na riwaya anaweza kukaa chini na mbunifu wa mitindo ya nguo na fasheni na waongozaji wa filamu na hivyo kufanya kazi bora katika kiwanda cha filamu na maonyesho na watu wote tukasimama kwa heshima. Hata mfanyabiashara wa viatu na nguo akikaa vizuri na mtaalam wa kutengeneza tovuti za mauzo (ecommerce website) wanaweza kutengeneza e-commerce platform moja, kila mtu duniani akanunua viatu na nguo na jamaa wa IT akapata gawio lake safi kabisa.

Pia kuna hizi makala ambazo ukizisoma zote zitakupa mwanga zaidi kuhusu namna ya kuimarisha biashara kwa kushirikiana na wafanyabiashara na wadau wengine. Cha kufanya, gusa link kisha makinika:

  1. https://rednet.co.tz/biashara-yako-inaweza-vipi-kuwa-taasisi-imara/ yenye kichwa “BIASHARA YAKO INAWEZA VIPI KUWA TAASISI IMARA?”
  2. https://rednet.co.tz/fahamu-siri-ya-kufanikiwa-katika-kuwekeza/ yenye kichwa “FAHAMU SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA KUWEKEZA”
  3. https://rednet.co.tz/ukiritimba-katika-biashara-ni-asali-au-shubiri/ yenye kichwa “UKIRITIMBA KATIKA BIASHARA, NI ASALI AU SHUBIRI?”

Huo ndo Urasinishaji katika biashara kwa ufupi, moja kati ya mbinu makini sana katika kukuza biashara kwa kutumia biashara ingine. Wazungu wanaita B2B au Business To Business. Ila sisi tunaita Harmonization of Business kama tulivyoiona definition kule juu. Una lolote? Tafadhali maoni yako ni muhimu.

KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?

Hebu fikiria wewe ni mgeni mahali fulani, baada ya kushikwa na njaa unaelekezwa migahawa miwili, mmoja ukiutafuta mtandaoni unaweza kupata taarifa zake mwingine hauna taarifa yoyote mtandaoni. Uelekeo wako utakuwa upande gani? Leo sasa tutakwenda kufahamu kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako. Makinika mpaka mwisho wa makala hii.

Kuishi katika ulimwengu wa kidijitali, tovuti ni zana muhimu sana katika biashara na masoko ya kidijitali. Cha kushangaza inakadiriwa 35% – 50% ya biashara ndogondogo duniani hazina tovuti zao binafsi, jambo linalozinyima fursa ya kuweka taarifa zao kirahisi mtandaoni na kupata wateja wapya kirahisi.

Kuna wanaosema kuwa matumizi ya Tovuti yanamezwa na uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo pia watu wanaweza kuweka na kutangaza biashara zao humo. Ni kweli, aghalabu, kwa kutumia Mitandao ya kijamii hauna uhakika wa kumiliki taarifa na maudhui unayoweka humo muda wote. Watengenezaji ambao pia ni wamiliki wa Mitandao hio wanao uwezo wa kusimamisha/kufuta akaunti au maudhui yako muda wowote ikiwa biashara/maudhui yako yanakwenda kunyume na matakwa na masharti yao.

Vile vile Mitandao ya kijamii unayotumia inaweza kupungua umaarufu au kufilisika muda wowote usioutegemea mfano kuna mitandao ilikua maarufu sana zamani kama Hi5 lakini umaarufu wake kwa sasa umepungua au kupotea kabisa. Hivyo, uwezekano wa kudorora kwa biashara yako kunategemea pia umaarufu wa mtandao wa kijamii unaoutumia, jambo linalichangiwa sana na ujio wa mitandao mipya ya kijamii kama Instagram, Whatsapp na TikTok. Hii kwako unaionaje? Nitaeleza Tofauti katika matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Tovuti wakati Ujao.

Faida ni nyingi sana za matumizi ya website katika kuimarisha biashara yako kupitia ulimwengu wa Teknolojia. Tayari tumekuandalia makala maalum kupitia link hii hapa WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?.

Leo hii ntakwambia mambo 10 kuhusu umuhimu wa kuwa na tovuti katika biashara yako:

1. 93% YA MAAMUZI YA MTEJA KUHUSU MANUNUZI HUANZIA MITANDAONI:

Ili kuweza kupata wateja wapya, huna budi kuelewa watu huenda wapi kutafuta vitu kama suppliers, bidhaa na huduma mbalimbali kabla ya kufanya manunuzi. Injini za matafuto mtandaoni zimekuwa kimbilio namba moja huku GOOGLE Ikiziacha mbali Injini zingine kama Yahoo, Bing na Ask. Maana yake hii ni kwamba kama huna tovuti, jua mauzo yako ni 7% tu ya soko zima ambalo hujui kuwa unalo. Upo apo? Yani unapoteza 93% ya mauzo yako kila siku bila hata wewe mwenyewe kujua.

2. UWELEDI (PROFESSIONALISM)

Kama una malengo ya kuifanya biashara yako iwe kubwa duniani, halafu bado huna tovuti rasmi, jua kuna sehemu kubwa ya soko haitakupa kipaumbele watakapokuwa na uhitaji wa huduma/bidhaa ulizonazo. Kwa biashara zenye malengo makubwa kuwa na tovuti huwaweka kwenye nafasi za juu katika kupata tenda na wateja, na huonyesha Uweledi bora katika utendaji wa biashara kuanzia katika muonekano na utendaji wa tovuti. Inakadiriwa 80% ya watu duniani huonyesha kutokua na imani na Biashara ambazo hazina tovuti pale wanapotaka huduma/bidhaa fulani mtandaoni.

3. KUPATIKANA KWA URAHISI

Hebu fikira ila ahueni ya kupata kila unachokihitaji kwa urahisi, tena kupitia katika simu yako tu iliyo kiganjani kwako. Ndivyo ilivyo kwa tovuti ambayo inajieleza kwa kila kitu kama ilivyo tovuti maridhawa ya http://rednet.co.tz . Ile raha ya kupata taarifa, huduma au bidhaa kirahisi kupitia simu yako ya mkononi, hufanya wateja waongezeke maradufu na kusambaza sifa bora kwa uharaka sana katika jamii na katika mitandao ya kijamii hali kadhalika.

Hii huongezwa chumvi ya SEO (Search Engine Optimization) ambayo ni teknolojia iliyowekwa katika Injini za matafuto ya kimtandao inayowasiliana na tovuti yako na kuweka taarifa katika Injini hizo na hivyo kufanya taarifa za tovuti yako kuonekana haraka zaidi katika matafuto. Biashara imerahisishwa sana kupitia SEO kuliko kutumia Mitandao ya kijamii. Kama watu wanakwenda Google kutafuta taarifa, basi fahamu taarifa hizo hupelekwa hapo GOOGLE kwa kutumia teknolojia iitwayo S.E.O. Kufahamu zaidi kuhusu SEO gusa hapa chini

4. TANGAZO LA BURE MUDA WOTE

Tovuti yako inapokuwa hewani, maana yake biashara yako ipo wazi na inajitangaza muda wote na kufika sehemu zote duniani ambapo huduma ya internet inapatikana. Tangazo la bure kabisa hili. Kama tovuti yako ina ubora wa kuvutia zaidi katika muonekano, maudhui na utendaji, basi bila shaka biashara yako ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri sokoni na kupata wateja wengi kila siku. Jiulize hivi, unapofunga ofisi/biashara yako wakati wa jioni kila siku, wateja wapya wanaweza vipi kupata taarifa sahihi muda watakaohitaji?turudi kwenye mada yetu, kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako? Hii pia inawezeshwa sana na teknolojia ya S.E.O.

5. KUTENGENEZA MABALOZI (TESTIMONIALS)

Nafahamu wafanyabiashara wengi ambao hulazimika kuonyesha shuhuda/testimonials katika kurasa zao mara kwa mara ili kuendelea kupata wateja wapya zaidi, ni jambo jema kabisa. Kupitia tovuti yako, unaweza kuweka testimonials kwa idadi uitakayo bila kurudia rudia na katika mpangilio maalum na watu wakaweza kuona ushahidi utakaowaridhisha kuendelea kutumia huduma/bidhaa zako. Mara nyingi Mitandao ya kijamii huzuia kuoneka kwa biashara kwa urahisi kutokana na wimbi la watumiaji wenye maudhui tofauti tofauti katika ratiba ya saa (timeline) yako unayopitia katika mitandao hio, hivyo kusababisha usumbufu (distractions) katika biashara yako.

6. UAMINIFU (TRUST)

Hamna kitu muhimu katika uendeshaji wa biashara na kukuza mahusiano na mteja kama UAMINIFU. Ili kupata wateja wa kudumu katika sekta nyingi, kuwa na tovuti hai ni muhimu katika kudumisha mahusianao katika ya mfanyabiashara kwa muda wowte mteja atakaohitaji.

7. POSITIVE ROI

Ikiwa ni Return On Investment (ROI) au Rejesho baada ya Uwekezaji, unapoendesha biashara ambayo ina gharama zake kama umeme, kodi, maji, mafuta n.k, ukijiuliza utaweza vipi kurudisha gharama hizo upate faida? Njia moja nzuri ni matumizi ya tovuti bora yenye uwezo kunasa wateja wapya kwa njia ya mtandao muda wote (24/7) kirahisi kabisa.

8. THAMANI INAYODUMU

Uzuri/Faida moja muhimu kuhusu tovuti ni kwamba, unapoitengeneza una uhakika wa kuimiliki milele na kuifanyia marekebisho muda wowote itakapohitajika kufanya hivyo. Hivyo thamani ya biashara yako itaendelea kuwepo muda wote tovuti yako inapokuwa hewani.

9. HUDUMA BINAFSI YA MSAADA KWA WATEJA

Tovuti yako inapokuwa hewani 24/7 una uhakika na kutoa huduma bora kwa mteja mmoja mmoja kuhusu maulizo ya huduma/bidhaa ulizonazo, bei, ushauri nakadhalika. Hivyo kuimarisha mahusiano na ukaribu wako na wateja wako wakiwa popote duniani kwa urahisi kupitia miundombinu mbalimbali unayoweza kuiweka katika tovuti yako kama matumizi ya chatbots na barua pepe maalum za kibiashara (zenye jina/domain name ya tovuti yako).

10. MASIJALA (DATA CENTER) RAHISI YA MTANDAONI

Tovuti yako inaweza pia kuwa masijala rahisi kwa wafanyakazi, wateja na mtu yeyote anayehitaji kujua taarifa kuhusu huduma/bidhaa unazohusika nazo. Mfano mzuri ni tovuti yetu maridhawa ya http://rednet.co.tz ambayo zaidi tu. ya kwamba inatoa taarifa kuhusu huduma tunazohusika nazo za kutengenza websites, softwares, apps n.k, lakini pia tovuti inatoa taarifa muhimu mbalimbali kuhusu Biashara, Uchumi na Teknolojia. Taarifa hizi zimetengenzwa mahsusi kwa ajili ya kuimarisha Biashara za wateja wakiwa popote duniani. Pia taarifa hizo zinalenga kuhamasisha matumizi ya Teknolojia katika njanja mabimbali za kiuchumi haswa kwa wafanyabiashara waliopo kusini mwa jangwa la Sahara.

NOTE: Katika ulimwengu wa kisasa wa Dijitali, ili kutengeneza nafasi ya kupata wateja zaidi huna budi kuwa na Tovuti hai itakayobeba taarifa muhimu kama jina la biashara, anuani, mawasiliano na maudhui kuhusu huduma na bidhaa zako. Zaidi, weka pia matumizi ya SEO kuongeza kasi.

BONUS POINT: Tovuti yako unapoisajili, unashauriwa pia upate kirurushi cha barua pepe yenye jina/domain name sawa na tovuti yako. Mfano, tovuti yako inapatikana katika anwani ya www.mfano.com, hivyo barua pepe yako ya kiofisi unaweza kuchagua kuwa info@mfano.com au maulizo@mfano.com au jinalako@mfano.com. Kwa kutumia barua pepe zenye jina sawa na anwani ya tovuti yako, unajiweka katika nafasi nzuri ya kuimarisha biashara yako na kuongeza wateja wapya na kazi zenya manufaa haraka zaidi katika biashara/kampuni yako. Hii ni sababu muhimu sana unapojiuliza kwanini ni muhimu kuwa na website (tovuti) rasmi ya biashara yako. Website inakufanya unakuwa official kiukweli kweli.

Pia kuna makala hizi hapa ambazo zitakupa mwanga zaidi kuhusu namna bora za kuimarisha uchumi wa biashara yako kwa kutumia Teknolojia:

  1. UKIRITIMBA KATIKA BIASHARA, NI ASALI AU SHUBIRI?
  2. BRANDING vs MARKETING, KIPI NI KIPI?
  3. KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA (AfCFTA), KUNA MANUFAA GANI KWAKO?
  4. IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO.

Umejifunza nini kupitia makala hii ya kuhusu kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako? Tafadhali unaweza kuwasilisha maoni yako kupitia sanduku la maoni (comments box) lililo hapo chini au kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yanayopatikana katika Footer Bar chini kabisa ya ukurasa huu. Pia usisite kuwashirikisha wenzako makala haya kwa kushare link yetu ya https://rednet.co.tz mara zote. Karibu!

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

Kwanini uwe na website ya biashara yako?