10 ZA JE WAJUA?
Kama unajua ni kheri, sasa unapata nafasi ya kujua zaidi. Na kama ulikuwa hufahamu basi leo unapata nafasi ya kujua mambo mapya zaidi. Katika jukwaa letu la @ElimikaWikiendi . Sasa leo tuzione zile 10 za je wajua katika Teknolojia na Biashara.
1. Je, wajua kuwa tovuti ya kwanza kabisa kuundwa duniani bado ipo hewani? Hii hapa kwenye link http://info.cern.ch Tovuti hio imetengenezwa kwa kutumia lugha ya HTML na inaonyesha mistari michache tu.
chanzo: https://rednet.co.tz/unawezaje-kutumia-teknolojia-ya-intaneti-na-kompyuta-katika-biashara-yako/
2. Ile Teknolojia ya kuongeza uwezekano wa Taarifa kupatikana kwa urahisi na kiwango cha juu katika injini za mitafuto za mtandaoni (Search Engine Optimization, SEO) ilianzishwa mwaka 1991. Teknolojia hii ina umri mkubwa kuliko GOOGLE ilioanzishwa mwaka 1998.
3. Mtandao maarufu wa kutizama mubashara filamu na tamthilia wa NETFLIX ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1997 huko Carlifonia nchini Marekani. Mtandao huo una umri mkubwa kuliko YouTube ambayo ilianzishwa mwaka 2005. Tuambie, Netflix umeijua lini wewe?
4. Takriban 10% ya pato la Taifa kwa nchi za Kusini mwa Afrika huchangiwa kupitia huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi. Hii ni zaidi ya 7% ya GDP kutoka Asia na chini ya 2% ya GDP kutoka sehemu zingine dubiani.
chanzo: https://rednet.co.tz/teknolojia-ya-huduma-za-fedha-kwa-njia-ya-kielektroniki-fintech/
5. Kusafirisha gari kutoka Japan mpaka Abidjan nchini Ivory Coast (km 14,075) hugharimu $1500. Lakini kusafirisha gari hilihilo kutoka Abidjan hadi Addis Ababa(km 6626) inagharimu takriban $5000. Gharama hii ni ghali mara 3 zaidi ya ile ya kutoka Japan.
Pia kusafirisha gari ndogo kutoka Japan mpaka Dar es salaam (km 11,256) inagharimu $900 bila makato na kodi. Hata hivyo, kusafirisha gari hilo hilo kutoka bandari ya Dar es salaam mpaka jijini Lusaka (km 1937.3), Zambia inafikia $650 bila makato na kodi.
Kutokana na hali duni ya miundombinu, gharama za usafirishaji barani Afrika ni kati ya zile ghali zaidi duniani. Hii pia huletwa na viwango vikubwa vya forodha, tozo za ucheleweshaji, ajali pamoja na ukosekanaji wa fursa zingine.
chanzo: https://rednet.co.tz/usafirishaji-na-miundombinu-katika-ustawi-wa-biashara-afrika/
6. Kufikia Octoba 2018, duniani tovuti bilioni 1.9 zilikuwa zipo hewani (online). Pia kuliripotiwa kuwapo na machapisho mapya (posts) zaidi ya milioni 5 kila siku kutoka kwenye tovuti na blogu mbalimbali duniani. Fikiria leo hali iko vipi..
chanzo: https://rednet.co.tz/unawezaje-kutumia-teknolojia-ya-intaneti-na-kompyuta-katika-biashara-yako/
7. Kila siku kunaongezeka watumiaji wapya wa huduma za Intaneti takriban milioni moja duniani kote. Kwa wastani mtumiaji wa kawaida hutumia masaa 6:42 akiwa mtandaoni kwa siku. Kama wewe ni mjasiriamali bila shaka umeshaona fursa hapa.
8. Unalikumbuka shambulizi lililoitwa NOTPETYA? June 27, 2017 malwares hizo ziliathiri kutoka biashara ndogo za software nchini Ukraine mpaka kusambaa duniani kote. Hilo liliitwa “SHAMBULIZI LA KIMTANDAO HARIBIFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI”
9. June 23, 2020 Jumuiya ya SADC ilipitisha muongozo wa kurasinisha(to harmonize) shughuli za kibiashara baina ya nchi wanachama. Sasa mtu akisema watu waende Burundi kutafuta unafuu wa maisha, watu watatumia fursa hio wakaenda Zambia na kwinginepo ndani ya nchi wanachama wa SADC kufanya biashara na maisha yataendelea kama kawaida.
chanzo: https://rednet.co.tz/unafahamu-nini-kuhusu-urasinishaji-harmonization-katika-biashara/
10. Kufikia mwaka 2022, mwakani tu hapo, 10% ya watu duniani watakuwa wakivaa nguo zilizounganishwa na Intaneti. Imagine nguo yako ina lebo ambayo inaweza kutumika kama tiketi ya kuingia kweny muvi, mpirani au club. Baunsa anascan nguo tu mzigo unajipa.
BONUS: Serikali za duniani zitaanza kutoza kodi katika jukwaa la Blockchain kwa mara ya kwanza mwaka 2023. Sasa wale Traders na Investors wa Bitcoins na Cryptos kupitia Blockchain mjiandae kisaikolojia mkimalizia Tax-holiday yenu huko kwenye Blockchain.
Hayo ndio tuliyotaka kukujuza leo katika 10 za je wajua. Jambo lipi limekushangaza zaidi? Tujuze katika comments hapo chini kisha share makala hii kwa ndugu, rafiki na jamaa zako ili nao wapate kufahamu haya tulokujuza leo.
Je umependezwa na makala yetu hii ya leo?
Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?
Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.
Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.
