Tag: agenda za siri

focus on your plans and make sure you win.

UKWELI KUHUSU ‘PROPAGANDA’

Wengine watakwambia ni maneno ya uchochezi, wengine “siasa za uhuni hizo”, wengine wanaita figisu, mara fitna. Lakini Propaganda ni mada inayowasilishwa kwa lugha ya picha katika mawasiliano ambayo mara nyingi hubebwa katika kampeni mbalimbali kwa agenda fulani ya kificho. Leo sasa tuone huo ukweli kuhusu ‘Propaganda’. Ni upi? Makinika.

Serikali na mashirika mbalimbali hufanya Propaganda katika kusukuma Agenda zao ambazo zina lengo la kushawishi jamii na kuchochea mapokeo ya kihisa kuhusu jambo fulani. Propaganda zilizokomaa hugeuzwa kuwa utamaduni, mfano Propaganda ya kuagamiza maadui wa “Ujinga, Maradhi na Umasikini” imesababisha watu wengi kwenda shule kupata elimu, kutibiwa kwa tiba za kisasa na kuachana na zile za kizamani pamoja na kufanya kazi kwa lengo la kuboresha hali ya kiuchumi. Ujinga, Maradhi na Umasikini vimeonekana ni adui wa kumuangamiza kabisa mbele ya kila mwananchi sasa na hii imesababishwa na Propaganda za serikali ya awamu ya kwanza katika kufikia lengo hilo.

Kwa upande mwingine Propaganda zimekuwa zikitumika kufanyiana hila za kisiasa katika kumkandamiza mpinzani ili kupata ushindi katika kinyang’anyiro fulani. Mfano kwenye michezo unaweza kumwona @hajismanara ambaye ni mmoja kati ya wana propaganda wazuri sana nchini. Maneno yake, tambo na kampeni anazozifanya kwa kiasi kikubwa ziliisaidia sana @SimbaSCTanzania na Yanga Kupata ushindi hata kabla ya mechi. Propaganda zinapigwa kwa kiwango sana hapa.

Kwingine ni kwenye ulingo wa siasa ambapo huku ndo Propaganda zilipozaliwa (kama wanavyosema Mapenzi yamezaliwa Tanga). Kwenye siasa mara kadhaa Propaganda zimekuwa zikipigwa kukandamizana kisiasa na kuaminisha umma kuwa fulani ni bora zaidi kuliko fulani, na sera hii ni bora zaidi kuliko sera hii. Ili kuweza kujenga ushawishi kwa wapiga kura, wanasiasa wamekuwa wakipiga propaganda za hali ya juu ili kuhakikisha wanapata ushindi. Ukiona mwanasiasa fulani anapendwa sana na ana wafuasi wengi, basi kwa kiasi kikubwa tambua Propaganda zake ni za kiwango cha juu sana.

Hata hivyo kufanya Propaganda si Dhambi, wala hakuna mtu anakatazwa kuzifanya isipokuwa tu usivunje sheria za nchi. Kuna baadhi ya watu huamini kuwa Propaganda ni Maneno ya Uongo na Ulaghai, Hapana. Propaganda ni sanaa ya kushawishi watu wafuate dhana fulani ili kuleta faida kwa mtu au jamii ya watu fulani, kampuni, shirika au serikali.

MBINU ZIPI HUTUMIKA KUFANIKISHA PROPAGANDA?

Mafanikio ya kufanya propaganda huja pale serikali/biashara fulani inapotumia mbinu hizi katika kushawishi jamii kufikia lengo fulani ambalo halionekani wazi kwa mara moja.

i. NJIA YA USHIRIKA (BRANDWAGON): Hii wahenga wanakwambia “Ndege wafananao huruka pamoja” au “Ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi”. Njia hii ni ile ambayo mpigapropaganda kujihusanisha na walengwa kwa ukaribu katika kuhakikisha propaganda zake zinakuwa na ushawishi. Najua umeshawahi kuona namna wanasiasa au makampuni wanavyotumia watu wa kitengo cha Masoko katika kuwafikia walengwa wao. Mara nyingi mpigapropaganda hubadili mavazi kuendana na walengwa, wakati mwingine huongea lugha ile inayozungumzwa na walengwa kabisa ili kuhakikisha propaganda zake zinakuwa na ushawishi unaotakiwa.

Pata huduma za Website, SEO, Social Media Marketing na nyinginezo nyingi kutoka Rednet Technologies Branding vs Marketing. Kipi ni kipi?
ukweli kuhusu 'Propaganda'

ii.KUTAFUTA HURUMA YA JAMII (SNOP APPEAL): Hii ni njia maarufu sana ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikitumika katika kutengeneza story ambayo itagusa moyo wa jamii na kuhamasisha watu kukubali Agenda ambayo imebebwa katika propaganda hio. Inakuwa hivi, mtu hueleza story yake ambayo mara nyingi huwa ni ya kusikitisha, kwa lengo (linaloonekana) la kuhamashisha watu kutokata tamaa au kujenga uaminifu juu yao na hivyo kupata lengo (lisiloonekana) la kupata wafuasi, wateja au/na kura. Propaganda hii hufanywa sana na wasanii, wafanyabiashara na kampuni zinazoanza(startups). Umeshaanza kuuona hapa ukweli kuhusu ‘Propaganda’.

iii. MANENO YENYE UJAZO: Wahenga wanasema, “Maneno yanaumba”.Hii ni kwasababu maneno yana nguvu sana linapokuja swala la mahusiano ya kijamii. Ndio maana wanapropaganda hutumia maneneo yenye ujazo kubadili mtazamo wa jamii. Hapa wanapropaganda hutumia maneno matamu sana kushawishi jamii katika kufanya jambo fulani. Hali kadhalika wanapropaganda hutumia maneno ya hasira, chuki, fitna na hila ili kuhakikisha Agenda zao za siri zinafanikiwa. Wakati mwingine agenda hizo huwa na manufaa mema kijamii na wakati mwingine huja na lengo la kubomoa jamii.

Mathalani sisi Rednet Technologies tunakwambia, #WeGiveYouTheWorld hatuna maana kuwa tutakupa dunia kama ilivyo, hapana. Dhima yetu ni kuhakikisha tunakupatia taarifa zote muhimu kuhusu Biashara na Uchumi katika muktadha wa kiteknolojia ikiambatana na ushauri wa kitaalam.

Ili kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanaimarisha biashara zao kupitia Matumizi ya teknolojia za kisasa kama Websites bora, softwares na chambuzi zisizokauka za kitaalam kupitia tovuti yetu maridhawa ya https://rednet.co.tz. Tufuatilie uendelee kuimarisha biashara yako.

iv. KULINGANISHA DHANA: Wanapropaganda hutumia njia za kulinganisha dhana zao na matukio ya historia katika kupata kile wanachokidhamiria. Mathalani, katika siasa, watu wengi hupiga propaganda za kulinganisha hotuba za Mwalim Nyerere na matukio yanayoendelea katika kupush agenda zao.

Katika nyanja ya kibiashara, makampuni na mashirika hulinganisha maendeleo ya Kiteknolojia/Uchumi na uwezo wao wa kisasa katika kushawishi na kupata wateja wengi zaidi kila leo. Lakini chumvi ikizidi sana hapa, propaganda hizo hugeuka utapeli na kupoteza wateja kwa haraka sana.

v. NJIA YA SHUHUDA: Katika kufanya propaganda kwa njia hii makampuni na mashirika wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuongeza wateja wapya na kukuza mauzo kwa viwango vikubwa sana. Makampuni/Mashirika yamekuwa yakiwatumia wasanii na watu mashuhuri kwenye jamii katika kueneza propaganda zao kuhusu huduma wanazotoa, bidhaa, kufungua matawi mapya ya ofisi pamoja na kufungua kampeni zao mbalimbali. Mara nyingi wasanii/watu mashuhuri wanaotumiwa kueneza propaganda hizo hawana elimu/taaluma kuhusu jinsi bidhaa/huduma inayoenezwa ilivyobuniwa/ilivyotengenezwa. Wao kikubwa ni kuhakikisha huduma/bidhaa hio inauzwa na kuketa faida kwenye kampuni/shirika hilo. Hapa ndipo unadhihirika ule ukweli kuhusu ‘Propaganda’.

mteja mshirikishe kwenye maamuzi. Msaidie aweze kununua huduma au bidhaa yako.

ukweli kuhusu 'Propaganda'

Hata hivyo mbinu hio inaweza kutumiwa kwa kupitia Masoko ya kimtandao (Network Marketing) au/na masoko kwa njia ya mitandao ya kijamii (social media marketing) ambapo mtandao wa twitter, facebook na LinkedIn imekuwa ikiongoza kwa kuwafanya watu washirikishane bidhaa/huduma zao. Mathalan kupitia twita, unaweza kusambaza bidhaa/huduma zako kwa kupitia watu ambao hawana ujuzi wa kutengeneza hizo bidhaa/huduma zako. Mfano sisi @RednetCompany tunasambaza huduma zetu kupitia rafiki zetu katika mitandao ya kijamii Ambao hata hivyo wengi kati yao hawana ujuzi kuhusu jinsi ya kutengeneza website, computer maintenance n.k. Lakini Agenda inayobebwa katika propaganda hio ni kuhakikisha tunahudumia Wafanyabiashara na watu wengine wengi zaidi kila leo.

Hivyo ukiwa kama mfanyabiashara hakikisha propaganda zako unazifanya kwa utaalam na weledi bila kufanya ulaghai au kusema uongo ili kujipatia faida. Kwa maana hio si njia bora ya kufanikiwa kipropaganda. Jipange vema kwenye uwanja huu uliosheheni ushindani wa kila namna.

Vile vile tayari hapa tumekuandalia makala ambazo zinarandana na somo ulilojifunza leo. Gusa links hizi kufahamu zaidi:

  1. IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO
  2. UNAWEZA VIPI KUKABILIANA NA HASARA KATIKA BIASHARA YAKO MWAKA HUU 2021?
  3. FAHAMU SIRI YA KUWEZA KUSHAWISHI WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO
  4. UMUHIMU WA TAKWIMU KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Umejifunza nini katika makal hii ya leo kuhusiana na ukweli kuhusu ‘Propaganda’? Tafadhali toa maoni yako kupitia comments hapo chini, nasi tutayafanyia kazi mara moja.