Jihudumie Leo

mageuzi ya Intaneti (iot) katika biashara na maisha. Jihudumie leo kutoka Rednet Technologies. Kwanini mteja akuchague wewe?

Jihudumie leo mwenyewe kwa huduma bora za TEHAMA zile uzipendayo kutoka kwetu kwa sababu wakati wako ndio huu. Chagua huduma unayoitaka ukiwa popote duniani na sisi kama ilivyo ada tutakuhumia haraka kwa sababu unakurahisishia maisha.

Kupitia fomu hapo chini, jaza taarifa zako muhimu, chagua huduma unayohitaji kutoka kwetu, kisha wasilisha mahitaji yako kupitia kitufe kilicho andikwa REQUEST QOUTE.

Sehemu zenye alama (*) ni Lazima kujaza.

Kuhusu Website, aina za Website unazoweza kupata kutoka kwetu ni kama ifuatavyo:

 • Normal Business Website: Hii ni website ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya biashara/kampuni changa. Pia aina hii ya website inaweza kutumika kwa matumizi binafsi kama Personal Portfolio/Profile.
 • Corporate Website: Hii ni website maalum kwa ajili ya matumizi ya kampuni na mashirika ya kati na makubwa. Website ya aina hii hujumuisha kipengele cha Blog ambacho hutoa nafasi kwa taasisi kuwataarifu na kuwasaidia wateja wake katika mambo mbalimbali yanayowapa changamoto katika shughuli zao za kila siku.
 • Funding Website: Aina hii ya website ni makhususi kwa ajili ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ambapo website hii inaipa taasisi uwezo wa kukusanya michango na misaada kutoka wa wadau na wabia wake waliopo popote duniani. Pia website hii inakuwa na kipengele cha Blog ambapo taasisi inakuwa na uwezo wa kutoa taarifa zake kuhusu Miradi inayofanya, Changamoto wanazopita, Watu walio nufaika na miradi ya taasisi.
 • E-commerce website: Nyakati hizi za Kidigitali biashara zinahamia mtandaoni na namna BORA zaidi ya kuuza bidhaa zako ni kupitia ecommerce website ambayo inakupa nafasi ya kuuza bidhaa zako moja kwa moja kupitia website yako. Website hii inaruhusu mteja kuchagua bidhaa anayotaka kutoka kwenye website yako, kisha inampa nafasi ya kulipia bidhaa hio kwa njia za kielektroniki (M PESA. TIGO PESA, AIRTEL MONEY, BENKI n.k). Kazi inayobaki baada ya hapo ni kufanya delivery kwa kutumia taarifa ambazo mteja anakuwa tayari ameshaziweka wakati anafanya manunuzi. Ongeza thamani ya biashara yako kwa kumruhusu mteja kufanya shopping kirahisi mtandaoni kupitia website yako leo.

Zaidi kuhusu manufaa na faida za website katika biashara yako unaweza kufuatilia makala hizi hapa tulizokuandalia:

 1. https://rednet.co.tz/kwanini-ni-muhimu-kuwa-na-websitetovuti-rasmi-ya-biashara-yako/ yenye kichwa “KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE (TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?”
 2. https://rednet.co.tz/website-inasaidia-vipi-kuimarisha-biashara-yako/ yenye kichwa “WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?”

Huduma zingine unaweza kupata kutoka kwetu ni kuandaa nyaraka muhimu kama ifuatavyo:

 • Business Plan: Lengo kuu la kuandaa nyaraka hii ni kukupatia mpango kamili wa biashara yako ukijumuisha ripoti ya jumla inayoakisi kiasi cha mtaji unaotakiwa, vyanzo vya mapato, matumizi, namna ya kukabiliana na washindani wako katika biashara, sehemu za biashara yako zinazoongoza kuwa na udhaifu, nguvu yako ilipo pamoja na fursa unazoweza kuzitumia ili unufaike zaidi ndani ya muda fulani (miaka miwili, miaka mitatu, miaka mitano, kumi, n.k). Hii ni nyaraka muhimu sana kuwa nayo kwa sababu inakuongoza kufikia malengo ya kufanikiwa katika biashara. Kuipata jaza fomu kisha, chagua huduma iliyoandikwa OTHERS pale chini.
 • Company/Business Profile: Nyaraka hii inaeleza kwa kirefu kuhusu biashara/kampuni yako katika vipengele vya Jina la biashara/kampuni yako, aina ya bidhaa/huduma unazojihusisha nazo, anwani na mawasiliano yako. Tofauti na business card, ukiwa unatembea na nyaraka hii na kupatia mtu unayekutana nae ni rahisi zaidi mtu huyo kukutafuta na kufanya biashara nawe kwa sababu tayari ameshasoma na kujua kwa undani kuhusu biashara/kampuni yako.
 • Research/Report writing: Kuna muda unaweza kuwa na kazi nyingi huku ukiwa unakimbizana na DEADLINE. Sasa ili kuokoa muda wako, fanya kazi nasi katika kuandaa ripoti mbalimbali na researches za chuo au taasisi fulani. Usihofu tena kuhusu swala la Deadlines na mrundikano wa kazi zinazo kungoja kwenye dawati lako.

Pia unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii kupitia links zifuatazo:

 1. twitter: https://twitter.com/RednetCompany
 2. Linkedin: https://www.linkedin.com/in/faustine-kimath-a53572b2/
 3. Instagram: https://www.instagram.com/kimath47/

Kifuatacho, Jihudumie leo huduma bora za tehama kutoka kwetu. Lengo letu ni kukupa fursa ya kujichagulia huduma inayokufaa, kisha tunakuhudumia. Rahisi hivyo yani..

JAZA FOMU HII ILI UJIHUDUMIE LEO HUDUMA UNAYOIHITAJI:


NJIA YA KUFANYA MALIPO BAADA YA KUJIHUDUMIA:

Kwanini uwe na website ya biashara yako? Jihudumia leo sasa..
One thought on “Jihudumie Leo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *