MAGEUZI YA INTANETI (IoT) KATIKA BIASHARA NA MAISHA

Jun 8, 2021 Technology Updates
cloud data storage

Teknolojia ya Internet of Things (IoT) inakuja kwa kasi sana. Mtandao wa Gartner uliripoti kuongezeka kwa vifaa vinavyounganishwa na huduma za internet kufikia 26 bilioni mpaka mwaka 2020. Sasa haya mageuzi ya intaneti (IoT) katika biashara na maisha ya mchango gani? Fuatana na makala hii mpaka mwisho kuahamu zaidi.

Leo hii utakapomaliza kusoma makala hii utafahamu kiundani juu ya namna Teknolojia ya Intaneti katika Vitu (Internet of Things au IoT) inavyoweza kubadili Biashara yako pamoja na vifaa vya kielekroniki unavyotumia nyumbani ama ofisini.

Maeneo kumi (10) muhimu ambapo mageuzi ya intaneti (IoT) katika biashara na maisha, inakwenda kuyagusa na kuleta mabadiliko makubwa katika mazingira ya kazi na jamii. Namba 7 itakushangaza sana:

1. IoT itapofika kwenye ubora wake wa matumizi, biashara nyingi zinazofanyika leo zitapotea sokoni. Mf: biashara za ugavi na usambazaji ambazo kwa sasa hutumia mtu wa tatu katika kufanya usafirishaji/usambazaji, hizi zitaweza kujiendesha kiautomatiki, yaani ukiagiza kitu mtandaoni inakupa namna ya kukufikishia bidhaa/huduma popote bila hata kujieleza. Fikiria upo Magomeni na unaagiza mafuta mtandaoni kutoka Singida, unapotoa oda yako tu, huna haja ya kusema uko wapi, unapokea zako tu ujumbe kuwa “mafuta yako yatakufikia siku fulani saa fulani mahali fulani (Mahali ambapo unakuaga muda mwingi). Life’s Simple.

mageuzi ya Intaneti (iot) katika biashara na maisha.

Jihudumie leo kutoka Rednet Technologies.

2. Moja kati ya athari hasi za IoT ni pamoja na kumlazimu mtumiaji kuhakikisha vifaa vyake vinavyotumia intaneti na vilivyoungwa katika teknolojia ya IoT vinakuwa updated muda wote. Hii itaongeza gharama za bando japokuwa “Mtaka cha uvunguni sharti ainame.”

3. Mpaka kufikia 2025 soko la IoT linatarajiwa kuwa na thamani ya kati ya 3.9 $ mpaka 11.1$ trilioni kwa mwaka. Vihisishi (Sensors, RFID na Bluetooth devices) vinatajwa kuchukua zaidi ya 50% ya matumizi ya IoT vikifuatiwa na huduma za Teknolojia ya Habari (IT). hapa ndipo utakapoona sasa mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha kwa ujumla.

4. Soko la Biashara Kwa Biashara (B2B IoT Market size): 2015: soko lilikuwa na thamani ya $195 bilioni na kufikia mwaka 2020 soko lilifikia thamani ya $470 bilioni ikiwa ni ongezeko la zaidi ya dola bilioni 250 ndani ya miaka mitano tu. Yaani IoT imeimarisha sana mapato katika biashara katika nyanja za mifumo ya udhibiti, uchambuzi wa data, vifaa, network na huduma bora. IoT imekuwa mkombozi haswa.

Mfano mzuri hapa ni mifumo ya ukusanyaji kodi ya TRA. Mifumo hio imefanywa imara katika kudhibiti makusanyo ya kodi kupitia mashine za EFD ambazo zimeungwa kielektroniki ili kuwapa TRA data sahihi za kodi.

mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha.

5. Ukuaji wa IoT unaathiriwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya Teknolojia zingine. Mfano: Teknolojia ya mawingu (cloud tech) inavyokuwa na IoT nayo inakuwa sambamba. Pia IoT inasambaa kwa kasi pale uwezo wa mitandao unaposambaa zaidi. Kifupi ni ngumu kuzuia kasi ukuaji wa IoT duniani.

6. IoT itapofikia ubora wake kwenye matumizi, inatarajiwa kuwezesha kufikia vifaa vingi kwa kutumia kifaa kimoja. Fikiria unarudi zako home, ukifika nje unawasha taa za nyumba, then unawasha feni, TV na sabufa yako na kuzima Friji yote kwa kutumia simujanja yako tu yani.

7. Unazijua RFID’s? Hizi kitaalamu zinaitwa Radio-Frequency Identifications. Yani vifaa vyenye uwezo wa kuratibu utambulisho wa bidhaa/huduma. Mfano vile vitochi unaviona ukienda supamaketi pale kabla hujalipia, bidhaa yako inamulikwa na mwanga flani hivi ili kujua bei. Sasa kile kitochi kinaitwa RFID scanner. Hizi skana zipo za aina nyingi kwa minajili ya kutambua bidhaa/mtu, zingine zipo viwanja vya ndege kukagua mizigo, watu na pasi za kusafiri.

RFID’s zinahusika vipi kwenye IoT?

Teknolojia ya IoT sasa inaziwezesha hizi RFID’s katika sekta ya Ugavi na Usafirishaji ili kutoa data sahihi kuhusu ubora na idadi ya bidhaa zinazosafirishwa na kutumiwa. Kupitia IoT bidhaa inaweza kujulikana ipo wapi na lini imenunuliwa inapopita kwenye skana ambayo hutuma taarifa sahihi za bidhaa kwa mtengenezaji. Kufahamu zaidi kuhusu mchango wa RFID’s katika nyanja ya Biashara na Uchukuzi tafadhali gusa link hii MAPINDUZI YA KITEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI

8. Namba ya Vifaa vya kielektroniki vinavyoweza kuwasiliana pasi na kuingiliwa na mtu M2M (Machine To Machine) inatajwa kuongezeka kwa kasi kubwa ndani ya muda mchache tu. 2018 kulikua na vifaa 1.5 bilioni na mwaka 2020 viliongezeka kufikia 2.6 bilioni. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Statista.

9. IoT ndio suluhisho sahihi katika kutoa huduma bora zaidi kwa mteja. Yani unapotumia teknolojia ya IoT katika biashara yako, unampa mteja nafasi ya kupata huduma nyingi (mfano: kununua bidhaa/huduma, kujisafirishia na kutoa maoni) ndani ya site moja kirahisi.

10. Kuongeza Mapato: Kwa kutumia IoT matumizi katika biashara yanapungua sana kwa kuwa shughuli nyingi zinafanyika kiautomatiki kupitia mawasiliano baina ya vifaa vinavyotumia huduma za intaneti. Hakuna tena gharama kubwa za usafiri wala kukusanya data. Kifupi, yajayo yanafurahisha sana katika IoT. Makampuni mengi duniani tayari wameshanza kutumia huduma hizi yakiongozwa na makampuni ya Ugavi na Usafirishaji kama DHL, XPO Logistics na FedEx.

Biashara zinazotumia IoT hujikuta zikitumia gharama ndogo na thamani kubwa sana katika kujiendesha, jambo linalowafanya waweze kujitanua zaidi na kupata mapato lukuki. IoT ndio teknolijia ya kibiashara haswa na wajanja ndio wanaoifaidi. Usisubiri uachwe.

Kuna msemo mmoja maarufu katika IoT unasema, “If an electronic device can be connected, it should get connected” yaani, “Kama kifaa kinaweza kuunganishwa, basi na kiunganishwe”. Msemo huu ndio kwa kiasi kikubwa unaipa nguvu kasi ya IoT kuenea duniani. Umegundua nini kwenye makala hii kuhusu mageuzi ya intaneti (iot) katika biashara na maisha? Tuambie kwenye comment hapo chini,..

Vyanzo: https://www.statista.com/statistics/1194677/iot-connected-devices-regionally/

https://www.huffpost.com/entry/8-ways-the-internet-of-th_b_11763836

https://www.newgenapps.com/blog/impact-of-internet-of-things-on-the-business-world/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *