KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?

Jun 25, 2020 Technology Updates

Hebu fikiria wewe ni mgeni mahali fulani, baada ya kushikwa na njaa unaelekezwa migahawa miwili, mmoja ukiutafuta mtandaoni unaweza kupata taarifa zake mwingine hauna taarifa yoyote mtandaoni. Uelekeo wako utakuwa upande gani? Leo sasa tutakwenda kufahamu kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako. Makinika mpaka mwisho wa makala hii.

Kuishi katika ulimwengu wa kidijitali, tovuti ni zana muhimu sana katika biashara na masoko ya kidijitali. Cha kushangaza inakadiriwa 35% – 50% ya biashara ndogondogo duniani hazina tovuti zao binafsi, jambo linalozinyima fursa ya kuweka taarifa zao kirahisi mtandaoni na kupata wateja wapya kirahisi.

Kuna wanaosema kuwa matumizi ya Tovuti yanamezwa na uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo pia watu wanaweza kuweka na kutangaza biashara zao humo. Ni kweli, aghalabu, kwa kutumia Mitandao ya kijamii hauna uhakika wa kumiliki taarifa na maudhui unayoweka humo muda wote. Watengenezaji ambao pia ni wamiliki wa Mitandao hio wanao uwezo wa kusimamisha/kufuta akaunti au maudhui yako muda wowote ikiwa biashara/maudhui yako yanakwenda kunyume na matakwa na masharti yao.

Vile vile Mitandao ya kijamii unayotumia inaweza kupungua umaarufu au kufilisika muda wowote usioutegemea mfano kuna mitandao ilikua maarufu sana zamani kama Hi5 lakini umaarufu wake kwa sasa umepungua au kupotea kabisa. Hivyo, uwezekano wa kudorora kwa biashara yako kunategemea pia umaarufu wa mtandao wa kijamii unaoutumia, jambo linalichangiwa sana na ujio wa mitandao mipya ya kijamii kama Instagram, Whatsapp na TikTok. Hii kwako unaionaje? Nitaeleza Tofauti katika matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Tovuti wakati Ujao.

Faida ni nyingi sana za matumizi ya website katika kuimarisha biashara yako kupitia ulimwengu wa Teknolojia. Tayari tumekuandalia makala maalum kupitia link hii hapa WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?.

Leo hii ntakwambia mambo 10 kuhusu umuhimu wa kuwa na tovuti katika biashara yako:

1. 93% YA MAAMUZI YA MTEJA KUHUSU MANUNUZI HUANZIA MITANDAONI:

Ili kuweza kupata wateja wapya, huna budi kuelewa watu huenda wapi kutafuta vitu kama suppliers, bidhaa na huduma mbalimbali kabla ya kufanya manunuzi. Injini za matafuto mtandaoni zimekuwa kimbilio namba moja huku GOOGLE Ikiziacha mbali Injini zingine kama Yahoo, Bing na Ask. Maana yake hii ni kwamba kama huna tovuti, jua mauzo yako ni 7% tu ya soko zima ambalo hujui kuwa unalo. Upo apo? Yani unapoteza 93% ya mauzo yako kila siku bila hata wewe mwenyewe kujua.

2. UWELEDI (PROFESSIONALISM)

Kama una malengo ya kuifanya biashara yako iwe kubwa duniani, halafu bado huna tovuti rasmi, jua kuna sehemu kubwa ya soko haitakupa kipaumbele watakapokuwa na uhitaji wa huduma/bidhaa ulizonazo. Kwa biashara zenye malengo makubwa kuwa na tovuti huwaweka kwenye nafasi za juu katika kupata tenda na wateja, na huonyesha Uweledi bora katika utendaji wa biashara kuanzia katika muonekano na utendaji wa tovuti. Inakadiriwa 80% ya watu duniani huonyesha kutokua na imani na Biashara ambazo hazina tovuti pale wanapotaka huduma/bidhaa fulani mtandaoni.

3. KUPATIKANA KWA URAHISI

Hebu fikira ila ahueni ya kupata kila unachokihitaji kwa urahisi, tena kupitia katika simu yako tu iliyo kiganjani kwako. Ndivyo ilivyo kwa tovuti ambayo inajieleza kwa kila kitu kama ilivyo tovuti maridhawa ya http://rednet.co.tz . Ile raha ya kupata taarifa, huduma au bidhaa kirahisi kupitia simu yako ya mkononi, hufanya wateja waongezeke maradufu na kusambaza sifa bora kwa uharaka sana katika jamii na katika mitandao ya kijamii hali kadhalika.

Hii huongezwa chumvi ya SEO (Search Engine Optimization) ambayo ni teknolojia iliyowekwa katika Injini za matafuto ya kimtandao inayowasiliana na tovuti yako na kuweka taarifa katika Injini hizo na hivyo kufanya taarifa za tovuti yako kuonekana haraka zaidi katika matafuto. Biashara imerahisishwa sana kupitia SEO kuliko kutumia Mitandao ya kijamii. Kama watu wanakwenda Google kutafuta taarifa, basi fahamu taarifa hizo hupelekwa hapo GOOGLE kwa kutumia teknolojia iitwayo S.E.O. Kufahamu zaidi kuhusu SEO gusa hapa chini

4. TANGAZO LA BURE MUDA WOTE

Tovuti yako inapokuwa hewani, maana yake biashara yako ipo wazi na inajitangaza muda wote na kufika sehemu zote duniani ambapo huduma ya internet inapatikana. Tangazo la bure kabisa hili. Kama tovuti yako ina ubora wa kuvutia zaidi katika muonekano, maudhui na utendaji, basi bila shaka biashara yako ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri sokoni na kupata wateja wengi kila siku. Jiulize hivi, unapofunga ofisi/biashara yako wakati wa jioni kila siku, wateja wapya wanaweza vipi kupata taarifa sahihi muda watakaohitaji?turudi kwenye mada yetu, kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako? Hii pia inawezeshwa sana na teknolojia ya S.E.O.

5. KUTENGENEZA MABALOZI (TESTIMONIALS)

Nafahamu wafanyabiashara wengi ambao hulazimika kuonyesha shuhuda/testimonials katika kurasa zao mara kwa mara ili kuendelea kupata wateja wapya zaidi, ni jambo jema kabisa. Kupitia tovuti yako, unaweza kuweka testimonials kwa idadi uitakayo bila kurudia rudia na katika mpangilio maalum na watu wakaweza kuona ushahidi utakaowaridhisha kuendelea kutumia huduma/bidhaa zako. Mara nyingi Mitandao ya kijamii huzuia kuoneka kwa biashara kwa urahisi kutokana na wimbi la watumiaji wenye maudhui tofauti tofauti katika ratiba ya saa (timeline) yako unayopitia katika mitandao hio, hivyo kusababisha usumbufu (distractions) katika biashara yako.

6. UAMINIFU (TRUST)

Hamna kitu muhimu katika uendeshaji wa biashara na kukuza mahusiano na mteja kama UAMINIFU. Ili kupata wateja wa kudumu katika sekta nyingi, kuwa na tovuti hai ni muhimu katika kudumisha mahusianao katika ya mfanyabiashara kwa muda wowte mteja atakaohitaji.

7. POSITIVE ROI

Ikiwa ni Return On Investment (ROI) au Rejesho baada ya Uwekezaji, unapoendesha biashara ambayo ina gharama zake kama umeme, kodi, maji, mafuta n.k, ukijiuliza utaweza vipi kurudisha gharama hizo upate faida? Njia moja nzuri ni matumizi ya tovuti bora yenye uwezo kunasa wateja wapya kwa njia ya mtandao muda wote (24/7) kirahisi kabisa.

8. THAMANI INAYODUMU

Uzuri/Faida moja muhimu kuhusu tovuti ni kwamba, unapoitengeneza una uhakika wa kuimiliki milele na kuifanyia marekebisho muda wowote itakapohitajika kufanya hivyo. Hivyo thamani ya biashara yako itaendelea kuwepo muda wote tovuti yako inapokuwa hewani.

9. HUDUMA BINAFSI YA MSAADA KWA WATEJA

Tovuti yako inapokuwa hewani 24/7 una uhakika na kutoa huduma bora kwa mteja mmoja mmoja kuhusu maulizo ya huduma/bidhaa ulizonazo, bei, ushauri nakadhalika. Hivyo kuimarisha mahusiano na ukaribu wako na wateja wako wakiwa popote duniani kwa urahisi kupitia miundombinu mbalimbali unayoweza kuiweka katika tovuti yako kama matumizi ya chatbots na barua pepe maalum za kibiashara (zenye jina/domain name ya tovuti yako).

10. MASIJALA (DATA CENTER) RAHISI YA MTANDAONI

Tovuti yako inaweza pia kuwa masijala rahisi kwa wafanyakazi, wateja na mtu yeyote anayehitaji kujua taarifa kuhusu huduma/bidhaa unazohusika nazo. Mfano mzuri ni tovuti yetu maridhawa ya http://rednet.co.tz ambayo zaidi tu. ya kwamba inatoa taarifa kuhusu huduma tunazohusika nazo za kutengenza websites, softwares, apps n.k, lakini pia tovuti inatoa taarifa muhimu mbalimbali kuhusu Biashara, Uchumi na Teknolojia. Taarifa hizi zimetengenzwa mahsusi kwa ajili ya kuimarisha Biashara za wateja wakiwa popote duniani. Pia taarifa hizo zinalenga kuhamasisha matumizi ya Teknolojia katika njanja mabimbali za kiuchumi haswa kwa wafanyabiashara waliopo kusini mwa jangwa la Sahara.

NOTE: Katika ulimwengu wa kisasa wa Dijitali, ili kutengeneza nafasi ya kupata wateja zaidi huna budi kuwa na Tovuti hai itakayobeba taarifa muhimu kama jina la biashara, anuani, mawasiliano na maudhui kuhusu huduma na bidhaa zako. Zaidi, weka pia matumizi ya SEO kuongeza kasi.

BONUS POINT: Tovuti yako unapoisajili, unashauriwa pia upate kirurushi cha barua pepe yenye jina/domain name sawa na tovuti yako. Mfano, tovuti yako inapatikana katika anwani ya www.mfano.com, hivyo barua pepe yako ya kiofisi unaweza kuchagua kuwa info@mfano.com au maulizo@mfano.com au jinalako@mfano.com. Kwa kutumia barua pepe zenye jina sawa na anwani ya tovuti yako, unajiweka katika nafasi nzuri ya kuimarisha biashara yako na kuongeza wateja wapya na kazi zenya manufaa haraka zaidi katika biashara/kampuni yako. Hii ni sababu muhimu sana unapojiuliza kwanini ni muhimu kuwa na website (tovuti) rasmi ya biashara yako. Website inakufanya unakuwa official kiukweli kweli.

Pia kuna makala hizi hapa ambazo zitakupa mwanga zaidi kuhusu namna bora za kuimarisha uchumi wa biashara yako kwa kutumia Teknolojia:

  1. UKIRITIMBA KATIKA BIASHARA, NI ASALI AU SHUBIRI?
  2. BRANDING vs MARKETING, KIPI NI KIPI?
  3. KUANZISHWA KWA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA (AfCFTA), KUNA MANUFAA GANI KWAKO?
  4. IJUE NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA BIASHARA YAKO.

Umejifunza nini kupitia makala hii ya kuhusu kwanini ni muhimu kuwa na website(tovuti) rasmi ya biashara yako? Tafadhali unaweza kuwasilisha maoni yako kupitia sanduku la maoni (comments box) lililo hapo chini au kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yanayopatikana katika Footer Bar chini kabisa ya ukurasa huu. Pia usisite kuwashirikisha wenzako makala haya kwa kushare link yetu ya https://rednet.co.tz mara zote. Karibu!

Unataka kufanya malipo kwa huduma zetu bila kuhofia makato ya miamala?

Sasa tumekuletea huduma ya LIPA NAMBA ya M-PESA (TILL NUMBER) – 5432715 ambapo unaweza kututumia TIP ya kutupongeza kwa kazi nzuri au Kulipia huduma unazozipata kutoka kwetu BILA MAKATO ya miamala.Tumia LIPA NAMBA yetu muda wowote yaani 24/7.

Kwanini uwe na website ya biashara yako?
9 thoughts on “KWANINI NI MUHIMU KUWA NA WEBSITE(TOVUTI) RASMI YA BIASHARA YAKO?”
  1. Hello my friend! I wish to say that this article is awesome, nice written and include approximately all vital infos. I would like to look more posts like this.

    1. Whatsapp yetu ipo active ndugu Saidi, tucheki kupitia namba hizi hapa 0765834754. Karibu sana aisee..

  2. Baada ya kusoma hili andiko nimejigundua kumbe nilikuwa napoteza muda tu sasa wacha nifanye kazi mpaka watu waniite freemason

    1. Muhimu sana hilo boss. Ukihitaji usaidizi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba yetu hii hapa ambayo pia inapatikana kwa WhatsApp: 0765834754. Mimi naitwa Faustine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *