KWANINI MTEJA AKUCHAGUE WEWE?

Feb 23, 2023 Technology Updates
Kwanini mteja akuchague wewe

Maisha ya biashara za mtandaoni ni marahisi sana kama ukizingatia tabia za wateja mtandaoni, na ni magumu sana ukipuuzia/usipozijua. Kwanza, hakikisha ukitafutwa unapatikana. Swala la kujiuliza ni, Kwanini Mteja akuchague wewe aache watoa huduma na wafanya biashara wengine?

Zipo sababu nyingi sana mtu akiwa mtandaoni anaziangalia ili ajiridhishe kabla hajawa mteja wako. Leo hapa tutaziona 6 tu. Zingine nitaziweka kwa status yangu ya WhatsApp. Ukihitaji kujifunza zaidi gusa hapa 0765834754 nitumie text yenye jina lako ili nikusave chap.

Mwaka 2022, niliweka story hapa kuhusu jamaa yangu fulani ambaye aliona kazi zetu mtandaoni, akashawishika kuchukua namba kisha akanitafuta tufanye kazi yake, na mpaka leo tumejenga uhusiano bora sana. Ile stori ni hii hapa kama ilikupita Faida za Kutumia Google kama Jukwaa la Biashara yako.

Baada ya kupublish stori hio, nilipokea requests nyingi sana kutoka sehemu mbali mbali yakiwemo mashirika ya kiserikali, binafsi ya yale ya kimataifa.

Leo hii sasa nataka nikwambie Kwanini Mteja achague kufanya kazi na wewe na awaache wengine? Fuatilia dondoo hizi hadi mwisho:

1. UBORA WA KAZI/BIDHAA/HUDUMA: Sikufichi, watu wanapenda vitu vizuri bwana. Hakuna anayependa bidhaa/huduma mbovu. Hata utumie mbinu gani za kunasa wateja mtandaoni, kama bidhaa/huduma zako hazina ubora unaotakiwa, jua apo unacheza tu. Utapata tabu yani.

Kama bidhaa/huduma zako zinatolewa na wafanyabiashara wengine, hio ni fursa nzuri kwako. Fanya uchunguzi, angalia wapi unaweza fanya improvements, ongeza ubunifu kidogo upande wako kisha peleka mzigo sokoni. Hakunaga miujiza kwenye hili. Lazima utie juhudi muda wote.

2. UBORA WA HUDUMA UNAYOTOA; Kama kuna kitu kinafanya wafanyabiashara wengi hawakui kibiashara licha ya kuwa na skills au bidhaa/huduma bora, basi ni hili la kushindwa kutoa huduma zinazomridhisha mteja. Angalia, watu wanatofautiana sana kwenye namna ya kutoa na kupokea maoni na changamoto. Wewe sasa kama mtoa huduma lazima ujue jinsi ya kujishusha kwenye kupokea maoni na changamoto na vile vile kwenye kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu. Huduma bora inaenda sambamba na kuijua saikolojia ya mteja wako. Cheza napo vizuri hapo.

Kuna makala hii kuhusu Umuhimu wa Takwimu kwenye utoaji wa huduma bora katika biashara yako. Ifuatilie hapa uelewe kwanini unapaswa kutoa huduma bora muda wote kwa wateja wako.

3. PATIKANA SEHEMU MBALIMBALI MTANDAONI; Katika mitandao ya kijamii, kila mahali watu hujihusanisha kitofauti. Mfano utagundua watu wa facebook na twita ni tofauti kabisa. Lakini sikufichi, wengi ni wale wale tu. So unapaswa kupatikana kwenye majukwaa yote makubwa kama Facebook, Twita, Linkedin, Instagram n.k Patikana huko kote kwasababu kila mtu ana mtandao wake ambao anautumia zaidi na wote hao unawahitaji leo. Na unachokitaka wewe ni kuifikisha biashara yako kwa kila mtu anayetumia smartphone yani. Si ndio? Fanyia kazi hilo.

nguvu ya mitandao ya kijamii unawezaje kutumia teknolojia ya intaneti na kompyuta katika biashara yako?

Kwanini mteja akuchague wewe?

4. TUMIA S.E.O; Hapa sitasema mengi kwasabau kule WhatsApp huwa natupia sana updates, tips, info na najibu maswali mengi sana kuhusu SEO. Pia kuna eBook maalum ambayo inaelezea siri zote unazohitaji kuzifahamu ili SEO iweze kuwa na manufaa kwako siku zote. Kuipata eBook hio pia hakikisha umesave namba yetu ya WhatsApp, kisha tuma ujumbe wenye jina lako na utapatiwa maelekezo.

In short hii SEO inakurajisishia biashara yako kupatikana haraka pale mtu akiwa anasearch taarifa kupitia Google. Yes, unaihitaji google zaidi sawa sawa na Google inavyohitaji taarifa za biashara yako kwa manufaa ya wateja wako duniani kote.

Mteja anayekutafuta ni mzuri sana kuliko yule unayemtafuta, si ndio? Sasa kwanini usijiweke kwenye mazingira ambayo yatamrahisishia mtu akiwa anatafuta bidhaa/huduma kule Google na kumpa majibu Kwanini mteja akuchague wewe kuliko wengine? Ukiitumia SEO vizuri itakujibu vema sana kwenye hili.

Takwimu za Internet Live Stats zinaonyesha kuwa kwa siku 1 tu kule Google huwa kunafanyika matafuto (searches) zaidi ya bilioni 3.5. Sasa linganisha na matangazo (Paid Ads) unayoyaonaga mtandaoni (Youtube, Insta na fb) na kuyaskip. Wapi utatoboa, kwenye Searches (SEO) au Ads?

5. TOA OFA KADHAA; Mwanaume huwezi kuoa ile siku ya kwanza unapokutana na Mwanamke, hali kadhalika, ni ngumu sana mtu akawa mteja wako siku ya kwanza tu amekutana na wewe huku mtandaoni. Ni muhimu sana kumpitisha mteja kwenye hatua kadhaa ili kusudi aweze kukujua zaidi akupende, akuamini na mwishowe sasa ndo aweze kuwa mteja wako wa kudumu.

Hii ni kwakuwa Biashara za Mtandaoni hutegemea sana kujenga Uhusiano Bora na watu usiowafahamu. Ndio maana unaona kuna wasanii wana mashabiki zao wanawapenda mpaka wakiwaona wanazimia japo hawafahamiani.

Hii ni kwasababu wasanii hao waliwapa values/ofa/zawadi nyingi ambazo ziliwafanya mashabiki zao wawapende sana hata kama hawajuani kiundani. Kadhalika, ukiwa unafanya biashara mtandaoni lazima ujifunze kutoa tips, info, updates, ujibu maswali na ujichanganye na wateja wako.

6. DHIHIRISHA KWAMBA BIDHAA/HUDUMA UNAYOTOA NI GHALI KULIKO GHARAMA ANAYOLIPA: Tunaishi kwenye zama ambazo kila mtu anauwezo wa kufanya biashara na akapanga bei itakayompa unafuu. Mfano, kwenye kutengeneza website ukizunguka huku mtandaoni utaona kila mtu ana bei yake.

mageuzi ya Intaneti (iot) katika biashara na maisha. Jihudumie leo kutoka Rednet Technologies.

Kwanini mteja akuchague wewe?

Biashara zimekuwa huru sana. Kila mtu anao uwezo wa kufanya biashara mtandaoni. Sasa unapaswa kujiweka kwenye nafasi ambayo mteja atakuchagua always akikutana nawe mtandaoni. Kwanini mteja akuchague wewe? Tips hizo hapo. Tips nyingine zipo WhatsApp hapa kwa kugusa namba hii 0765834754

Umejifunza nini kwenye makala hii ya leo kuhusu Kwanini mteja akuchague wewe? Kuna mahali hujaelewa? Niulize swali.. Share, Like na ucomment hapo chini maoni na maswali yako.

Cheers.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *