FAHAMU KUHUSU MFUMO WA MAWASILIANO YA SIMU (MOBILE ECOSYSTEM) NA FAIDA ZAKE KATIKA BIASHARA

Je Wajua?

Mfumo wa mawasiliano ya simu (mobile ecosystem) huchangia shemu muhimu sana katika uchumi wa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara? Uchumi wa nchi hizo kwa pamoja umefikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 110 ($110 b) ambayo ni sawa na 7.1% ya pato la taifa (GDP) katika mwaka 2017. Hii inajumuisha faida za moja kwa moja za mfumo huo, faida zisizo za moja kwa moja (indirect impact) pamoja na ukuaji wa uzalishaji unaoletwa na matumizi ya huduma za simu na teknolojia.

Tukigusia faida za moja kwa moja za mfumo huu wa mawasiliano ambao unajumuisha makampuni ya simu, watengenezaji wa huduma za miundombinu ya kiteknolojia, wasambazaji wa huduma/ bidhaa za simu, wafanyabiashara wa reja reja, watengenezaji wa simu na vifaa vyake pamoja na watengenezaji wa maudhui/applications/huduma za mtandaoni; mchango wao katika uchumi hukadiriwa kwa kupimwa thamani wanayochangia katika uchumi wa nchi husika ambayo hujumuisha bima ya wafanyakazi, faida ya ziada ya biashara pamoja na kodi.

Mwaka 2017, thamani iliyozalishwa na mfumo huu wa mawasiliano katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara ulikuwa dola bilioni 40 ambayo ni sawa na 2.5% ya pato la Taifa (GDP) ambapo makampuni ya simu peke yake yalijumuisha takribani 75% ya mchango huu.

Ukiachana na faida za moja kwa moja, zipo pia faida ambazo si za moja kwa moja (indirect impact) ambapo sekta hii hununua vifaa/huduma mbali mbali kutoka sekta nyingine. Kwa mfano makampuni ya simu hulazimika kununua umeme kutoka sekta ya nishati hali kadhalika wasambazaji na wafanya biashara wa reja reja wa vifaa/huduma za simu huhitaji usafiri kuwafikia wateja wao.

Kwa pamoja uzalishaji huu wa faida isiyo ya moja kwa moja ulitengeneza takribani 60$ mwaka 2017 (ambayo ni takribani 4% ya pato la taifa). Kiujumla ukiongezea na faida za moja kwa moja, sekta hii ya mawasiliano ya simu ilitengeneza 110$ bilioni sawa na 7.1% ya pato la taifa katika ukanda huu.

Hii inaleta picha gani Kibiashara?

Matumizi ya teknolojia ya simu pamoja na maendeleo ya simu za rununu (smartphones) huendesha uchumi kwa kuboresha uzalishaji, kupunguza costs za uendeshaji pamoja na kurahishisha upatikanaji wa huduma/bidhaa za kibinadamu.

Chanzo: Ripoti ya shirika la mawasiliano ya simu duniani la GSMA toleo la mwaka 2019.

Pia unaweza kupitia makala hizi hapa chini ambazo zinarandana na somo ulilolipata kwenye makala ya leo. Zitakusaidia sana ukimaliza kuzisoma zote.

  1. https://rednet.co.tz/unawezaje-kutumia-ujasusi-katika-biashara-yako-business-intelligence/ yenye kichwa “UNAWEZAJE KUTUMIA UJASUSI KATIKA BIASHARA YAKO?”
  2. https://rednet.co.tz/uwiano-wa-mali-assets-na-madeni-liabilities-katika-biashara-ukweli-ni-upi/ yenye kichwa “UWIANO WA MALI(assets) NA MADENI(liabilities) KATIKA BIASHARA, UKWELI NI UPI?”
  3. https://rednet.co.tz/changamoto-katika-biashara-mpya-inayoanza-funzo-lisiloepukika/ yenye kichwa “CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA MPYA/INAYOANZA, FUNZO LISILOEPUKIKA.”
  4. https://rednet.co.tz/fahamu-mchango-wa-ict-katika-maendeleo-ya-sekta-binafsi-barani-africa/ yenye kichwa “FAHAMU MCHANGO WA ICT KATIKA MAENDELEO YA SEKTA BINAFSI BARANI AFRIKA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *