JITAFUTE KWANZA ILI UFANIKIWE
Mwaka 2017 wakati tunaanzisha Rednet Technologies tulikua na vision kubwa sana, kama ile watoto wadogo wanavyoota kuwa Marubani na Wanasheria. Hata hivyo kuifanyia kazi vision hio haijawahi kuwa rahisi. Jasho, Damu na Machozi haviepukiki. Mwaka 2020 nikagundua kwamba unatakiwa u jitafute kwanza ili ufanikiwe.
Vision ya Rednet Technologies ilikuwa ni “Kuhakikisha Tunawafikia Wafanyabiashara wote wadogo na wale wa kati wanaofanya shughuli zao katika eneo la Afrika Mashariki na Kati, na kuimarisha Biashara zao kwa matumizi ya Teknolijia za kisasa kutoka kwetu”.
Hio Vision inahitaji Maarifa, Ujuzi, Muendelezo (Consistency), Ubunifu na zaidi, Teamwork. Kama wewe ni mfanyabiashara na una ndoto za kufanikiwa katika shughuli zako basi hili la Teamwork unapaswa kulitazama kwa macho matatu. Leo tutachambua kwa undani hapa kwenye TEAMWORK.
Ile Team yetu ya kwanza tulitamani ingeweza kufanikiwa kuifikisha Rednet pale inatakiwa kufika. Lakini haikuweza kufanya hivyo. Hivyo, mwezi March, 2018 kwa huzuni kubwa Rednet Technologies ilisitisha Operations zake kwa kipindi cha Mwaka mzima mpaka May 2019. Kilikua ni kipindi kigumu mno kwangu binafsi kwa sababu mimi ndiye nilikua Visionary Leader.
Nilitamani sana Rednet Ifanikiwe, roho yangu ilikua ikiniuma sana kuona juhudi zangu hazikuwa zikizaa matunda. Kila mbinu niliyokua naitumia haikunipa majibu ya kufurahisha. Nilikata tamaa kabisa. Hata hivyo hio 2019 tulipata kazi chache za kuwahudumia wateja wetu, lakini bado hatukuweza kutanua vizuri mtandao wa wateja wetu na kushirikiana nao kwenye shughuli zao vile inavyotakiwa.
Hali hii ilikwenda mpaka Octoba, 2020, kabla ya ule Uchaguzi Mkuu ndipo ambapo ndugu yangu wa zamani sana, JEOFFREY alinipa idea ya kimapinduzi sana.
JEOFFREY NI NANI?
Huyu Jeoffrey ni rafiki yangu wa zamani sana. Tulisoma wote shule ya msingi japo yeye alinizidi darasa moja. Na zaidi tuliishi wote mtaa mmoja kwa kipindi kirefu sana katika maisha yetu, zaidi ya miaka 18. Kipindi chote icho sikuwahi kujua kuwa mfumo wake wa biashara utanifaa.
Huyu jamaa ana biashara yake ya kusambaza vifaa vya miundombinu ya maji kama koki, elbows, mabomba n.k. Zaidi yeye amejisajili kwenye mfumo wa manunuzi ya serikali (TaNEPS). Huko anapata tenda nyingi sana kuhusu miradi ya maji ya serikali nchi nzima. Kifupi anafanya vizuri sana sokoni.
Hio siku sasa alinijia akihitaji nimtengenezee ecommerce website ili kusudi aweze kuuza bidhaa zake kwa rejareja kwa wateja wake walio nje ya mfumo wa manunuzi. Hivyo akanipatia nyaraka za wasifu wa kampuni (Company Profile) yake. Sasa wakati naifanya hio kazi yake nikawa najiuliza, hivi mimi nashindwaje kutanuka kama jamaa yangu hapa. Hapa kuna kitu muhimu sana, jitafute kwanza ili ufanikiwe.
Najua hata wewe unayesoma unajiuliza hili swali “NAWEZAJE KUTANUA BIASHARA YANGU?” Well, kupitia vikao vichache nilivyokaa na huyu jamaa yangu, nikaweza kugundua namna ambayo tunaweza kusambaza Bidhaa na Huduma zetu kwa watu wengi na kwa haraka zaidi.
Hivyo, tukaanzisha Huduma ya Kusambaza Vifaa vya Ofisini na Computer kama mafile, diaries , flash disks, antivirus na vitu vya stationery unavyovijua. Wateja wetu wakubwa tuloanza nao walikua ni makampuni na taasisi ambazo kimsingi wametupa ushirikiano mkubwa sana.
Tumekuwa tukipokea Oda kutoka sehemu mbalimbali na tumeweza kukuza mtandao wa wateja wetu haraka na kwa ufanisi mkubwa kupitia huduma hii. Jambo hili likatulazimu kwenda mbele zaidi ambapo sasa kupitia tovuti yetu ya https://rednet.co.tz unaweza ku-request oda na tukakufikia.
Urafiki wetu na Jeoffrey ukazidi kuota mizizi ambapo sasa tunashirikiana kwenye mambo mengi sana ya kikazi. #VijanaWenzangu mimi huwa nawaambia “Tutumiane vizuri katika shughuli zetu za kiuchumi. Delegate your tasks kwa kuwa baraka zipo kwenye KUTOA zaidi kuliko kwenye KUPOKEA“.
Mimi rafiki zangu nawapa michongo mingi sana, ya muda mrefu na ile ya muda mfupi. Kadhalika rafiki zangu wananipa michongo mingi sana, ya muda mrefu na ile ya muda mfupi. Wataalam wanakwambia “Your Network is Your Net worth“. Kuna maana kubwa sana kwenye huo msemo ukitafakari.
Kama connections ulizonazo hazikutumii vizuri sasa usilalamike, watumie wewe kwenye mishe zako. Yes, maana hai-make sense kuwajua watu wazuri wanaoweza kuipush biashara yako halafu huwatumii eti kwa kuwa wao hawakutumii kwenye mishe zao. How? Make sure you get upper hand on it.
KARIBU KATIKA HUDUMA MPYA:
Website yetu sasa tumeiweka ili kusudi kukupa wewe uwezo wa kuchagua huduma unayotaka kisha sisi tutapata request yako, tutakutumia Quotation ukiridhia tunakupatia huduma yako katika muda ambao utapanga wewe. Upewe nini zaidi?
Kwa vifaa vya Ofisini (stationeries) kama wino wa printa, flash disks, rim paper, peni (box) n.k gusa link hii https://rednet.co.tz/services/your-order/… Link hio itakupeleka direct kwenye ukurasa utakaokupa nafasi ya kutuambia huduma unayohitaji ukiwa popote Duniani.
Pia tumekuletea huduma mahsusi kwa ajili yako iitwayo “JIHUDUMIE” kupitia link hii https://rednet.co.tz/services/jihudumie-leo/… ambapo humo ndani utajipatia huduma kama zinavyoonekana kwenye picha hapa.
CHANGAMOTO:
1. KUWA RASMI: Najua watu wengi humu mitandaoni biashara zenu si rasmi, kwa maana ya kwamba hazijasajiliwa katika Mamlaka za Kiserikali (BRELA, TRA, HALMASHAURI, BENKI etc). Sasa mtindo huu wa Usambazaji unakutaka kusajili biashara yako kwa kuwa biashara/kampuni yako sasa inakwenda kufanya kazi na biashara/kampuni zingine (B2B). Matumizi ya Quotations, Proforma Invoice, Tax Invoices, EFD receipts na Delivery Notes kwenye mtindo huu wa Biashara ni kama Katiba katika utawala wa Nchi. Eneo hili kama Mjasiriamali unapaswa kuwalo makini sana yani.
Hivyo ifanye biashara/kampuni yako kuwa rasmi kwanza ili kujihakikishia unafanya shughuli zako bila kubughudhiwa na mtu yeyote.
2. UCHELEWESHWAJI WA MALIPO: Kuwa msambazaji/Supplier maana yake ni kwamba unafanya kazi kwa pesa yako na pesa hio utaingiziwa baada ya mwezi mmoja mpaka miezi sita. Hivyo, kukaa muda mrefu bila kuingiziwa pesa si kazi ndogo, uvumilivu lazima uchukue nafasi yake hapa.
3. MTAJI: Kama ulivyoona hizo changamoto zingine hapo juu, kufanya usambazaji lazima uwe na Mtaji wa kutosha kuweza kuhudumia Wateja wako kikamilifu kabla wao hawajakuingizia pesa siku za mbeleni. Hapa lazima uwe na pesa ya kufanya kazi mkononi ili usije ukatolewa katika game.
Hata hivyo, changamoto hizi hazitakiwi kukurudisha nyuma, katika harakati jitafute kwanza ili ufanikiwe lazima uhakikishe unapambana kwa njia zozote ili kusudi mafanikio yako yakapate kujidhihirisha. #VijanaWenzangu muda wa kupambania future zenu ndio sasa. Pambaneni haswa.