JE WAJUA KUWA BANDO LAKO NI MTAJI?

Je wajua kuwa bando lako ni Mtaji unawezaje kutumia Ujasusi katika biashara yako (Business Intelligence)?

Imagine una ofisi yako (eneo la biashara) na pia unayo akaunti yako ya twita, Instagram au facebook. Lakini hujui namna ya kutengeneza mvuto kwa watu ili wakutafute, wakufollow, wakuamini na wafanye biashara na wewe. Unafanyaje? Je wajua kuwa bando lako ni Mtaji tosha? Fuatilia makala hii mpaka mwisho kufahamu kiundani.

Imagine hujawahi kutengeneza mahusiano ya kibiashara na followers wako, hata mmoja yani, na kila siku upo mtandaoni kufuatilia habari mpya zinazojiri kwenye Bongo Fleva, Bongo Muvi, Mpira, Umbea, Siasa n.k. Kuna muda unatamani biashara yako iwe kubwa lakini hujui mbinu gani unaweza kutumia ili kuhakikisha biashara yako inazidi kuwa Imara kila siku. LEO hii Nazungumza na wewe hapa.

1. CHANGAMKA KIBIASHARA UWAPO MTANDAONI:

Kabla ya yote, fahamu kuwa biashara inafanyika vizuri katika mazingira yaliyojengwa kwa mahusiano imara, hivyo hebu tizama unahusiana vipi na watu waliokuzunguka na followers wako. Hili ni eneo pana ambapo unatakiwa ufahamu saikolojia ya watu wako hasa wateja na kujua namna ya kukabiliana nao positively. Maana mitandaoni kuna kila aina ya watu na tabia zao, kuna wenye kiburi, kuna wababe, wachechi, wajeuri, wanafunzi, wenye hekima, wapole, wenye lugha chafu na micharuko. Sasa jukumu lako ni kuwajua na kukabiliana nao bila kukwazana. Cha kufanya ni kuhakikisha unatumia vizuri bando lako tu hapa.

Mtandao saidizi jinsi ya kukabiliana na hasara kwenye biashara mbinu za kuwa tajiri

Humu mitandaoni wewe kama sio mtu maarufu basi hakikisha unakuwa mchangamfu kwa kadiri ya inavyowezekana. Kuwa “mchangamfu” haina maana uwe mwenye kiherehere, shobo au mtu wa kujipendekeza, lakini ujue namna kuchangia mijadala mbalimbali na kujihusanisha na watu vizuri.

2. JE WAJUA KUWA BANDO LAKO NI MTAJI WA KUJIJENGA KUWA MTAALAM?

Kwenye biashara hili ni eneo muhimu sana, yani sawasawa na uti wa mgongo. Watu wengi hudhani biashara ni kuuza na kununua tu, of course wako sawa. Hata hivyo ili biashara yako iweze kunawiri katika mazingira ya mtandaoni yaliyojaa ushindani wa kila aina, unapaswa kujua zaidi ya “kuuza na kununua”. Humu mtandaoni watu hukwepa sasa matangazo, hivyo “unapoweka tangazo lako hakikisha halionekani kama TANGAZO bali lionekane kama HABARI MPYA kwa yeyote anayesoma.”

Mtego ndo upo hapo. Lazima uwe mtaalam wa kuhudumia faida zinazotokana na bidhaa/huduma zako. Usiuze tu ukaishia hapo, hebu kuwa MLEZI wa mteja wako. Binafsi nina LIST ya wateja wangu ambapo huwa nawatumia updates mbalimbali kuhusu hali ya biashara na uchumi katika muktadha wa teknolojia BURE kabisa. Ungependa kuwa kwenye list hio? Nitumie ujumbe kwa WhatsApp sasa hivi kwa kugusa namba hii hapa 0765834754

3. JE WAJUA KUWA BANDO LAKO NI MTAJI WA KUFUNGUA WEBSITE:

Kwa kasi ambayo teknolojia inakwenda nayo nina uhakika usingependa kupitwa na fursa lukuki zinazokoja na mapinduzi haya ya 4 ya viwanda yanayoendelea duniani. Fikiria, Kusini mwa Jangwa la Sahara kunakadiriwa kuwa na watumiaji wa internet zaidi ya milioni 400. Nchini Tanzania kunaripotiwa kuwa na watumiaji wa internet zaidi ya milioni 29 mpaka kufikia mwaka 2022 Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA.

jinsi ya kuanzisha website

Je wajua kuwa bando lako ni Mtaji

Sasa kwa kutumia hilo Bando lako la internet, unalitumiaje kuwafikishia watu hawa bidhaa/huduma yako? Website ni kifaa (Digital tool) muhimu na mahsusi kwa kuwafikia watu wengi ndani ya muda mchache sana. Kwenye website unao uwezo wa kutoa huduma za kushauri na mafunzo nakdhalika. Zaidi unaweza kujua faida za kuwa na website kupitia hapa WEBSITE INASAIDIA VIPI KUIMARISHA BIASHARA YAKO?

Kuweza kupata website yako wasiliana nasi kupitia namba 0765834754 au email info@rednet.co.tz ili tukusaidia kutatua changamoto zinazokukabili. USIBAKI NYUMA.

4. JE WAJUA KUWA BANDO LAKO NI MTAJI WA KUWA MKWELI/AMINIKA UKIWA MTANDAONI:

Moja kati ya eneo ambalo linawapa changamoto wafanyabiashara wengi ni hili la kuwa mkweli na Muaminifu. Wateja wengi huwa wanakwazika sana wanapofanya kazi na wafanyabiashara ambao si wakweli/waaminifu. Hiki ni kitu kibaya sana na hata wewe usingependa kikutokee.

Uongozi vs Utawala katika miradi/biashara, kipi kinafaa zaidi? gharama vs thamani, kipi kinafaa zaidi?

Je wajua kuwa bando lako ni Mtaji

Unapojijenga kwa kuwa mkweli unatengeneza mazingira ya kuaminika ambayo yatakufanya upendwe na watu na wao waweze kufanya biashara na wewe bila wasiwasi. Hata wewe mfanyabiashsra, siku ukiwa mteja usingependa kukutana na mtoa huduma ambaye si mkweli/mwaminifu, si ndio?

Ni matumaini yangu umegundua kwamba Bando lako ni Mtaji muhimu sana katika uendeshaji wa biashara yako katika zama hizi za kidijitali? Lazima ujue namna nzuri ya kuendesha akaunti yako ya mtandao wa kijamii ili ilete tija kiuchumi katika biashara yako. Unahitaji mtu wa kuendesha akaunti yako? Wasiliana nasi mara moja.

2 thoughts on “JE WAJUA KUWA BANDO LAKO NI MTAJI?”
  1. This is my first time I have met with this platform. Nawapongeza saana kwa kazi nzuri. I also have a dream of doing business via internet so I hope that I’m gonna be among of your customers.

    1. karibu sana Elifuraha. Endelea kutembelea tovuti yetu hii ili kupata taarifa muhimu kuhusu kuanzisha biashara na kuiimarisha kiuchumi kila siku. Zaidi tuzidi kuwasiliana tafadhali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *