KWANINI HUPATI WATEJA MTANDAONI?
Kila mtu anapenda maisha mazuri, kufanikiwa kibiashara, kuwa na amani na uhuru wa kufanya kile kinachokupa furaha muda wowote. Sasa uko tayari kuingia gharama ili kuyapata matamanio yako? Umeshajiuliza Kwanini Hupati Wateja Mtandaoni licha ya Juhudi unazoweka?
Mwaka 2010 wakati nafungua account ya Facebook nilikua nafurahi sana kukutana na rafiki zangu tuliopotezana miaka mingi baada ya kumaliza Primary School na sekondari. Ilikua safi sana kuona picha za washkaji wakiwa na maisha yao baada ya shule.
Baadae tukaanza kupata marafiki wengine katika mtandao pendwa wa facebook. Nyakati hizo Mtandao wa Twita ulionekana kama mtandao wa Wanasiasa, Instagram ya Wasanii na Masuperstar. Ila Facebook kule wote tulionana kuwa ni level moja. So kule ndo tuliona kuna lile vibe la wote.

Lakini miaka ilivyozidi kwenda, Matumizi ya Mitandao ya Kijamii yalikua yakibadilika mdogo mdogo, hasa baada ya kushuhudia Wasanii na watu waliokuwa na Followers wengi mitandaoni waliposhindwa kuimarisha Uchumi wao kupitia Nguvu ya Mitandao. Hapa kitu kipya kikatambulishwa.
Ilifika mahali sasa ule utaratibu wa kuwa na urafiki na wale tu uliowahi kusoma nao sasa ulipitwa na wakati na badala yake, Rafiki/Followers/Follows wa mtandaoni wakawa ni wale ambao tunashare nao “Interests” Hapo ndipo mbinu za kufanya biashara mitandaoni zilipoanza kushamiri.
Tayari nimeshakuandalia makala maalum itakayokupa mbinu muhimu za kunasa wateja mtandaoni. Kama unataka kuzifahamu mbinu hizo ili uzitumie kwenye biashara yako basi fuatana na makala hii hapa Jinsi ya kuongeza mbinu za kulifikia soko mtandaoni.
MAMBO SABA (7) YANAYOKUKOSESHA WATEJA MTANDAONI
Tumeshaona jinsi Mitandao imebadilika kutoka ilipoanza, sasa kuna mambo unayoyafanya kwa kujua au kutokujua yanayokukosesha wateja. Jambo la 5 litakushtusha sana. Hebu tuyaone hapa;
1. Kutokuwa na Bidhaa/Huduma inayokutambulisha;
Hapa unatakiwa kuwa makini na kuelekeza focus yako kwenye bidhaa/huduma fulani specific. Inaweza isiwe bidhaa/huduma moja, lakini hakikisha unakuwa na ile bidhaa/huduma inayokutambulisha. Mfano: Unauza fenicha, shikilia hapo hapo.

Zile zama leo unapost fenicha, kesho unapost computers keshokutwa unapost picha uko unasafiri, mara unapost unakula chakula., hivyo ni vitu ambavyo vinakupunguzia mvuto mtandaoni. Sisemi usipost kabisa, hasha, katika post 10, 7 ziwe ni kuhusu fenicha, 3 maisha binafsi.
2. Kushindwa kuingia kwenye Orodha ya Wanaofanya biashara kama yako mtandaoni;
Kuna ile dhana ya kuogopa ushindani au ile kuwekeana mtimanyongo na washindani wako. My friend, huku mtandaoni make sure unajenga uhusiano na kila unayekutana naye. Itakusaidia sana kuendelea kudumu sokoni.
Kuingia kwenye orodha(list) ya wafanyabishara huna budi kuwa support wafanyabiashara wenzako mtandaoni. Ndio, Wasukuma wana msemo wao wanakwambia “Scratch my back, I’ll scratch yours.”
3. Kutokua na muendelezo wa Maudhui kutasema kwanini hupati wateja mtandaoni;
Je wajua kwamba kwa siku huwa kunakuwa na posts zaidi ya milioni 50 katika mitandao mbalimbali duniani. Sasa ndugu unapost mara 1 kwa wiki unategemea nani ataiona hio biashara yako? Hakikisha unapost mara nyingi kadiri iwezekanavyo.

4. Kushindwa Kuwasiliana Vema;
Kupost bidhaa/huduma zako mtandaoni ni jambo moja, lakini uwezo wa kuwasiliana ndio muhimu sana. Shuleni tulisoma ile Communication Skills, sasa mtaani unatakiwa uwe na uwezo wa kuwasiliana na kujua wapi, sangapi useme nini. Ni maarifa hayo.
Mtaalam wa mitandao bwana @GillsaInt ana mbinu yake anakwambia katika maudhui yako unayopost mtandaoni, hakikisha 80% ni yanahusu thamani (value) za bidhaa/ huduma zako kama Faida, Jinsi ya Kutumia, Changamoto nk. Na 20% zinazobaki ndo upost sasa Matangazo ya kuuza hio biashara.
5. Kutokuwa na Miundombinu ya Kurahisisha biashara Mtandaoni;
Umeshaona wale wanakwambia No Facebook Acc, No Insta Acc, No twitter etc. Skia, kama unataka kufanya biashara ukafanikiwa mtandaoni USIFUATISHE hizo akili zao. Hakikisha una miundobinu humu mtandaoni.
Mitandao ya kijamii ndipo ilipo NGUVU halisi ya biashara ya mtandaoni. Jifunze namna unavyoweza kuitumia kwa faida ya biashara yako. Kama unataka kuifahamu NGUVU hio ya mitandao, basi fuatana na makala hio hapa kufahamu zaidi.
Lengo la kufanya biashara mtandaoni ni kuhakikisha unakuwa na wateja wengi kadiri iwezekanavyo, si ndio? Kama ni hivyo, fanya research, kisha tambua wateja wako ni kina nani na wako wapi. Fungua website yako, accounts za Insta, Facebook, Linkedin, Twitter n.k Kuwa available.
6. Kukosa Ushawishi na Ujuzi wa Kuuzia wateja Mtandaoni;
Sasa hapa naongelea uwezo wa kumshawishi mtu akapenda bidhaa/huduma zako kabla hajawa mteja wako. Kwenye hili @iamKaga pale twita anakupa funzo gani? Cha kwanza hakikisha watu wanakujua, kisha Wakupende au wapende maudhui yako, hapo ndipo watakujia.
Huo ushawishi hauji tu by default wala haujengwi ndani ya siku moja. Ushawishi ni tabia ya kuhoji na kutoa ufumbuzi juu ya changamoto zinazowakabili watu katika namna bora ya uwasilishaji. Hapa ndipo wanasiasa wanatupiga coz anaijua siri iliyopo kwnye ushawishi.
7. Kutokuwa na Njaa ya Mafanikio;
Tunarudi kulee mwanzo, unapost mara 1 kwa wiki, au mara 2 kwa mwezi halafu unasingizia huna muda wa kuandaa maudhui. Bro, ni vile tu huna njaa ya kufanikiwa. Njaa ya mafanikio ikikushika vizuri huo muda LAZIMA uupate na utautumia vizuri tu.
Kuna nyakati unabanwa na shughuli zako nyingine to the point unashindwa kuendesha biashara yako mtandaoni. Kuna nyakati nyingine unakata tamaa kwa sababu huna followers au huna idea uanzaje kuandaa maudhui ili ufikie yale matamanio yako. Ukifikia hapo wala usiwe na shaka..

Hata hivyo, katika biashara sio lazima kila jambo ufanye wewe mwenyewe. Nyakati hizi za mapinduzi ya teknolojia kila siku, ni muhimu kugawa majukumu kwa wataalam wa kuaminika ili kuhakikisha lengo na mipango yako inazidi kwenda kama utakavyo.
Hio ndio sababu sisi Rednet Tech. LEO hii tunakupa nafasi ya kuikuza biashara yako mtandaoni kwa;
1. Kukutengenezea Website bora.
2. Kukufanyia huduma ya SEO. Inafanyeje kazi hii? Gusa hapa kuifahamu zaidi.
3. Kukushauri aina ya maudhui ya kuyatumia kwenye kurasa zako za mitandao. Gusa hapa tuchati pale WhatsApp na upate huduma unayohitaji.
So, mambo haya 7 tuliyoyaona leo kwa uchache wake ndio yanakwambia kwanini hupati wateja mtandaoni. Umeshajua cha kufanya sasa? Hebu niambie wewe ni lipi umegundua leo kuwa ndio linakukosesha wateja? Mtandaoni hamna miujiza. Ni kuwa na maarifa na kuhakikisha unajifunza kila siku. Umependa makala hii? Share..